Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Tamim, Ashraf kupima uzito Send to a friend Thursday, 10 March 2011 20:04

Imani Makongoro
MAHASIMU wawili katika ngumi za kulipwa wa uzani wa juu, Ashraf Suleiman na mpinzani wake Awadh Tamim bingwa wa Afrika Mashariki na kati leo wanapima uzito tayari kwa pambano lao lililopangwa kufanyika kesho.

Zoezi hilo la kupima uzito litakwenda sambamba na kupima afya huku pambano hilo likitarajiwa kutimua vumbi kesho saa mbili usiku kwenye Ukumbi wa DDC Mliman Park, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Mabondia hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitambiana huku Awadh bingwa mtetezi akiahidi kuurudisha mikononi mwake mara ya tatu mfululizo.

Ofisa habari wa Kampuni ya Ulinzi ya Aurora waandaaji wa pambano hilo, Shomari Kimbau alisema kuwa mabondia wote wako fiti huku wakiendelea kujifua kwa ajili ya pambano hilo.

Alisema kuwa pambano hilo litakuwa na ulinzi wa kutosha tofauti na mwaka jana ambapo mabondia hao walitunishiana msuli ingawa mshindi hakupatikana kufuatia pamabno hilo kuvunjika baada ya mashabiki wa pande zote mbili kufanya vurugu.
 
Mwananchi FC, Uhuru kundi moja NSSF Send to a friend Thursday, 10 March 2011 20:03

Sweetbert Lukonge
TIMU ya soka ya Mwananchi FC, imetupwa kwenye Kundi la Kifo la Michuano ya Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii nchini (NSSF) inatarajia kuanza kutimua vumbi Machi 19.

Bingwa wa michuano hiyo mwaka huu, anatarajia kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 3.5 kutoka kwa wadhamini wa michuano hiyo, NSSF,
ambayo michezo hiyo itafanyika katika viwanja vya TCC Changombe na Chuo Kikuu cha Ualimu, DUCE.

Mwananchi FC imepangwa Kundi C pamoja na Uhuru Publications, Sahara Communication, Tumaini Media na Mwanahalisi kwenye michuano itakayoendeshwa kwa mtindo wa Ligi.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori alisema jijini jana kuwa katika michuano hiyo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha sh3.5milioni huku mshindi wa pili akiondoka na sh2.5milioni.

Mshindi wa tatu katika mashindano hayo ataibuka na sh1.5 milioni kwa upande wa wanaume, kwa upande wa wanawake mshindi wa kwanza ataondoka na na sh3milioni.

Mshindi wa pili ataibuka na kitita cha sh2milioni na watatu kuondoka na sh1milioni wakati mchezaji bora na wafungaji bora kwa wanawake na wanaume wataondoka na kitita cha Tsh 250,000 kila mmoja.

Shirika hilo jana limekabidhi vifaa vya michezo kwa timu 17 za wanaume na 11 za wanawake tayari kwa michuano hiyo mikubwa kwenye vyombo habari.
 
Mwaikimba amkuta Ngassa ufungaji Send to a friend Thursday, 10 March 2011 20:02

Calvin Kiwia
MSHAMBULIAJI wa Kagera Sugar, Gaudence Mwaikimba ameendeleza kasi yake ya ufungaji msimu huu baada ya kuzifumania nyavu mara12 kwenye Ligi kuu ya Vodacom na kumfikia Mrisho Ngassa wa Azam FC.

Mwaikimba tangu alipotemwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars amekuwa na mabadiliko makubwa kwenye kuzifumania nyavu katika mzunguko huu wa lala salama.

Nyota huyo wa zamani wa Ashanti ya Ilala na Yanga, juzi aliifungia Kagera mabao yote mawili dhidi ya Toto African ya Mwanza mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Mabao ya Toto African yakifungwa na kiungo Maregesi Mwangwa na mkongwe Sammy Kessy huku yale ya Kagera Sugar yakisukumizwa wavuni na Mwaikimba.

Kocha wa timu hiyo, Mrange Kabange ameliambia Mwananchi jana kwa simu kuwa amefurahishwa na kiwango alichonacho Mwaikimba kwani amekuwa akizifumania nyavu kila mchezo isipokuwa mchezo wa pekee baina yao na Yanga waliofungwa bao 1-0.

"Ni jambo la kujivuni kwangu kumwona Mwaikimba anafunga mabao kila mchezo na kuipa timu yangu ushindi ama sare katika ligi," alisema Mrange.
 
Spurs 'inaishi kweny ndoto' Send to a friend Thursday, 10 March 2011 20:00

LONDON, England
KOCHA Harry Redknapp amekiri kuwa Tottenham ipo kwenye nchi ya ahadi baada ya kufanikiwa kufuzu kwa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AC Milan.

Vijana hao wa Redknapp walionekana kuwa kwenye wakati mgumu mbele ya Milan kwenye Uwanja wa White Hart Lane, lakini walifanikiwa kupata suluhu na kufuzu kwa 16 bora baada ya kupata bao moja kwenye mchezo wa kwanza shukrani kwa Peter Crouch aliyefanya vitu vyake kwenye uwanja wa San Siro.

Wakati Redknapp alipowasili White Hart Lane, na kuichukua timu hiyo ikiwa kwenye janga la kushuka daraja, lakini sasa timu hiyo imejiwekea ndoto ya kucheza fainali ya Ulaya kwenye Uwanja wa Wembley.

Baada ya miaka mingi ya kufunikwa na kivuli cha mahasimu wao Arsenal, sasa Tottenham imerudi kwenye mstari wake, huku Gunners watakuwa mashuhuda wa michuano hiyo kwenye televisheni baada ya kutolewa na Barcelona, Redknapp amewataka mashabiki wake kuongeza ushirikiano kwa kufikia mafanikio hayo.

"Sijui ni wapi tutaishia, lakini kwa sasa tumefanya kazi kubwa," alisema Redknapp. "Kama ningesema miaka miwili iliyopita kwamba tutafikia kwenye nane bora ya Ligi ya Mabingwa mgeweza kuniambia kwamba ninawazimu.

"Mashabiki wetu sasa wanaishi. Kwa tulipofika sasa ni kitu cha kusadikika tu. "Hii ni mara ya kwanza kwenye historia ya klabu hii kwenye Ligi ya Mabingwa. Kufanya hichi tulichokifanya, kwanza tulikuwa kwenye kundi gumu na tumeweza kuifunga AC Milan, watakuwa wakifurahi kwa muda mrefu zaidi.
xxxxxxxx
Raul ashangilia kuibeba Schalke
MUNICH, Ujerumani
MSHAMBULIAJI nyota wa Schalke 04, Raul amefurahishwa na kitendo cha timu yake kufuzu kwa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa ushindi wa 3-1 na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2 dhidi ya Valencia.

Mshambuliaji huyo mkongwe wa Hispania, aliyewahi kutwaa taji hilo mara tatu akiwa na Real Madrid katika mwaka 1998, 2000 na 2002, aliongeza kusema kuwa sasa wamefurahishwa na kupiga hatua hiyo kubwa.

"Ulikuwa mchezo mgumu, lakini ukiwa sawa kwa pande zote," alisema Raul, ambaye yuko kwenye msimu wake wa kwanza na Schalke.

"Hata hivyo sisi tulikuwa na bahati zaidi. "Nimefurahi kwa sababu ili ni jambo zuri zaidi kwangu.

"Tunasubili kuona ni nani tutakutana naye kwenye robo fainali, lakini si jambo linalotuumiza sana kichwa kwa sababu ni sehemu ya mchezo huo.."

Mara ya mwisho kwa klabu hiyo kutinga kwenye hatua hiyo ni mwaka 2008, Schalke ilijihakikishia nafasi yake kwa mabao yaliyofungwa na winga Jefferson Farfan na mshambuliaji Mario Gavranovic.

Wenyeji hao walilazimika kusawazisha kwanza baada ya Valencia kupata bao la mapema kupitia Ricardo Costa.

"Ni vigumu kuanza kupambana na presha toka mwanzo, lakini baada ya kufungwa 1-0 hatukuwa na chakupoteza," alisema kocha wa Schalke, Felix Magath.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom