Apple walipointroduce retina display walikuwa na imani ndio display ambayo ndio mwisho wa binadamu kudifferenciate between pixels kwenye kioo yaani kuiona pixel moja kwenye kioo kwa macho ya kawaida ni ngumu, suala kawa nini Apple kastuck kwenye retina display hajaenda kwenye 4K kama wengine, Apple anapodesign hardware zake huwa anazioptimize na OS yake (iOS), kutokana na udogo wa betri ya simu yake tuchukulie iPhone 7 yenye betri 1960mAh na kioo cha 4.7" ukaiwekeea 4K display efficiency ya utumiaji betri itapungua si ajabu ukakuta simu inakaa na betri hata masaa manne au matatu, kumbuka the more display resolution the more battery usage na usishangae ni kwa nini simu za Android zinazopack battery zaidi ya 3000mAh lakini matumizi yake hayana utofauti mkubwa na simu za Apple ambazo zinatumia battery za 1900mAh. Hata mimi nawaunga mkono Apple kwenye suala la display, simu ikiwa na display ya HD au FHD inatosha kabisa hizi 4K nahisi tuzipeleke kwenye PC na TV
Mkuu, kwenye suala la technology kila kampuni ina sehemu yake ya kujidai kama pioneer, na kuigana ni muhimu kama hicho kitu kina manufaa kwake kutokana na demand ya soko lake, water and dust resistant kaanzisha Sony kama sikosei hata huyo samsung kuiga kwa Sony, kwa hiyo usishangae Apple naye kuiga