Mifuko ya jamii sasa kuwekeza katika umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mifuko ya jamii sasa kuwekeza katika umeme

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by pareto 8020, Apr 22, 2010.

 1. p

  pareto 8020 Member

  #1
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 7, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wednesday, 21 April 2010 19:36 0diggsdigg

  Frederick Katulanda, Dodoma

  MIFUKO ya Hifadhi ya Jamii Nchini, imekubaliana na Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco), kuwekeza mabilioni ya fedha katika sekta ya umeme, ili kusaidia kuzalisha umeme wa kutosheleza mahitaji ya ndani ya nchi na kumaliza tatizo la nishati hiyo.

  Hayo yalisemwa jana bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya hesabu za mashirika ya umma ya mwaka wa fedha wa 2008/9.

  Akizungumza uwekezaji huo, Zitto alisema hatua hiyo imekuja baada ya kamati yake kuzungumza na mifuko hiyo na kuiomba iangalie uwezekano wa kuwekeza katika uzalishaji wa nishati ya umeme.

  "Mazungumzo hayo yamekamilika na yako katika hatua nzuri. Mheshimiwa spika, naomba kulialifu Bunge lako tukufu kuwa wakati Tanzania ikiadhimisha miaka 50 ya uhuru, Shirika la Umeme Tanzania na mifuko hii ya hifadhi ya jamii itakuwa ikizindua kuanza kwa miradi huu mkubwa," alisema Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.

  Mifuko ya hifadhi ya jamii itakayoshiriki katika mradi huo ni NSSF, PPF, PSPF, LPSF na ile ya Tanzania visiwani.

  Akizungumzia mwenendo wa faida na hasara wa Tanesco, Zitto alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2006/2007 shirika lilipata hasara ya Sh.67, 234 milioni na lakini lilifanikiwa kupunguza hasara hiyo katika kipindi cha mwaka 2007/2008 hadi baada ya kupata Sh. 21,605.

  "Lakini katika kipindi hiki hasara imeongezeka tena na kwa Sh.48 milioni," alisema.

  Alisema Tanesco ni miongoni mwa mashirika mengi yanayothiriwa na tatizo la serikali kutolipia huduma zinatolewa na mashirika hayo.

  Kwa mujibu wa Zitto, mashirika mengine ni pamoja na Boharia ya Dawa inayoidai serikali kiasi cha Sh. 30 bilioni.

  Kamati ya Zitto iliiomba serikali kurudisha dola za kimarekani 4, 865,000 ilizoilipa Kampuni ya Dowans kwa ajili ya kukodisha ndege maalum ya kusafirishia mashine na kusafirishia umeme kuja Dar es Salaam bila ya kuwa na mkataba.

  Alisema kama serikali itarudhisha fedha hizo zitasaidia kuongeza mtaji wa Tanesco na hivyo kuliongezea ufabnisi katika utendaji wake"

  ======================
  Siku hizi imejitokeza trend ya kukimbilia Social Security Funds kufinance activities mbalimbali. Kwa mtazamo wangu, mifuko ya JAmii, ni mali ya wanachama wanaochangia. Aidha mifuko hii, ina wajibu na dhamana ya kuhakikisha kwamba wanachama wake wanatoa michango yao bila kukosa, na wanapostaafu wanapata pensheni zao kwa wakati.

  Idea ya Social Security Funds kuwekeza kwenye miradi yenye 'faida' in both social and monetary terms, ni jambo la kawaida. Hata hivyo decision ya wapi pa ku invest lazima izingatie maslahi mapana ya wanawanachama (owners). Ni kwa jinsi hiyo, Investment ambazo zatakiwa kufanywa lazima ziwe za uhakika kabisa kupata returns.

  Hivi karibuni Social Security zimejikita katika investments ambazo nina uhakika ukifanya proper appraisal it will take so many years kupata returns if you are lucky, na kwa baadhi ya projects kuna hatari ya kula hasara kabisa.

  It is too bad, kwamba Politicians wetu, wameiona mifuko hiyo kama kimbilio lao la kupata quick and easy money....actually Politicians wana act as if wao ndio wana own mifuko hiyo..something which is very wrong....

  Kusema ukweli sote twajua investment katika power generation ni capital intensive na mara nyingi returns hakuna (especially mahala ambapo infrastructure ni duni/chakavu.
  Kwakweli pesa ya wanachama kwenda kwenye umeme....ni kucheza pata/potea...too bad..member's lifetime contributions is sunked in to such project ambayo..kwa mfumo uliopo sasa, it is bound to be a loss making investment...

  Hizi project kubwa...jamani zinatakiwa kutafutiwa fedha kwa utaratibu mwingine..kupitia Sovereign Bonds, long-term soft loans kutoka WB, ADB na nchi tajiri kama China. Hivyo ndivyo ilivyofanyika huko nyuma na ndivyo inavyofanyika duniani kwote...
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Wanaweza kuamua chochote na hizi fedha za hifadhi ya jamii, maana ni katika fedha ambazo wenye nazo hawana hata chembe ya kauli nazo, zinakuwa controlled na watu wengine wanaoletewa tu!...na wanazitumia kwa discretion yao wenyewe!...Wenyewe wakizitaka wanageuka mbogo hawa watu!..
   
 3. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Well said!
  Cdhani kama hawa politicians ni members wa Social Security Funds, no wonder wanakimbilia huko coz hawana hasara (If at all sio members).
  Na kama ni members, inakuwaje una invest kwenye shirika kama TANESCO?!
  Unapewa historia ya kupata hasara mfululizo and yet unapeleka investment yako hapo?!
  Kwa upembuzi wa haraka haraka, wanatarajia TANESCO wataanza kupata faida kweli over the next 20 years kwa infrastructure mbovu kama hizo walizonazo na mikataba mibovu waliyoingia kama ya IPTL kweli?!

  Inauma sana!
   
 4. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hii mifuko ya jamii inafanya biashara na kupata faida ya mabilioni kila mwaka. Kwanini basi kusiwe na gawio (dividents) kwa wanachama wake kutokana na kiasi cha pesa mtu alichonacho huko? Say share moja ni sawa na Shilingi 1000 mwenye mil. 10 anakuwa na share 10,000 na anapata gawio sawa na faida iliyopatikana badala ya pesa hizi kuwakopesha akina Manji wanajenga majumba na kuwauzia hao hao kwa bei mara dufu. Nafikiri ifike mahali waafrika tuanze kuishi maisha ya kutenda haki na kujua namna ya kuwasaidia wananchi wetu badala ya utapateli na ubinafsi uliotawala mioyo ya viongozi wetu.
   
 5. p

  pareto 8020 Member

  #5
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 7, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I agree with you rmashauri...kwamba mifuko hii inawekeza katika miradi na kupata faida.....maybe idea ya kutoa dividend direct inaweza kuwa ngumu lakini one thing they could consider ni kuwekeza katika projects ambazo wanachama wao wanaweza kubenefit- kwamfano investment katika low-cost housing---kwakuwa ni vigumu kwa mtu wa chini kuwa na savings za kujenga nyuma....wanachama wangeweza kukopeshwa kwa riba nafuu kwa kipindi kirefu nyumba hizo...ili wawe na maisha bora kuanzia sasa....na sio kusubiri wafikie miaka 60. Huko ndio kuwekeza kwenye faida kwa wanachama... NSSF wana projects za Low-cost housing, lakini hakuna utaratibu wa makusudi wa kuwakopesha wanachama wake ambao wangehitaji.....it is just a general scheme open to anyone.... there should be a priority to members na tena wakapewa better terms kuliko watu wengine wasio wanachama...

  KWa jinsi hiyo, it will be very easy to attract members katika mifuko hiyo....especially vijana...
   
 6. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Si kwa lolote jema bali ni sababu ya ufisadi.

  Construction industry inasifika kwa rushwa/ufisadi mkubwa hapa nchini. Ndiyo maana hii mifuko sasa inahangaika na ujenzi tuuuu! Ndiyo njia rahisi ya kuiba pesa za umma.
   
 7. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Haya mashirika yatafanya kazi nzuri sana katika kujua na kuona jinsi gani ya kuwekeza katika jamii yetu
   
 8. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #8
  Apr 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Hizo hadithi hazijaanza leo.
   
Loading...