Microsoft yatoa punguzo la 40%

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
98,089
Points
2,000

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
98,089 2,000
Microsoft yatoa punguzo la 40%

na Tamali Vullu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

KATIKA juhudi za kuwezesha wananchi kununua vifaa vya Teknolojia ya Habari (ICT) nchini, Kampuni ya Microsoft, imetangaza kutoa punguzo la asilimia 40 ya vifaa vyake kwa watumiaji wa nyumbani na wanafunzi.

Meneja wa Microsoft Kusini Mashariki mwa Afrika, Ian Joule, alisema mwishoni mwa wiki kuwa kampuni hiyo imepunguza gharama za kununua ikiwa ni mkakati wao wa kuwezesha watu wa hali ya chini kuweza kumudu bei hizo.

“Punguzo hili la bei kwa ajili ya programu ya Microsoft Office 2007, ili kuwawezesha watumiaji wa nyumbani na wanafunzi kuitumia katika shughuli zao za kila siku,” alisema Joule.

Alisema chini ya progarmu hiyo ya kupunguza gharama, Kampuni ya Microsoft itaendelea kubuni programu nyinigine ili kuweza wananchi kunufaika na kutumia teknolojia na kutumia programu halali za kompyuta.

“Nimefurahishwa na kitendo cha Microsoft kupunguza bei za software hasa zikiwalenga wanafunzi,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Yustus Mkinga.

“Katika kuendelea kulinda hakimiliki, COSOTA inakubaliana na upunguzaji wa gharama kwa programu za Microsoft Office 2007 kwa watumiaji wa nyummbani na wanafunzi,” alisema Mkinga na kuongeza kupatikana kwa programu halisi kwa bei nafuu na elimu kutachangia dunia kuweza kupambana na watu wanaoiga kazi za watu.

Meneja Masoko wa Microsoft Kusini Mashariki mwa Afrika, David Ndungu, alisema kampuni hiyo pia inashirikiana na wadau wake, ili kuhakikisha programu halisi za Microsoft Office zinapatikana mahali popote ambako zinauzwa kompyuta.

“Pamoja na hayo, tunaongeza upatikanaji wa bidhaa zetu sokoni kwa kuongeza idadi ya wauzaji,” alisema.

Ndungu, alisema progamu ya Microsoft Office 2007 imetengenezwa maalumu kwa ajili ya watumiaji wa nyumbani na wanafunzi, ili waweze kutengeneza nyaraka mbalimbali.

Programu hiyo inajumuisha, programu ya Microsoft Office Word 2007, Microsoft Office Excel 2007, Microsoft Office PowerPoint 2007 na Microsoft Office One Note 2007.
 
LazyDog

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Messages
2,478
Points
1,195

LazyDog

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2008
2,478 1,195
Microsoft yatoa punguzo la 40%

na Tamali Vullu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

KATIKA juhudi za kuwezesha wananchi kununua vifaa vya Teknolojia ya Habari (ICT) nchini, Kampuni ya Microsoft, imetangaza kutoa punguzo la asilimia 40 ya vifaa vyake kwa watumiaji wa nyumbani na wanafunzi.

Meneja wa Microsoft Kusini Mashariki mwa Afrika, Ian Joule, alisema mwishoni mwa wiki kuwa kampuni hiyo imepunguza gharama za kununua ikiwa ni mkakati wao wa kuwezesha watu wa hali ya chini kuweza kumudu bei hizo.

"Punguzo hili la bei kwa ajili ya programu ya Microsoft Office 2007, ili kuwawezesha watumiaji wa nyumbani na wanafunzi kuitumia katika shughuli zao za kila siku," alisema Joule.

Alisema chini ya progarmu hiyo ya kupunguza gharama, Kampuni ya Microsoft itaendelea kubuni programu nyinigine ili kuweza wananchi kunufaika na kutumia teknolojia na kutumia programu halali za kompyuta.

"Nimefurahishwa na kitendo cha Microsoft kupunguza bei za software hasa zikiwalenga wanafunzi," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Yustus Mkinga.

"Katika kuendelea kulinda hakimiliki, COSOTA inakubaliana na upunguzaji wa gharama kwa programu za Microsoft Office 2007 kwa watumiaji wa nyummbani na wanafunzi," alisema Mkinga na kuongeza kupatikana kwa programu halisi kwa bei nafuu na elimu kutachangia dunia kuweza kupambana na watu wanaoiga kazi za watu.

Meneja Masoko wa Microsoft Kusini Mashariki mwa Afrika, David Ndungu, alisema kampuni hiyo pia inashirikiana na wadau wake, ili kuhakikisha programu halisi za Microsoft Office zinapatikana mahali popote ambako zinauzwa kompyuta.

"Pamoja na hayo, tunaongeza upatikanaji wa bidhaa zetu sokoni kwa kuongeza idadi ya wauzaji," alisema.

Ndungu, alisema progamu ya Microsoft Office 2007 imetengenezwa maalumu kwa ajili ya watumiaji wa nyumbani na wanafunzi, ili waweze kutengeneza nyaraka mbalimbali.

Programu hiyo inajumuisha, programu ya Microsoft Office Word 2007, Microsoft Office Excel 2007, Microsoft Office PowerPoint 2007 na Microsoft Office One Note 2007.Yeah right! Leo ndio mmekumbuka kufanya haya?!.
 
Forum statistics

Threads 1,344,378
Members 515,441
Posts 32,818,494
Top