Mifuko ya kuhifadhia nafaka zisioze inapatikana wapi Dar?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,425
13,935
Ndugu zangu naomba mnijuze wapi na bei gani Dar es Salaam nitapata mifuko ya kuhifadhia nafaka kama mahindi zisioze bila kuweka dawa.
 
Mkuu jarbu kuwasiliana na kiwanda cha A TO Z kipo Arusha.nimesikia tangazo lao wanayo iyo mifuko au magunia. Mm nitawatembelea SABA SABA kwenye banda lao. Wamesema watakuwepo pale
 
Habari njema
 
Chuo cha Sokoine pia wanamifuko maalumu ya kuhifadhi mahindi mpaka miaka 3 bila dawa. Niliiona kwenye maonyesho yao ya kilimo, ukiweza kuwasiliana nao wanaweza kukupa taarifa zaidi
 
Ndugu zangu naomba mnijuze wapi na bei gani Dar es Salaam nitapata mifuko ya kuhifadhia nafaka kama mahindi zisioze bila kuweka dawa.
ile mifuko ina bei sana kati ya efu 5-6 per mfuko, tembelea maduka ya pembejeo za kilimo uataikuta, mi niliionaga shinyanga
 
Hapana, sasa kuna kiwanda Tanga wanatengeneza hiyo mifuko (PICS) ni Tsh 3000 hadi 3500 tu. Ila ipo inayotoka Asia inaitwa Pro Super Grain ni ghali kidogo kati ya USD 3 hadi 5 iko pale Balton (Mikocheni) Jirani na MARI (kituo cha utafiti wa kilimo mikocheni).
 
mkulima gani anamudu bei hizo? Asilia 90 ya chakula nchini kinazalishwa na wakulima wadogo sana wa jembe la mkono ambao 60% ya mazao yao yanapotea kwa njia mbalimbali kabla ya kumfikia mlaji wa mwisho. wadudu waharibifu wanachangia asilimia 40 ya upotevu huo. Mkulima mdogo hawezi kununua mfuko kwa sh. 4000 - 6000 kwa mfuko. Lazima technolojia iendane na hali ya walaji/watumiaji.
 
Hii ya AgroZ iko vipi?
 
Hii ya AgroZ iko vipi?
Kwa bahati mbaya siijui hiyo ya A to Z, but yote inafanya kazi kwa principal moja, inazuia hewa ya oksijeni kuingia ndani ya mfuko na hivyo wadudu waharibifu na fangasi hawawezi kuishi ndani ya huo mfuko. Tafuta hiyo ya PICS iko nchi nzima kwa bei ya rejareja yaweza kuwa Tsh 4000 (Kg 100). Hakikisha nafaka imekauka kabisa ndo uhifadhi. Imethibitishwa pia kucontrol kiasi cha sumu kuvu kwenye nafaka.
 
mkulima gani anamudu bei hizo? Asilia 90 ya chakula nchini kinazalishwa na wakulima wadogo sana wa jembe la mkono ambao 60% ya mazao yao yanapotea kwa njia mbalimbali kabla ya kumfikia mlaji wa mwisho. wadudu waharibifu wanachangia asilimia 40 ya upotevu huo. Mkulima mdogo hawezi kununua mfuko kwa sh. 4000 - 6000 kwa mfuko. Lazima technolojia iendane na hali ya walaji/watumiaji.
mi nilivoona vile nikaamua kunnuua dawa kuwekea mahindi yangu, bora utie dawa japo mara 3 kama umeweka store gharama inakuwa chini kidogo.
 
Hata hivyo wanasema mifuko hiyo inaweza kutumika kwa misimu 3 tofauti bila kuhitajika kununua mifuko mipya. Kuweka dawa kuna gharama zake pia kama vile kununua mifuko, kununua dawa, kulipia vibarua wa kuweka dawa na kuyatia sumu mazao.
 
kariakoo ipo inauzwa 7000 kwenye maduka yanayouza pembejeo na mbegu
Nimewasiliana sales office A to Z Arusha kuhusu mifuko yao hii, kasema Dar wana kituo chao Chang'ombe Mbozi road kwa bei ya jumla ya sh. 200000 kwa mifuko 50.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom