Migahawa kukosa "Menu List" ni kero na si weledi

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
892
1,226
Habari wanaJf wenzangu,

Hili suala la migahawa mingi kukosa menu list kwangu mimi ni kero inayoipunguzia thamani migahawa hiyo.

Unaweza kukuta mtu unaenda mgahawani, muhudumu anakusimamia mbele akikutolea macho akisubiri ubuni list ya vyakula yeye kazi yake kujibu " kipo, kipo.." Bei yenyewe mpaka uulize kimoja kimoja, utaskia "ugali nyama shilingi ngapi? Na wali mbogamboga je?"

Hii kwangu naona ni kero, muda mwingine huwa nakula hata msosi ambao sijapanga; yaani majibu nayapata hapohapo mdomoni kwa mhudumu aliyenisimamia akitikisa miguu, ishara ya kuwa sema haraka kuna wengine wananisubiri.

Hili pia linafanya mteja unakuwa uncomfortable yaani unaingia sehemu hujui bei ya wali wala njegere mpaka umuulize mteja anayeonekana mzoefu pembeni yako, (mteja mzoefu yaani ni yule mteja anayeongea sana kwa sauti na wahudumu na meneja na kuchekesha chekesha) utasikia unamuuliza aise "hapa wanauzaje wali kuku?" Anakujibu kwa sauti buku 3 tu alafu bila ridhaa yako anamuita mhudumu, "naniii..mrembo" kama mhudumu ni wa kike, "mletee wali sijui na nini muulize embu!"

Sehemu kama hizo wahuni huogopa hata kwenda na demu mpya wasije kuaibika ndiyo maana huwapeleka kwa wauza chipsi ambayo bei zake zinajulikana worlwide yaani chipsi kanda ya Dar, Pwani, Kaskazini inajulikana kavu 1500, yai 2500, kuku 3500.

Huko kusini ni buku kwa buku jero, viazi si vinatoka huko bana. Maeneo kama haya hakuna menu, bei tunazijua.

Mimi mwenyewe nikiona mgahawa siuelewi na nina buku 2 mkononi nakula chipsi kavu na Coca nasepa; naogopa nsije kula bila kujua bei nikaacha cheni na kimeo kwa meneja kuzuia deni.

Kama kuna mtu anamiliki mgahawa Menu List anapaswa aiandike nje kwenye ubao na iwe ndani kwenye karatasi, tena siyo chakavu yenye bei za zamani (iwe updated kila mara).

Siyo menu yenye lamination ina ukungu, toka imetengenezwa kwenye debut mpaka watu wengine washastaafu na ina bei za kipindi cha Mkapa hadi leo.

Wenzetu hoteli kubwa Menu List mpaka ina picha za vyakula na bei, bonus, addition, mapunguzo ya bei, vyakula vya siku maalumu, vyakula vya wenye mahitaji maalumu - yaani unaweza kuletewa menu kama kitabu na unapewa muda usome na uchague siyo kama kwingine, muhudumu anakusimamia mbele na macho kodo mpaka umwambie nenda kwanza, hapana hawa wapo professional.

Migahawa ya online inawezaje wewwe ushindwe bwana hata kuandika kwa chaki unashindwa?

Ukifanya hivyo utanishukuru baadaye.

Admin ipandishe kwenye page zenu za social network tuondoe hii kero.

WanaJF, nisaidie kero nyingine za migahawa yetu hapo chini tuzijadili, yangu ni hiyo.

Nafungua mjadala, sakafu ni yenu, karibuni.

Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama anataka kujaribu new taste je?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo aseme chakula gani anachotaka kujaribu.

Sasa mfano ndo amepewa menu list na katika hiyo list ni chakula kimoja tu ambacho anakijua na hataki kula hicho kwasababu amekizoea, utajilazimisha kuchagua hata kama hukijui?

Hapo ndo watu hujikuta wamekula nyoka kwa kukutaka kila kitu uonje
 
Wewe jamaa inaonesha huna hata Exposure na masuala ya vyakula na migahawa kuna maelfu ya aina ya chakula kwahiyo hata uhifdhi aina 10000 za chakula bado kuna vyengine.

Chakula ni starehe kama starehe nyingine inatakiwa upate MENU uanze kuchagua nini u-test siku hiyo kwakuangalia jina, mchanganyiko na picha sio unaenda mgahawani MENU utoe wewe utaishia kutaja nipe ugari maharage tu.

Ngumu sana kuelewa kwa mtu aliuezoea kula basic food ili ashibe aendelee kuishi, ila FOODIE kama Ontario ataelewa nini mtoa mada anamaanisha.

Ujui chochote kuhusu ulimwengu wa chakula na hata Menu inaonesha ujawai kushika...kwenywe Menu wanaweka wame mix nini na nini kama nyoka wataweka tu snake...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwamba unapo plan ukale mgahawani unakua huja plan aina gani ya chakula utakayokula ukifika mpaka uhitaji menu?
Wewe jamaa inaonesha huna hata Exposure na masuala ya vyakula na migahawa kuna maelfu ya aina ya chakula kwahiyo hata uhifdhi aina 10000 za chakula bado kuna vyengine.

Chakula ni starehe kama starehe nyingine inatakiwa upate MENU uanze kuchagua nini u-test siku hiyo kwakuangalia jina, mchanganyiko na picha sio unaenda mgahawani MENU utoe wewe utaishia kutaja nipe ugari maharage tu.

Ngumu sana kuelewa kwa mtu aliuezoea kula basic food ili ashibe aendelee kuishi, ila FOODIE kama Ontario ataelewa nini mtoa mada anamaanisha.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe jamaa inaonesha huna hata Exposure na masuala ya vyakula na migahawa kuna maelfu ya aina ya chakula kwahiyo hata uhifdhi aina 10000 za chakula bado kuna vyengine.

Chakula ni starehe kama starehe nyingine inatakiwa upate MENU uanze kuchagua nini u-test siku hiyo kwakuangalia jina, mchanganyiko na picha sio unaenda mgahawani MENU utoe wewe utaishia kutaja nipe ugari maharage tu.

Ngumu sana kuelewa kwa mtu aliuezoea kula basic food ili ashibe aendelee kuishi, ila FOODIE kama Ontario ataelewa nini mtoa mada anamaanisha.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa kama ndo hivo kwanini usiende hyatt kwenye menu list za uhakika

Yani katika buku jero yako hiyo hiyo unataka mabanda umiza nayo yawe na menu list, unataka kufanya ela yako iwe ngumu kulika?
 
Back
Top Bottom