Mifuko ya hifadhi ya jamii kunganishwa na kupata mifuko miwili (Sekta Umma&Binafsi)

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,067
10,936
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iliyopo kuunganishwa na kupata mifuko 2 tu, Mmoja sekta ya Umma na mmoja sekta binafsi na sekta isiyo rasmi. Nimefurahishwa na uamuzi huu ambao nilishauri tangu mwaka 2011. Ni hatua itakayowezesha wanachama kuhudumiwa vizuri, kupunguza ushindani usio na maana yeyote na kuboresha mafao ikiwemo fao la Bima ya kukosa kazi.

Zitto
 
Ni kweli utitiri wa mifuko ya hifadhi ya jamii ulianzishwa ili kuwaongezea watu fulani mianya ya ulaji bila kuwa na usimamizi thabiti
 
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iliyopo kuunganishwa na kupata mifuko 2 tu, Mmoja sekta ya Umma na mmoja sekta binafsi na sekta isiyo rasmi. Nimefurahishwa na uamuzi huu ambao nilishauri tangu mwaka 2011. Ni hatua itakayowezesha wanachama kuhudumiwa vizuri, kupunguza ushindani usio na maana yeyote na kuboresha mafao ikiwemo fao la Bima ya kukosa kazi.

Zitto
Taarifa hii kama ni kweli itakuwa jambo jema sana tupunguze wezi wa mafao yetu.
 
Good decision.Kwa sasa hakuna haja ya kuwa na mamifuko yote hayo kwa kuwa afterall mafao yanalingana.
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iliyopo kuunganishwa na kupata mifuko 2 tu, Mmoja sekta ya Umma na mmoja sekta binafsi na sekta isiyo rasmi. Nimefurahishwa na uamuzi huu ambao nilishauri tangu mwaka 2011. Ni hatua itakayowezesha wanachama kuhudumiwa vizuri, kupunguza ushindani usio na maana yeyote na kuboresha mafao ikiwemo fao la Bima ya kukosa kazi.

Zitto
 
Kwa nini iwe 2 tu? Kwa nini iliruhusiwa kuwa mingi kama ilivyo? Kuna mengi ya kujadili hapa
 
Kwa mantiki hiyo sioni kazi ya SSRA mana inakuwa inatumia gharama nyingi na kusimamia vitu viwili tu.Ni bora ifutwe
 
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iliyopo kuunganishwa na kupata mifuko 2 tu, Mmoja sekta ya Umma na mmoja sekta binafsi na sekta isiyo rasmi. Nimefurahishwa na uamuzi huu ambao nilishauri tangu mwaka 2011. Ni hatua itakayowezesha wanachama kuhudumiwa vizuri, kupunguza ushindani usio na maana yeyote na kuboresha mafao ikiwemo fao la Bima ya kukosa kazi.

Zitto

Taratibu mnawarudisha kwenye ukitimba?
Kila siku watu wapiga kelele juu ya Tanesco kwa sababu uzembe mmowapo unatokana na ukiritimba wa kuwa hakuna mbadala/mshindani?
Je mumewauliza wanachama?
 
Sasa hapa ni kwenda tofauti na 'nia njema' ya JK ya kuongeza ajira kwa wasio na ajira.
Maana yeye aliiongeza mpaka akaiundia na mamlaka yake!
Angalizo: Hii inaweza ikawa janja ya kuficha hasara za mifuko inayosemekana kuwa katika hali mbaya baada ya uwekezaji usio na tija kama machinga complex, madaraja ya kulipia na majengo yasiyopangishika ...nssf/pspf.....
 
Ina Maana Dau ndio Bye bye tena maana ile Kauli ya Magufuli kusema kuna viongozi wa Mashirika fulani wanalipwa Mishahara zaidi ya Million 32 na zaidi na pesa zao wamezisambaza kwenye mabenki mbali mbali ya biashara zaidi ya billion mia tatu akili zikatua pale Hifadhi... Japo kwa Msech na Tanroad hawakwepeki Mishahara kama sio watanzania huku wengine wakili na kima cha chini... Raisi haoni sababu ya hawa jamaa walipwe kufuru...

Ila Mtu umezoea Mshahara mnono Gari Full ac Safari kila kukicha nje ya Nchi kusign mikataba ghafla tu after october 25 hali inabadilika.... unaweza usibanwe na haja mwezi mzima... tulikuwa tunasisitiza fanyeni Changes before changes kuwa change....

Mdogoye Ni Mbunge atamtetea huko
 
Ajira zitaombwa upya au? Akina siye tuliopata kwa kamlete tekiniki:)
 
Back
Top Bottom