Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,508
- 911,249
- Thread starter
-
- #9,541
Alex Msama afuta tamasha Mwanza
na Mwandishi wetu
WARATIBU wa tamasha la Pasaka wameamua kulifuta tamasha la Mwanza na sasa tamasha hilo litafanyika katika miji ya Dar es Salaam, Dodoma na Shinyanga pekee.
Mwenyekiti wa Kamati ya Msama Promotions waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama, alisema kuwa jijini Dar es salaam tamasha hilo litafanyika Aprili 24 na mjini Dodoma litafanyika siku ya Aprili 25 ambayo ni Jumatatu ya Pasaka na Shinyanga litafanyika Aprili 26.
Alisema sababu za kufuta onyesho la Mwanza zimekuwa nje ya uwezo wao hivyo wakawaomba radhi wapenzi na mashabiki wa nyimbo za Injili kwa kufutwa kwa onyesho hilo la Mwanza.
"Tunasikitika kwamba tumelazimika kulifuta tamasha la Mwanza, tunawaomba radhi wote ambao wameathiriwa na kufutwa huko lakini tunawaahidi kuboresha katika maeneo ambako litafanyika," alisema Msama.
Aliwaomba wapenzi wote wa nyimbo za Injili kujitokeza kwa wingi siku ya Pasaka Aprili 24, ambapo tamasha hilo litafanyika kwenye Ukumbi wa Dimond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Msama alisema tamasha la Pasaka la mwaka huu litashirikisha waimbaji kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, DR Congo, Afrika Kusini, Zambia na Tanzania na lengo lake kubwa ni kukusanya fedha za kuwasaidia watoto yatima pamoja na mitaji ya wanawake wajane kote nchini.
Aidha, pia fedha zitakazopatikana kutokana na matamasha hayo zitatumika kuwasaidia wahanga wa mabomu yaliyotokea katika kambi ya jeshi Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.