Mihadhara ya katiba ya Prof. Shivji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mihadhara ya katiba ya Prof. Shivji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by HOMOSAPIEN, Jun 7, 2012.

 1. HOMOSAPIEN

  HOMOSAPIEN JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 719
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Naomba msaada kidogo wa kutaka kuelimishwa,kuna jambo limenitatiza jana wakati naangalia kipindi cha Prof. Shivji cha Katiba,kipindi kinachorushwa na ITV,kuna Mshirika mmoja aliimuuliza Prof.kuwa anapata tabu kidogo wakati ikiongelewa Tanganyika,ambayo haipo kwa sasa kutokana na muungano lakini Zanzibar nchi iliyoungana na Tanganyika bado ipo na wanajitambulisha kama wanachi wa Zanzibar na wana serikali yao.sisi wa bara tunajitambulisha kama wa Tanzania Bara kwa nini na sisi tusijitambulishe kama wa Tanganyika?

  Majibu ya Prof. yalikuwa kuwa hiyo Tanganyika haikuwepo, na kama ilikuwepo ni kwa muda wa miaka mitatu tu kabla ya muungano hivyo haikuwepo,nashindwa kumuelewa huyu Prof. Kwani katika historia nimejifunza na kuelewa kuwa Tanganyika ilikuwepo zaidi ya mwaka 1885 wakati wazungu walipokaa Berlin na kugawana bara la Afrika kuwa makoloni yao je Zanzibar nayo haikugawiwa?au ilikuwepo kabla ya Berlin?au kabla ya muungano? Kwa nini iendelee kuwepo wakati sisi tumevunja Tanganyika yetu?

  Je huyu Prof. tumueleweje? kwanini anapotosha watu kwa mihadhara yake hii,tena kwa macho maangavu! ashauriwe aongee ya ukweli siyo kuwapotosha watu eti kwa kuwa wamezaliwa baada ya muungano.

  Historia itamsuta pomoja na kuwa na mazuri yake yote anayoongea,hii inaamsha ari ya vijana kutaka historia ijirudie yaani kuwepo na Tanganyika kama vile ilivyo Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Somalia
   
 2. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Ni kweli hata mimi jana aliniboa sana kwa jibu lake, hata kama Tanganyika ilipotea baada ya miaka 3 haina maana kuwa aliyezaliwa 1970 au 2000 asihoji ilipotepoteaje? Ni lazima tuhoji. Kama prof. alighafilika sawa lakini kama ametumwa tunamtahadharisha kuwa vijana wa leo sio wa jana, kila kitu lazima kiwe na maelezo yakinifu.

  Hata hivyo hiyo mihadhara ya Prof. Shivji nimekuwa naifuatilia na sijaona umuhimu wake, hayo ilitakiwa ayafundishe kwa wanafunzi wake darasani wananchi kazi yetu ni kutoa maoni tu, halafu kazi ya kupangilia hayo maoni ni ya wataalamu, kwa hiyo prof asitake kutuchanganya.

  Muungano ni lazima tuuhoji na tuulize Tanganyika yetu ilikwenda wapi na nani aliipoteza na kwa malengo yepi. Lazima tuambiwe, tutang'ang'ana mpaka kieleweke.
   
 3. L

  Lindongo Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  NIMEANGALIA KIPINDI CHA MHADHARA WA KATIBA KINACHORUSHWA NA ITV. KWENYE KIPINDI HICHO Prof. ANAELEZEA NAMNA KATIBA INAVYOUNDWA NA MISINGI MIKUU YA UUNDAJI WA KATIBA. NIMESHANGAZWA KUSHINDWA KUJIBU SWALI ALILOULIZWA NI KWA NAMANA GANI DOLA YA TANGANYIKA ILIKUFA NA DOLA YA ZANZIBAR KUBAKI.

  MUULIZA SWALI ALIELEZA "MZANZIBAR ANAJITAMBULISHA KUWA NI MZANZIBAR WAKATI MTANGANYIKA ANAJITAMBULIUSHA KUWA NI MTANZANIA BARA"

  BADALA YA KUJIBU SWALI HILO ALICHOFANYA NI KUPIGA POROJO KUWA MUULIZA SWALI AMEZALIWA BAADA YA MUUNGANO NA KUWA TANGANYIKA ILIDUMU KWA MIAKA 3 TU, HIVYO HAKUNA HAJA YA KUULIZA TANGANYIKA KWANI ILITOKANA NA UKOLONI NA MUULIZA SWALI AMEZALIWA AKIWA MTANZANIA.

  IMETIA HOFU KWA KUSHINDWA KUJIBU SWALI LA MSINGI, KWANI MARA ZOTE INASEMWA MUUNGANO UMETOKANA NA NCHI ZA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR.IKUMBUKWE KUWA SHERERE YA UHURU YA TAREHE 9 DESEMBA INASEMWA NI UHURU WA TANZANIA BARA NA SIO UHURU WA TANGANYIKA.

  HIVI KWANINI HAISEMWI NI UHURU WA TANGANYIKA? KUNA SIRI GANI KWA JINA NA NCHI YA TANGANYIKA?
   
 4. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Nadhani alimaanisha Tanganyika huru iliishi miaka isiozidi mitatu tu.. Kabla ya hapo tulikuwa na Tanganyika ambayo haikuwa huru..
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Labda kwanza tuulizane- Tanzania Bara imezaliwa lini?
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,325
  Likes Received: 19,493
  Trophy Points: 280
  hilo swali tuulizane watanganyika
   
 7. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Mimi ni mtanganyika bana...na rais wangu ni Dr wa ukweli Slaa.Over
   
 8. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tahadharini sana na Shivji yeye na wadosi wa Zanzibar wanajuana, mimi sipo.
   
 9. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mbona ile ya wakoloni wekundu ilikuwa huru zaidi ya hii ya wakoloni weusi? Ililikuwepo?
   
 10. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chonde chonde huyu mdosi asiaminiwe, anajua sana na wenzake walioko nyuma ya Uamsho.
   
 11. m

  mamajack JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  he said tanganyika ilikuwepo for only four years them muungano ukatia nanga bana,wewe acha kumwonea mzee wa watu.
   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Na Zanzibar nayo ilikuwepo kwa miezi tisa tu Muungano ukaikumba.
   
 13. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  [​IMG] Class room in German East Africa
  German East Africa (German: Deutsch-Ostafrika) was a German colony in East Africa, which included what are now Burundi, Rwanda and Tanganyika (the mainland part of present Tanzania). Its area was 994,996 km[SUP]2[/SUP] (384,170 sq mi),
   
 14. m

  mharakati JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  he he he Dr wa kanuni za kikatoliki ni DR wa ukweli...kwa kejeli tanzania tuna talent
   
 15. k

  kula kulala Member

  #15
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi nilitaka kujuwa ikiwa baba amekufa ndio tusiuliza mali alizoziwacha au alikuwa vipi mpaka akafa wacheni kutubambikiza mambo yaliokuwa sio yetu shivji na ccm wenzio
   
 16. k

  kumchaya Member

  #16
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mwalimu nyerere alishawahi kuulizwa kuhusu Tanganyika nakusema hata yeye hajui ilitokea wapi,akimanisha wakati wadhungu wakigawa bara letu ndio waliitupatuia jina hilo,hata hivyo kama unapenda nchi yako irudi katika uasilia wake basi wazee wanatuhadithia nchii hii ilikuwa ikiitwa MRIMA,cha msingi kama nilimuelewa prof shivji anatutaka tujikite zaidi katika mambo ya msingi kuliko kuanza kufikiria upuuzi wa jina la nchi maana hilo jina halikupi mustakabali wa maisha yako,na alieleza nyakati kama huzi ni nadra kuzipata hivyo tutumie vizuri kwa ustawi wa taifa letu.
  sio kila jambo kulitizama kiitikadi zaidi,kama zanzibar tatizo lao ni utaifa wao,sie tunamambo mengi zaidi ya kutafakari zaidi ya huo utaifa wa tanzania au tanganyika.nampa pongezi kubwa sana prof kwa uchambuzi wake hasa katika suala muhimu na nyeti la ardhi.
   
 17. l

  lost account Member

  #17
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni dhahiri wasomi washaingiwa na uwoga kuongelea masuala ya muungano, Prof Shivji alishindwa jibu maswali mengi kifasaha ambayo yalilenga yeye kutoa msimamo wake, same applies to Dr Lwaitama, yeye alipoulizwa kwa nini Raisi kakataza tusiongelee muungano wetu kuelekea katiba mpya, akashindwa jibu!
   
 18. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  1st Century B.C. Cushites from Ethiopia settle in Tanganyika. 2nd Century A.D. Agriculturists from Cameroun and Nigeria settle in Tanganyika and Iron Age Civilization develop. 7th Century A.D. Arabian merchants settle on the island of Zanzibar off the Tangayikan coast. 10th Century A.D. Traders from China and India visit Tanganyika in boats on a regular basis. 10th Century A.D. About this time the fabled emigration of Fijians from Tanaganyika takes place. 12th Century A.D. Swahili Civilization established in Zanzibar and Coastal Area of Mainland Tanganyika. 15th Century A.D. Organized Kingdoms and Chiefdoms established in various regions of Tanganyika. 1866-1873 European adventure trips to Tanganyika including the visit of Dr.David Livingstone. 1880 German Colonization of Tanganyika. 1885 Partition of Africa; German Rule of Tanganyika recognized by European powers. 1885-1905 Wars of Resistance by African tribes against the Germans. 1890 British Rule in Zanzibar recognized by major powers. 1914-1918 British Allies over-run Tanganyika taking the country from the Germans. 1919 League of Nations decide to place Tanganyika under British Rule. 1946 Tanganyika becomes UN Trust Territory under British Administration. 1961 Independence of Tanganyika. 1962 Tanganyika becomes a Republic.

  Now Black nano colonialism that will end 2015.
   
 19. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Mkuu Communist naamini wazee wetu waliogombea na kupata uhuru walikuwa na mawazo ya watoto na wajukuu wao na vizazi vinavyofuatia wawe na maisha mazuri ambayo wamejichagulia wenyewe.. Huko walipo hawaamini kama hii ndo Tanganyika yao walioipigania..
   
 20. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #20
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Naanza kujiuliza Prof Shivji ni wa wapi kiuzawa? Bara au ZNZ? Kama Bara wapi asili yake katika mikoa ya bara ukiachana na India?
   
Loading...