Uongozi Simba wamkomalia Mbaga Send to a friend Monday, 07 March 2011 12:38
Clara Alphonce na Doris Maliyaga
HUKU vumbi la mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga likitua, uongozi wa klabu ya Simba umemkomalia mwamuzi Oden Mbaga.
Mwenyekiti wa klabu hiyo, , Ismail Aden Rage amesema kuwa anatarajia kumshitaki mwamuzi huyo katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Rage alidai juzi kutoridhishwa na maamuzi ya Mbaga kila anapochezesha mechi inayoihusu timu yake.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaamu juzi timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Rage aliiambia Mwananchi kuwa katika uchunguzi ambao ameufanya unaonyesha wazi kuwa mwamuzi huyo amekuwa haitendei haki Simba kila anapochezasha iwe katika mechi nyingine tofauti na Yanga, jambo ambalo alidai kuwa linalenga kuiua timu hiyo ishindwe kufanya vizuri kwenye ligi hiyo.
ìTunatarajia kumshitaki Mbaga TFF kutokana na kutolizishwa na maamuzi yake kila anapochezesha mechi zinazoihusu Simba ukilinganisha na waamuzi wengine.
ìKatika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Yanga kwa hakika mwamuzi huyo alilenga kutuumiza kutokana na kutokuwa na maamuzi mazuri kwa upande wetu, hivyo kufuatia hali hiyo tunatarajia kumshitaki TFF na tunacho subiri ni kupata baadhi ya mikanda ya video ya mechi zote alizochezesha dhidi yetu,î alisema Rage.
Alisema katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Yanga mwamuzi huyo alikuwa haitendei haki timu yake na kuongeza kuwa wapinzani wao walikuwa wakifanya makosa ya wazi na hakuchukua hatua yoyote.
Naye makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Godfrey Nyange ëKaburuí alieleza kumshangaa mwamuzi Mbaga akidai kuwa kiwango chake kilikuwa kidogo.
Alisema Super Sport ilimuumbua mwamuzi huyo kutokana na maamuzi yake yasiyo ya halali baada ya kuwekwa wazi.
Aliiambia Mwananchi kuwa, maamuzi yake hayakuwa sahihi na kama si televisheni hiyo ya Afrika Kusini iliyokuwa inarusha wazi kurudia tukio la bao la Simba yangekuwa mengine.
"Mechi ilikuwa nzuri, lakini mwamuzi aliuharibu mchezo hasa bao lililofungwa na Simba, yeye alishindwa kuamua hadi mshika kibendera wa pili alipoingilia kati,ííalisema Kaburu.
ëíHii ni kwa sababu ya televisheni ile ilimuumbua baada ya kurudia tukio lile mara kwa mara naweza kusema kiwango cha waamuzi wetu bado ni kidogo sana,ííaliongeza Kaburu.
Katika mchezo huo Yanga ilikuwa ya kwanza kupata bao kwa penalti iliyotokana na Davies Mwape kudondoshwa eneo la hatari na Juma Nyosso na beki Stephano Mwasika kufunga wakati Simba ilisawazisha kupitia kwa Mussa Hassan ëMgosií.