Mifumo Nje ya Mifumo (MNM): Ya Nini, Nani, Kwanini na ya Nani...

Hapana, ninachoona hapa ni dalili kwamba Mwanakijiji amechoka kumbeba Magufuli. Nadhani taratibu anarudi kule alikokuwa mwanzo. lakini uso umeumbwa na aibu. tusubiri tutaweza kuhukumu vizuri zaidi. Magufuli ni gunia la misumari. HALIBEBEKI.
 
Sasa ukisoma yaliyotokea Marekani na jinsi yalivyoshugulikiwa, utaona kuna tofauti kubwa na jinsi the so called MNM ilivyofanya kazi kwa Saudi Arabia, Israel na Tanzania, ambazo zote ni nchi za kidhalimu!
Pole sana TL lakini angalau hapa unakubaliana na MMM,Kwamba haya mambo yapo na yanatendeka.
 
Pole sana TL lakini angalau hapa unakubaliana na MMM,Kwamba haya mambo yapo na yanatendeka.
Nakubaliana na MM kwamba haya mambo yapo; wapi hasa? Kama Tanzania kwani kuna asiyejua udhalimu unaoendelea wapi?! Kwenye hiyo mifano ni mfano upi unafanana na Tanzania kama sio Saudi Arabia peke yake ambayo nalo ni taifa la madhalimu tu!
 
Hapana, ninachoona hapa ni dalili kwamba Mwanakijiji amechoka kumbeba Magufuli. Nadhani taratibu anarudi kule alikokuwa mwanzo. lakini uso umeumbwa na aibu. tusubiri tutaweza kuhukumu vizuri zaidi. Magufuli ni gunia la misumari. HALIBEBEKI.
Endelea kufuatilia posts zake kuanza sasa kama hujaamini ninachokisema! Yaani hapa anachofanya ni kuuma na kupulizia, and that's it! Ikiwa hakumchoka Magu baada ya TL kupigwa risasi, Ben Saanane na Azory kupotezwa, ndo aje kuchoshwa sasa kisa Musiba kawasemangana akina Kinana?! Na fuatilia tu posts zake za nyuma, matukio yote ya hovyo hovyo alikuwa anayahalalisha kwa kusema "hii si mara ya kwanza kwa Tanzania kutokea matukio kama hayo" kama ambavyo anavyojaribu kutuambia kwamba umafia kama huu aliouita MNM unafanyika duniani kote, iwe nchi za kidikteta au za kidemokrasia lakini ameshindwa kutoa mfano wa hizo nchi za kidemokrasia zinazopoteza raia wake!
 
Hatimaye jf ya 2015
imerudi.Hongrra kwa hoja mujarabu na wachangiaji mujarabu.Hapa Vilaza lazima wakae pembeni.Naamini uzi utapata wachangiaji wengi sana
 
Hizi ndefu hizi zinatia shida sana ku'maintain concentration' Lakini ukishajua 'theme' ya mwelekeo ni rahisi kujua zinakoelekea.

'Common denominator' ya yote hayo - uwe mfumo 'rasmi' au wa 'pembeni' ni lazima pawepo na kiongozi mkuu kabisa anayeruhusu mifumo yote hiyo iendelee kwa pamoja.

Hata huo mfumo usiokuwa rasmi, pakianza kujitokeza alama za u'rogue', kama mhusika mkuu au kikundi kidogo kinachomhusisha mkuu hakikubali au kunyamazia u'rogue' huo, hapawezi kamwe kuendelea kuwepo vitendo vya aina hiyo.

Mfumo usiokuwa rasmi, kwanza unamnufaisha nani? Ni nani anataka aina ya mambo yanayotendeka huko yawepo?
Kiongozi mkuu au kikundi kinachomhusisha yeye kama vitendo vyao na maneno yao yanaonyesha bila ya wasiwasi wowote kuwa hawawezi kuvumilia mambo yanayotendeka huko, hao ma'rogue' hawawezi kuendelea kuwa na ujasiri wa kufanya mambo ambayo yanatia hofu wananchi.

Kama kwa mfano watu wanatekwa, na wengine wanapotezwa au kupigwa risasi na watu walioko huko kwenye 'mfumo usiokuwa rasmi' halafu pasiwepo na uchunguzi wowote au hata kwa mkuu au kikundi chake maalum wasionyeshe kwa matamko na vitendo vya kuchukizwa na hayo na kufanya juhudi zote zionekane zinafanywa kwa dhati kukomesha vitendo hivyo, kwa nini watu wasiamini kwamba hawa ma'rogue' wana baraka zote za mfumo rasmi kufanya wanayofanya.

Inapoanza kuwa hivyo, mipaka ya 'rasmi' na 'rogue' inaishia wapi?

Hata kama mifumo ya aina hii ipo katika nchi zote duniani, tofauti iliyopo kati ya nchi na nchi ni kwa vipi 'mfumo rasmi' ulivyo imara na kiongozi/kundi alilomo wanavyoruhusu na kuvumilia yatokanayo na 'mfumo usio rasmi'.

Panapotokea 'mfumo usiokuwa rasmi kuonekana kuelemea ule uliorasmi, hapo ndipo panakuwepo na tatizo kubwa. Na yote haya ni kiasi cha 'tolerance' na jinsi gani mkuu au/na kundi lake wanavyotaka makundi haya mawili yaonekane yanavyofanya kazi.
 
Huyu ndie Mwanakijiji tuliyekuwa tunamfahamu,
Eeeenh, pole sana mkuu wangu kama unashindwa kujua maana ya mada yake. Juhudi hizi ndizo zinazofanya watu waelewe kiini cha msukumo wake ni nini. Hapa hakuna 'conviction' kama iliyokuwepo enzi zile. Hapa kuna msukumo maalum nyuma yake. Uwasilishaji hauwezi kuwa tofauti.

Kwa hiyo kama unapongeza 'staili ya uandishi', hapo ninakubaliana nawe.
 
Naona watu wanataka kuhalalisha ushetani wao, kwa vile Nyerere aliua kwa hiyo si ajab na jiwe naye kuua watu,
 
siku hizi kidogo kidogo umeanza kunishawishi tena tofauti na siku za nyuma baada ya jiwe kuingia madarakani.

i hope in few month time, yule Mwanakijiji wa enzi zile atakuwa full activated.
 
You have a point: Edward Sokoine!
 
Hapana, ninachoona hapa ni dalili kwamba Mwanakijiji amechoka kumbeba Magufuli. Nadhani taratibu anarudi kule alikokuwa mwanzo. lakini uso umeumbwa na aibu. tusubiri tutaweza kuhukumu vizuri zaidi. Magufuli ni gunia la misumari. HALIBEBEKI.

Mwanampotevu arudi tu tuwashe moto wa fikra
Anayelaumu na kukosoa ni bora kuliko anayesifu
Anayesifu humlevya mtu amsifuye
Bali akosoaye humwamsha alalaye
 

Mzee MMM, nimekusoma vizuri sana na nimependa uchambuzi wako....

Lakini kusema hadi wiki ijayo tena ndipo package ikamilike unatukata stimu.....

Kwanini ustupie mzigo mzima mzima? Acha basi kubana kwa kutuletea kwa "series" kana kwamba hii ni Tamithilia za Kaole....!!

Najua unayo hii kitu kwenye flash yako. Wewe achia package yote, watu wasome na kisha watoe maoni yao kamili.....!!
 
MNM Kwa lugha nyepesi ni magenge ya uhalifu kama yalivyo magenge ya mafia au dawa za kulevya, tofauti ipo kwamba katika nchi za magharibi walau magenge haya hutumika kwa kwa ajili kufanya kazi zao chafu katika mataifa ya kigeni kwa ajili ya maslahi ya nchi zao,magenge ya aina hiyo katika nchi za kiimla za Afrika,Asia,Uarubuni na Latin America hutumika kufanya uhalifu na ukatili wa hali ya juu kwa raia wa nchi zao wenyewe ambao ni wakosoaji wa serikali hizo za kiimla.
 
Mzee karibu tena, naona umeamua kurudi kijijini, tulikukosa,
 
kwa vile Nyerere aliua kwa hiyo si ajab na jiwe naye kuua watu,

Heee, hii sikuiona mkuu.
Sikusoma tangazo lake refu lote lile. Kuna mahali ameandika hivyo, kwamba kwa: 'kuwa Mwalimu Nyerere alitumia 'Mfumo Nje ya Mfumo'' na kutolea mfano wake wa kuua?

Kuna mifano iliyojitokeza iliyokaribiana na aina ya mfumo huo. Lakini tunajua baadhi ya matokeo ya matukio kama hayo yalipojitokeza. Mzee Mwinyi ni ushahidi tosha wa mfano kama huo ilipobidi ajiuzuru.

Mwalimu Nyerere hakulea tabia za namna hiyo hata kidogo. Ndio maana watu walielewa uzalendo mkubwa aliokuwa nao kwa nchi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…