Mifumo Nje ya Mifumo (MNM): Ya Nini, Nani, Kwanini na ya Nani...

Ka- inzi kameamka. "Wanaharakati wataendelea kusema hizi ni njama-matope. Yaani wao wanacheza na matope lakini ya kwao hayachafui, yaani kama tope la ugali, haliachi rangi kihivyo' lakini kumbuka tope lelote hukauka na kujionyesha na Tope ni Tope tu
 
View attachment 1157012
Marehemu Jamal Khashoggi​
Na. M. M. Mwanakijiji

Tarehe 2 Oktoba 2018 mwandishi wa habari na mwanablogu kutoka Saudia Bw. Jamal Khashoggi alienda kwenye ubalozi wa Saudia huko Istanbul, Uturuki akiwa na lengo la kufuatilia nyaraka ambazo zingemwezesha kufunga ndoa na mchumba wake. Mchumba wake hakuingia kule Ubalozi bali alibaki kwenye mgahawa Fulani karibu akimsubiria na walikubaliana kuwa endapo hatotoka nje basi dada yule awataarifu watu kadhaa wa kuaminika. Na kweli, muda wa kazi ulikuwa unaishia saa 9:30 jioni lakini ilipofika saa 10 Ubalozi ukafungwa na Khashoggi hakuonekana kutoka. Mchumba akawasiliana na watu wao wa karibu na mara moja Rais wa Uturuki Erdogan akaagiza uchunguzi wa haraka kuanza mara moja.

Haikuchukua muda ushahidi wa awali ulionesha kuwa Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi ule. Uturuki ulidai kuwa kikosi cha wauaji (death squad) kilikuwa kimeingia masaa machache kabla na ndege binafsi. Kikosi hicho kilikuwa cha maafisa wa usalama ambao walikuwa na kazi moja tu kummaliza Bw. Khashoggi ambaye alijulikana kama mkosoaji mkubwa wa serikali ya Saudia ambayo inaongozwa (kwa maana zote) na mwana wa mfalme Bw. Mohammed Bin Salman. Serikali ya Saudia ilikanusha vikali mwanzoni, na ilidai kuwa Khashoggi alitoka ubalozini na kuwa kuihusisha na uuaji ilikuwa ni uchokozi tu wa Uturuki.

Hata hivyo, uzito wa ushahidi kutoka vyanzo mbalimbali ulilazimisha hatimaye Saudia kukiri kuwa kweli Khashoggi aliuawa pale ubalozini na kuwa maafisa wake wa usalama waliohusika na tukio hilo walifanya hivyo bila kutumwa na mtu yeyote, na kuwa 11 kati ya wale 15 ambao walipanga na kutekeleza tukio hilo watakabiliwa na adhabu ya kifo. Mkuu wa kikosi cha Usalama kilichotekeleza hilo alifukuzwa pamoja na msaidizi wake. Mwisho wa siku, licha ya kauli kali kutoka nchi mbalimbali na licha ya ushahidi mzito wa mauaji ya mwanahabari huyo serikali ya Saudia imeng’aka na kuwa Mwana wa Mfalme hausiki, na wale waliohusika wanaweza kunyongwa peke yao.

Mfumo Nje ya Mfumo ni Nini?

Katika utendaji wa serikali karibu zote duniani – ziwe za kidemokrasia au kidikteta, zilizoendelea au zinazotaka kuendelea kuna mifumo miwili mikubwa ya kiusalama. Upo mfumo rasmi wa vyombo vya usalama ambavyo huundwa na majeshi, polisi, taasisi za inteligensia na hata za binafsi ambazo zinaongozwa na kanuni, taratibu na sheria zinazojulikana. Vyombo hivi vya “mfumo rasmi” vina uongozi unaojulikana na unaoweza kuwajibishwa. Kama ni jeshi una mtu wa cheo cha chini kabisa (Private) hadi mwenye cheo cha juu kabisa (General). Mnyororo wake wa amri (chain of command) unaeleweka katika ngazi zote.

Lakini pia kuna mfumo mwingine wa usalama na ulinzi; mfumo ambao unafanya kazi nje ya sheria, taratibu na amri zinazoelweka. Ni mfumo ambao hauna uongozi unaojulikana (wenyewe wanajuana) na unafanya kazi kwa maelekezo na maagizo ambayo hayaachi alama za maandishi (no paper trail) na kwa kadiri inavyowezekana unafanya yale yote ambayo mifumo na watendaji rasmi hawawezi kufanya. Ni mfumo wa usalama na ulinzi ambao unafanya mambo yote ambayo yakijulikana ni rahisi kuyaruka na kuwaruka wahusika wote.

Wahusika ni Watu Ndani na Nje ya Serikali

Mfumo Nje ya Mfumo hufanya kazi kwa kuhusisha watu ndani na nje ya serikali. Unahusisha wafanyabiashara, wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za umma na hata binafsi. Lengo lake kubwa nikilirudia tena ni kufanya mambo yale yote ambayo yakifanywa na mtu mwingine ni ya uhalifu na kwamba endapo yatakuja kujulikana basi wahusika wa mfumo rasmi wanaweza kuyaruka maili nyingi za mbali.

Mifano Mikubwa ya MNM

Kama nilivyosema hapo juu MNM ipo katika nchi zote bila kujali kama ni nchi zilizoendelea au la, zilizo na demokrasia au hapana. Kuna mifano michache ya matukio makubwa ambayo yamewahi kutokea kama nilivyotolea mfano wa Khashoggi. Nitaje mifano michache tu hapa mikubwa:

Kashfa ya Watergate – Marekani

Kati ya mwaka 1972 na 1974 huko Marekani kulitokea kashfa kubwa ambayo iliishia kwa kujiuzulu kwa Rais wa nchi hiyo Bw. Richard Nixon. Kwa ufupi kabisa kashfa hii ilimhusisha Rais Nixon na chama chake cha Republican ambapo iligundulika kuwa Rais alikuwa anatumia njia za MNM kuwapeleleza wapinzani wake. Juni 17 mwaka 1972 vibaka watano walikamatwa wakijaribu kupekua ofisi za chama cha Democrat kwenye jingo la Watergate (ndio jina la kashfa). Ilikuwa jambo dogo lakini baada ya kufuatilia na waandishi kuchunguza mwisho wa siku ikaonekana mpango mzima ulisukwa na kuihusisha Ikulu. Maafisa 69 wa Serikali ya Nixon walikamatwa na kushtakiwa; 48 kati yao walikutwa na hatia na kati yao wapo waliopata vifungo jela, kupigwa faini na wengi kupoteza kazi zao. Nixon mwenyewe alikuwa aondolewe kwa mashtaka ya kibunge (impeachment) lakini akaamua kujiuzulu. Hata hivyo, mrithi wake Gerald Ford alimsamehe. MNM ndio iliyomuangusha Rais Richard Nixon.

Kashfa ya Iran-Contra - Marekani

View attachment 1157016 ni kashfa ya mwanzoni mwa miaka ya themanini huko huko Marekani. Maafisa wa Marekani walikula njama kuiuzia Iran silaha licha ya kuwepo kwa zuio la kuuza silaha kwa nchi hiyo. Japo mwanzoni Serikali ya Rais Reagan ilijaribu kuelezea jambo hilo kuwa ililazima ili kuwafungua wafungwa wa Kimareni huko Iran uchunguzi ulikuja kuonesha kuwa kulikuwa na zaidi ya hilo. Kanali Oliver North (kushoto) wa Baraza la Usalama alitumia baadhi ya fedha za mauzo kwenda kuwapatia waasi wa huko Nicaragua. Uchunguzi wa Bunge ulipofanyika maafisa kadhaa wa serikali ya Reagan walijikuta wanapoteza kazi zao akiwemo Waziri wa Ulinzi na maafisa kadhaa walishtakiwa na kukutwa na hatia mahakamani, akiwemo Kanali North. Hata hivyo, Rais George H. W. Bush aliwasamehe hao wote na kufuta hatia zao.

Operesheni “Ghadhabu ya Mungu” – Israel

Baada ya wanariadha wake 11 kuuawa na wapalestina huko Munich, Ujerumani mwaka 1972. Tukio hilo lilikuja kujulikana kama “Septemba Nyeusi”. Israeli iliapa kulipiza kisasi na kushughulikia wale wote waliohusika kufanikisha hilo kwa hali na mali. Na miezi michache baadaye vikosi maalum vya MNM vya Israeli vilianza kuwaaua (assassinations) watu mbalimbali waliohusika. Zilitumika kila aina ya mbinu na haikujali watu hao walikuwa nchi gani. Hata hivyo, mpango ulivurugika baada ya MNM kumuua mtu asiye na hatia (walimchanganya) huko Norway. Maafisa watano wa Israeli walikamatwa na ndio siri nyingi zilizidi kufichuka kuhusu “Ghadhabu ya Mungu”. Serikali ya Israeli ikasitisha operesheni zake hizo mwaka 1973. Hata hivyo, ikafufuliwa kwa muda mwaka 1979 kumshughulikia yule waliyemkosa kule Norway; walifanikiwa kumuua kwa bomu la gari. Israeli bado imeendelea kutumia mbinu za MNM kwa kushirikisha hata vikosi rasmi kuwashughulikia wale wanaoonekana ni tishio kwa Israeli mahali popote duniani.

MNM Haiwezi Kuzuiliwa; Inaweza Kufichuliwa Tu

Kimsingi ni vigumu sana kuzuia utendaji wa MNM. Hata hivyo, mifumo hii nje ya mifumo inaweza kufichuliwa tu kwa sababu kama nilivyosema hapo mwanzo mara nyingi inajihusisha na vitendo ambavyo kama vingefanywa na mtu mwingine au taasisi nyingine vingeitwa ni vya kihalifu na endapo wahusika wakikamatwa wanaweza kushtakiwa kwa uhalifu na serikali ikawaruka. Ikumbukwe tena kuwa hakuna nchi ambayo haina mifumo hii.

Katika Afrika mifumo hii ilitumiwa sana wakati wa utawala wa Makaburu kule Afrika ya Kusini lakini pia ilitumiwa na nchi zilizokuwa katika Mstari wa Mbele zikiongozwa na Tanzania. Tanzania ilikuwa imetengeneza mtandao mpana sana wa majasusi ambao waliwezesha kupitisha silaha kwenda Afrika ya Kusini na kuwapitisha wapigania uhuru hadi Tanzania ambako walipatiwa hifadhi. Mifumo hii iliendelea kufanya kazi kwa namna nyingi hata baada ya kuanguka kwa utawala wa makaburu.

Kwanini Mifumo Hii Inakuwepo?

Unaweza kuona kuwa mifumo hii ya nje ya mifumo ipo mara nyingi kwa sababu kubwa mbili na zinahusiana. Moja ni kulinda maslahi mapana ya nchi kutoka kwa matishio ambayo hayawezi kushughulikiwa kwa njia halali. Lakini la pili, mifumo hii ipo pia kulinda tawala, viongozi dhidi ya wapinzani wa kisiasa. Mfano wa Nixon hapo juu ni mmoja tu wa kuonesha jinsi gani Nixon alijaribu kutumia ofisi yake na watendaji wengine wa serikali kutimiza malengo ya kisiasa. Kurekodi wapinzani wake wa kisiasa na kuagiza vitendo ambavyo ni vya kihalifu Nixon alitumia vibaya zaidi MNM; lengo ikiwa ni kutaka kushinda uchaguzi. Hata mfano wa Khashoggi hapo juu unahusiana na hili zaidi.

Mifumo hii Haikomi Yenyewe

Mara nyingi mifumo hii inakuwa na matatizo makubwa zaidi pale ambapo inakutana na wapinzani wengi zaidi. Kwa kadiri inavyokutana na wapinzani ndivyo inavyozidi kufanya kazi yake – ya uhalifu kimsingi. Ni muhimu sana kutofautisha hapa utendaji wa vyombo halali na rasmi na hivi vya MNM. Utendaji wa MNM hauwezi kuacha - viongozi wanaoingia na wale wanaotoka hawana umiliki hasa; kila mmoja huwa na timu yake na wengine wanapewa timu na wanaona jinsi wanavyotumia. Njia pekee ya uhakika ni uwepo wa serikali ambayo haiogopi kuficha vitu, haiogopi kuhojiwa au watu kuiangalia kwa karibu.

Wakati wowote serikali inajaribu kuficha vitu, hasa kama hairuhusi vyombo vya habari kuangalia ndani kama kwa kurunzi basi ujue MNM inaanza kuwa na nguvu zaidi. Alama kubwa ya uwepo na nguvu ya MNM iko katika kutokuwepo uhuru mkubwa wa maoni, mawazo, na habari. Mara zote na sehemu zote duniani mifumo ya MNM imejulikana na kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari.

Swali kubwa ni je, kwa nchi yetu MNM imefikia kiwango gani, inaongozwa na nani na inawajibikwa hadi wapi? Je, wale wanaoitwa “wasiojulikana” ni kweli hawajulikani? Naomba kupendekeza kuwa majibu ambayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara hayajaukaribia ukweli hata kwa sentimita moja. Ukweli bado uko pembeni.

Nini Kinawakuta watu wa MNM

Wiki ijayo inshallah, nitaendelea na sehemu muhimu zaidi. Nini huwa kinawakuta wahusika walioko ndani ya MNM? Je, wanaweza kweli kujificha au kufichwa miaka yao yote? Ipo mifano ya kusikitisha na kushtusha. Je watekaji wanaweza kuwa ndio MNM; nita -activate ka-nzi KIDOGO.
Uelezee na yaliyo mkuta lissu.
 
MNM wa nchi hii ni vichekesho vitupu mbinu wanazotumia niza kishamba sana halafu hazina maana yoyote ile wala faida yoyote ile kwa nchi yeye zaidi ya Yona na kundi lake .
 
Hivi unatumia logic gani? Unaelezea mfumo nje ya mfumo lakini unatoa mifano hai inayohusisha maafisa waandamizi wa serikali akiwemo rais, sasa kuna mfumo gani nje ya mfumo hapo? Kwa mfano unasema Khashogi aliuwawa ndani ya ubalozi na maafisa wa usalama wa Saudia, sasa hapo kuna mfumo gani hapo nje ya mfumo rasmi? Kuna mfanyabiashara gani hapo?

Mifano yako yote inahusisha maofisa wa serikali lkn unauita mfumo nje ya mfumo! Kweli? Yaani serikali ya Marekani kuiuzia Iran silaha ni mfumo nje ya mfumo? Unajaribu justify mauwaji yanayofanywa na kikosi kazi ya Bashite kwa kulipa jina la mfumo nje ya mfumo!
 
Endelea kufuatilia posts zake kuanza sasa kama hujaamini ninachokisema! Yaani hapa anachofanya ni kuuma na kupulizia, and that's it! Ikiwa hakumchoka Magu baada ya TL kupigwa risasi, Ben Saanane na Azory kupotezwa, ndo aje kuchoshwa sasa kisa Musiba kawasemangana akina Kinana?! Na fuatilia tu posts zake za nyuma, matukio yote ya hovyo hovyo alikuwa anayahalalisha kwa kusema "hii si mara ya kwanza kwa Tanzania kutokea matukio kama hayo" kama ambavyo anavyojaribu kutuambia kwamba umafia kama huu aliouita MNM unafanyika duniani kote, iwe nchi za kidikteta au za kidemokrasia lakini ameshindwa kutoa mfano wa hizo nchi za kidemokrasia zinazopoteza raia wake!
Inawezekana uko sahihi Mkuu, ila ushauri wako kwamba tuendelee kumfuatilia, ndio suluhisho.
 
Sasa nani anawapa amri kama sio yule yule anaetoa amri kwenye majeshi halali?
 
Back
Top Bottom