Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
- Thread starter
- #14,861
JKT yapanga kuitibulia Simba Send to a friend Sunday, 03 April 2011 20:25
Sosthenes Nyoni
NAHODHA wa timu ya JKT Ruvu, Shahibu Nayopa ameiambia Simba wao sio daraja la kuchukulia ubingwa hivyo wajiandae kutibuliwa malengo.Simba na JKT zitakabiliana katika pambano la Ligi Kuu litakalofanyika jijini Dar es Salaam Aprili 6.
Mchezo huo ambao unasubiriwa na wengi unahesabiwa kuwa mtihani wa mwisho kwa Simba yenye pointi 45 kabla kutangazwa ubingwa ili hali ikisubiri kuivaa Majimaji ambayo tayari imeshuka daraja.
Akizunguza na Mwananchi jana, Nayopa alisema kuwa hawatarudia makosa kama yale yaliyowasababisha wakafungwa katika mechi ya mzunguko wa kwanza.
"Sisi si daraja bwana, kama wanafikiri watatangaza ubingwa kwetu watakuwa wanajidanganya tu kwa sababu hata sisi tunataka pointi tatu,"alisema Nayopa.
"Tuliangalia makosa yaliyosababisha tukafungwa katika mpambano wa mzunguko wa kwanza hivyo kila mmoja wetu alilitambua hilo na amelifanyia kazi,"alisema Nayopa.
Alisema kuwa ana uhakika wataibuka kidedea kwa kuwa hata katika mpambano wao wa mzunguko wa kwanza walionyesha kiwango cha hali ya juu, lakini walishindwa kutumia nafasi walizopata tofauti na wenzao.

PRINT