Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Cricket
Pakistan party like it's 1999
Bowlers take credit as defending champs skittled for 176 to hand Australia first Cricket World Cup defeat in 12 years.

Last Modified: 19 Mar 2011 17:59





2011319175726499876_20.jpg
Afridi said the Pakistan bowlers 'stuck to their plans' to restrict Australia to a low total [AFP]
Australia's 34-match unbeaten run in the Cricket World Cup was finally broken as Ricky Ponting's team lost to Pakistan by four wickets, leaving Shahid Afridi's side on top of Group A.
Australia, who have won the last three World Cups during the run and were unbeaten in five matches in Group A in this tournament, were skittled out for 176 in Colombo on Saturday.
Pace bowler Brett Lee was on fire at the R Premadasa Stadium and raised hopes of an Australian fightback when he got rid of opener Mohammad Hafeez in the third over but his haul of four for 28 could not prevent Pakistan from cruising to victory with 54 balls to spare.

Abdul Razzaq (20 not out) finished off match in style by slamming spinner Jason Krezja for two consecutive fours to end on 20 not out. Pakistan finished on 178-6.
"We certainly had a tough game today. We didn't do ourselves any favours. I thought our batting effort was particularly ordinary," said Ponting, who suffered his first World Cup defeat as captain.
"We stuck at it really well with the ball. I thought the guys bowled really well and gave ourselves a bit of a sniff when we got them six down but not enough runs on the board."
Saturday's result threw the tournament wide open as there is no undefeated team left in the competition heading into next week's knockout stage.
Australia had already qualified for the quarter-finals but will now finish third in the group rather than top, a place now occupied by Pakistan.
'Good plans'

Asked to reveal how his team gave Australia their first World Cup defeat since 1999, Pakistan captain Shahid Afridi said: "We made some good plans against these guys and I think the boys all stuck to these plans.
"We didn't try to take some wickets early on, we tried to bowl maiden, good overs ... and all the bowlers did a great job. The credit goes to the bowlers."
Umar Akmal, who finished unbeaten on 44, added: "It's a different sort of enjoyment playing against Australia. They may be world champions but there was no pressure on us so we pulled it off today."

Ponting's men struggled for momentum throughout their innings after opting to bat first.
Pakistan's pace and spin attack, backed up by sharp fielding, never allowed the Australian batting to settle down.
A 63-run second wicket stand between Brad Haddin (42) and Ponting (19), who failed once again with the bat, was the only notable partnership in the Australian innings.
Michael Clarke (34) and Steve Smith (25) were the only other batsmen to make any worthwhile contributions on a difficult surface that offered spin and some uneven bounce which the Australian batsmen failed to cope with.
Paceman Umar Gul (3-30) bowled superbly with both the new and the old ball for the 1992 champions, who were the last team to defeat Australia in a World Cup match in 1999.
Gul made the first breakthrough by bowling Shane Watson for nine and returned to clean up the tail by taking the wickets of Jason Krezja and Lee.
 
Sikinde wajipanga kumtambulisha Jumbe


na Ruhazi Ruhazi


amka2.gif
BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Mlimani Park 'Sikinde Ngoma ya Ukae' imepanga kutumia maonyesho yake ya wiki hii kumtambulisha mwanamuziki wake iliyemrejesha kundini Hussein Jumbe.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salama jana Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Sikinde, Jimmy Chika, alisema kuwa wamepanga kumtambulisha Jumbe katika bonanza litakalofanyika Jumamosi hii kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo na Jumapili mchana katika bonanza lao kwenye ukumbi wa TCC Club-Chang'ombe.
Alisema kuwa Jumbe aliyerejea siku moja kabla ya kuwavaa mahasimu wao Msondo katika mpambano uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee wikiendi iliyopita, ameanza mazoezi na wenzake kuandaa albamu mpya.
"Tunapenda kuwaambia wapenzi wa Sikinde wafike katika maonyeshio yetu ya wiki hii ambapo tutamtambulisha Hussein Jumbe ambaye amerejea kundini baada ya kuwa nje kwa muda," alisema Chika.
Alisema mbali ya kumtambulisha katika maonyesho hayo ya bonanza lakini pia watamtambulisha rasmi kwa mashabiki watakaohudhuria onyesho lao kwenye ukumbi wao wa nyumbani wa SUWATA, ulioko Kariakoo, jijini Dar es Salaam, Jumapili usiku.
 
Mashujaa kujitambulisha upya Makumbusho


na Mariana Mathias


amka2.gif
BENDI ya musiki wa dansi ya Mashujaa Musica inatarajia kutambulisha rasmi uongozi wake mpya wakiwemo wanamuziki na wanenguaji katika onyesho litakalolindima Aprili mosi, Kijiji cha Makumbusho Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, meneja wa bendi hiyo, Mujibu Hamisi, alisema wamefanya mabadiliko makubwa upande wa uongozi, wanamuziki na wanenguaji wapya ambayo yataijenga Mashujaa mpya.
Alisema, utambulisho huo utawaweka wazi mashabiki juu ya meneja huyo mpya, wanamuziki watano na wanenguaji sita, wakiwemo wanawake wanne na kwamba, hiyo itakuwa chachu ya kufanya vitu vya kushangaza kiburudani.
Mujibu alisema, jitihada hizo na madhumuni makuu ya bendi hiyo, ni kwaajili ya kutoa burudani itakayowafanya mashabiki wazidi kuhamasika na kujenga ukaribu zaidi kwa mashabiki na bendi hiyo.
Meneja huyo ambaye alitokea bendi ya FM Academia alisema katika wanamuziki wapya, mmoja wao ni rapa Sauti ya Radi ambaye anatarajiwa kufanya vitu vipya katika kuboresha zaidi bendi hiyo.
Mujibu alisema, kwa sasa wanaandaa albamu mpya ambayo iko jikoni, ila hadi kufikia Juni itakuwa imekamilika ambayo itawashangaza wengi na kuwataka wapenzi wa bendi hiyo wawe tayari kuipokea.
Hata hivyo, mkurugenzi wa bendi hiyo, Sakina Maisha ‘Mamaa Sakina’, alisema changamoto ni nyingi, ila anajitahiji mashabiki wafurahi kutokana na kile kinachotolewa na bendi yake.
Aliongeza kuwa, endapo kuna chochote mashabiki wake watakihitaji katika kuwaburudisha, atajitahidi kulingana na uwezo wake, kushirikiana na viongozi na wanamuziki wake, ili mashabiki wapate wanachohitaji ikiwa ni pamoja na kuboresha bendi.



h.sep3.gif
 
Twanga kutwanga siku ya Wajinga Rufita


na Mwandishi wetu


amka2.gif
BENDI ya muziki wa dansi ya Twanga International inatarajiwa kuwarusha wakazi wa viunga vya Tabata na maeneo ya jirani kwenye onyesho lake litakalofanyika siku ya Wajinga Aprili Mosi mwaka huu.
Siku ya Wajinga huadhimishwa ulimwenguni kote, na Twanga watakuwa kwenye ukumbi wa Rufita ulioko Tabata Segerea.
Kwa mujibu wa mratibu wa onyesho hilo, Abdul Omari ‘Abdul Tall', kupitia onyesho hilo, Twanga watatambulisha nyimbo zao mpya mbili, ikiwemo ‘Mtoto wa Mwisho'.
Alisema kuwa mbali na nyimbo hizo, pia watatambulisha rapu zao mpya za ‘Sharobaro' na ‘Kamata Mwizi Men' inayokuja kwa kasi hivi sasa.
Hivi sasa Twanga wanatamba na nyimbo mbili mpya ambazo wamekuwa wakizitambulisha katika maonyesho yao mbalimbali, ambazo ni ‘Kiapo cha Mapenzi' uliotungwa na Saleh Kupaza na ‘Kauli' ikiwa ni kazi yake Roggert Hegga ‘Caterpillar' .
 
Simanzi, vilio vitupu Dar Send to a friend Tuesday, 22 March 2011 19:44

majeruhiajari.jpg
Mwanamuziki wa kundi la taarab la Five Star ambaye ni majeruhi kwenye ajali ya basi waliyopata kundi hilo mkoani Morogoro usiku wa kuamkia jana, Issa Kamongo (kulia) akipewa pole na baadhi ya waombolezaji wakati akitokakwenye ukumbi wa Equator Gril, Mtoni, jijini Dar es Salaam.Picha na Joseph Zablon

Vicky Kimaro
VILIO, simanzi na huzuni vimegubika kwa sehemu kubwa jiji la Dar es Salaam kufuatia vifo vya wasanii 13 wa muziki wa taarabu vilivyotokea usiku wa kuamkia jana Mikumi mkoani Morogoro.

Wasanii hao walikumbwa na mkasa huo wakiwa safarini kutoka ziara ndefu maalum ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.Katika ziara hizo, wasanii hao walitumbuiza katika mikoa ya Iringa, Mbeya na na Ruvuma mjini Songea.

Akizungumza mwenyekiti wa kamati maalum ya mazishi ambaye pia ni mlezi wa kundi la Jahazi Modern Taarabaliyetambulishwa kwa jina la Ferouz Juma alisema fani ya muziki huo imepata pigo kubwa.

Vilio hivyo jana vilitanda kwenye ukumbi wa baa maarufu ya Ikweta Grill, Mtoni jijini Dar es Salaam, mahali ambako miili ya marehemu hao ililetwa kutoka Morogoro tayari kwa mazishi huku ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu hao wakiwa wamekusanyika kwa wingi wakisubiri kupokea miili ya wapendwa wao na kwenda kuistiri.

Kamati maalum ikiongozwa na Ferouz na Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan ilitangaza harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia familia za marehemu hao.

Mkurugenzi wa Five Stars, Hamis Slim alishindwa kuzungumza na kusema: "Sina la kusema, sijui niseme nini, ni msiba usioelezeka, nimepoteza wasanii
wangu karibu wote, siamini mpaka sasa hiki kilichotokea, Mungu pekee ndiye anaywejua, ni msiba usioelezeka sijui kama nitaweza kusahau katika maisha yangu yote."

Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi alisema: Kwa niaba ya serikali nasema familia ya taarabu nchini imepata msiba mzito sana, ni msiba wa taifa kwa kweli, serikali tumeupokea kwa mshtuko mkubwa, tunaungana na familia zote katika kipindi hiki kigumu."

Naye Abood Aziz ambaye ni Mbunge wa Morogoro alitoa magari maalum kwa ajili ya kusafirishia maiti za marehemu wasanii hao tayari kwa mazishi.

Mama mzazi wa msanii Issa Kijoti, Amina Said akilia alisema: "Mwanangu aliniaga Jumatano iliyopita akaniambia mama mi nasafiri Nasra huyo
mama niangalizie mlee vizuri mama, mi narudi Jumatatu, akaniachia na fedha, kumbe mwanangu ndo alikuwa ananiaga, siamini kama Issa amekufa, jamani mimi nimeumbuka, nani atanisaidia jamani mimi....

"Nilikuwa namtegemea mwanangu kwa kila kitu yeye ndio msaada wangu pekee, kaondoka na miguu yake akiwa na furaha tele, leo anarudi kwenye jeneza na kuniacha mkiwa mimi jamani,"alilia kwa kwikwi.

Kijoti alitarajiwa kuzikwa jana kwenye makaburi ya Mtoni Relini, na ameacha mtoto wa kike wa miaka mitatu aitwae Nasra.

Mjomba wa marehemu OmaryAbdallah aliyejitambulisha kwa jina la Hatha Bui alisema, "Omary amekufa akiwa mdogo sana miaka 25, alikuwa mtoto wa pekee wa kiume kwa dada yangu kati ya watoto wake tisa, mazishi tumepanga yatafanyika kijiji cha Magawa Kisiju,"

Msanii wa kundi hilo aliyenusurika Joha Kassim alisema: "Ni msiba mzito sitaweza kuusahau katika maisha yangu, ni Mungu pekee ndio anayejua kwani kama si kuumwa ungekuta na mimi nipo kwenye msafara huo.

Naye Hadija Kopa alisema: "Msiba hausemeki, nimeanza nao Zanzibar Stars ingawa nilikuwa na kundi langu la TOT, ikawa Five Stars safari nilitakiwa niwepo bahati mbaya kikundi changu kilianza shoo, huwezi kuamini mtu aliyewapeleka Songea alinipigia
simu ili Jumapili niwepo kule (Songea), lakini nilikataa kutokana na majukumu ya kazi kwenye kikundi changu, jamani Mungu,"alishindwa Kopa na kisha kuangua kilio.

Omary Tego: Nimepokea kwa masikitiko makubwa nakumbuka Five Stars wapo waliotoka kundi langu la Coast Modern Taarab, wasanii watano waliotoka kwangu mmoja ,Ally Jay ndiye amenusurika wengine wote wamefariki, ni msiba mzito sijui nisemeje."

Asha Baraka, ambaye ni Mkurugenzi wa African Stars, Twanga Pepeta: :"Huu msiba sio wa Slim na ndugu wa marehemu peke yao ni msiba wetu
sote jamii ya muziki na wapenda burudani, kupitia kamati yetu maalum ya mazishi inayoongozwa na Ferouz na mbunge Idd Azan, tunaomba wadau mbalimbali watuchangie ili tuweze kuwafariji wafiwa, ajali hii ni ya kitaifa.

Tunaomba michango kama ile ya Gongo la Mboto msituachie wasanii wenyewe, haijapata kutokea msiba kama huu,"alisema Asha Baraka na tayari wadau mbali mbali wameshaanza kutoa rambi rambi zao mpaka jana mchana tayari Shilingi 1.7milioni zilikuwa zimeshapatikana, kati ya hizo Shilingi 1.5 m zikitolewa ahadi.

Kundi hilo la Five Stars likiongozwa na Issa Kijoti litakumbukwa na nyimbo zao kama Wapambe Msitujadili, Riziki Mwanzo wa Chuki, Uzushi Haunitii doa na Alonacho Kajaliwa. Wimbo ulikuwa unatamba ni Msitujadili 'Mchumu....Mchumu tena mwaa."
 
Waathirika Gongo la Mboto wachezewa Send to a friend Tuesday, 22 March 2011 19:31

Calvin Kiwia
MCHEZO wa wachezaji wakongwe wa Simba, Yanga kuchangia waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto uliingiza Sh 13.6 milioni, lakini ni Shilingi milioni moja pekee zilizokwenda kwa walengwa.Mchezo huo wa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam uliishuhudia Simba ikishinda kwa bao 1-0

Akizungumza na wanahabari kwenye ofisi za shirikisho la soka nchini, TFF jana jijini Dar es Salaam, mratibu wa pambano hilo, Seleman Mathew alisema Sh 13.6 milioni ndizo zilizopatikana kwenye mchezo huo ulioingiza mashabiki 10,796.

Alisema kati ya hizo Shilingi milioni zitapelekwa kwa waathirika hao wa mabomu ."Nafikiri wengi mtakuwa mkijiuliza maswali mengi kwanini zipatikane 13.6 m na milioni moja pekee ndiyo ipelekwe kwa waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto.

"Sababu zilizofanya kupeleka kiasi hichi nikutokana na kuwa na gharama nyingi za kulipia kama vile uwanja ambapo tumelipa kiasi cha Shilingi 5.6 milioni

"Kuwalipa waamuzi wa mchezo ule, nauli ya kuja Dar es Salaam na kwenda Kigoma, wauza tiketi, walinzi wa milangoni na watoa huduma ya kwanza," alisema

Alisema fedha hizo watazikabidhi kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki wakati wowote kwa ajili ya kwenda kuzikabidhi kwa waathirika .Aliongeza kuwa baada ya mchezo ule uliofanyika jijini Dar es Salaam wamepata mwaliko wa kwenda kucheza mchezo mwingine wa kirafiki jijini Dodoma.

"Mchezo huo utafanyika Aprili 24 kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma, nia ya mchezo ni kuwapa burudani wakazi wa Dodoma na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," alisema Mathew.
 
Kamati TFF yaiogopa Yanga Send to a friend Tuesday, 22 March 2011 19:29

Clara Alphonce
KAMATI ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekimbia lawama kwa kushindwa kutoa adhabu kwa Yanga baada ya wachezaji wake kufanya fujo baada ya kumalizika kwa mechi yake dhidi ya Majimaji ya Songea na kuiachia kamati ya Nidhamu kutoa uamuzi.

Wachezaji wa Yanga wanadaiwa kufanya vurugu kwa kuvunja viti na kuvunja mlango wa mama lishe katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea baada ya mchezo wao kumalizika kwa madai kuwa mwamuzi wa mchezo huo kutowatendea haki.

Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa maamuzu hayo yametolewa na Kamati ya Mashindano ambayo ilikutana Machi 16 kujadili mambo mbali mbali yaliyojitokeza kwenye michezo ya Ligi kuu Tanzania Bara.

Alisema baada ya kujadili na kuona kuwa madai yote yaliyowasilisha kwao yanamakosa na yote ni yale ambayo yanajirudia kila siku waliamua kupeleka madai hayo kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF, ambayo ndiyo itatoa adhabu hizo.

Alitaja madai ambayo walikuwa wajijadili ukiacha suala la Yanga kuwa ni mechi kati ya Toto African ya Mwanza na Simba uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ambapo kocha wa Toto, Choke Abeid alimtukama mwamuzui wa mezani wa mchezo huomatusi ya nguoni na kutupa chupa ya maji chini kutokana na kitendo hicho mwamuzi alimtoa kwenye benchi.

Alisema mchezo mwingine ambao ulikuwa na malalamiko ni mchezo wa Kagera na Yanga uliochezwa Kaitaba Mkoani Kagera ambako wachezaji wa Kagera, Msafiri Devo na David Luhende waliwarushia chupa na maji waamuzi na kuwatukana matusi ya nguoni.

Wambura aliongeza kuwa kosa lingine lilikuwa ni lile la Shabani Kado, kipa wa Mtibwa aliyeripotiwa kumtukana mwamuzu matusi ya nguoni katika mchezo wao dhidi ya Toto African ambapo alitolewa nje kwa kadi nyekundu japo alitakiwa kukaa nje mechi tatu na faini ya Shilingi 500,000 lakini kamati hiyo imetaka mchezaji huyo apewe adhabu zaidi.
 
TFF yapangua mechi ya Simba, Kagera Sugar Send to a friend Tuesday, 22 March 2011 19:28

Clara Alphonce
SHIRIKISHO la Soka Tanzania ( TFF) limesogeza mbele kwa siku moja mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya Simba na Kagera Sugar na sasa utachezwa Jumatatu, Machi 28.

Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa mchezo huo awali ulipangwa kufanyika Machi 27 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam lakini umesogezwa mbele kutokana na mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Afrika ya Kati ambao utachezwa Jumamosi huku Simba ikiwa nawachezaji watano katika timu hiyo.

Wambura alisema wameamua kusogeza mbele mchezo huo ili kuwapa nafasi wachezaji hao kurejea katika kikosi chao na kupumzika baada ya mchezo wa kimataifa dhidi ya Afrika ya Kati.

Katika hatua nyingine, mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amesema kuwa uwezo wa kuwafunga wapinzani wao, TP Mazembe katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika wiki mbili zijazo upo tena zaidi ya mabao mawili.

Alisema katika mchezo uliopita ambao Simba ilichapwa mabao 3-1, mabeki wao walifanya makosa matatu ya kujichanganya ambayo yalizaa magoli matatu ya Mazembe.

''Makosa hayo matatu ambayo walifanya wachezaji wetu ni katika goli la kwanza beki yetu ilishindwa kujipanga vizuri, goli la pili wa wachezaji wake hasa safu ya ulinzi walijua ni offside (kuotea) na lile la tatu pia ni uzembe wa wachezaji wetu kushindwa kujipanga na kuzuia goli lisiingie kirahisi," alisema Rage.

Alisema kocha wao (Patrick Phiri) aliliona hilo na atalifanyia kazi kabla ya kukutana na Mazembe Aprili 2 na kwamba alimsifu mwamuzi wa mchezo huo kutoka Misri kuwa alichezesha vizuri kwani hakupendelea upande wowote.

Rage alisema tayari wamekwishaanza kujiandaa na mchezo huo ambao utafanyika saa 9.00 za mchana ili waweze kuwachanganya wapinzani wao kwa joto kwani hali ya hewa ya kwao ni baridi na huku ni joto sana.

''Bado hatujakata tamaa kwani Simba ni kama mnyama wa porini hakati tamaa kabisa, hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani siku hiyo kuja kuishangilia timu yao,''alisema Rage.

Aliongeza kuwa kuhusu suala la mchezo huo kufanyika lini na uwanja upi kamati ya utendaji wa klabu hiyo ilikutana jana kupanga hayo na leo itatangaza ni wapi mchezo huo ufanyike ingawa utakuwa jijini Dar es Salaam.
 
Mwananchi Queens yaanza vyema NSSF Cup Send to a friend Tuesday, 22 March 2011 19:26

Calvin Kiwia
TIMU ya netiboli ya Mwananchi Queens juzi ilianza vyema michuano ya Kombe la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kuinyuka New Habari kwa magoli 15-5 kwenye mchezo wake wa ufunguzi wa Kundi D uliofanyika kwenye viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe.

Mwananchi Queens ikiwatumia wachezaji wake, Imani Makongoro, Oliver Albert na Salome Milinga ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa magoli 8-3 dhidi ya New Habari.

Katika mchezo huo, mchezaji mahiri wa Queens, Imani Makongoro alikuwa mwiba mkali kwa New Habari baada ya kufunga magoli yote 15 huku akiwaacha kipa na beki yote ya New Habari ambao walikuwa wakimkamia muda wote wakiwa awaamini.

Mwananchi Queens ambao walionyesha kujiamini na kutwaa ubingwa huo kabla hata ya mchezo kuanza walionyesha na mchezo safi na kutoa burudani kwa mashabiki wa Queens ambao walifurika viwanjani hapo kushuhudia timu yao ikichukua ubingwa.

Kocha wa Mwananchi Queens, Noel Kiunsi alisem kuwa timu yake imecheza mchezo mzuri ingawa walitakiwa kushinda magolizaidi ya hapo na kuongeza kuwa wanajipanga kutoa dozi katika mechi ijayo dhidi ya Uhuru.

Mbali na Mwananchi Queens, timu ya soka ya Mwananchi , kesho itashuka dimbani dhidi ya Sahara Communications ukiwa ni mchezo wao wa pili kwa Kundi C iliyopangwa kufanyika kwenye viwanja vya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu ( DUCE), Chang'ombe.

Mwananchi FC inahitaji pointi tatu muhimu ili kusonga mbele na kutinga katika hatua ya robo fainal huku kocha msaidizi wa timu hiyo, Allan Goshashy akitamba kwa timu yake kuibuka na ushindi.
 
Blatter, Bin Hammam waanza kampeni urais Fifa Send to a friend Tuesday, 22 March 2011 19:24

PARIS, Ufaransa
IKIWA imebaki zaidi ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa kumtafuta Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa ( Fifa), rais wa sasa, Sepp Blater anakabiliwa na upinzani kutoka kwa Mohamed bin Hammam, rais wa shirikisho hilo Asia (AFC).

Tayari, wawili hao wameanza kampeni za kutafuta kura za wanachama wa shirikisho hilo barani Ulaya.

Blatter na Hammam wote walilala katika hoteli moja ya kifahari karibu na Arc de Triumph mjini Paris ambapo wajumbe wote wa Shirikisho la Ulaya, Uefa watakutana kwa ajili ya mkutano wao mkuu.

Pia, katika uchaguzi huo, mwandishi wa habari wa Marekani, Grant Wahl anawania nafasi hiyo ya urais wa Fifa.

Uchaguzi mkuu wa Fifa unatarajiwa kufanyika Juni 1 mjini Zurich, Uswisi ambapo wajumbe 208 wa shirikisho hilo watapiga kura huku wajumbe 53 wa Ulaya wakionekana muhimu kwa ajili ya kufanikisha kumpa ushindi mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo.

Bin Hamman ambaye ni mzaliwa wa Qatar, alikuwa rafiki wa karibu wa Blatter , lakini tayari amesema kwamba kiwango cha soka kimeshuka duniani chini ya swahiba wake, Blatter.

"Blatter alikuja akaomba aongoze Fifa kwa miaka minane ikiwa ni vipindi viwili, baadaye akarudi na kuomba kipindi kingine cha tatu ikafika miaka 12 na hivi sasa anaomba kipindi cha nne, lakini hakuna mabadiliko makubwa katika soka," alisema Bin Hamman akizungumza na waandishi wa habari.

"Mimi ndiye nimechangia katika maendeleo ya soka kupitia shirikisho la soka Asia kwa sababu ya upendo wangu kwa mchezo wa soka, pia kwa sababu nilikuwa ni mjumbe wa Fifa, lakini kwa uongozi wa Blatter sioni maendeleo yoyote, sioni mabadiliko,"alisema.

Juzi, bin Hamman alikutana na Rais wa Shirikisho la Soka la Amerika ya Kusini (CONMEBOL), Nicolas Leoz.

Kama ilivyo kwa Blatter na Bin Hammam, Uefa pia imemwalika Leoz ambaye aliiambia Shirika la Habari la Reuters kwamba wao (CONMEBOL) bado haijaamua wampigie nani kura zao.

Wakati huo huo, Wahl anayewania nafasi ya urais, pia anatafuta chama cha soka ambacho kitamuunga mkono kwa maandishi kabla ya Aprili Mosi.

Kwa upande wake, Wahl alisema mpaka hivi sasa ameishawasiliana na vyama 150 wanachama wa Fifa akisaka kuungwa mkono.
 
Messi, Mourinho watajwa vinara wa malipo kwa wanasoka duniani Send to a friend Tuesday, 22 March 2011 19:25

PARIS, Ufaransa
MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Lionel Messi ndiye mshambuliaji anayelipwa zaidi wakati kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho akilipwa zaidi kuliko makocha wote kwa mujibu wa jarida la michezo la Ufaransa.

Ukichanganya mshahara wa Messi na Mourinho kwa pamoja, wawili hao wanapokea mshahara dola 63 milioni kwa mwaka.

Messi ambaye ni mchezaji bora wa dunia kwa miaka miwili mfululizo, mshahara wake pamoja na matangazo katika mwaka 2011 unafikia euro 31 milioni ambazo ni sawa na dola 43.87 milioni, wakati Mourinho aliingiza euro 13.5 milioni ambazo ni sawa na dola 19.11 milioni.

Mchezaji anayemkaribia Messi kwa mapato ni nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ambaye anaingiza euro 27.5 milioni ambazo ni sawa na dola 38.92 milioni.

Jarida hilo limesema, nafasi ya tatu inashikwa na mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney ambaye anaingiza euro 20.7 milioni ambazo ni sawa na dola 29.29 milioni.

Wachezaji nyota wa zamani katika Ligi Kuu ya England, David Beckham na Thierry Henry ambao hivi sasa wanacheza Ligi ya Soka Marekani (MLS ) Marekani wanashika nafasi ya tano na 11 katika orodha hiyo.

Katika nafasi ya tano yupo David Beckham ambaye anapata euro 19 milioni ambazo ni sawa na 13.6 milioni, wakati Thiery Henry katika nafasi ya 11 akijiingizia euro13.6 ambazo ni sawa na dola 19.25 milioni.

Kwa upande wa makocha, Mourinho anaongoza baada ya kuwapita wenzake wengi kwa kupata mapato mengi.

Katika nafasi ya pili kwa upande wa makocha nafasi hiyo inashikwa na Pep Guardiola wa Barcelona ambaye anaingiza euro 10.5 milioni ambazo ni sawa na dola 14.86 milioni.

Nafasi ya tatu kwa upande wa makocha inashikwa na kocha aliyekuwa akiifundisha Inter Milan, Rafael Benitez anayeingiza euro 10.2 milioni ambazo ni sawa na dola 14.43 milioni.

Kocha wa timu ya taifa ya England, Fabio Capello anashika nafasi ya nne akiwa anapata mshahara wa euro 8.5 milioni ambazo ni sawa na dola 12.03 milioni.
 
Ni aibu Yanga kupoteza hati za uwanja wa Kaunda Send to a friend Sunday, 20 March 2011 20:59

nchunga2.jpg
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Lyod Nchunga

MWISHONI mwa wiki uongozi wa Yanga ulisema unashindwa kuendeleza ujenzi wa Uwanja wa Kaunda kwa sababu ya kutojulikana ilipo hati za kumiliki eneo hilo.

Hivi sasa kamati inayoshughulikia ujenzi wa uwanja huo pamoja na jengo la timu hiyo lililopo mtaa wa Mafia na Twiga inaendelea na mchakato wa kuhakikisha inapata hati hiyo ili ujenzi uweze kuanza mara moja.

Mwishoni mwa jana uongozi huo ulitangaza kutumia sh. bilioni 4.5 kujenga jengo la kitega uchumi pamoja na kumalisha ujenzi wa kiwanja kilichopo Kaunda.

Ujenzi wa uwanja na jengo hilo, ulipangwa kuanza mwaka huu mwezi Januari chini ya kampuni ya NEDCO ambayo ilipewa kazi ya kusimamia ujenzi huo.

Huku uwanja huo ukitegemea kuchukua mashabiki 2,500 watakaokuwa wamekaa utakapokamilika na utatumika kwenye mechi baadhi ya mechi za ligi pamoja na mazoezi kwa timu hiyo.

Yanga ilitarajiwa kupata fedha za ujenzi huu baada ya kuandaa hafla na kuwaalika watu maarufu na wanachama wa klabu hiyo ili waweze kuchangia, pia walitarajia kupeleka maombi mbalimbali kwa kampuni za ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kudhamini miradi hiyo miwili.

Kabla ujenzi huo haujaanza uongozi wa Yanga umewataka wanachama kushirikiana nao ili kuhakikisha hati ya uwanja huo inapatikana kwa sababu mpaka sasa haijulikani hati hiyo ipo kwa nani.

Uongozi huo wa Yanga, pia umetoa taarifa kwamba mtu yeyote anayejua hati za uwanja wa Kaunda zipo wapi awasiline na uongozi au atoe taarifa katika kituo chochote cha polisi ili suala la ujenzi wa uwanja wa Kaunda lianze mara moja.

Kwa hakika tumeshangazwa na taarifa hizo za uongozi wa Yanga kushindwa kufahamu zilipo hati hizo muhimu za uwanja wa Kaunda.

Tunasema hivyo kwa sababu tunafahamu ukipoteza hati inabidi utoe taarifa polisi halafu polisi wanakupa cheti kuonyesha umepoteza hati, ambapo cheti hicho utakipeleka mahakamani na mahakama ndiyo yenye haki ya kutoa kibali cha kutangaza kwenye vyombo vya habari kupotelewa kwa hati hiyo.

Hivyo tunaamini uongozi wa Yanga utakuwa umefuata utaratibu huo tulioeleza na kama hawajafanya hivyo,waanze sasa kufuata utaratibu huo ili kuweza kupata hati yao au hati mpya.

Ni wazi kuwa kama uongozi wa Yanga unataka hati yao ya uwanja wa Kaunda inabidi washirikiane na polisi kwa sababu inaonekana kuna itapeli mkubwa unaendela kufanyika Yanga.

Pia, tunashangazwa na taarifa za uongozi wa Yanga kudai hauna hati za uwanja wa Kaunda wakati kila wanapofanya mabadiliko ya uongozi huwa wanakabidhiana nyaraka zote muhimu zinazohusu klabu hiyo.

Tunaamini jambo hili walikuwa wanalifahamu na kama walikuwa hawalifahamu watatushangaza sana kwa sababu wakati Iman Madega amemaliza muda wake wa kuiongoza alimkabidhi nyaraka zote muhimu.

Tunatarajia mwenyekiti wa Yanga hivi sasa, Lloyd Nchunga na mwenyekiti aliyepita, Imani Madega watalitolea ufafanuzi suala hili kwa sababu linarudisha nyuma maendeleo ya klabu hiyoambayo ilitaka kujikombo kwa kujenga uwanja.

Comments




0 #5 uncle 2011-03-23 05:34 hamakweli timu kubwa kama hii na viongozi wasomi wenye taaluma mbalimbali hawajua hati iko wapi inatia shaka sana waliwezaje kupokea madaraka bila hati ? Je walikuwa wanakabkidhiana nini ? Wanachama wa Yanga wafungulieni mashitaka hawa viongozi Jengo litaumwa pamoja na uwanja wa Kaunda wawajaja wamekopea fedha benki na sasa wanajiosha huu ni utapelimkumbwa kwa klabu kubwa kama hii kamata Mchunga, Mwalusako,,Made nge na viongozi wote waliongoza Yanga.
Quote









0 #4 Mushongi Kakuru 2011-03-22 18:10 hapo tumekwisha..
Quote









0 #3 Mdanganyika 2011-03-21 17:15 kuna harufu ya ufisadi hapa
Quote









0 #2 Mzalendohalisi@yahoo 2011-03-21 13:38 Hiyo hati ya Kiwanja viongozi wamechukulia mkopo Benki. Viongozi wa Yanga wanajua hiyo hati ipo Benki gani kwa kuwa ndiyo walioikopea.
Quote









0 #1 KZ 2011-03-21 12:35 ufisadi kila kona.
 
Vyama vya michezo nchini vikubali kujipanga upya Send to a friend Saturday, 19 March 2011 11:57

jk-cecafa.jpg
MARA baada ya Rais Jakaya Kikwete kuchaguliwa kwa mara ya pili kuiongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwishoni mwa mwaka jana, tuliandika maoni kusuhu sekta ya michezo na kuamini atamteua waziri makini atakayeshughulikia masuala ya michezo ili kuongeza tija na ufanisi katika sekta hiyo.

Tulisema nchi inapokuwa na uchumi imara hujionyesha kupitia siasa zake, maisha bora ya wananchi, ukuaji wa uchumi, usimamizi mzuri wa uchumi pamoja na michezo na utamaduni kuwa chanzo cha mapato.

Pia, nchi inapokuwa na uchumi mdogo hujikuta ikiwa na kiwango kikubwa cha watu wasio na ajira, wenye maradhi, waliotenganishwa kwa kuwa na miundombinu mibovu hali inayosababisha watu wengi kukimbilia mijini kwa ajili kujikwamua na maisha na kusababisha makazi holela, watu wasio na makazi, uhalifu na michezo husahaulika.

Tulisema hivyo kwa sababu tulitambua Rais Kikwete ni mpenzi mkubwa wa michezo na anatambua michezo ni chanzo kikubwa kabisa cha mapato. Pia tuliamini wizara inayojishughulisha na michezo ikiwa na waziri anayeijali, basi Tanzania atafanya mapinduzi makubwa katika sekta ya michezo.

Wiki hii, Waziri wa Vijana, Habari na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi alianza kufanya kile ambacho tulitarajia kwa waziri anayehusika na michezo akifanye yaani kuanza kukutana na viongozi wa michezo ili kujadili matatizo mbalimbali yanayokwamisha maendeleo ya michezo nchini.

Waziri huyo mwenye dhamana ya michezo alikutana na viongozi wa vyama vya riadha na viongozi wa mchezo wa ngumi za ridhaa nchini.

Tunaamini alichofanya Waziri Nchimbi ni kitu kizuri na tunamwomba aendelee kukutana na viongozi wa vyama vingine vya michezo ili kufahamu yanayowasibu na kufanyia kazi kwa haraka masuala yanayokwamisha sekta ya michezo kufanya vizuri.

Waziri huyo alipokutana na viongozi wa ngumi pamoja na wale wa riadha aliwaambia wazi kuwa anasikitishwa na tabia za viongozi wa vyama vya michezo kupitapita kuomba fedha badala ya kukaa chini na kuandaa na kupanga mikakati endelevu itakayowaondoa katika hali ya utegemezi.

Nchimbi alisema hayo huku akionyesha viongozi wa michezo kukosa uaminifu, hivyo kushindwa kupata wadhamini ambao wangewawezesha kusaidia timu zao zinapotaka kuingia kambini au kushiriki mashindano ya kimataifa.

Kwa upande wetu kama wadau wa michezo, tunamuunga mkono Waziri Nchimbi kwa kulitambua hilo kwa sababu siku zote kuandaa timu au kuendesha ligi ni gharama kubwa na huhitajika wadhamini kusaidia chama cha mchezo husika kwa sababu wadhamini hutumia michezo kwa ajili ya kujitangaza na kutangaza biashara zao kwa lengo la pande zote kunufaika.

Lakini, hapa nchini ni kinyume chake kabisa kwa sababu wadhamini wamekuwa wakiviogopa vyama vya michezo kwa sababu viongozi wa vyama hivyo wamekuwa wakiongoza kwa mazoea.Pia wamekuwa siyo waaminifu kwa wadhamini hivyo kukosa udhamini.

Viongozi wa vyama vya michezo mbalimbali nchini ukiacha chama cha mchezo wa soka, wamejikuta wakishindwa kutengeneza katiba bora za vyama vyao na kuwa na viongozi wasomi na kutengeneza kanuni za utaratibu wa mapato na matumizi ya fedha na kwa uwazi kwa kutangaza mapato wanayopata kila mwaka.

Kutokana na vyama hivi vya michezo kushindwa kutoa ripoti ya mapato na matumizi kila mwaka vimejikuta vikishindwa kuandika mapendekezo ya kuyashawishi makampuni mbalimbali kutoa udhamini katika vyama vyao.

Kampuni ili iweze kudhamini chama cha mchezo, inataka kupata taarifa za benki, kanuni za fedha, akaunti zilizokaguliwa na mipango ya biashara.

Kwa maana hiyo, haiwezekani chama cha mchezo wowote nchini kikose wadhamini kama kina viongozi wasomi wanaohakikisha wanakuwa na taarifa za benki , kanuni za fedha, akaunti zilizokaguliwa na mipango imara ya biashara kwa sababu makampuni yapo mengi nchini ambayo yanajitangaza kila siku katika vyombo mbalimbali vya habari na kutoa matangazo mengi.

Tunaamini viongozi wa michezo waliopo wa michezo wasipotafuta udhamini na kutegemea makisio ya kuomba fedha ili kuweka timu kambini kwa ajili ya kwenda kushiriki mashindano, wafahamu wanajidanganya wenyewe kwa sababu michezo haindelei kwa kusaidiwa, ila kwa udhamini wa makampuni ambayo hutoa fedha kwa makubaliano maalumu.
 
Ukaidi wa dereva waua wasanii 11

Imeandikwa na John Nditi, Morogoro; Tarehe: 22nd March 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 646; Jumla ya maoni: 0








UKAIDI wa dereva wa basi dogo aina ya Coaster ndiyo uliosababisha vifo vya wasanii 13 wa kikundi cha taarabu cha Five Stars Modern Taarab cha Dar es Salaam.

Inadaiwa kuwa dereva huyo aliyetajwa kwa jina moja la Chala alikaidi ushauri wa abiria waliomtaka apunguze mwendo, akalogonga lori la mizigo lililokuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara kuu ya Iringa – Morogoro katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

Basi hilo namba T 351 BGE lililokuwa katika mwendo mkali liligonga lori aina ya Scania namba T 848 APE lililokuwa na tela namba T559BDL lililokuwa limesheheni mbao na kuegeshwa katika kijiji cha Doma, wilayani Mvomero baada ya kuharibika.

Katika ajali hiyo watu 12 walikufa papo hapo na mwingine aliaga dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Marehemu alikuwa mwimbaji katika bendi hiyo, ndugu zake wamemtambua kuwa ni Haji Mzaniwa ( 38).

Miongoni mwa waliokufa ni pamoja na Meneja wa bendi hiyo, Nassoro Madenge , mwimbaji mahiri wa taarab, Issa Kijoti na wasanii wengine mashuhuri.

Kijoti ndiye aliyeimba wimbo maarufu wenye maneno Nichumu Nichumu tena, Mwaah, amekufa siku yake ya kuzaliwa, alizaliwa Machi 21, 1985.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, Ibrahim Mwamakula, alisema ajali hiyo ilitokea saa 2.30 usiku.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, dereva huyo aliligonga lori hilo wakati akijaribu kukwepa lori lingine lililokuwa likitoka mbele yake ambalo pia ni Scania lenye namba T 530 BHY na tela namba T 182 BKB.

Baada ya kuona hali hiyo dereva alibabaika, basi likayumba na kujibamiza kwenye lori hilo na paa la basi hilo kung'oka.

"Ni ajali mbaya iliyohusisha magari matatu, na waliokufa wote ni waliokuwa kwenye basi dogo la wasanii wa Five Stars na kusababisha majeruhi tisa kulazwa," alisema Mwamakula.

Kati ya waliokufa 10 ni wanaume na watatu ni wanawake, ambapo majeruhi ambao wote ni wasanii waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa ni pamoja na Mwanahawa Ally (55) wa Kundi la East African Melody ambaye alikuwa mwalikwa katika safari hiyo , Susana Benedict (32), Zena Mohamed (27), Samrla Rajab (22) na Mwanahawa Hamis ( 36) walioko wadi namba
tatu.

Akihojiwa jana akiwa hospitalini alikolazwa, Mwanahawa alisema, dereva alionywa na abiria kuhusu mwendo wake wa kasi, lakini akakaidi na kuendelea na uendeshaji wake mbovu uliowasababishia ajali.

"Kwa kweli dereva wa gari letu alikuwa akiendesha kwa kasi tangu tulipokuwa kukiteremka kwenye milima ya Kitonga … niliingiwa na wasiwasi juu ya mwendo wake na ndipo tulipofika karibu na Doma, tumepata ajali mbaya sana, iliyosababisha wenzetu 13 kufa na sisi kama watu tisa kupata majeraha wengine ni makubwa," alisema Mwanahawa.

Alithibitisha kuwa dereva wa gari lao alitaka kulipita lori lililoharibika, lakini ghafla kukawa na gari lingine likitoka mbele yao, "aliligonga hili lililobeba mbao na kuhama njia kwenda kujigonga usoni mwa lori lingine na kuangukia bondeni," alisema msanii huyo mkongwe wa muziki huo.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wasanii wengine waliolazwa katika hospitali hiyo ni Ally Juma (25), Rajabu Kondo ( 25), Issa Hamis, Shaaban Hamis (41) na Msafiri Musa (22).

Wakizungumza katika eneo la ajali usiku huyo, mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo, Joseph Njiwa na Nania Msemwa, ambao walikuwa na gari kubwa la mizigo wakitoka Dar es Salaam kwenda Makambako, Iringa, kwa nyakati tofauti walisema ajali hiyo ilitokea saa mbili usiku.

"Ni ajali ya kutisha, tumeshuhudia basi dogo hilo likigonga lori kwa nyuma na kuhama na kwenda kugonga kichwa cha lori lingine, na watu walikatika vichwa na viungo vyao … hata sisi tuliingiwa na hofu kubwa ya kutoa msaada, lakini tulikazimika kufanya hivyo," alisema Msemwa.

Njiwa alisema, iwapo dereva wa basi dogo angekuwa na mwendo wa wastani , ajali hiyo ingeepukika kwa kusubiri lori hilo lililokuwa katika upande wake kupita na yenye kuendelea na safari hiyo.

Hata hivyo alitoa lawama kwa lori lililoharibika eneo hilo kwa kushindwa kuweka alama za kuashiria kuharibika na hivyo kuepusha ajali hiyo.

Baadhi ya ndugu wa marehamu waliwasili usiku wa manane siku ya tukio baada ya kuarifiwa na majeruhi na kuchukua hatua za kuchukua miili ya wasanii hao kwa ajili ya kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa mazishi.

Hata hivyo miili ya marehemu hao ilihifadhiwa katika mochwari ya Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya utaratibu mwingine zaidi.

Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi kutokana na vifo hivyo.

"Binafsi nimeguswa na msiba huu kwa vile umetupotezea wasanii ambao walikuwa na mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza sanaa ya muziki wa taarab nchini kwetu. Hili ni pigo kubwa si kwa usanii wa taarab bali kwa Taifa letu zima la Tanzania," alisema Rais Kikwete katika salamu zake.

Aliongeza: "Nakutaka Waziri kupitia kwako ufikishe salamu zangu hizi za rambirambi kwa ndugu wa wafiwa wote. Wajulishe kuwa moyo wangu uko nao katika wakati huu mgumu na kuwa msiba wao ni msiba wetu sote."

Rais Kikwete alisema anamwomba Mwenyezi Mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu wote huku akiwaomba waliopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo mbaya kuwa na moyo wa uvumilivu, ujasiri na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Vilevile aliwaombea kwa Mwenyezi Mungu wote waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo mbaya wapone haraka ili waweze kurejea katika hali yao ya kawaida na kuungana tena na familia, ndugu, jamaa na marafiki zao.

Waziri Nchimbi amesema, amepokea kwa mshituko mkuvwa taarifa za ajali hiyo, na kwamba ni pigo kubwa kwa tasnia ya muziki wa taarab nchini.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali hiyo na linaungana na familia za wafiwa na wasanii wote nchini kwa maombolezo ya msiba huu mkubwa na wa kihistoria.

"Kifo cha wasanii hawa ni pengo kubwa kwa familia na sekta ya sanaa nchini, kwani kupungukiwa na wasanii wabunifu 13 kumerudisha nyuma kimaendeleo sekta hii nchini na pengo hilo haliwezi kuzibika kwa njia yoyote iwayo," ilisema taarifa ya Basata.

Baraza limetoa Sh. 500,000 za rambirambi kwa kundi la Five Star Modern Taarab ili zigawanywe kwa wafiwa na kusaidia shughuli za msiba huo mkubwa katika tasnia ya sanaa nchini.

Mmoja wa waratibu wa shughuli za msiba huo, Kiongozi wa African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka amesema, wengi waliokufa alikuwa ni wasanii vijana, na kwamba, kabla ya kujiunga na bendi hiyo walikuwa katika bendi nyingine ya taarab iitwayo Jahazi Modern Taarab.

Kiongozi wa Jahazi, Mzee Yusuf, amesema, vifo vya wasanii hao ni janga la taifa kwa kuwa vinawahusu hata wasiopenda muziki.

"Hili janga si la Five Stars, ni letu sote Watanzania, wapenda muziki na wasiopenda muziki" amesema na kuongeza kuwa wote waliokufa aliwahi kufanya nao kazi kwa muda mrefu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom