Mihayo Primary school

Nkungulume

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
2,988
1,209
Kwa wale waliosoma Mihayo Primary school na kumaliza mwaka 1974 Tabora hebu tukumbushe ni kitu gani kilichokufurahisha sana au kukuchukiza kipindi kile.
 
Kwa wale waliosoma Mihayo Primary school na kumaliza mwaka 1974 Tabora hebu tukumbushe ni kitu gani kilichokufurahisha sana au kukuchukiza kipindi kile.
Hii post ni ya zamani sana lakini hata hivyo imenivutia kuchangia. Ila mimi nimesoma shule hiyo zamani zaidi japo sikumailza kwani nilipata uhamisho pale wazazi wangu walipohamia Morogoro. Nilisoma darasa la tano na la sita mwaka 1968. Wakati huo ilikuwa ni Mihayo Upper Primary School na ilianzia darasa la tano. Wakati huo ulipaswa kufaulu mtihani wa darasa la nee toka lower primary school. Lower primary school niliyosoma ilikuwa ni Gongoni White Fathers iliyokuwa jirani sana na Mihayo Upper Primary school. Ninachokumbuka nakujivunia sana shule hiyo hadi leo ni mafundisho makini toka kwa walimu. Nakumbuka wakati huo adhabu ya viboko ilikuwa marufuku kutolewa na walimu wa kawaida isipokuwa mwalimu mkuu tu, Binafsi sijawahi kupigwa viboko nilipokuwa nasoma shule hiyo hadi nilipohamia Morogoro, lakini wee achaa mbadala wake ulikuwa ni mkali zaidi watoro na wachelewaji walikuwa wakifungiwa katika majengo yaliyokuwa bafu zamani, kumbuka shule hiyo zamani ndiyo ilikuwa St Marys secondary school, na kubadilishwa kuwa shule ya msingi, hivyo ikawa na majengo mengi kiasi kwamba mengine yalikuwa hayatumiki. Nakumbuka kuwepo kwa mafunzo ya Scout, nami nilivutika nakujiunga na mafunzo hayo walimu walikuwa wakitoka Kipalapala seminary. Nawakumbuka sana rafiki zangu Emilly. Michael Sikwala na Jumanne Idrisa hawa wawili tuliunda kundi letu tukajiita JIMSAM (Jumanne Idrisa, Michael Sikwala na Anthony Marwa). Nilifanikiwa kukutana na Jumanne Idrisa mwaka 1989 na siku moja alioniona akiwa anaendesha gari alijisahau na kuiacha gari katikati ya barabara na kuzusha mtafaruku lakini hakujali alinikimbilia kunisalimu. Lakini sijapata kukutana naye tena pia hata Michael Sikwala wala Emily. Jambo kubwa sana lillotokea mwaka niliojiunga na darasa la tano ni kufutwa kwa darasa la nane, Mwaka huo wanafunzi wa darasa la saba na darasa la nane walifanya mtihani mmoja. Jambo lingine ninalokumbuka ni kwamba Japo nilikuwa nasoma hapo sikujua kwamba Mihayo ni jina la Askofu wa kanisa la Roman Catholic pale Tabora hadi siku tulipokutana naye njiani (shule ilikuwa karibu na makazi ya askofu), wanafunzi wenzangu wakasema huyo ndiye askofu Mihayo, mtu mnyenyekevu sana kwani alitusalimu, ndipo nilipojua asili ya jina la shule yetu.
 
Back
Top Bottom