Miezi Mitatu ya Serikali ya awamu ya tano bado binafsi sioni mwelekeo

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Wapo wanaojitokeza na kuzungumza kukosoa mwelekeo wa serikali ya awamu ya tano na wengi wanaokosoa maoni yao yanapokelewa na jamii kwa hasira kwa maana jamii imeridhika na kile kinachofanywa na Serikali hii.

mimi naona wanaokosoa wako sahihi na jamii kutoa mtizamo wao juu ya maoni ya wanaokosoa iko sahihi. kwa njia hiyo wale walioko madarakani wanapata mrejesho wa kile wanachokifanya kama kinakidhi jamii wanachokitaka, walioko madarakani wanapata changamoto juu ya mipango na utekelezaji wao kwa watu kuwakosoa.

hawa wanajamii wanaojiona wana uwezo wa kuwa viongozi wanapata nafasi ya kujua fikra zao kama kweli zinawawezesha kuwa viongozi. hivyo naona kukosoana ni jambo ambalo tunatakiwa kuliendeleza.

kwa mtaji huo mimi binafsi mpaka sasa sioni mwelekeo wa serikali ya awamu ya tano.

sisemi hawa jamaa hawafanyi kazi bali ninachokisema kama ni timu ya mpira ninaona wachezaji wakipiga chenga nyingi, pasi nyingi lakini bila timu kuonekana kuwa na mipango ya kutafuta goli.

magoli katika serikali ni kuwaletea wananchi maisha mazuri kwa kasi. tunapochagua viongozi tunachagua wale ambao kodi zetu zinaweza kutuletea maisha mazuri kwa kasi.

wananchi tunatakiwa kuangalia kwa rasilimali zetu hizi tunalinganisha tukimpa uongozi huyu maisha yetu ndani ya miaka kadhaa yatakuwaje na yule ambaye tunaona maisha yetu yatapiga hatua kwa kasi ndio best option.

sioni muelekeo katika serikali hii kwa sababu wanaonekana kutokuwa na dira moja wanayoitekeleza na kila mmoja anacheza akiwa na malengo yake na hawabebi jambo moja kulitoa mwanzo mpaka mwisho bali wanachukua hili na kulitupa kuchukua lile.

mfano serikali ya awamu ya tano imeokana kuibuka na hoja namba moja ikiwa ni kukusanya mapato, kuondoa mianya ya matumizi mabaya. hapa inajumuisha kuondoa ukwepaji kodi, inajumuisha kuhakikisha kila taransaction inayostahili kulipa kodi inalipa kodi kwa maana ya kupanua wigo wa kodi, inajumuisha fedha hizi za kodi ya watanzania hazitamhudumia mtu asiyestahili kuhudumiwa na kodi hizi kwa maana ya kuthibiti wageni, kuhakikisha fedha za watanzania zinanunua bidhaa za watanzania kwanza na pale tu watanzania wanaposhindwa kuzalisha lakini wanahitaji ndipo zikanunue bidhaa za wageni hapa ikizungumzia kudhibiti bidhaa na huduma za kutoka nje.

hapa inajumuisha kuongeza tija katika fedha za watanzania na hapa unaongelea kupanga miji na vijiji ili watu wakae pamoja kwa utaratibu ili iwe rahisi kuwahudumia kwa maana ya kupunguza gharama za kuwapatia hudumia na kurahisisha kazi ya kuwapatia huduma.

serikali imeanza vizuri kwa kufuatilia mianya ya ukwepaji kodi bandarini na TRA na kuanza kuwashughulikia watendaji wa umma wanaofuja fedha za umma. serikali imeonekana kutokupenda watu kukiuka taratibu za makazi.

lakini serikali hii imeonekana kuwa na "new body but the same old engine". ninasema hivyo kwa kuwa serikali ilitakiwa kuacha mfumo wa kizamani wa mwanasiasa kuibuka na hoja akaangalia upande mmoja wa hoja hiyo na kuanza kuitekeleza bila kutumia wataalamu kukaa chini na kutafakari njia sahihi ya kutatua jambo kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

kufuatilia mapato na matumizi ya serikali bila mifumo katika nchi inayosaidia kufanya kazi hiyo ni kazi ngumu sana. kutoa huduma kwa wananchi bila kuwa na mifumo katika nchi inarahisisha huduma hizo ni sawa na kuendelea kutwanga mahindi kwa kinu wakati mashine za kutumia umeme zinawezekana.

vitambulisho vya taifa na mpangilio wa makazi ni nyenzo muhimu sana katika mambo haya. ukisha kuwa na mambo haya ni rahisi sana kurasimisha biashara zote na si kwa lengo tu la kuwawezesha kupata mikopo bali kuhakikisha kila biashara inalipa kodi. ni rahisi sana kumonitor mambo mengi yanayotendeka ndani ya nchi.

kwa mtizamo wangu vitambulisho vya taifa na kupanga makazi kwa mantiki ya arrangement on ground hata bila hati vingekuwa vipaumbele namba moja katika bajeti ya 20162017.

huko nyuma mwalimu nyerere alibaini kuwa watu wa vijijini wakikaa wametawanyika anashindwa kuwahudumia akaanzisha mpango wa kuwakusanya watanzania katika vijiji ili awaweke pamoja awahudumie. mantiki ya kupanga mji ni hiyo hiyo. lakini leo hii tunashindwa kudhibiti miji yetu, wataalamu wanashindwa kubaini hili na hawa wanajikita katika kutengeneza fedha kutoka katika concept ya kupanga mji hivyo wao wanaona kuhalalisha makazi holela ndio jukumu lao. kama nina kiwanja katika makazi holela eti ninyi wao niwape fedha waje kupima kiwanja changu na kunipa hati na hivyo ndivyo wanavyopanga mji!!!!!!. au wanachukua kipande cha ardhi eti wanapima huku watu hawa wanaopimiwa sometimes wanachangamoto za kupata huduma kuliko hata makazi holela kutokana na location.

baada ya vitambulisho na arrangement ya miji yetu nilitegemea kipaumbele cha tatu kingekuwa kuwawezesha watanzania kujihudumia na hizo project tatu kubwa zingetosha kuwa kipaumbele kwa mwaka wa 2016/2017 maana bajeti haituwezeshi kufanya kila kitu na mengine inekuwa kusukuma wizara ziendelee kuboresha utendaji.

je wewe ulitegemea nini?
nilitegemea serikali hii kutambua kuwa kazi ya

serikali ya awamu ya tano imeonekana kubaini
 
hebu fikiria muhimbili imekuwa MRI, CT scan na vitanda. kwangu mimi raisi kwenda pale siku moja na akatumia vitu hivi kutoa mwongozo sawa lakini kila siku zinatolewa ripoti za vitu hivyo hivyo tu na kama vinafanya kazi tumeshachukulia ndio best performance ya muhimbili. kweli hapa malengo yatatimia?
 
Mi naona wewe ndio huns mwelekeo. Yote haya yanayofanyika huoni kitu loh!!! Watz watu wa ajabu sana

kuona kwako kunategemea na upeo wa muonaji

miji yetu imepimwa lini? na tunaposema kupima si swala la kuchukua eneo dogo ukapima viwanja.

ni swala la kutengeneza plan juu ya existing miji na kutunga sheria na kanuni za kutoka kwenye miji ya zamani kwenda miji mipya. tukiwa tunajua huduma Fulani mwananchi anatakiwa azipate ndani ya umbali gani kama public transport, shule, hospitalli, masoko na mengine.

maeneo ya viwanda yawe wapi? starehe, ibada

na hapa kama ni dar es salaam tunaangalia dar nzima tuanze mchakato wa kuitoa ilikokuwa inaelekea tuipeleke kwenye planned dar.

kuona kwako wewe unaona miji inapimwa lakini mimi naona tunalegalise squatters.

angalia miji yetu inavyokua ikiwa watu wanajenga wako very scattered na bila mpangilio, haya yamesimamishwa lini na sio kwa mzembe kukaa ofisini na kusema ni marufuku kujenga holela bali kuweka utaratibu unaotekelezeka wa kupanga makazi na hata kama watu hawana hati lakini wanaishi karibu karibu na katika mpangilio kiasi huduma yeyote kuwapelekea ni kwa urahisi.

kama hayo huyaoni yakifanyika watu wanajenga ovyo unakuta maeneo ya karibu hayajajaa lakini watu wanajenga mbali, watu wanajenga maeneo hawaachi sehemu za barabara, shule. mabaa yanazidi kujengwa kwenye makazi ya watu yanapiga kelele usiku kucha watu hawalali mbali na kushinda kwenye kazi ngumu, makanisa, misikiti iko mitaani inapiga kelele na mtu akisema wanamuita mpagani hivyo watu wanavumilia usumbufu kutokana na mtizamo ya jamii.

je unaona mpango wowote wa kutatua changamoto za mipango miji kwa mji wowote au wewe ukiona wanachukua eneo dogo wanapima na kuacha maeneo yaliyozunguka makazi holela unadhani ndivyo tutapanga miji yetu hivyo au unaposema yanafanyika ni yapi hayo unayoyaona wewe?

tunaposema kipaumbele maana yake ni kwamba hilo linakuwa tatizo ambalo unalipa special attention ili ulitatue kwa haraka ndani ya mda mfupi and then likurahisishie kutekeleza mambo mengine.

Mi naona wewe ndio huns mwelekeo. Yote haya yanayofanyika huoni kitu loh!!! Watz watu wa ajabu sana
 
100 days kwa nchi iliyochoka na kuibiwa kama Tanzania ni siku chache sana kuona makubwa yakifanyika,anachofanya Dr Magufuli ni kujaribu kujenga mfumo wa utendaji katika utumishi wa umma,then mambo mengine yataendelea.Huwezi kufanya kila kitu kwa siku 100 hata umpe Obama leo 100 days itakuwa ngumu.Tanzania ni sawa na mgonjwa mwenye magonjwa lukuki tena yupo ICU lazima kwanza afya yake iimarike then arudi wodini ,ndio aanze kujitegemea etc
 
Hata mtoto wa miezi mitatu hawezi kutembea. Kadri miezi inavoenda ndio anaanza kukaa kisha kutambaa halafu kusimama na hatimaye kutembea. Miezi mitatu kwa nchi iliyokuwa na matatizo ni michache kuanza kumtolea jicho mh. Rais kuwa hawaoni mabadiliko. Tatizo letu ni kuwa tunamwangalia Rais kana kama yy pekee ndio anapaswa kuleta mabadiliko. Sisi wote tunahitaji kumsaidia . Aliyoyafanya kwa kipindo kifupi hata mtoa mada asingeweza kuyafanya. Tanzania ni yetu wote mtoa mada atuambie yeye amelifanyia nini taifa hili hata awe na guts za kusema haoni lolote. Ushabiki tu
 
kwa nafasi yangu nimelifanyia taifa hili mengi na hata kuanzisha mada hii ni moja ya mchango wangu katika taifa. yeye amepata nafasi ya kufanya makubwa kwa nchi yetu tutamuuliza makubwa kwa nafasi yake.

tatizo ninalolipata kwa watanzania wengi ni kutokujua wanakokwenda na kukaa kusubiri au kinachofanyika hawawezi kupima bali mpaka hapo miaka imepita hawaoni kitu ndio wanaanza kusema Fulani mbaya. mfano awamu ya nne walipata muhula wa kwanza kwa kura nyingi sana na kuongezewa muhula wa pili kwa kura kupungua kidogo. leo hii watu wanaibuka na kulalamika kwenye mitandao eti awamu ya nne ilitupeleka pabaya na hapo ndipo mtu anaweza kutuuliza sisi tulikuwa wapi wakati tunapelekwa kubaya. leo hii wakisema bandarini kumeoza ndio tunampima raisi wa nne na kusema alitupeleka pabaya.

swali langu ni kumpima raisi aliyekwisha kutoka madarakani inatusaidia nini?

je kumchalenji raisi aliyeko madarakani na aliyekwisha kutoka madarakani ni lipi ambalo linaweza kusaidia nchi hii alafu mchangia mada anajiona yuko sahihi na kunihoji nimelifanyia nini taifa hili na mimi nasema kuibua mjadala juu ya utendaji wa raisi mapema ili katika mijadala jamii ione kama tuko njia sahihi au yawezekana hatuko njia ya zamani lakini yawezekana isitufikishe tunakotaka kwenda ili tujisahihishe.

nikirudi kwenye mada. yapo mambo mengi ambayo yanafanyika na kwa mtizamo wangu naona ni kikwazo katika kutekeleza tunayoyataka. mfano raisi juzi amehoji kwenye hotuba iweje mfanyakazi wa serikali alipwe milioni 35. kwangu mimi nikiangalia jinsi ambavyo mashirika ya umma mengi yamekufa huku tukiwa na sekita binafsi zinafanya vizuri mtizamo huo wa raisi mimi naona utamkwamisha.

mashirika mengi ya serikali yanakufa kwa sababu serikali inatumia watendaji wasio na sifa kutokana na sababu mbalimbali. moja ya sababu ni kuchukua watu wenye vyeti (madokta na maprofesa, na wasomi wa juu) wasio na uzoefu. watu wengi wanasema ukimchukua profesa amfanyie mgonjwa operesheni mgonjwa anakufa lakini profesa huyo anamfundisha daktari na daktari huyo anatibu watu wanapona.

hii ni kutokana ili kumfanyia operesheni mwanadamu kunahitaji elimu ya nadharia na uzoefu wa kufanya vitendo. yupo profesa anaweza kutambua kila kiungo cha mwanadamu katika kitabu lakini bahati mbaya akikuta mwili wa mwanadamu umepasuliwa hawezi kutambua mshipa huu ni upi au kiungo Fulani ni kipi. inahitaji mtu aliyesoma makaratasi na kufanya mazoezi ya kutosha kupasua miili ya watu ndiye anayeweza kumfanyia upasuaji mwanadamu na akabaini sehemu yenye tatizo na akaitibu na kumshona bila kudhuru viungo vingine.

madaktari hawa wenye uzoefu wa theories na practical hawako katika mashirika ya serikali yaliyokufa kwa maana hawa ni sawa na madaktari wanaofanyia upasuji wagonjwa wanakufa maana mashirika wameshindwa kuyaongoza yakafa.

mfano tuna shirika la ndege na tunataka kulifufua, kwangu mimi kumchukua mkurugenzi wa precision tukamlipa milioni 50 ili tumshawishi aje kwetu aache milioni 40 anayopata na atuendeshee shirika la ndege ambalo tutaweka mtaji na akalifufua likawa linatuletea faida kuna tija kuliko kumchukua profesa katika chuo Fulani ambaye amechukua kozi Fulani ya ndege kuendesha shirika letu la ndege huku tukipata hasara kila mwaka na tukimlipa mshahara mdogo kama wa mtumishi wa kawaida wa umma.

tukigangania mashirika yanayotakiwa kuendeshwa kibiashara kuwa na scale zilizo tofauti na mashirika ya binafsi katika soko daima tunakuwa na wafanyakazi rejects katika mashirika ya umma na wazuri wote watachukuliwa na sekita binafsi kwenye mafao mazuri.

unapoona raisi ana changamoto ya kufufua mashirika ya umma na yeye mwenye anaziba tundu ambalo angetokea kwa nini usiseme kuwa hii serikali inapiga chenga sana lakini haina mpango wa kufunga goli.

yawezekana kuna sehemu watu wanapeana mishahara minono si kwa mantiki ya kuboresha bali kufanya ufisadi na katika hayo ni raisi kuwa mkali lakini sikutegemea aongee kwenye public kusema mtumishi wa umma iweje alipwe milioni 35 kwa maana maneno yake yanaweza kumkwamisha pale itakapokuwa ili apate watu sahihi wa kufufua mashirika inabidi kuchukua watu wenye uzoefu wanaolipwa vizuri sana kutoka sekita binafsi la sivyo ataangalia vyeti lakini hatapata mabadiliko.

Hata mtoto wa miezi mitatu hawezi kutembea. Kadri miezi inavoenda ndio anaanza kukaa kisha kutambaa halafu kusimama na hatimaye kutembea. Miezi mitatu kwa nchi iliyokuwa na matatizo ni michache kuanza kumtolea jicho mh. Rais kuwa hawaoni mabadiliko. Tatizo letu ni kuwa tunamwangalia Rais kana kama yy pekee ndio anapaswa kuleta mabadiliko. Sisi wote tunahitaji kumsaidia . Aliyoyafanya kwa kipindo kifupi hata mtoa mada asingeweza kuyafanya. Tanzania ni yetu wote mtoa mada atuambie yeye amelifanyia nini taifa hili hata awe na guts za kusema haoni lolote. Ushabiki tu
 
Wapo wanaojitokeza na kuzungumza kukosoa mwelekeo wa serikali ya awamu ya tano na wengi wanaokosoa maoni yao yanapokelewa na jamii kwa hasira kwa maana jamii imeridhika na kile kinachofanywa na Serikali hii.

mimi naona wanaokosoa wako sahihi na jamii kutoa mtizamo wao juu ya maoni ya wanaokosoa iko sahihi. kwa njia hiyo wale walioko madarakani wanapata mrejesho wa kile wanachokifanya kama kinakidhi jamii wanachokitaka, walioko madarakani wanapata changamoto juu ya mipango na utekelezaji wao kwa watu kuwakosoa.

hawa wanajamii wanaojiona wana uwezo wa kuwa viongozi wanapata nafasi ya kujua fikra zao kama kweli zinawawezesha kuwa viongozi. hivyo naona kukosoana ni jambo ambalo tunatakiwa kuliendeleza.

kwa mtaji huo mimi binafsi mpaka sasa sioni mwelekeo wa serikali ya awamu ya tano.

sisemi hawa jamaa hawafanyi kazi bali ninachokisema kama ni timu ya mpira ninaona wachezaji wakipiga chenga nyingi, pasi nyingi lakini bila timu kuonekana kuwa na mipango ya kutafuta goli.

magoli katika serikali ni kuwaletea wananchi maisha mazuri kwa kasi. tunapochagua viongozi tunachagua wale ambao kodi zetu zinaweza kutuletea maisha mazuri kwa kasi.

wananchi tunatakiwa kuangalia kwa rasilimali zetu hizi tunalinganisha tukimpa uongozi huyu maisha yetu ndani ya miaka kadhaa yatakuwaje na yule ambaye tunaona maisha yetu yatapiga hatua kwa kasi ndio best option.

sioni muelekeo katika serikali hii kwa sababu wanaonekana kutokuwa na dira moja wanayoitekeleza na kila mmoja anacheza akiwa na malengo yake na hawabebi jambo moja kulitoa mwanzo mpaka mwisho bali wanachukua hili na kulitupa kuchukua lile.

mfano serikali ya awamu ya tano imeokana kuibuka na hoja namba moja ikiwa ni kukusanya mapato, kuondoa mianya ya matumizi mabaya. hapa inajumuisha kuondoa ukwepaji kodi, inajumuisha kuhakikisha kila taransaction inayostahili kulipa kodi inalipa kodi kwa maana ya kupanua wigo wa kodi, inajumuisha fedha hizi za kodi ya watanzania hazitamhudumia mtu asiyestahili kuhudumiwa na kodi hizi kwa maana ya kuthibiti wageni, kuhakikisha fedha za watanzania zinanunua bidhaa za watanzania kwanza na pale tu watanzania wanaposhindwa kuzalisha lakini wanahitaji ndipo zikanunue bidhaa za wageni hapa ikizungumzia kudhibiti bidhaa na huduma za kutoka nje.

hapa inajumuisha kuongeza tija katika fedha za watanzania na hapa unaongelea kupanga miji na vijiji ili watu wakae pamoja kwa utaratibu ili iwe rahisi kuwahudumia kwa maana ya kupunguza gharama za kuwapatia hudumia na kurahisisha kazi ya kuwapatia huduma.

serikali imeanza vizuri kwa kufuatilia mianya ya ukwepaji kodi bandarini na TRA na kuanza kuwashughulikia watendaji wa umma wanaofuja fedha za umma. serikali imeonekana kutokupenda watu kukiuka taratibu za makazi.

lakini serikali hii imeonekana kuwa na "new body but the same old engine". ninasema hivyo kwa kuwa serikali ilitakiwa kuacha mfumo wa kizamani wa mwanasiasa kuibuka na hoja akaangalia upande mmoja wa hoja hiyo na kuanza kuitekeleza bila kutumia wataalamu kukaa chini na kutafakari njia sahihi ya kutatua jambo kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

kufuatilia mapato na matumizi ya serikali bila mifumo katika nchi inayosaidia kufanya kazi hiyo ni kazi ngumu sana. kutoa huduma kwa wananchi bila kuwa na mifumo katika nchi inarahisisha huduma hizo ni sawa na kuendelea kutwanga mahindi kwa kinu wakati mashine za kutumia umeme zinawezekana.

vitambulisho vya taifa na mpangilio wa makazi ni nyenzo muhimu sana katika mambo haya. ukisha kuwa na mambo haya ni rahisi sana kurasimisha biashara zote na si kwa lengo tu la kuwawezesha kupata mikopo bali kuhakikisha kila biashara inalipa kodi. ni rahisi sana kumonitor mambo mengi yanayotendeka ndani ya nchi.

kwa mtizamo wangu vitambulisho vya taifa na kupanga makazi kwa mantiki ya arrangement on ground hata bila hati vingekuwa vipaumbele namba moja katika bajeti ya 20162017.

huko nyuma mwalimu nyerere alibaini kuwa watu wa vijijini wakikaa wametawanyika anashindwa kuwahudumia akaanzisha mpango wa kuwakusanya watanzania katika vijiji ili awaweke pamoja awahudumie. mantiki ya kupanga mji ni hiyo hiyo. lakini leo hii tunashindwa kudhibiti miji yetu, wataalamu wanashindwa kubaini hili na hawa wanajikita katika kutengeneza fedha kutoka katika concept ya kupanga mji hivyo wao wanaona kuhalalisha makazi holela ndio jukumu lao. kama nina kiwanja katika makazi holela eti ninyi wao niwape fedha waje kupima kiwanja changu na kunipa hati na hivyo ndivyo wanavyopanga mji!!!!!!. au wanachukua kipande cha ardhi eti wanapima huku watu hawa wanaopimiwa sometimes wanachangamoto za kupata huduma kuliko hata makazi holela kutokana na location.

baada ya vitambulisho na arrangement ya miji yetu nilitegemea kipaumbele cha tatu kingekuwa kuwawezesha watanzania kujihudumia na hizo project tatu kubwa zingetosha kuwa kipaumbele kwa mwaka wa 2016/2017 maana bajeti haituwezeshi kufanya kila kitu na mengine inekuwa kusukuma wizara ziendelee kuboresha utendaji.

je wewe ulitegemea nini?
nilitegemea serikali hii kutambua kuwa kazi ya

serikali ya awamu ya tano imeonekana kubaini
Tehe tehe wewe sawa na anayeenda kupanda mbegu huku ameshika kapu la kuvunia.
 
Back
Top Bottom