Mifuko imeamua kuwadhulumu watumishi kwa kutumia kalamu na kanuni

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Kwa uzoefu wa siku za nyuma ,mtumishi wa kiwango cha chini,yani anaestaafu na mshahara wa TGS/TGTS E alikuwa analipwa kiinua Mgongo cha Zaidi ya mil 70 kutegemea miaka aliyoitumikia serikali.

Hii mil 70+ ambayo ni Kiinua mgongo(Lampsum)ndio fedha ambayo mtumishi ilihangaika kupata nyumba nzuri walau atakapofia siku umauti ukimkuta.

Ni kupitia fedha hiyo ndio ilikuwa inasaidia kutatua changamoto za Extended family.

Lakini ujio wa PSSSF imekuwa kilio kwa watumishi wa umma.

Kama serikali itaruhusu kanuni mpya ya PSSSF itumike kulipa mafao basi wastaafu wengi watakufa mapema kwa mshtuko.

Yaani mtu ambae matarajio yake ni mil 70+ atapata chini ya mil 17,

Kanuni yao ni hii hapa,kila aliesoma walau hisabati kwa ngazi ya shule ya msingi anaweza kukokotoa mwenyewe ajiandae kisaikolojia.

KANUNI KUKOKOTOA KIINUA MGONGO(LAMPSUM)

CPG=PF x PS x APE x CF x CR.

PF=1/580
PS=360
APE=MISHAHARA MINONO 36 ULIYOPATA NDANI YA MIAKA 10 YA MWISHO YA UTUMISHI WAKO÷KWA 3.

MFANO MSHARA MIL 1X36=36MIL÷3=12Mil.

APE=MIL 12.

CF=12.5

CR=25%

Sasa twende pamoja.

0.0017x360x12,000,000x12.5x0.25

Hapo unakuwa umebadili kila kitu kuwa kwenye desimali.

Kiinua mgongo=22,950,000/=

Hapo tumetumia mshara mnono wa mil 1000000,

My take.

1.Mifuko imeamu kuwadhulumu watumishi kwa kutumia kalamu na kanuni.

Bahati mbaya kanuni hii inamuhusu kila mtumishi wa umma bila kujali cheo chake.

2.Kama kuunganishwa mifuko kulilenga kumnufaisha mtumishi,je huko ndiko kuboresha maslahi ya watumishi?au kuwakomoa watumishi?

3.Wapo wanaosema kuna mifuko ilikuwa hoi bin taabani,lkn sababu za wao kuwa hoi ni fedha zao kukopwa na wakubwa na si watumishi waliosababisha iwe hoi,kwanini gharama za kuifufua zibebwe na wastaafu?

Au wastaafu sio wanyonge?
 
Kwa sasa unalipwa lumpsum kidogo ila unaendelea kula asilimia 90 ya mshahara uliostaf nao so unakuwa kama bado upo kazini sababi ile helea ulikuwa unapokea utaendelea kuipokea yote pengine na zaidi sababu haina kodi
 
Bado hai justify kikotoo hicho kichingu kwa mstaafu!

Ni unyonyaji. Mtu unayemlipa 90% ya mshahara wake kwa mwezi baada ya kustaafu unampa milioni 20,000 kama mafao yake unategemea atajenga walau kibanda cha uani wakati alipokuwa anapewa 100% ya mshahara wake alishindwa hata kununua baiskeli?

Sheria hii ni nyonyaji, na serikali kama kweli imepitisha sheria hii ni nyonyaji vilevile!

Ukiisha staafu ni kwamba unakaribia KUFA umefika ukingo wa maisha yako na kama utaendelea kuishi hutaishi zaidi ya miaka 20!

Sasa hiyo asilimia 90% itafikia kiwango cha malipo kama ungelipelwa kwa sheria ya zamani?

Hivi wabunge ninyi kweli ni wazalendo?
 
Kwa sasa unalipwa lumpsum kidogo ila unaendelea kula asilimia 90 ya mshahara uliostaf nao so unakuwa kama bado upo kazini sababi ile helea ulikuwa unapokea utaendelea kuipokea yote pengine na zaidi sababu haina kodi
Alafu utaifanyia nini hiyo hela? Ni sawa na umkopeshe mtu mil 50 alafu awe anakulipa laki kila mwezi? Toeni hela za watu, ni jasho lao.
 
Kwa sasa unalipwa lumpsum kidogo ila unaendelea kula asilimia 90 ya mshahara uliostaf nao so unakuwa kama bado upo kazini sababi ile helea ulikuwa unapokea utaendelea kuipokea yote pengine na zaidi sababu haina kodi
Kwa muda gani utapata
 
mawazo ya huyo jamaa ni ya kuyapuuzia tu kifupi mfumo huo utaleta usumbufu mkubwa sana hasa hali ya uchumi ikiendelea kuyumba yumba kama alivyosema waziri bunheni hapo juzijuzi. Huwezi kumlipa mstaafu huku mfanyakazi bado hajalipwa mshahara wastaafu watapata tabu sana.
Miaka uliyohenyeka ni mingi kuliko hiyo utakayolipwa 50% plus other stress za kufuatilia. Si tunaona wanavyohangaika kupata mafao yao kwa wakati!
 
Kwa sasa unalipwa lumpsum kidogo ila unaendelea kula asilimia 90 ya mshahara uliostaf nao so unakuwa kama bado upo kazini sababi ile helea ulikuwa unapokea utaendelea kuipokea yote pengine na zaidi sababu haina kodi
Anyway unayo haki kutoa maoni ya hivyo..

Lakini hebu jiulize life span yetu nj miaka mingapi?

Je huyo mstaafu atapokea malipo hayo kwa muda gani kabla ya kifo based on life span?
 
Kwa muda gani utapata
Hadi utakapo kufa, ila kuna uhakiki kila baada ya miaka mitatu hivi, ili kuthibitisha kama uko hai.
Ila kama utalipwa asilimia 90 ya msahala unaotokanao kidogo itasaidia kuvuta siku.
Wastaafu wengi hata wakichukua milioni mia, miezi sita tu au mwaka pesa yote inakuwa imeisha na huishia kufa kwa msongo wa mawazo.
 
Back
Top Bottom