Miiko ya wafu na kaburi

Usingenialika kwenye hii mada ningelia sana! Shukrani zikuendee mkuu Waterbender umeniita kunakonihusu kwa asilimia miamoja
Mengi yaliyoandikwa hapa ni kweli kabida na baadhi nina mada zake
Nimemiss Sana mada zako Kaka,japo mleta Uzi nae kaanza kurithi mikoba yako Kabla hujafa.
 
Hivi kaburi likichimbwa likanyeshewa likawa na maji inakuaje tunaweka hivo hivo au tunaahirisha
Mimi Kuna Bibi yangu alizikwa mvua imenyesha hatari maji yanachotwa na ndoo,Ila mwaka huohuo tulizika wajomba wawili wa maana,wale wajomba wenye msaada kwa familia😭 yaani hapa nimesoma ndio naunganisha dots..
 
Hapo number 12 Ina maana tutasimamisha saa kwa muda gani?

Na hapo 16,kitanda kitabaki na hizo shuka kwa muda gani?
 
Hizo ni roho mbili zinapingana, automatically moja yenye nguvu inaweza kuizidi isiyo na nguvu na kuivutia kwakwe
Wakati wa ujaUzito wa kwanza bibi yangu alifariki alikuwa mlokole sana niliweka udongo na hakuna mtu alinikataza ,nadhani ni mila na desturi hutofautiana kati ya kabila na kabila
 
Ame
Amen. Dah...pole sana
 
"19. Marehemu azikwe mahali alipo pachagua wakati wa uhai wake, au la sivyo endapo mtaenda kinyume chake, vifo vitatokea katika familia hiyo. Na kama mtalazimisha kusafirisha mwili wa marehemu, basi msafara huo lazima utapata ajali njiani, na mtu mmoja lazima atakufa."


Hapo umenikumbusha kisa na mkasa wa Ajali ya Kologwe iliyo ua watu zaidi ya 19 mwezi huu
 
marehemu hawana mchezo wakikwambia usifanye hichi acha kwel
 
Hayo yote ni utumwa wa shetani na hayanihusu wala sishauri mtu yeyote kuyaamini na kuyafanya. Ondokeni katika utumwa huu wa Kiafrika kupitia mizimu. Hizi ni sheria za mizimu na hazina maana yoyote ni kutaka tu kumtega mwanadamu anayeamini hayo ili kummaliza, achana kabisa na imani hizi na zingine zote mbaya. Mwamini Yesu Kristo na wema wake kila kitu kitakuwa kizuri na shwari.
 
too slow
 
Kunyooshea kaburi kidole na kakalia kaburi au kukanyaga kaburi lisilo la ndugu, ni nuksi. Najikuta naziishi hizi kanuni bila hata ulazima.
 
Wachagga na ajali ya Tanga na vifo vya wanafamilia 14 ni mfano hai wa mwiko huu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…