Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
Siku ya tarehe 02/01/2017 mifupa ya bunadamu imekutwa na kwenye mfuko wa sandarus Vingunguti Dar es salaam. Kijana ambaye alikuwa anaokota chupa za maji katika jalala ndiye aliyeona mfuko huo na kuufungua kwa kudhani atakutana na machupa lakini ikawa tafauti baada ya kukuta mifupa ya binadamu mti mzima.
Pamoja na kwamba mwili ulibaki mifupa lakini, mwili huo umekutwa ukiwa na nguo zinazo ashiria marehemu ni mwanaume. Alivaa suruali ya kitambaa nyeusi, shati leupe lina mistari ya pundamilia meusi, na shati kifuani lilikuwa limejaa damu. Kwa jinsi nguo zilivyo inaonekana huyo mtu hakufa muda mrefu sana.
Taarifa ilitolewa polisi na wakauchukua mwili na kuendelea na taratibu zao, lakini nina shaka huenda jambo hili halijaangaziwa kabisa na vyombo vya habari, na huenda jambo hili pia linafichwafichwa!
Wakati haya yakitokea huko Vingunguti Sprenko, bado kama taifa tuko na wasiwasi juu ya miili iliyookotwa katika mifuko ya sandarusi huko Ruvu, lakini kubwa hata sasa hatujui alipo msaidizi wa karibu wa mwenyekiti wa CHADEMA, Bw Ben Saanane.
CHANZO. MKAZI WA ENEO LA VINGUNGUTI.