Mifuko ya plastiki kupigwa marufuku

Wakati sasa umefika kuchagua, kuharibu mazingira ya nchi yetu au kuwahurumia wenye viwanda vya Mifuko ya Plastiki. Lakini tukumbuke wazalishaji wote wa Mifuko ya Plastiki waliopigwa marufuku kwenye nchi za wenzetu Afrika ya Mashariki kama Kenya, Uganda na Rwanda watakimbilia TZ ili wayahatibu mazingira yetu. It’s time now to make positive decision.
Hiyo wizara ni bora apewe hata joti tu aiongoze, maana kwa hizi sarakasi inaashiria wazi kabisa kuna rushwa kubwa inatembea humo
 
Serikali ya Tanzania imesema iwapo watakubaliana na taasisi mbalimbali wanazotarajia kukutana nazo wiki hii wanaweza kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia Julai mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu Aprili 8, 2019 na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kaliua (CUF) Magdalena Sakaya. Sakaya amesema majibu ya Serikali kuhusu upigaji marufuku wa mifuko hiyo hayaonyeshi dhamira ya dhati ya kupiga marufuku.

“Mifuko mbadala ipo, wakinamama wanasuka vikapu vya ukili lakini haina masoko, mifuko ya plastiki inatolewa bure. Tatizo si mifuko mbadala bali kulinda viwanda vinavyoharibu mazingira,” amesema.

Amesema hakuna asiyejua madhara ya mifuko ya plastiki na kuhoji Serikali ina mpango gani wa kupiga marufuku mifuko hiyo badala ya kupoteza muda na gharama kama nchi nyingine zilivyofanya za na kufanikiwa.

Akijibu swali hilo, Makamba amesema bajeti inayokuja ya ofisi yake Aprili 16 mwaka huu wanaweza kutangaza hatua watakayoichukua.

Amesema kuwa wiki hii Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza kukutana na taasisi mbalimbali ikiwemo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baraza la Mazingira Nchini (Nemc) na Wizara ya Mambo ya Ndani kujadili suala hilo. “Kanuni tayari zinangoja kuchapishwa kwenye gazeti la Serikali.

Kama tukikubaliana inaweza Mei ukawa mwisho wa matumizi ya plastiki,”

Huyo waziri ni miongoni mwa mawaziri hopeless kabisa aiyefaa kwa lolote kwenye uongozi
 
Hahaaa,hapo lazima uwe mpole.
Alafu katika hali ya kusikitisha unasikia kauli ya waziri mwenye dhamana..?
Eti, "wanaandaa kikao na wadau"

Hapo ndo taabu inapoendelea. Kama bunge lingepitisha sheria ya hizo takataka na kutiwa muhuri na king of jude hauwezi kusema eti "kikao na wadau"
 
Rwanda wameweza na kenya, hapo kuna serikali hawapo tayari kupoteza chanzo chake cha mapato huku wakijua kabisa wakivifunga wahana vyanzo vipya vya kodi... Wawekezaji ndiyo kwanza wanakimbia na kuhamisha mitaji yao
 
Sasa unakaa kikao na mbuzi unaetaka kumchinja? Unategemea mbuzi akupe ruhusa umchinje? Hicho kikao ni wanatengeneza tu mazingira ya kupewa rushwa.
 
Rwanda wameweza na kenya, hapo kuna serikali hawapo tayari kupoteza chanzo chake cha mapato huku wakijua kabisa wakivifunga wahana vyanzo vipya vya kodi... Wawekezaji ndiyo kwanza wanakimbia na kuhamisha mitaji yao
Viwanda vya mifuko mbadala vitalipa kodi pia. Tatizo ni rushwa wanayoendekeza toka kwa wahindi..!!!
 
Huyu dogo anatuchezea akili. Eti wadau wote wakikubaliana huenda Mei ikawa mwezi wa mwisho. NONSENSE
Nani hajui kwamba baadhi ya wadau hususan wahindi wanaoizalisha na kuiagiza hawatakubali ipigwe marufuku.
Hata wengine kutoka baathi ya hizo taasisi washahongwa mijipesa na kwenye vikao watakwenda kusinzia na kutoa ushuzi tu.
 
Umeongea kinyume mkuu!!
 
Wanahongwa na wahindi wanaotengeneza hii mifuko huko viwandani ndo maana hili suala linapigwa danadana.
Kwa sasa hivi watafanya kweli mkuu wahindi zaidi ya wote waliyo kuwa wana tengeneza mifuko ya plastic wameshaingiza machine za kutengeneza iyo mifuko wanayo sema inalinda mazingira Ila mfuko mmoja utakuwa buku 1,000 sasa hivi pesa wana kula ya kuipiga marufuku hii ya nylon!!
 
Kama wakifanya kweli itakua safi ila hilo jibu lake halishawishi kabisa. Alivyo ingia hiyo wizara nilimsikia akiongea kwa kujiamini kuwa wataipiga marufuku mifuko ya plastic ila miaka imepita sasa!! Wadau wanaleta tuhuma za rushwa kama ni kweli hiko kikao ni kama cha harusi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rwanda Kenya wamepiga marafuku matumizi ya mifuko ya plastic siku nyingi ,uamuzi ambao umeboresha mazingira kwa kiwango kikubwa -Impact is immediate and visible.
 
Back
Top Bottom