Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Mbunge azimwagia vifaa timu za magereza, polisi


na Sitta Tumma, Mwanza


amka2.gif
MBUNGE wa Musoma mjini, mkoani Mara, Vincent Nyerere (CHADEMA), amekabidhi vifaa mbali mbali vya michezo kwa timu za jeshi la Magereza
na polisi mjini hapa, ikiwa ni katika lengo la kuboresha sekta hiyo bila kujali makundi.
Nyerere ambaye amekuwa akipigania ukuaji na ufufuaji wa vipaji vya michezo kwa vijana jimboni humo, alikabidhi vifaa hivyo juzi kwa uongozi wa magereza na polisi Musoma.
Vifaa vilivyotolewa na mbunge huyo ni pamoja na seti.
mbili na mipira miwili kwa timu mbili za Jeshi la Magereza, na timu mbili pia za Jeshi la Polisi mjini hapa na king'amuzi cha DSTV cha kunasa chaneli nyingi za michezo duniani, ambapo misaada kama hiyo imeanza kusambazwa katika kata zote 13 za jimbo hilo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo vya michezo, Nyerere ambaye ameanza kwa kasi kubwa kutekeleza ahadi zake jimboni humo alisema, msaada huo utazisaidia timu za majeshi hayo kufanya mazoezi na kutoa upinzani mkali kwa mahasimu wao.
Alisema, siku zote michezo ni furaha, ajira na inasaidia pia kujenga mwili na urafiki hivyo ameshawishika kutoa vifaa kwa timu hizo ili kuchochea zaidi upinzani wa kimichezo na hatimaye Musoma kuweza kuzalisha wachezaji wa kimataifa.
"Niliahidi kusaidia michezo, na ahadi zangu nimeshaanza kutekeleza, vifaa hivi vya michezo naamini vitasaidia sana kuchochea upinzani latika timu zenu kwani lengo hasa ni kutaka Musoma tuwe na wachezaji wa kimataifa kama walivyo kina Essien (Michael), Nasri (Samir), Drogba (Didier) na Beckham (David)…naomba tushirikiane katika kulijenga taifa letu," alisema Nyerere.
Akizungumza baada ya kupokea msaada wa vifaa hivyo, Mkuu wa Gereza la Musoma, Patrick Obwero Kang'a (RPO), alieleza kufurahishwa na hatua ya mbunge wao huyo kuzikumbuka timu za magereza na polisi.
Alisema, msaada huo wa seti mbili na mipira utawatia moyo wachezaji wa timu husika, hivyo alimuomba Nyerere aendelee na moyo huo, ikiwa ni pamoja na kuvisaidia vilabu na timu nyingine jimboni humo na mkoa wa Mara kwa ujumla.
 
COREFA yaichinjia baharini Bagamoyo Friends


na Dina Ismail


amka2.gif
KAMATI ya Rufaa ya Chama cha soka mkoa wa Pwani (COREFA), imetupilia mbali rufaa ya timu ya Bagamoyo Friends iliyokuwa ikipinga maamuzi ya Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi iliyotupilia mbali rufaa yao dhidi ya timu ya Maili Moja United ikidai katika mchezo nambari 4, wa fainali ya kombe la taifa ngazi ya mkoa wa Pwani, uliochezwa Januari 8, mwaka huu, katika uwanja wa Ikwiriri, Rufiji, Maili Moja ilichezesha baadhi ya wachezaji ambao usajili wao haukuzingatia sheria na kanuni za mashindano.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Corefa inasema kuwa kikao cha kamati hiyo kilichoketi juzi jijini Dar es salaam kikiongozwa na Mwenyekiti Mark Shayo, Makamu wake Joseph Mpuya ambao kitaaluma wote ni wanasheria na katibu Salehe Lubawa, waliitangaza rasmi timu ya Maili Moja United kuwa mabingwa wa soka wa mkoa wa Pwani msimu wa mwaka 2011/12.
Mwenyekiti Shayo kamati ilitupilia mbali rufaa ya Bagamoyo Friends kutokana na kuwa barua waliyoiwasilisha katika kamati yake kuwa kama ya pingamizi hivyo, kukosa sifa ya kuwa rufaa halali inayoweza kusikilizwa na kamati yake.
"Barua hiyo ilijaa mapungufu ambayo ni pamoja na kutokufuata kanuni ambazo zingeifanya iwe rufani kama inavyoelekezwa na kanuni ya 16 na 17 ya mashindano ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF), kamati yangu ilizingatia maelekezo ya kanuni ya 16 (C) kwa kuwa barua au rufaa hiyo haikuwa na vielelezo wala haikulipiwa ada hivyo, barua hiyo ni batili, kwa kuzingatia sheria tukalazimika kuitupilia mbali," alisema Shayo.
Aliongeza kuwa iwapo rufaa ya Baga Friends ingekuwa halali bado kamati ingeitupilia mbali kwani, maelezo ya barua hiyo yanaelezea kupinga maamuzi ya kamati ya rufaa ya Corefa ambayo haijawahi kukaa kujadili na kutoa maamuzi yoyote kuhusu pingamizi ama rufaa yoyote kutoka timu hiyo ya Baga Friends.
Kwa upande wa rufaa ya timu ya Maili Moja, kupinga maamuzi ya Kamati ya Nidhamu na usuluhishi kufuta matokeo ya mchezo kati yake na Baga Friends ikidaiwa kuchezesha wachezaji ambao usajili wao haukuwa halali, Shayo alisema kamati yake ilikubaliana nayo.
Alisema katika maamuzi, kamati ilizingatia kanuni ya 34 ya kanuni ya ligi ya taifa ya TFF inayomzuia mchezaji kucheza klabu yoyote ya ligi mpaka usajili wake uwe umethibitishwa na chama cha soka ngazi husika ama TFF ambacho kabla ya kumthibitisha mchezaji kitatoa siku 7 hadi 14 kuwasilisha malalamiko ama pingamizi kwa maandishi kuhusu usajili tangu kutangazwa kwa majina ya wachezaji katika klabu husika.
Alisema uthibitisho utakaotolewa na chama ngazi husika au TFF ndio utakuwa wa mwisho na havitapokea rufaa yoyote inayohusu rufaa ya usajili wa mchezaji ambaye hakuwekewa pingamizi mwanzoni isipokuwa, iwapo klabu itafanya udanganyifu kwa jina la mchezaji.
 
Wachezaji 33 waunda Kindai Shooting


na Jumbe Ismailly, Singida


amka2.gif
CHAMA cha soka mkoani Singida (SIREFA) kimetangaza kikosi cha wachezaji 33 ambao wataunda timu ya mkoa wa Singida ‘Kindai Shooting Stars' watakaouwakilisha mkoa huo kwenye mashindano ya kombe la taifa ‘Kili Taifa Cup' mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na katibu wa Sirefa, Hussein Mwamba, wachezaji haona na timu walizotoka kwenye mabano kuwa ni pamoja na makipa Juma Majojo (Mughanga), Jacksoni Muna (Aston Villa) na Mbutu (Irisya).
Wengine ni Salvatory Kibauri (Kijota FC), Buruhani Haji (Mughanga), Marco Mwakifamba (Kisimba), Yahaya Ramadhan (Aston Villa), Hamis Hamis (Aston Villa), Charles Msuke (Samaria), Musa Haruna (Mughanga), Joramu Kimolo (Samaria) na Musa Boazi (Reli), Ismaili Kisuke (Mughanga), Nasoro
Issa (Aston Villa), Haji Hamis (Iguguno), Henry Jikito (Kisimba) na George Martin (Computer).
Pia wamo Peter Masaga (Samaria), Abdallah Sabebe (Mughanga), Dotto Michael (Mughanga), Samwel Michael (Kisimba), Hassani Hassani (Reli), Shafii Daudi, David Marco (Polisi Singida) na Msengi Selemani.
Aidha wachezaji wengine ambao wanatoka nje ya mkoa kuwa ni pamoja na Amri Sambiga (Polisi Tanzania), Paschal Maige (Polisi Tanzania), Agaton (U20 Polisi Tanzania),Noeli Luka (African Lyon), Rajabu Mohamed (African Lyon), Hassan Hatibu (U20 Simba) na Zuberi Ubwa (African Lyon)
 
Hongera Simba SC kuwavua gamba mafisadi wa jengo

ban_tahariri.jpg

amka2.gif
MWENYEKITI wa klabu ya Simba Alhaj Ismail Aden Rage juzi alitangaza klabu yake kusitisha mikataba ya wapangaji wote wa jengo lao la makao makuu lililo mtaa wa Msimbazi kwa kutoa notisi hadi Aprili 30.
Rage, alisema hatua hiyo inafuatia kuwepo kwa baadhi ya wajanja ambao waliingia mkataba kinyemela kwa kusaini mkataba mpya ambao ulikuwa unakwisha mwaka 2014 badala ya ule wa awali unaomalizika Aprili 30 mwaka huu.
Kupitia mikataba hiyo hewa baadhi ya wajanja wamekuwa wakivuna mamilioni kwa mgongo wa vitega uchumi hivyo huku klabu ikiendelea kuwa ombaomba na kujikusanyia kiasi cha shilingi bil.17.
Tanzania Daima tunachukua fursa hii kuwapongeza viongozi wa klabu ya Simba kwa kuvaa ujasiri huo kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakitembeza bakuli kwa akili ya masuala mbalimbali ya kuendesha timu wakati fedha zinazopatikana katika vitega uchumi hivyo zingewawezesha kutatua shida zao.
Inasikitisha sana kwani wazee wa zamani wa klabu hiyo kwa uchungu waliokuwa nao walijikusanya na kujenga jengo hilo kwalo leo hii baadhi ya wajanja wananenepa matumbo na kuacha klabu ikiaibika.
Pamoja na hatua hiyo, tunapenda kuwashauri viongozi wa Simba wasiishie kuvunja mikataba bali wawasiliane na wanasheria wao kuona uwezekano wa kuwashtaki wale walioamua kuingia mikataba kinyemela na kuvuna mamilioni ya shilingi.
Sisi Tanzania Daima tunaamini huo ni wizi wa kuaminika ambao unapaswa kulaaniwa na kupigwa vita kwa nguvu zote katika medani ya michezo kwani unarudisha maendeleo ya klabu nyuma.
Ni vema uongozi wa Simba ukaanzisha utaratibu utakaokuwa wazi na ambao utajulikana na viongozi watakaoingia madarakani wakati wowote tofauti na hii siri iliyokuwepo kwenye mikataba hii ambayo ilisababisha viongozi waliopita wasibaini kuibiwa huko.
Sisi Tanzania Daima tumelazimika kutoa pongezi hizi kutokana na kuridhishwa kwetu na ushupavu uliofanywa na viongozi wa sasa wa Simba chini Al hajj Ismail Aden Rage ambaye amekuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya timu hiyo.
Hii ni kutokana na kwamba walioingia mikataba hii kinyemela ni wana Simba wenzao na huenda ndio maana viongozi waliopita walishindwa kuchukua hatua stahiki kwa sababu ya kulindana au kuoneana haya.
Kwa waliokuwa wapangaji kwenye klabu hiyo ni vema kutoa ushirikiano kwa viongozi wa Simba na wakubali kuingia nao mikataba mipya kama bado wanataka kuendelea kufanya kazi hapo ili kodi zao zisaidie kuijenga Simba.
Pia tuchukue fursa hii kuwakumbusha wanachama wa Simba kuwa jukumu la kulinda na kutetea mali za klabu hiyo liko mikononi mwao, hivyo kila wanapoona hujuma inafanyika ni vyema wakaufahamisha uongozi wao kungali na mapema kuliko kusubiri mambo yaharibike.
Kama alivyosema Rage ‘kuanzia sasa kuibiwa basi' Tanzania Daima tunaamini mapambano hayo na mafisadi wa mali za Simba yaliyoanzishwa na uongozi wake yataendelea kwa nguvu zote, huku tukiwashauri viongozi wa timu nyingine kuiga mfano huo kwa maendeleo ya michezo nchini.
 
PST, TPBO navyo vijivue gamba
ban.mtazamo.jpg


Salum Mkandemba​

amka2.gif
APRILI 16 mwaka huu, wapenzi, mashabiki na wadau wa mchezo wa ngumi, walikuwa ndani ya ukumbi wa PTA ulio ndani ya viwanja vya Mwalimu Nyerere (zamani Sabasaba) kushuhudia pambano kali lisilo la ubingwa la uzito wa kilo 72 la mchezo huo baina ya mabondia gumzo nchini Japhet Kaseba na Mada Maugo.
Ni pambano lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wake, kutokana na ukali wa mabondia husika, huku tambo za hapa na pale na kunyoosheana vidole vikichagiza uhasama, uliowalazimisha mashabiki kusubiri kujua nani atafanya nini siku hiyo. Wakajazana kwa wingi pale PTA, wakiamini kuweza kuona na kupata kile walichotarajia.
Pambano hilo lilichezeshwa na mwamuzi John Chaku, ambaye alimtangaza bondia Mada Maugo mshindi, kwa kile kilichodaiwa kuwa Japhet Kaseba kushindwa kuendelea na mtifuano huo kwa kuvua glovu zake – kitendo kinachotafsiriwa katika mchezo huo kama ni ‘kujisalimisha' kwa kushindwa kuendelea na mchezo.
Kabla ya kumpa ushindi Maugo kwa kitendo hicho, Chaku alisimamisha pambano hilo katika raundi hiyo baada ya Kaseba kumkwatua mpinzani wake. Wakati akijaribu kumpa mwongozo Kaseba juu ya kitendo alichomfanyia mwenzake, inadaiwa bingwa huyo wa mataji mawili ya dunia wa Kick-Boaxing (WKL na WKC), alivua glovu na kuhesabika kama ‘aliyejitoa' mchezoni.
Wakati mwamuzi huyo akimuonya Kaseba, bondia huyo naye alikuwa akilalamika kwa mwamuzi juu ya vitendo sawa na hivyo anavyofanyiwa na Maugo, bila kuonywa wala kupewa mwongozo wowote. Mashabiki wake (Kaseba) wakavamia jukwaa na kulazimisha mchezo kufikia tamati kwa staili hiyo ya aibu kwa mchezo husika.
Si lengo langu kuangalia kwa mapana kile kilichojiri siku ya pambano hilo, bali kile kilichokuja kutamkwa na Kaseba katika mahojiano ya kwanza kwangu mimi kuyasikia tangu alipodaiwa kuharibu pambano hilo. Awali ikatangazwa kuwa ameamua kuachana na mchezo huo, ili kuepuka aibu.
Mengi yanayofanana na hayo yakasemwa, huku vyombo mbalimbali vya habari vikiandika katika namna unayoweza kuiita ya kishabiki, isiyo na maslahi kwa mchezo huo na wachezaji wake. Hapa ndipo nilipopata hamu kumsikia mwenyewe anasemaje juu ya pambano hilo lililoanza kuzua gumzo mapema, kwa madai ya Kaseba kuzidi uzito.
Kwa watazamaji wa kipindi cha Spoga, kinachorushwa na kipindi cha televisheni cha Mlimani ‘Elimu Kwanza', juzi Jumamosi usiku, watakuwa mashahidi wa kweli wa kile bondia huyo alichozungumza. Katika mahojiano yake na mwenyeji wake Anuary Mkama, Kaseba akakiri kupoteza mechi hiyo kwa hila za waandaaji waliokusudia ‘kumkimbiza' kwenye ulingo wa mchezo huo.
Baadhi ya wadau muhimu wa mchezo huo, vikiwemo vyama, viongozi, mapromota na waandaaji wa mapambano, hawakupendezwa na kitendo cha yeye kukacha ‘Kick-Boxing' na kuingia katika ndondi, hivyo kupanga mikakati ya kuhakikisha wanammaliza. Ushahidi anao na kiasi fulani aliutoa katika mahojiano yale.
Si hivyo tu, Kaseba akaenda mbali zaidi na kubainisha yanayoendelea katika mchezo huo, ambao kwa hapa nyumbani una vyama zaidi ya viwili vinavyousimamia – kitu alichokiona kama moja ya sababu zinazokwamisha mabondia wengi, akiwemo yeye. Kila chama, kiko nyuma ya bondia wake na kitatumia hata hila kuhakikisha anamshinda bondia aliye chini ya chama ama rais fulani.
Akaongeza kuwa uhasama uliopo baina ya PST na TPBO, ni kati ya vikwazo ambavyo yeye anaweza kumudu kuvikwepa na kusonga, lakini tatizo litakuja kwa mabondia wadogo wanaoibukia. Kwa madai yake ambayo nayaunga mkono, ifikie kipindi viongozi wa vyama hivyo wawe na malengo ya kuwapa mafanikio mabondia, sio kujinufaisha kupitia migongo yao.
Kaseba akiwa na bondia wa kike Pendo Njau, akasema kila uchao mchezo huo umekuwa ukipoteza dira na mwelekeo kutokana na viongozi wakuu wa vyama hivyo na wadau wake muhimu, kujiweka ‘ki-maslahi zaidi' kuliko ki-uanamichezo, hali inayochangia ‘kuwakimbiza' sio tu mabondia wasio na ‘watu wao', bali pia wafadhili wanaojitolea kuusaidia mchezo huo.
Ni madai mazito, yaliyobeba uhalisia wa kile kinachoshuhudiwa katika mchezo huo katika siku za karibuni. Vilio vya hujuma vimekuwa vingi, vurugu katika mapambano zimeongezeka na kila aina ya matukio ya aibu yanauandama mchezo. Hapa ndipo mtazamo unaponituma kuwaasa viongozi wa vyama vinavyosimamia mchezo huo, nao kujivua magamba kwa faida ya mchezo.
Katika siku za karibuni – imekuwa ni kitu cha kawaida kumsikia rais wa PST akiiponda mikanda fulani ya ubingwa wa bondia aliye chini ya TPBO – ama wa TPBO kuiponda ya PST na kuiita ya bandia, kwani haitambuliki kitaifa na kimataifa. Pia imekuwa ni kawaida kusikia bondia fulani anapambana na mpinzani kutoka Argentina, lakini ukimchunguza huyo bingwa wa Argentina unapata shaka juu ya uwezo wake.
Tunaupeleka wapi mchezo huu ambao miaka michache iliyopita tuliwashuhudia kina Rashid Matumla, Joseph Marwa na wengineo wakishinda bila kupigiwa kelele za hujuma? Mbona hatukuwahi kumsikia kiongozi yeyote akiita mikanda ya ‘Snack Boy' ni ya bandia? Mbona udanganyifu wa kutuletea mabondia ‘feki' haukuonekana kushamiri? Kulikoni?
Kama mnahisi au kuona kuwa Kaseba anapenda kulalamika, hilo ni juu yenu – lakini mbona haya malalamiko yake yana mashiko makubwa kwetu? Na sio yeye pekee, vilio vya aina yake viko kila pambano linakochezwa, kuna mikakati gani ya kuondoa hali hiyo na kuhakikisha wadau muhimu wakiwemo wafadhili hawasusi kuusaidia mchezo huu?
Lakini wakati nikitamani kuona mabadiliko muhimu yanafanyika kwa manufaa ya mchezo, wachezaji wake na taifa kwa ujumla, nichukue fursa hii kumpongeza Kaseba kwa kila aina ya mchango wake kwa tasnia hiyo. Pia kwa mabondia wengine ambao wanapaswa kuchukulia changamoto hizi kama njia za kuwabaini wababaishaji wanaopaswa kujivua gamba.


h.sep3.gif

Barua pepe; mkandemba@yahoo.com
Simu namba; 0715 339 355 au 0763 339 355
 
h.sep7.gif
master.gif

Katika hili la Samata, lawama TFF haziepukiki
ban.nachonga.jpg


Tullo Chambo​

amka2.gif
KARIBUNI tena katika Jumatatu hii ya Uwanja wa Kuchonga, kama kawaida ni kupeana changamoto za kimichezo ili kuchochea ufanisi katika sekta hii muhimu katika jamii ya Michezo.
Bila shaka mu wazima wa afya njema na mnaendelea na makukumu yenu halali ya kila siku, kwa Wakristo naendelea kuwatakia maadhimisho mema ya sikukuu hii ya Pasaka, ambayo leo ni ‘Jumatatu ya Pasaka',.
Kama ilivyo ada na kwa manufaa ya wale ambao kwa namna moja ama nyingine hatukuwa pamoja Jumatatu iliyopita Uwanjani, tupeane dondoo kidogo ya mada ya iliyopita. Wiki iliyopita Uwanjani, tulizungumzia jinsi ubabaishaji ama ubovu, udhaifu au ulaghai unaofanywa na baadhi ya kampuni ambazo hivi sasa zinajishughulisha na shughuli ya kuandaa mapambano ya ngumi za kulipwa hapa nchini.
Kwa takribani miaka kadhaa sasa, mchezo wa ngumi, hususan zaidi ngumi za kulipwa umekuwa ukijipunguzia mashabiki na hata kukubalika kwake katika jamii ya kitanzania kutokana na kutawaliwa na vitendo visivyo vya kiungwana na ambavyo hata wakati mwingine ni kinyume cha sheria, hivyo kupoteza maana nzima ya michezo.
Katika kuzidi kujipambanua kwa mambo hayo, hivi karibuni ilizidi kujidhihirisha kuwa ngumi za kulipwa ni ubabaishaji mkubwa na mchezo usio wa kistaarabu, baada ya kuzidi kugubikwa na vurugu badala ya furaha na upendo, kama ilivyo dhana nzima ya michezo.
Tulilazimika kulaani tabia hizi katika ngumi za kulipwa pale, kwa mara nyingine iliposhuhudiwa katika pambano lililowakutanisha mabondia maarufu, Mada Maugo na Japhet Kaseba kugubikwa na vurugu na uvunjifu wa amani.
Basi, baada ya ukumbusho huo kwa ufupi, sasa turejee katika mada yetu ya leo. Hivi sasa imeshuhudiwa anga la michezo likigubikwa na masuala ya usajili hivi sasa hapa nchini.
Lakini kubwa lililonisukuma leo, ni suala la malumbano ya uhalali wa klabu ambayo inammiliki mchezaji chipukizi mwenye kipaji, ambaye hivi sasa ametokea kuliteka wimbi la usajili hapa nchini, Mbwana Samatta anayekipiga klabu ya Simba ya jijini Dar es Saalam.
Mchezaji huyu ambaye amecheza nusu msimu katika klabu ya Simba, baada ya kushindwa kuafikiana na uongozi wa klabu hiyo msimu wa kwanza, ambako alikuwa akitokea African Lyon pia ya jijini Dar es Salaam, hivi sasa ameibua malumbano makubwa juu ya uhalali wake, hasa baada ya klabu ya TP Mazembe ya DRC kutangaza kumnyakua kwa kitita cha dola 100,000 za Marekani baada ya kukunwa naye wakati walipokutana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mara baada ya klabu ya Simba kuweka bayana mipango yake ya kumuuza Samatta TP Mazembe, African Lyon ambayo asili yake ni iliyokuwa Mbagala Market, iliibuka na kudai kuwa mchezaji huyo ni wa mali yao na kuwa ndio wenye kustahili kupokea kitita hicho kutoka Mazembe.
Kwanza suala hili unaweza kuliona kama sinema, ambayo hadi sasa ilipofikia, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ndilo muhusika mkuu katika uhalali wa sakata hili lilivyoibuka.
Lakini kwa haraka haraka, embu jiulize, inakuwaje Samatta ambaye TFF ilimpitisha msimu uliopita wa usajili kuwa ni halali kuichezea Simba, leo baada ya kuibuka suala la neema ya ‘faranga' kupitia chipukizi huyu, Lyon inakuja na kudai ni mali yake! Inashangaza sijui wakati wote wa Ligi ilipoanza ilikuwa wapi?
Lakini, wao TFF tayari kupitia katibu mkuu wake, Angetole Osiah imeabainisha kuwa, kwa mujibu wa taratibu zao za usajili, Samatta ni mali ya Simba na kulikuwa kuna kipengele cha makubaliano kati ya klabu hizo mbili, Lyon basi wawasilishe vielelezo katika Shirikisho hilo ili iweze kuapta haki yake.
Inashangaza! Kama TFF inasema Samatta ni hali Simba, inakuwaje kuitaka Lyon iwasilishe vielelezo vingine, ina maana Shirikisho hili ambalo linaendeshwa na watu walioaminika na wadau na kuchaguliwa au kupewa dhamana ya ajira, kufanya kazi kwa ubabaishaji na udhaifu wa hali ya juu.
Bila shaka kanuni, miongozo na sheria za usajili TFF ziko wazi kabisa, leo hii inakuwaje zinashindwa kusimamiwa ipasavyo na kuepuka malumbano yasiyo na maana na hata kulidhalilisha soka la Tanzania na hata ikiwezekana kumuharibia mipango yake mchezaji husika.
Nasisitiza kuna udhaifu mkubwa katika baadhi ya watendaji wa TFF kushindwa kusimamia na kuzitekeleza kanuni na taratibu zinazohusiana na usajili, kutokana na baadhi ya vielelezo ambavyo Lyon ilivianika hewani siku moja tu, baada ya Osiah kuwataka kufanya hivyo.
Lakini kilichonisukuma zaidi kuitupia lawama TFF, ni baada ya kuona baadhi ya nyaraka za Lyon, ambazo kimsingi zinaweza kutowahalalisha kuwa Samatta ni wao asilimia 100, ambazo ndizo zinawapa kiburi cha leo kulianzisha hili, ingwaje sijui nusu msimu mzima tangu aanze kuichezea Simba hawakuwahi kuibuka kudai taratibu hazikukamilishwa au kufuatwa.
Baadhi ya vielelezo hivyo ni kama ile barua ya Novemba 15, 2010 ya Lyon kwa TFF kuomba kibali cha mchezaji huyo kufanya majaribio katika klabu ya Lisboa ya Ureno, kupitia barua yenye kumbukumbu ALFC/KB/TFF/15-2010, ikieleza majaribio yake yaanze Desemba 3 hadi Januari mwaka huu. TFF ilishughulikia suala hili, ambako pia lilikuwa likumuhisha mchezaji mwingine Hamis Thabit yenye kumbukumbu namba TFF/ADM/Vs-10/32, ya Novemba 20, ikiwatambua ni wachezaji wa African Lyon kwa msimu wa 2010/11.
Lakini pia, katika kuonyesha kuwa kulikuwa na longolongo au baadhi ya makubaliano hasa ya malipo hayakuwa yamekamilishwa ndani ya muda muafaka, kulikuwa na vikao vya kumalizia usajili vichochoroni, kimojawapo kikiwa cha Julai 21, 2010 cha viongozi wa Lyon na Simba ambacho kiliwashirikisha Kassim Dewji, Mohamed Dewji ‘Mo', Crencentius Magori, Godfrey Nyange ‘Kaburu' na Mulamu Ng'ambi, ambako inadaiwa ilikubaliwa uandaliwe utaratibu wa kuwalipa kupitia mechi mbili, ambazo ni African Lyon na Simba na ile ya Simba na Yanga, lakini hakuna mafanikio.
Inasikitisha, lakini ndivyo mambo yalivyo, ambako wakati huo Lyon nao hawakudiriki kupaza hewani sauti zao kulalamika kuwa wanadhulumiwa au kuna sheria zimepindishwa. Huu ndio usanii unaobarikiwa na TFF kwa baadhi ya vigogo na hatimaye kuja kuibuka mitafaruku kama hii.
TFF ingekuwa makini katika kusimamia utekelezaji wa kanuni na sheria zake, muda wa usajili ukipita basi umepita na kutoruhusu mikataba ya pembeni ambayo hata yenyewe haikumbuki kuisajili, bila shaka kwa kuwa inafanyika kinyume na taratibu, masuala kama haya ya Samatta yasingeibuka na kuleta matatizo haya.
Haya Lyon mbali ya Samatta, imeibuka na madai mengine kuwa, hata mchezaji mwingine Rashid Gumbo naye si halali kwa Simba bali mali yao, kazi nyingine hiyo, lakini kimsingi ni udhaifu wa usimamizi na utekelezaji ndani ya TFF.
Hivi ikija kuthibitika malalamiko ya Lyon yana hoja hasa kutokana na kujikanganya kwenyewe kwa TFF athari zake mbele zikoje? Sijui kama wanaliona hili, au wanategemea yale yale ya uungwana na kusaidiana kumalizana nje ya taratibu.
Yote kwa yote, ubabaishaji TFF ndio chanzo cha malumbano au matatizo haya ya uhalali wa Samatta na iwe tayari kupokea lolote litakalotokea. Kila la heri, tukutane wiki ijayo.



h.sep3.gif
 
Klabu zalala badala ya kusaka viwanja sasa
ban.blank.jpg


Mwandishi wetu​

amka2.gif
MSIMU wa Ligi Tanzania bara 2010/11 umemalizika, timu zimeenda likizo baada ya misukosuko na pilika pilika za msimu ulioanza Agosti mwaka jana, katika Ligi kuu tulikuwa na jumla ya timu 12.
Kati ya hizo Yanga waliobuka mabingwa wapya, Simba, Azam FC, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, Toto African, Polisi Tanzania na African Lyon zimebaki Ligi kuu, huku AFC Arusha na Majimaji ya Songea zikishuka daraja.
Timu zilizosalia zinaungana na nyingine nne za JKT Oljoro, Coastal Union, Villa Squad na Moro United, zilizopanda kutoka daraja la kwanza kujiandaa kwa msimu mpya wa Ligi wa 2011/12.
Ingawa timu hizi zina miezi mitatu na ushee kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi, lakini ni moja pekee ya Azam FC na Mtibwa Sugar pekee, zenye viwanja vyake, timu nyingine zote hazina viwanja na kwa bahati mbaya bado hajizaanza kufanya maandalizi ya viwanja.
Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba timu hizi zinaendelea kulala usingizi wa pono, wala hazijihangaishi kuanza kufanya mazungumzo na wamiliki wa viwanja wanavyotarajia kuvitumia kama viwanja vyao vya nyumbani katika msimu ujao wa Ligi.
Matokeo yake ni Ligi kuanza huku viwanja vikiwa vibovu visivyostahili hata kufanyia mazoezi achilia mbali kutumika kwa mashindano magumu ya Ligi kuu, lakini kutokana na timu kutokuwa na viwanja vinajikuta vikilazimika kuvitumia hivyo hivyo.
Matokeo yake wachezaji wanaumia mara kwa mata vifundo vya mguu ‘ankle' na pia wanashindwa kuonyesha uwezo wao na wakati mwingine timu kupata matokeo mabaya ambayo yanazuia kufikia malengo waliyojiwekea mwisho wa msimu.
Ni jambo la kusikitisha kwamba viongozi wa klabu zetu wanashindwa kuwa walipaswa kuketi na wamiliki ili kukubaliana na kuanza kuvifanyia ukarabati viwanja hivyo kuanzia sasa ili walau viwe katika kiwango bora msimu mpya utakapoanza.
Kitendo cha viongozi wa klabu visivyo na viwanja kulala usingizi na kuja kukurupuka na kuanza kuwalaumu wamiliki wa viwanja au Shirikisho la soka nchini (TFF) kwa ubovu wa viwanja ni upuuzi.
Naita upuuzi kwa sababu jukumu la kujua ubora wa kile utakachokitumia uko kwako, kwa sababu sio kila mmiliki wa kiwanja anaelewa kiwanj bora kinatakiwa kiweje na pia ikumbukwe wamiliki wengine wa viwanja wamevipata ‘kihuni' kwa hiyo wataviendesha kihuni pia.
Viwanja havina usimamizi wowote kinachoangaliwa hapo ni mapato pale vitakapotumika, havipandwi nyasi, havimwagiliwi maji, havisafishwi, havijengewi au kufanyiwa ukarabati wa vyoo, haviboreshwi yaani vipo kwa maana ya kuwepo, hivyo lilikuwa jukumu la wale watakaoutumia kuketi mapema na kuwapa masharti wamiliki.
Wanapaswa kuwaambia kuwa tutavitumia viwanja vyenu kwa msimu mzima lakini lazimi viwe na viwango vinavyokubalika na kwa kuwa wenye kumiliki viwanja hivyo nao wapo kibiashara lazima watakubaliana na masharti hayo.
Aidha kwa kuwa kila mmoja ameshajua umuhimu na thamani ya uwanja, huu ulikuwa wakati wa kila klabu kusaka eneo la kutosha ambalo watajenga uwanja wao, kuliko kuendelea kusubiri kupata uwezo.
Kila kukicha viwanja vinazidi kuwa adimu nchini, hivyo ninahisi siku ambapo klabu hizi zitakuja kupata uwezo au kupata viongozi wenye nia ya kujenga uwanja basi wakati huo hakutakuwa tenana viwanja maeneo ya karibu na yalipo makazi yao.
Leo kwa timu za Dar es Salaam viwanja vinapatikana BOko, Bunju, Chanika, Kisarawe, Mbagala, Mji Mwema, Tua Ngoma na maeneo mengine huko Kigamboni, lakini miaka kumi ijayo viwanja vya kuanzia hekari tano labdada vitapatikana jirani na Lindi na kwenye mapori ya hifadhi ya Taifa.
Kwa maana hiyo, klabu zilipaswa kusaka maeneo sasa hata kama bado hazina uwezo wa kuyajenga kwa sasa lakini walau wakiwa nayo na wakawa wanafanyia walau mazoezi japo mara mbili au moja kwa wiki ingekuwa bora kwao, kuliko kuendelea kuazima.
Nachelea siku moja wamiliki wa viwanja hivi tunavyovilalamikia kila kukicha kuwa vibovu watajaamua vitumike kwa michezo mingine tu isiyokuwa soka, wakati Ligi ya soka ikiendelea.
Hakika kwa staili hii hatufiki, viongozi wa timu za soka hasa zinazoshiriki Ligi kuu, wanapaswa kujua maana na umuhimu wa viwanja, kuendelea kulalamika timu haina uwezo wa kujenga sio suluhisho.
 
Samata sasa gari la nini nenda Mazembe
ban.blank.jpg


Kenneth Mwaisabula​

amka2.gif
Katika maisha kuna wakati ukitaka mpaka usifiwe unaweza ukafa bila kupata bahati hiyo na kwa kulijua hilo nikaona hapana nami ngoja nijisifu kidogo hata kama hamtaki basi siwalazimishi.
Nimewahi kuandika makala nyingi sana na za kila aina lakini ni vyema nikajisifu angalau tatu ambazo nakiri zimefanyiwa kazi,mosi niliwahi kuwashauri Shirikisho la Soka Tanzania (TFF )kuwa idadi ya timu katika Ligi ya Vodacom hazitoshi Inshalaa kila mwaka sasa zinaongezwa.
Pili, niliwahi kuandika makala ya kuitaka (TFF) kuacha kusimamia ligi na ijikite katika kushughulikia masuala ya timu za Taifa tu, inshallaa na lenyewe hilo limekaa vizuri sasa kwa nini nisijisifu, Hata kama watasema hawakuliona toka kwangu ni mawazo yao basi kumbe hata mimi nastahili kutoa mawazo mazuri
La tatu ni hili la kijana Mbwana Samata ambaye mimi kwa makazi ni jirani yangu,katika moja ya makala zangu niliwahi kumkalia kidedea akaripoti Simba asihangaike na gari na kwamba huko atapata magari mengi tu kwa kutambua uwezo wake nashukuru Mungu alinielewa.
Na aliporipoti siku ya kwanza tu tuliwasiliana na kunifahamisha kuwa anakwenda katika mazoezi ambayo yalikuwa katika ufukwe,kwa kufurahia mafanikio yake leo nimeona niirudie tena ile makala ambayo niliiandika wakati hataki kutia timu Simba Sports Club.
Makala yangu iliyokuwa na kichwa cha habari Samata unataka gari kwa mpira gani? Ilianza kama ifuatavyo:,
Maisha yangu yametawaliwa na soka, nikilala nikiamka nikitembea nawaza soka, ninao uwezo wa kuongea masaa yote mambo ya soka tu.
Wale rafiki zangu wanaonifahamu hilo wanalielewa vyema. Wazazi wangu walikuwa wanapata taabu sana kunitafuta katika chakula cha mchana kwa sababu ya soka, na punde nirudipo usiku kutokana miguu yangu kujaa vumbi ilibidi lazima nipite mlango wa uani ili kuepuka bakora za baba, pamoja na kuwa baba yangu alikuwa ni mchezaji mzuri wa soka pale Tabora lakini hakupenda kuniona mie nikipiga soka.
Kwa tabia hiyohiyo ya kupenda soka, nimejikuta nikipenda mno kuandika makala zinazohusu soka, na inaniwia vigumu kukaa kimya kila ninapohisi nastahili kutoa mawazo yangu.
Kila ninapomuona Samatta katika viwanja vya Mbagala shule ya msingi rangi tatu naujutia umri wangu jinsi mpira leo ulivyokuwa ni moja kati ya ajira kubwa sana duniani, kijana Samatta anachezea maisha.
Wakati leo wenzetu wa Nigeria, Ghana, Cameroon wanauza vitu kama tv, radio, basikeli n.k wapate nauli ya kwenda kutafuta maisha ya soka nje;,Samatta leo amelala kwao Mbagala anacheza katika vumbi na akirudi anakwenda chumbani kwenda kuangalia tv, hataki kuripoti Simba kisa hajapewa gari; ni kichekesho kwelikweli.
Wakati wenzake wanatafuta fomu za usajili kwa kununua na kupigana hadi tone la mwisho kuwabembeleza viongozi, Samatta anadengua eti anataka gari.
Navuta hisia zangu mwaka 2004 mwishoni niliwaita wachezaji waje kwa ajili ya majaribio wakati nafundisha Yanga African ili niwasajili kwa msimu unaofuata. Miongoni mwa wachezaji waliokuja ikiwa na wengine kuwaleta mimi ni Danny Mrwanda, Mohamed Mwarami, Henry Joseph, na Idrisa Rajabu anayekipiga Sofapaka ya Kenya.
Wachezaji wote hao walitaka kuja Yanga bure na leo wote hao wanakipiga Ulaya, Mbwana Samatta anasubiri gari, ni ajabu kweli kweli.
Mwanangu Mrwanda leo ana bonge la bangaluu lake pale Mbezi, huwezi kumwona kirahisi kwa sababu anakimbia huku amekaa (anaendesha gari) alitaka fomu Yanga bure, iliposhindikana nikamtupa AFC na beki mmoja wa kushoto Mrundi anaitwa Carlos, leo anakula kuku wake Vietinam, Samatta anataka apewe gari na Simba kwa mpira gani sijui!?
Tatizo la washauri wa Mbwana waliomzunguka wote wana roho ya kwa nini, wanataka wapaki magari yao pale shuleni Rangi tatu kwenye uwanja wenye vumbi na usio na alama na akitoka wampe elfu kumi na yeye anajiona bonge la mchezaji, namsikitikia sana Mbwana anavyoichezea bahati kwa kiburi chake na washauri wake.
Aron Nyanda mchezaji wa zamani waYanga alimleta mdogo wake wa pale mwanza, Henry Joseph Shindika aje acheze Yanga bure. Ni matatizo tu ya meneja wa Yanga wakati ule, Robert Ikerege ya kutokujua mchezaji mzuri ni yupi.
Shindika leo yupo kwa wazungu anapigana na baridi la ulaya. Samatta kajificha Mbagala anasubiri gari aletewe nyumbani kwao, sio kwake na Rage.
Samatta anashindwa kuelewa kuwa soka linakwenda na umri na kwamba huu ni wakati wake wa kutafuta maisha ya kesho na wala sio gari, na ajue kwamba Simba ni njia tu ya kupita kutafuta maisha ya kesho. Mbwana leo hana timu ya kufanya mazoezi, hachezi mashindano yeyote, anategemea nani atakaye mwona ikiwa kajificha Mbagala.
Inasikitisha mno.wachezaji leo wanapigana kucheza Simba na Yanga bure, mdogo wangu anataka gari. Watu wanalala katika vituo vya mabasi ulaya kutafuta maisha ya soka, wewe leo unachezea bahati.
Simba leo imepoteza mechi moja tu na inaendelea kushinda, bado kidogo tu jina lako litafutika katika ramani ya soka, inasikitisha mno.
Mpira umemfanya David Beckham kama mtume pale Uingereza akitokea timu ya watoto pale Manchester United akicheza bure. Michael Essien anaabudiwa kama Mungu pale Ghana na akitoka katika familia duni tofauti na Mbwana Samatta mtoto wa kocha mkongwe wa jeshi la polisi nchini.
George Weah ilibaki almanusura apewe nchi, yaani uraisi. Soka ni zaidi ya gari. Kama kuna kitu ambacho kinawaathiri wachezaji wa Kitanzania wa aina ya Samatta ni kwamba hawajui thamani ya soka.
Emeh Izuchukwu alipita Simba leo yupo ulaya, Simba ni njia tu.Tatizo la Samatta ana macho lakini haoni, masiko anayo lakini hasikii, lakini ningekuwa mimi ningerudisha nyuma nyakati zile ambazo nilirudi nyumbani na vumbi nikiwa mchafu, sitamaniki huku Baba akiwa hataki kuniona,ningepigana hadi tone la mwisho na kama hizo timu zingenitaka ningeenda bure kwa kutambua pale ndio njia panda ya mafanikio, kule ambako Haruna Moshi amekataa kuishi.
Huenda Mbwana hajui soka ni zaidi ya soka. Mchezaji wa leo anaweza kulipwa zaidi ya shilingi milioni 200 kwa wiki, miye hata nifanye kazi miaka 30 sizipati. Ushauri wangu wa bure kwako, kwa sababu hutaki kuonana nami kila ninapokutafuta, nenda karipoti kwa Phiri (Patrick) na Mziray(Sylersaid aliyekuwa kocha wa saikolojia wa Simba ambaye sasa ni marehemu) uanze mazoezi. pale ni njia tu, Mbagala hakuna njia, kuna giza nene. Achana na wapambe, kesho watakucheka
Hiyo ndio ilikuwa makala inayomhusu Mbwana Samata ambaye wapambe wake walitaka waue kipaji chake pale Mbagala katika vumbi kwa kumdanganya asiende hadi apewe gari leo anatua TP Mazembe unataka nini tena gari la nini tena kila kitu kimekaa vizuri, nenda Mwanangu sisi tunataka maendeleo yako tu na wala hatuitaji chochote kutoka kwako,nenda mwanangu,fungua njia kwa wenzako na nchi ijidai.



h.sep3.gif

Mwandishi wa makala hii kocha mzoefu nchini pia ni mfanyakazi wa mamlaka ya bandari kitengo cha uhandisi anapatikana 0713-243711 au Email kennymwaisabula@yahoo.com
 
Wenger: Title chances minimal


Par6228741_20110424114403718_1280_1280_20110424221305726_660_320.JPG




RivalsDM



PRINT RSS

42

Updated Apr 24, 2011 10:14 PM ET
Arsene Wenger admitted Arsenal now had a "minimal" chance of winning the Premier League title after slipping to a late 2-1 defeat at Bolton.
Tamir Cohen scored a late winner for the Trotters - a week after they lost 5-0 to Stoke at Wembley - to all-but end their opponents' title hopes.


"It's hard to lose a game like that," Wenger said on Sky Sports 1. "We gave everything. Our attitude was fantastic. We were 1-0 down and had chances to win it.
"We have to give as much as we can until the last game, but of course the chances are minimal now.
"The players fought very hard and the players are disappointed."
Wenger claimed the past week, in which his side also let leads slip to draw with Liverpool and Tottenham, had cost them dear.
But he said he does not see any need for drastic changes.
"I feel this week we could have taken nine points and we have taken two," he added. "We do not have to change our way of playing.
"I feel we have to be more mature in some situations when we are looking too frail.

Wed., Apr. 20
Chelsea 3-1 Birmingham
Tottenham 3-3 Arsenal | Recap
Sat., Apr. 23
Man Utd 1-0 Everton | Recap
Aston Villa 1-1 Stoke City | Recap
Blackpool 1-1 Newcastle | Recap
Liverpool 5-0 Birmingham | Recap
Sunderland 4-2 Wigan | Recap
Tottenham 2-2 West Brom | Recap
Wolves 1-1 Fulham | Recap
Chelsea 3-0 West Ham | Recap
Sun., Apr. 24
Bolton 2-1 Arsenal | Recap
BPL Scores | Table | Fixtures


"If you look at the way we dropped points it makes it even more frustrating."
Striker Daniel Sturridge claimed Bolton owed their fans victory over Arsenal following their FA Cup semi-final humiliation.
"We're just delighted to come out here and work hard," said Sturridge, who is on loan from Chelsea. "After last week's result we wanted to come here and show the fans we had the passion.
"A lot of fans were very unhappy with last week, we did this for the fans today."
Cohen took his shirt off after scoring the winner to reveal a t-shirt paying tribute to his late father, Avi, who died in December last year following a motorbike accident.
"I came on to protect the 1-1," he said. "I am very happy to score this goal, it's been a very emotional season for me.
"I am happy we won and collected another three points."
Bolton boss Owen Coyle was delighted with his side's response to their Wembley humiliation.
"The boys have been magnificent all season," he said. "We had one terrible, horrible day last week when everything that could go wrong went wrong.
"We didn't feel great about ourselves and that will stay with me till the day I die, but today I think everybody has seen the true Bolton.
"Every one of them worked their socks off.
"I'm absolutely delighted to get the late winner."
 
Today's Games
Today's Games Week 1: 01/07/11 - 01/09/11 Week 2: 01/14/11 - 01/16/11 Week 3: 01/21/11 - 01/23/11 Week 4: 01/28/11 - 01/30/11 Week 5: 02/02/11 - 02/06/11 Week 6: 02/11/11 - 02/13/11 Week 7: 02/18/11 - 02/20/11 Week 8: 02/25/11 - 02/27/11 Week 9: 03/04/11 - 03/06/11 Week 10: 03/11/11 - 03/13/11 Week 11: 03/18/11 - 03/20/11 Week 12: 04/01/11 - 04/03/11 Week 13: 04/08/11 - 04/10/11 Week 14: 04/12/11 - 04/13/11 Week 15: 04/16/11 - 04/17/11 Week 16: 04/22/11 - 04/24/11 Week 17: 04/29/11 - 05/01/11​

Sunday, April 24, 2011​
Week 16​

Estadio Morelos
Expand
expandInfo.jpg


0 : 3
Final




Match Stats | Match Trax
Goals Lucas Lobos (14')
goal.gif

Alan Pulido (84')
goal.gif

Alberto Acosta (88')
goal.gif

yellow-card.gif
(34') Miguel Sabah
yellow-card.gif
(60') Joel Huiqui
Cards Israel Jiménez (44')
yellow-card.gif

Héctor Mancilla (50')
yellow-card.gif

Jesús Molina (56')
yellow-card.gif

greenArrow.gif
(46') Francisco Dorame
redArrow.gif
Adrián Aldrete

greenArrow.gif
(65') Marvin de la Cruz
redArrow.gif
Adrián García Arias

greenArrow.gif
(78') Angel Sepúlveda
redArrow.gif
Rafael Márquez

Substitutions Alan Pulido (75')
greenArrow.gif

Héctor Mancilla
redArrow.gif


Alberto Acosta (76')
greenArrow.gif

Damián Alvarez
redArrow.gif


Francisco Acuña (87')
greenArrow.gif

Danilo Verón
redArrow.gif



Estadio Nemesio Díez
Expand
expandInfo.jpg


4 : 4
Final




Match Stats | Match Trax
goal.gif
(10') Néstor Calderón
goal.gif
(18') Antonio Naelson Sihna
goal.gif
(33') Emmanuel Cerda
goal.gif
(39') Emmanuel Cerda
Goals Edgar Dueñas (48')
own-goal.gif

Eduardo Lillingston (55')
goal.gif

Eduardo Lillingston (81')
goal.gif

Juan Carlos Leaño (85')
goal.gif

yellow-card.gif
(42') Mario Méndez
yellow-card.gif
(67') Luis Carlos Arias
Cards Gustavo Cabral (41')
yellow-card.gif

Oswaldo Alanís (78')
yellow-card.gif

greenArrow.gif
(46') Luis Carlos Arias
redArrow.gif
Néstor Calderón

greenArrow.gif
(58') Héctor Acosta
redArrow.gif
Edgar Dueñas

greenArrow.gif
(75') Diego de la Torre
redArrow.gif
Luis Carlos Arias

Substitutions Juan Carlos García (46')
greenArrow.gif

Mario Rodríguez
redArrow.gif


Taufic Guarch (74')
greenArrow.gif

Rubens Sambueza
redArrow.gif


Alberto Ramírez (80')
greenArrow.gif

Israel López
redArrow.gif



Estadio Azteca
Expand
expandInfo.jpg


1 : 1
Final



Match Stats | Match Trax
goal.gif
(36') Angel Reyna
Goals Giancarlo Maldonado (38')
goal.gif

yellow-card.gif
(17') Israel Martínez
yellow-card.gif
(60') Diego Reyes
yellow-card.gif
(90') Oscar Rojas
Cards Arturo Muñoz (42')
yellow-card.gif

Daniel Guerrero (76')
yellow-card.gif

Sonny Guadarrama (78')
yellow-card.gif

greenArrow.gif
(33') Miguel Layún
redArrow.gif
Israel Martínez

greenArrow.gif
(62') Matías Vuoso
redArrow.gif
Pável Pardo

greenArrow.gif
(65') Enrique Esqueda
redArrow.gif
Daniel Montenegro

Substitutions Sergio Sergio (46')
greenArrow.gif

Arturo Muñoz
redArrow.gif


Sonny Guadarrama (60')
greenArrow.gif

Jorge Hernández
redArrow.gif


Jerónimo Amione (70')
greenArrow.gif

Giancarlo Maldonado
redArrow.gif
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom