Hivi
Ushimen kwa hilo unalosema tutakuwa tunaenda mbele au tunarudi nyuma?kilichotushinda hapo ni kipi,hivi ni kweli tumeshindwa kabisa kuwa na sheria kali ya ku control utupaji taka hovyo hususa ni hii mifuko ya plastiki mpaka turudie vikapu na mifuko ya makaratasi?hii ni sawa na ile ya kushindwa kutengeneza utaratibu au sheria kali kwa madereva wanao kiuka sheria za barabarani na badala yake tunaweka matuta ambayo yanaharibu magari...
Mkuu, swala la sheria kali ya uchafuzi wa mazingira sio jambo tu pekee ama sababu ya msingi ililo pelekea mifuko hii ya plastic kupigwa marufuku.....
Mara nyingi mifuko laini na miepesi ya nailoni au Rambo kama inavyojulikana na wengi Tanzania imekuwa ikitumiwa na baadhi ya wananchi katika kufungashia chakula na hasa vyakula vya haraka kama chips au wali kwa wale wenye migahawa midogo kabisa.
Hata hivyo kuna baadhi ya familia wao huchana mifuko ya nailoni na kuitumia kufunikia vyakula pale wanapokua wakipika kwa Imani kuwa inasaidia kuivisha chakula haraka, kwani hufunika vizuri na kuganda kwenye sufuria hivyo mvuke wote hubaki ndani, mfano kufunikia wali, wakati wa kuchemsha mahindi, viazi au mihogo.
Tofauti na mifuko, kumekuwa na matumizi makubwa ya vyombo vya plastiki katika familia nyingi hapa Tanzania.
Na vyombo hivyo kama vikombe sahani na hata majagi vimekuwa vikitumika sana kuhifadhia chakula tena mara nyingi ni cha moto.
Kwa mujibu wa taasisi ya kilimo na sera ya biashara IATP, plastiki zote zinaundwa kwa kemikali ambayo inauwezo wa kuharibu afya ya mtu.
Baadhi ya kemikali hizo ni BPA na DEHA, na zinatajwa kuhusika na mabadiliko ya tishu, kuharibiwa kwa vina saba, kuharibu mimba, matatizo wakati wa uzazi na mabadiliko ya homoni.
Wakati kwa watoto kemikali hizo zinatajwa kuharibu kinga yao ambayo inatakiwa kuongezeka hali inayosababisha homoni kubadilika na kusababisha matatizo katika tabia .