Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
- Thread starter
- #16,301
Okwi atakiwa Kaizer Chiefs
Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu; Tarehe: 15th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 14; Jumla ya maoni: 0
MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi anaenda kufanya majaribio ya kucheza soka klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage alisema Ijumaa kuwa wamepokea maombi kutoka timu hiyo kwa ajili ya kumfanyia majaribio mshambuliaji huyo.
"Hivi sasa Okwi yupo kwao Uganda kwa ajili ya mchezo wa timu ya Taifa ya vijana ya Uganda na ya Tanzania utakaofanyika Jumamosi baada ya hapo ataenda Afrika Kusini kwa majaribio
hayo.
"Simba haina tatizo naye inamtakia kila la heri kwenye majaribio yake maana ndiyo mafanikio ya Simba kama akipata nafasi," alisema Rage.
Rage alionya kuwa mshambuliaji huyo ana mkataba na Simba hadi mwaka 2014 hivyo kama kuna timu inataka kutumia ujanjaujanja kumsajili haitafanikiwa.
"Mpaka sasa ninaowajua ni hao Kaizer Chiefs, sasa kama kuna mtu anajifanya kutaka kupita njia za panya kumsajili itakula kwake, hiyo ni mali ya Simba mpaka mwaka 2014," alisema Rage.