leveroi
JF-Expert Member
- Sep 23, 2016
- 374
- 321
Zile zilikuwa kauli za kisiasa tu na hazikuwa na uhalisia wowote, pamoja na wale viongozi wa vyama vya wafanyakazi kushangilia kama mazuzu. Hakuna hata siku moja utasikia kauli ya kumnufaisha mwananchi halafu ikatekelezwa mara moja, lakini ngoja itolewe kauli ya kumlemea mwananchi asubuhi inayofuata tu itaanza kutekelezwa tena kwa vitisho.Yaani NSSF wamepuuza kauli ya Raisi?
FAO LA kujitoa
Waziri nae kimya
Ina maana Raisi haheshimiwi au ni Kauli ya kisiasa tu?
Na hapo ndo utagundua nini maana ya kuambiwa mtu ni mtawala wa wanyonge. Ni lazima watu wote wageuzwe kuwa wanyonge ili kauli mbiu hiyo ya kuongoza wanyonge itimie, huku watu wasiotafsiri hiyo kauli tata wakipiga makofi na kushangilia Mithili ya kuku walio bandani kumshangilia mchinjaji wao huku kashikilia kisu mkononi mwake.
Sent using Jamii Forums mobile app