Miiko ya kuvaa barakoa

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,267
12,565
Miili yetu inafanana na magari yanayotumia mafuta ya petrol na diseli kutembea pole pole na kutembea haraka. Ili gari litembee lazima itafutwe namna mafuta na hewa ya oxygen vitakutana na cheche ya moto ili vilipuke na kutoa nishati itakayolitembeza gari. Hivyo ni lazima uwe na tank lenye mafuta, fuel pump, plugs na betri. Mafuta yatakutana na hewa ya oxygen inayotoka kwenye air cleaner kwenye cylinder. hivyo mkandamizo wa mafuta, hewa na cheche za moto toka kwenye plugs ni muhimu sana.

Kama ukiongeza speed ya gari, kupanda mlima au kubeba mzigo mkubwa kwenye gari utahitaji pia kuunguza mafuta mengi na hewa nyingi ili kupata nguvu nyingi. Hivyo hakikisha kuwa air cleaner inapitisha hewa nyingi kwa kuisafika mara kwa mara au usiweke tambara au kitu chochote cha kuzuia hewa kuingia kwenye cylinder.

Binadamu pia ili kupata nguvu za kutembea, kukimbia, kucheza, kusex, moyo kudunda na seli za mwili kufanyakazi atahitaji kupata glucose (fuel) ambayo itakutana na hewa ya Oxygen kwenye mitochondria (cylinder) ambako glucose hivyo itaunguzwa na kutoa nishati inayohitajika kuupa nguvu mwili zA KUFANYAKAZI. Unapotembea, kimbia, cheza, sex, fanya mazoezi, kubeba mizigo mwili utahitaji glucose nyingi na oxygen nyingi ili kuunguza glucose kutoka kwenye vyakula vya kutia nguvu ili kupata nishati nyingi kulingana na kazi unayoifanya kwa wakati huo. Hivyo hakikisha kuwa hakuna kitu chochote kitazuia hewa ya kutosha isisafirishwe kutoka kwenye pua na mdomo, koromeo, mapafu, kwenye damu hadi ndani ya seli/mitochondria ambako glucose inakutana na hewa na kuunguzwa kutoa nishati inayohitajika kuuendesha mwili kwenye matukio mbalimbali.

Hivyo ndugu yangu mpendwa pamoja na jitihada za kujizuia na homa ya mapavu lakini usivae barakoa kama unatembea, unakimbia, unapandisha ngazi, unzacheza, unafanya mazoezi au hata kusex. Kazi hizi zote zinahitaji hewa nyingi na chakula/glucose nyingi ili kupata nishati ya kuutosheleza mwili wako kulinga na kazi unayoifanya. Barakoa inaziba njia ya kuingizia hewa kwenye mapafu hivyo inaruhusu hewa kidogo sana kuliko matarajio ya mwili na kusababisha yafuatayo:

1. Nishati ndogo sana mwilini kuzalishwa
2. Mlundikano mkubwa wa hewa ya carbon mwilini
3. Unyevu mwingi kwenye njia ya hewa
4. Mlukano mkubwa wa acid/lactic acid kwakuwa mwili haupati mahitaji kamili ya oxyen hasa wakati wa kufanya strenuous excises
5. Ubongo kufanyakazi chini ya kiwango, hauwi sharp kwenye kufikiria na unaweza kuwa na hasira nyingi hata kwa mambo madogo ya kawaida.

stay tuned, nitakuletea zaidi....
 
Back
Top Bottom