M๐—ถ๐—ณ๐˜‚๐—บ๐—ผ ๐˜†๐—ฎ ๐—บ๐—ถ๐˜๐—ฎ๐—ป๐—ฑ๐—ฎ๐—ผ๐—ป๐—ถ ๐—ง๐—ฎ๐—ป๐˜‡๐—ฎ๐—ป๐—ถ๐—ฎ ๐—ถ๐—ธ๐—ผ ๐˜€๐—ฎ๐—น๐—ฎ๐—บ๐—ฎ ๐—ธ๐—ฎ๐—ฏ๐—ถ๐˜€๐—ฎ!!

M๐—ถ๐—ณ๐˜‚๐—บ๐—ผ ๐˜†๐—ฎ ๐—บ๐—ถ๐˜๐—ฎ๐—ป๐—ฑ๐—ฎ๐—ผ๐—ป๐—ถ ๐—ง๐—ฎ๐—ป๐˜‡๐—ฎ๐—ป๐—ถ๐—ฎ ๐—ถ๐—ธ๐—ผ ๐˜€๐—ฎ๐—น๐—ฎ๐—บ๐—ฎ ๐—ธ๐—ฎ๐—ฏ๐—ถ๐˜€๐—ฎ!!

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,221
Reaction score
2,425
Serikali Tanzania _20250521_210628_0000.png


Baada ya vuguvugu la mitandao mbalimbali ya kijamii kuvambiwa na wadukuzi (wahalifu wa mitandao), ambao waliweza kudukua mitandao ya kijamii ya taasisi za serikali na ambazo zisizo za kiserikali.

Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na msemaji mkuu Wa Serikali Gerson Msigwa amesema Anga la Mtandao la Tanzania (cyberspace) lipo salama na kwamba kilichojitokeza jana ni kuingiliwa kwa akaunti binafsi chache za Watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Msigwa amesema akaunti hizo zinaendeshwa na Watu wenye akaunti zao au Watu ambao wanasimamia akaunti za taasisi, na ambao ndio wanaochapisha maudhui mbalimbali.

"Serikali inawakumbusha wote wanaoendesha akaunti za mitandao za Serikali kuimarisha uangalizi wa akaunti hizo na kuzingatia miongozo yote ya kuepusha wahalifu kuingilia na kuchapisha maudhui yasiyofaa".
 
Back
Top Bottom