Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
- Thread starter
- #16,101
Tanzania kushiriki tenisi ya vijana
na Samia Mussa
TANZANIA inatarajiwa kushiriki mashindano ya tenisi ya vijana kati ya miaka 12 na 14 yatakayoanza Aprili 19 hadi 28 jijini Nairobi, Kenya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kocha mkuu wa mchezo huo hapa nchini, Salum Mvita alisema, Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wachezaji wanane, ambao walichaguliwa hivi karibuni katika viwanja vya Gymkhana jijini.
Alisema kuwa, wachezaji hao baadhi yao wamechaguliwa kutoka Arusha, ambako wanatarajiwa kuondoka Aprili 18 mwaka huu kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo.
Aidha, Mvita aliwataja wachezaji hao kuwa ni pamoja na Martin John, Omary Hamisi, Fred Benard, John Njau, Godluck Shelemo, Zuhura Baraka, Sarah Bura na Zuhura Isihaka.
Mvita alisema kuwa, katika kuhakikisha Tanzania inanyakua ushindi katika mashindano hayo, timu hiyo inaendelea kufanya mazoezi ya nguvu, pamoja na wachezaji ambao hawakuchaguliwa kwenye viwanja vya Gymkhana.
Wachezaji tuliowachagua, tuna uhakika watatuwakilisha vizuri kwenye mashindano hayo, kwa sababu wana uwezo mzuri na kuchangia na maandalizi mazuri tuliyofanya, alisema Mvita.