Mi nakumbuka kucheza chandimu,tulikuwa hatufuati ile sheria ya watu 11 kila upande,ilikuwa ilimradi mlingane idadi.Ukifika umechelewa,huingii uwanjani mpaka upate pair yako ya timu pinzani,kwa kuwa hatukuwa na jersey,tulikuwa tunapeana zamu,sisi leo tunavaa mashati ninyi mtacheza bare chest.Mtu akishika mpira kwa mkono tunasema enzi(hands),inapigwa faulo.Tulikuwa tuna aina tatu za wachezaji,kipa anakaa golini,mabeki wanakaa mbele ya kipa na ma-forward wao ni daima mbele,nyuma mwiko hata timu ikizidiwa.Mpira sio dakika 90 tu,ni mpaka jua lizame,dah!I miss my childhood moments.