Michirizi ya Damu

Michirizi ya Damu

IMG_1680.JPG



Welcome Ramadhan..........
 
SEHEMU YA 127

Muda huo Mustapha alikuwa pembeni yao, macho yake yalikuwa katika saa aliyokuwa ameivaa. Huku zikiwa zimebaki dakika tatu hata kabla ya treni kufika, Mwarabu mmoja akafika mahali hapo na kusimama pembeni ya Mustapha na kuanza kuzungumza naye.

Fareed alisikika lakini hakufahamu watu hao walikuwa wakizungumzia mambo gani. Mwanaume huyo aliyekuwa akizungumza na Fareed alikuwa na kifaa kama rimoti mkononi mwake, hakujua kazi ya hicho ila kwa jinsi kilivyoonekana, alijua kwamba hakikuwa kitu kizuri.

“Guys! I think this is our last time to meet each other! Have the good journey,” (jamani! Nafikiri huu ndiyo mara ya mwisho kuonana sisi nanyi! Muwe na safari njema) alisema Mustapha huku akiwaangalia wanaume hao.

“Thank you sir,” (ahsante bwana mkubwa)
Mustapha na yule mwanaume hawakutaka kusubiri mahali hapo, wakaondoka mahali hapo na kuelekea nje ya kituo hicho. Fareed na wenzake wakabaki kituoni hapo wakiwa na mabegi yale yaliyokuwa na mabomu.

Bado kichwa chake kilikuwa na mawazo tele, alikuwa na maswali mfululizo juu ya kile kilichokuwa ndani ya mabegi yale. Hakutaka kuridhika, akawaaga wenzake kwamba anakwenda chooni kujisaidia na angarudi muda si mrefu.

Akaondoka harakaharaka, alipofika chooni, kitu cha kwanza kilikuwa ni kuliweka chini lile begi, zipu zilifungwa kwa kufuli ndogo alichokifanya ni kulichana, ndani, akakutana na mfuko mweusi na alipoufungua, macho yake yakatua katika bomu moja kubwa lililokuwa likiwaka kitaa chekundu.

“Mungu wangu!” alisema kwa mshtuko, ghafla akasikia huko nje treni ikiwa inaingia, muda ambao bomu hilo lilitakiwa kulipuliwa.
 
SEHEMU YA 128

Mustapha na mwenzake wakatoka nje, wakaelekea kwenye gari lao huku akiwa na furaha tele. Moyo wake aliona kwamba alifanikiwa katika kile walichokuwa wamekipanga kwamba mabomu yalifika salama nchini Marekani na muda huo yalikuwa kituoni.

Wakalifuata gari lao na kutulia humo. Mudda wote macho yao yalikuwa katika saa zao huku masikio yao yakisikiliza kwa makini kile kilichokuwa kikiendelea katika kituo kile.

Kama treni ingekuwa inaingia kituoni hapo, kusingekuwa na ugumu wa kujua hilo, wangesikia mlio wake na hivyo kukaa kwa sekunde chache, litakaposimama tu waweze kulipua bomu hilo.

“Muda unakwenda tu! Subiri tusubiri,” alisema Mustapha.
Walisubiri kwa dakika tatu tu wakasikia treni likiwa linaingia, hawakutaka kuwa na presha kubwa, walisubiri mpaka waliposikia limesimama na abiria kuanza kuteremka.

Mwanaume aliyekuwa na Mustapha akachukua kirimoti kile kwa lengo la kulipua mabomu yale.
“في سبيل الله,” (kwa ajili ya Mungu) alisema mwanaume yule kisha kubonyeza kitufe kile. “Puuuuuuuu…..” ilisikika milio ya mabomu makubwa matatu yaliyopuka ndani ya kituo hicho.

**** Bilionea Belleck alikuwa na kila kitu, kila siku alikuwa akikusanya fedha nyingi kutokana na biashara mbalimbali alizokuwa akizifanya. Aliingiza kiasi kikubwa cha fedha na kila siku katika maisha yake aliendelea kuogelea kwenye dimbi kubwa la utajiri.

Alipendwa kutokana na sura nzuri aliyokuwa nayo, alipendwa kutokana na utajiri mkubwa aliokuwa nao. Kila siku kazi yake ilikuwa ni kubadilisha wanawake, alikuwa akienda kununua wanawake barabarani na kwenda kufanya nao mapenzi.

Aliyazoea maisha hayo, hakutaka kutulia nyumbani, alikuwa mtu wa safari, kusafiri kuelekea Ufaransa, Uholanzi, Italia, kila alipokuwa ilikuwa ni lazima kulala na wanawake kitu ambacho alipenda kufanya katika maisha yake.

Hakumfikiria mtu aliyeitwa Fareed, kwake, alijua kabisa mtu huyo hakuwepo katika uso wa dunia, alikumbuka jinsi alivyowatuma watu na kwenda kumtupa baharini, tena hakutupwa huku wakiwa watu hao, alitupwa huku akishuhudia kitu kilichompa uhakika kwamba mtu huyo alikuwa chakula cha samaki mpaka muda huo.nonozephrineUmechanganya mafaili hapa aliemtupa baharini Fareed ni Keith na cyo Belleck
 
Back
Top Bottom