Mie sikani, mauno ulinikatia na mchezo waujua! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mie sikani, mauno ulinikatia na mchezo waujua!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Rutashubanyuma, May 25, 2012.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,715
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280
  Msema ukweli kipenzi cha Muumba hivyo sikani!
  Ya kuwa mie nawe tulikuwa beneti sana tena sana!
  Nakumbuka tulivyokutanishwa na aliyetutambulisha!
  Unyenyekevu wako ulinikoga na Kiswahili kuniyeyuka!
  Mie sikani mauno ulinikatia na mchezo waujua!

  Haba haba hujaza kibaba na penzi la kasi tulilifukizia
  Hapa na pale tukajikuta tumo ndani ya lindi la mahaba
  Bila ya kutarajia tukajikuta kitanda twalala sote bila mbinde
  Huko tulinogewa na hata kusahau kuwekana sawa ya kesho
  Mie sikani mauno ulinikatia na mchezo waujua!

  Kesho na kesho kutwa tuliiweka kapuni bila kukusudia
  Bila ya kuipangilia mie nilijionea sawa na hata wewe vivyo
  Hapa na pale mjuaji akaja na kutumbukia mawazoni mwangu
  Kauli yake ilinitikisa na kesho yetu tukaipangilia bila zengwe!
  Mie sikani mauno ulinikatia na mchezo waujua!  Kosa langu nielimishe hadi sasa kuniita mdanganyifu.
  Hakuna ahadi niliyokupa au hata wewe kunipatia pia
  Yawaje sasa udai umetapeliwa khali hatuna makubaliano?
  Manung'uniko yako yamenifikia lakini mwenzio kakuwahi!
  Mie sikani mauno ulinikatia na mchezo waujua!


  Mengi unazoza lakini yote ni tisa tu hakuna jawabu.
  Kama ungelikuwa makini ungelinitonya juu ya kesho yetu.
  Mie nilidhani tunapita tu na hivyo sikukutilia maanani
  Mbona mwenzio aling'aka na kutaka ajue yatakayomsibu?
  Mie sikani mauno ulinikatia na mchezo waujua!
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Kasheshe kweli Mkuu na Methali zako unaniacha hoi.
   
 3. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,659
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Ulimuaminisha sana kiunon kanogewa,
  Si lazima kwa maneno hata vitendo vya changia,
  Na inavyoonekana si mara moja umemuingia,
  Ungesema kama umewahiwa malalamiko hayo yasingetokea.
   
 4. d

  debito JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Duh! Mkuu mi mpitaji tu
   
 5. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mauno ndo nini jamani?
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Chizi kweli huyo! Yaani hamjajadili contract akakupa cha uvunguni? Some women...
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Ni ugonjwa flani, wewe mtu wa Mungu hauwezi kukupata achana nao
   
 8. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Aisee!
   
 9. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  Mchezo bila mauno sio mchezo Ruta......
   
 10. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  maneno yako yakuhadaa, yalimwacha kazuba, Asijue la kufanya, kesho yake ikifika,chonde chonde ruta, usimtupe mwana.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  So wakati uko naye huyo mnyenyekevu (anayekuTII) mkata nauno, u started seing someone else? Duh!
   
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  sasa wewe ulidhani viuno vya bure bure?
  halafu ulivyomfukuzia si ulimwambia unataka muwe wote maishani?
  iweje umemtosa?
   
 13. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Rutashubanyuma, sasa kama alikukatia mauno kweli unakumbuka uliyo ahidi wakati upo kwenye kazi? anake nijuavyo mim yakikukolea utaahid wewe hata usiyokuwa nayo Asprin kwakuwa wewe ni babu hebu mwambie huyu manakae naskia bibi alikukoleza kweli na mauno yake.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,802
  Likes Received: 2,575
  Trophy Points: 280
  Ni wingi wa buno/uno.
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  May 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,715
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280
  MziziMkavu bila methali na nahau somo halieleweki
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  May 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,715
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280

  Kaunga unafikiri leo nimekulegezea masharti lol.....................utii nao lazim auje na maelekezo ya kesho na kesho kutwa bila y ahayo ujue mambo yanaweza kwenda mrama..........................
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  May 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,715
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280
  Mapi nani kwakwambia ana mtoto wangu?........................lol hii ni simulizi tofauti na ile ya wakati ule
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  May 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,715
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280
  promiseme..mweleze aridhike ya kuwa alinifaidi vya kutosha.........lol
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  May 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,715
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280
  simplemind achana na Bishanga huyo ndiye mkufunzi mkuu wa mauno....lol
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  May 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,715
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280
  gfsonwin basi mweleze anikumbushe bila ya kukumbushia..................lol
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...