alinanuswe
New Member
- Nov 13, 2011
- 2
- 0
Nchi yetu ilipoingia katika mfumo wa vyam vingi haikuandaa mazingira mapya ya siasa nadio chanzo kikubwa cha migogoro. Chama Tawala hakikuruhusu mfumo huo kwa moyo mweupe. Katiba ya nchi iliendelea kuwa na vikwazo vingi kwa watu kushiriki kikamilifu katika siasa na badala yake kila chama kikawa na genge la watu wachache wanaoonekana kuwa na hati miliki ya chama.Iwapo utatofautiana tu nao unatupwa nje ya chama. Katiba za vyama hivi haziko sawa. Mfano mzuri ni David Kafurila wa NCCR-MAGEUZI na Ahamad Rashid wa CUF wanapohoji wanatishiwa kuvuliwa uanachama. mimi napendekeza katiba za vyama hivi viangaliwe upya.Asante!