Midomo mibaya

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,845
Si ubaya wa umbo la hasha. Wala si tafsiri ya midomo michafu. Uchafu kwa maana ya kutokuwa msafi. Na uchafu kwa maana ya matusi na maneno yasiyo na staha

Tunaishi kwenye jamii ambazo ni jambo la kawaida kusikia kuwa fulani ana mdomo mbaya. Na anaweza kuwa ndugu jamaa rafiki ama hata wewe mwenyewe. Mdomo uliobeba roho hasi. Kuna watu wakisema nimeota msiba. Basi jua utatokea msiba.. Ni afadhali asiseme. Kuna mtu akisema kutatokea jambo baya basi ni lazima iwe

Je, ni nguvu gani hii? Kuna nini ndani yake? Kuna uhalisia na uhusiano gani kati ya matamshi yake na kile kitakachotokea kwa usahihi wake?

Maneno huumba roho lakini kuna midomo pia ina mapepo wabaya.. Mtu mwenye mdomo wa aina hiyo akikunenea mabaya lazima udhurike

Tuna mapepo na roho hasi tumebeba miilini mwetu. Yapo ya kila aina
Ya roho mbaya
Ya uzinzi
Ya ulevi
Ya ubatili
Ya umbea
Ya kujisifu
Ya uchawi, ushirikina na ulozi nknk
Yote haya tumeyabeba maungoni mwetu... Na tunapoyapa nafasi kidogo tu basi huitumia vilivyo.

Na yanatumiaje vilivyo? Kupitia milango mitano ya fahamu na katika yote hiyo inayokamilisha mambo ni kauli.

Chunga sana kauli kwakuwa mkono hauwezi kukufikia mbali lakini kauli husafiri na kubeba Roho ya maangamizi.

Kauli ina nguvu kauli ina uhai na ndio maana kwenye mambo mengi huambiwa toa kauli yako ya mwisho. Maandishi yapo lakini maandishi bila kauli si chochote. Viapo laana na manuizi vyote hivi vimebeba roho.

Epukana na mtu mwenye mdomo mbaya ni hatari kuliko mchawi wa tunguli.
 
Si ubaya wa umbo la hasha..... Wala si tafsiri ya midomo michafu... Uchafu kwa maana ya kutokuwa msafi... Na uchafu kwa maana ya matusi na maneno yasiyo na staha

Tunaishi kwenye jamii ambazo ni jambo la kawaida kusikia kuwa fulani ana mdomo mbaya.. Na anaweza kuwa ndugu jamaa rafiki ama hata wewe
Fafanua kidogo mkuu huenda wanatufaa ktk kubashiri yajayo pia kuna wengine husema mtu ambaye aliota meno ya juu kabla ya chini akisema jambo lazima liwe,hili ni liroho pia? Au imekaaje?
 
Fafanua kidogo mkuu huenda wanatufaa ktk kubashiri yajayo pia kuna wengine husema mtu ambaye aliota meno ya juu kabla ya chini akisema jambo lazima liwe,hili ni liroho pia? Au imekaaje?
Hili liko kiimani zaidi uhalisia ukiwa kwenye asilimia chache.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom