'Nendeni mahakamani' simba wang'aka Send to a friend Saturday, 23 April 2011 14:46
Vicky Kimaro
WAKATI African Lyon ikidai shilingi milioni 5.5 zilizochukuliwa na mmoja wa viongozi wa Simba, Kasim Dewji zirudishwe, kiongozi huyo amewataka Lyon waende mahakamani kama wanadhani fedha hizo wamedhulumiwa na zimechukuliwa isivyo halali.
Kauli ya Kasim Dewji ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wa African Lyon alitoa kauli hiyo mara baada ya ofisa habari wa Lyon, Sherally Abdallhah kusema kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), na klabu ya Simba inawadhulumu wachezaji wao na pia imewadhulumu kiasi hicho cha fedha ambacho walistahili kupewa ikiwa ni zawadi ya Vodacom baada ya Lyon kushinda ya timu yenye nidhamu kwenye msimu wa ligi ya mwaka jana.
Dewji amejibu mapigo na kusema "Kama wanaona wananidai waende mahakamani, kimsingi wanahangaika wakati Lyon inapata zawadi ya Vodacom kama timu yenye nidhamu ilikuwa bado ipo chini yetu kama viongozi wa Lyon wa zamani na tulikuwa hatujaiuza, hawana haki ya kudai fedha za zawadi kwa kuwa ilipata timu yenye nidhamu ikiwa chini yetu,"alisema Dewji na kuongeza
"Hawana mamlaka yoyote ya kudai hela za zawadi, mamlaka wanayo hivi sasa tangu tulipowakabidhi rasmi timu Julai 17 mwaka jana kwa hiyo kama timu ingetwaa ubingwa, ikishinda timu bora, au yenye nidhamu mwaka huu ndio wanahaki ya kudai sio mwaka jana, hii hela haiwahusu, kama wanaona wameonewa waende mahakamani,"alisisitiza Dewji.
Naye Katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah akizungumzia suala hilo alisema " Afrika Lyon waliandika barua TFF na ushaidi tunao wa kutaka fedha hizo za zawadi apewe Kassim Dewji kwa sababu wanadaiwa milioni 7 wakati zawadi za Vodacom zinatolewa akaunti ya TFF ilikuwa imeshikiliwa na TRA na ilipoachiwa ndio hizo hela akapewa Dewji,"alisema Osiah
Hata hivyo ofisa huyo wa Lyon alisema Rais wa TFF, Leodegar Tenga alishamwagiza aliyekuwa kaimu katibu mkuu wa shirikisho hilo Sunday Kayuni wafanye kikao na fedha hizo zirudishwe lakini wanashangaa mpaka hivi sasa fedha hizo hawajapewa na kwamba bado zipo mikononi wa wajanja.
Ofisa habari huyo wa Lyon pia alidai kuwa Junuari 16 mwaka jana kulikuwa na makubalio ya wamiliki wa awali Mohamed Dewji na TFF pamoja na viongozi wa Simba na Yanga kuhusu malipo ya mchezai Yahaya Issa kuwa alipwe stahili zake zote shilingi milioni 1,000,000 kati ya mchezo wa Yanga na Lyon na Simba na Lyon pia kiasi kama hicho lakini kitendo hicho hakikufanyika na badala yake mzigo huo wameachiwa Lyon peke yake.
Lakini Katibu Mkuu wa TFF, Osiah alifafanua suala hilo na kusema "Lyon waliandika barua kuwa Yahaya Issa anawadai hivyo tumlipe fedha hizo kutoka kwenye makato ya mechi zao na mara ya mwisho mwezi uliopita tumemmalizia malipo yake ya shilingi 700,000.