Serikali ya Tanzania imesema iwapo watakubaliana na taasisi mbalimbali wanazotarajia kukutana nazo wiki hii wanaweza kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia Julai mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu Aprili 8, 2019 na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kaliua (CUF) Magdalena Sakaya. Sakaya amesema majibu ya Serikali kuhusu upigaji marufuku wa mifuko hiyo hayaonyeshi dhamira ya dhati ya kupiga marufuku.
“Mifuko mbadala ipo, wakinamama wanasuka vikapu vya ukili lakini haina masoko, mifuko ya plastiki inatolewa bure. Tatizo si mifuko mbadala bali kulinda viwanda vinavyoharibu mazingira,” amesema.
Amesema hakuna asiyejua madhara ya mifuko ya plastiki na kuhoji Serikali ina mpango gani wa kupiga marufuku mifuko hiyo badala ya kupoteza muda na gharama kama nchi nyingine zilivyofanya za na kufanikiwa.
Akijibu swali hilo, Makamba amesema bajeti inayokuja ya ofisi yake Aprili 16 mwaka huu wanaweza kutangaza hatua watakayoichukua.
Amesema kuwa wiki hii Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza kukutana na taasisi mbalimbali ikiwemo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baraza la Mazingira Nchini (Nemc) na Wizara ya Mambo ya Ndani kujadili suala hilo. “Kanuni tayari zinangoja kuchapishwa kwenye gazeti la Serikali.
Kama tukikubaliana inaweza Mei ukawa mwisho wa matumizi ya plastiki,”