Microsoft Mwaka Huu

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Nipo mbele ya komputa nasoma mambo kadhaa kuhusu bidhaa za microsoft , Kama Office , operating systems na nyingine nyingi tu , Lakini natilia mkazo katika operating system haswa Windows 2000 ,Xp, Server 2003 pamoja na Vista kisha bidhaa za Office kama Office XP , 2003 , 2007 Pamoja na nyingine nyingi zinazotumika sehemu kadha kwa kadha .

Nakutana na habari kuhusu Microsoft Kuja na Antivirus kwa ajili ya bidhaa zake , nakumbuka zamani kidogo kampuni hii ya microsoft iliwahi kupandishana kizimbani na kampuni kadhaa za Antivirus , kisha ilipandishana kizimbani na kampuni ya Sun sijui sasa antivirus hiyo ikitoka italeta madhara kwa kampuni zingine au la ngoja tuone lakini upo uwezekano wa kuleta mabadiliko makubwa .

Watu sasa wameunganishwa na vitu vingi sana wanavyobeba mkononi kama simu za mkono , flash , digital camera na alarm na kadhalika , watu hawa wanataka sasa antivirus inayoweza kuwakinga wasidhurike na vyote hivyo akiwa na simu akiichomeka katika komputa yake basi antivirus ifanye kazi yake , au digital kamera au alarm za magari

Kama unavyojua kwa sasa Microsoft iko katika wakati mgumu kidogo baada ya Search engine yake kupelekwa puta na Google , wakaja na internet explorer 8 hii nayo kwa inapelekwa puta na firefox , pamoja na chrome bidhaa mpya ya Google na pia kuna browser fulani inaitwa Flock , ukiwa na flock kila unachotaka kufanya basi kiko humo na imeunganishwa na vitu vingi muhimu kuanzia tovuti za habari na zingine nyingi nzuri nzuri .

Nimeachana na mambo hayo sasa naangalia operating system mwaka jana niliwahi kutumia Windows 2003 server cd nikaweka katika computer moja nikaisajili baada ya muda nikaja kuitumia sehemu ingine ikafanya kazi na nikaisajili ikafanya kazi kama kawaida tu katika licence agreement haikutakiwa iwe hivi sikuishia hapo nilikuwa kuweka katika kumbu kumbu

Kila ninaposoma kuhusu bidhaa za microsoft narudi katika kumbu kumbu hizi , mwaka huu nimefanya kazi sana na windows vista wakati una install windows vista inakupa nafasi kama unataka kuweka product key baadaye ili uendelee na shuguli zako na itakaa kwa siku 30 ndio ije kujifunga sasa kwa kutumia njia hii watu wanaotumia windows vista wanapata muda muafaka wa kutafuta crack na kuweza kufanya activation na tatizo la windows vista nimeona moja Haina njia nzuri ya kuverify product kama ilivyo WGA kwa windows xp -- sijui microsoft walijisahau nini katika hili .

Kwa mtindo huu sasa hata ukiweka Namba ambayo ni bandia itaendelea kufanya kazi tu kwa siku hizi tajwa juu unaweza kuchomeka katika internet na unafanya kazi zako kama kawaida na updates zote unapata , programu yoyote unaweza kuweka na kufanya updates kwa siku hizo 30 kweli mwaka huu kazi ipo si ndogo .

Nimeona baadhi ya CD za windows xp zilizokuwa Customized zina internet explorer 7 au 8 pamoja na media player 11 hizi kwa kawaida zinakubali kuwa installed mpaka ukisha register product key zako ila zipo cd zinafanya kazi kwahiyo hii WGA haina maana tena na ni ngumu sana mtu kufanya kukuru kakara zingine

Natamani Ndoto zangu ziwe kweli na Microsoft ianze mwaka ujao kwa kishindo kwa kuzindua hiyo antivirus bomba ya MORO , halafu ituletaa update ya internet explorer 7 kwa sababu 8 imeleta matatizo kidogo kwa baadhi ya watu , sijui Windows Defender itakuwa hewani tena , na katika operating system tumechoka kubypass product key za windows vista wawe na suluhisho kuhusu hili katika mtandao kuna Crack nyingi sasa za windows vista kwahiyo watu wana bypass na kuactivate kuirahisi sana kuliko windows XP .

Usiku mwema

Mwaka unaisha huu tunaangalia mambo mbali mbali ya mwaka huu

Kwaheri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom