Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Sikubaliani nao- Kaijage Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 20:20

Sosthenes Nyoni

ALIYEKUWA ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Florian Kaijage ameibuka na kupinga ripoti ya kamati ya uchunguzi ya tukio la kutopigwa nyimbo za taifa wakati wa mechi Taifa Stars na Morocco iliyofanyika Oktoba 9 mwaka jana ambayo inamtuhumu kuwa mhusika mkuu.

Kamati hiyo iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hamidu Mbwezeleni ilitoa ripoti ya uchunguzi Jumanne wiki hii na kumtaja Kaijage kuwa chanzo cha tukio hilo kwa madai alishindwa kutekeleza majukumu yake kama alivyoagizwa na kamati ya maandalizi ya mchezo huo iliyokuwa chini ya Leonard Thadeo.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam jana, Kaijage alisema hakubaliani na utaratibu uliotumiwa na kamati ya uchunguzi hasa namna ya kutoa taarifa zake baada ya kumaliza kazi iliyopewa na TFF.

Alisema kwa uzoefu wake na akiwa ameshuhudia kamati mbili zilizoundwa kuchunguza matukio ya timu ya taifa ya umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys kudanganya umri na waamuzi kula rushwa,mara baada ya kamati ya Mbwezeleni kumaliza uchunguzi wake ilitakiwa kuwasilisha taarifa TFF ambao ndio walitakiwa kuchukua hatua.

"Mimi sikuwa mwajiriwa wa kamati bali TFF,ilichotakiwa kufanya kamati ni kuikabidhi TFF taarifa badala ya wao kuutangazia umma,"alisema Kaijage.

Kaijage alisema ameshindwa kuyaelewa matokeo ya kamati hiyo hasa kwa kuwa ni wajumbe wawili tu kati ya watano walioteuliwa ndio alionana nao kwa ajili ya mahojiano.

"Sote tunajua kamati ilikuwa na wajumbe watano walioteuliwa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga, kimsingi kamati ilinihoji mara mbili, mara ya kwanza ilikuwa Jumanne Januari 25 kuanzia saa sita 6 mchana na mara ya pili ilikuwa Februari 12, 2011, mara zote mbili ni mwenyekiti na katibu wa kamati ndiyo walionihoji. Sikutarajia mara zote mbili wajumbe wangekuwa wawili tu hasa ukizingatia tayari TFF ilikuwa imenitaja kama mhusika mkuu,"alisema Kaijage.

Alisema hata shahidi aliyeelezwa na kamati kwamba alidanganya kwa nia ya kuwapumbaza wajumbe yeye hakuwahi kumwita wala kumpendekeza na kudai kama shahidi alifanya hivyo ilikuwa ni kwa matakwa yake.

Aidha, alisema ameshangazwa na kitendo cha kuondoka kwa fundi ambaye ni raia wa China kwenye mitambo na kuonekana ni kosa la lake yeye (Kaijage).

"Ifahamike kuwa fundi huyo wa mitambo alikuwa anaonana na ofisa habari siku ya mchezo kwa sababu ndiyo sehemu yake ya kazi na uhusiano baina yetu ni kwenye mitambo, pia tukumbuke kwamba hajui Kiingereza zaidi ya Kichina, sasa najiuliza kama alikuwa anamtafuta Kaijage alimuuliza nani na yeye anaongea Kichina tu? Kosa langu hapa ni lipi,ili ni swali ambalo halina jibu,"alisema Kaijage.

Katika mechi hiyo ambayo iliyoshuhudiwa pia na Rais Jakaya Kikwete, CD iliyopaswa kupigwa nyimbo za taifa za Morocco na Tanzania ziligoma na kusababisha shughuli hiyo kufanywa kipindi cha pili cha mchezo, hivyo Tenga kutangaza kumsimamisha kazi kwa Kaijage .

 
Tuhuma za uhusiano kimapenzi nje ya ndoa zamkumba Ngassa Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 20:19

Jackson Odoyo

WAKATI timu yake ya Azam leo ikisaka nafasi ya kurudi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom katika mchezo dhidi ya Majimaji, mshambuliaji wake mahiri Mrisho Ngassa amekumbwa na kashfa ya kimapenzi.

Ngassa anadaiwa kukutwa akiwa na mwanadada mwingine nje ya ndoa yake, kisha kunusurika kupigwa na mama mzazi wa mkewe (mkwe).

Tukio hilo ambalo lilivuta umati wa watu linadaiwa lilitokea Yombo Dovya, Manispaa ya Temeke na baadaye mkasa huo kuhamia Mtoni Sabasaba, nyuma ya viwanja vya maonyesho, Sabasaba anapoishi mwanasoka huyo kinara wa mabao.

Akisimulia mkasa huo kwa Mwananchi, mke wa mchezaji huyo, Latifa Mrisho Ngassa alisema kwa simu, ì Kama wewe ni mwandishi wa habari, kimbia njoo hapa Sabasaba na ikibidi chukua hata pikipiki ili uwahi, uje na kamera umtoe huyu jamaa kwani nimemfumania na ameamua kujifungia ndani."

Hata hivyo, baada ya dadika 30 mwanadada huyo akapiga tena simu akisema kwamba mjumbe wa nyumba kumi alikuwa tayari ameshafika katika eneo la tukio kwa ajili ya kuwasuluhisha.

ìHuyu jamaa yangu amezidi kunidhalilisha kwani hata majirani wameshamchoka kwa tabia yake hii ( si vyema kuitaja gazetini),îaliongeza mke wa mchezaji huyo.

Ndipo Mwananchi ilipoamua kumtafuta mke wa mshambuliaji huyo kwa ajili ya kufahamu undani wa suala hilo, ndipo alipoeleza, ìHuyu ni mme wangu wa ndoa tena ndoa iliyofungwa kihalali kabisa, lakini kwa kipindi kirefu sasa amekuwa akinisumbua kwa tabia zake.î

ìKweli mimi nimechoka na tabia zake kiasi kwamba siwezi kuendelea kuvumilia ujinga wake huu kama ndio imeshindikana siwezi kulazimisha ndoa ni bora niondoke nirudi kwetu nikafiche aibu hii.

Alisema baada ya kupata taarifa kutoka kwa majirani kule Dovya alimchukua mama na mjomba wake, kisha wakaenda eneo la tukio, lakini walipofika mumewe akajifungia ndani na kukataa kutoka.

ìKwa sasa mimi ninakaa kwetu Tabata, lakini kila wakati majirani wamekuwa wakiniambia juu ya tabia zake za kukutwa na wanawake na wakati mwingine anaondoka nao kwenda kustarehe huku mimi akiniacha,îalidai mke huyo wa mwanasoka.

Alipoulizwa juu ya hatma ya ndoa yake, alisema ni mapema mno kuzungumzia hilo kwa sababu liko kwenye ngazi ya familia yao, hivyo ni vyema asubiri kwanza mpaka familia itakapokaa na kulizungumzia.

Lakini, Mwananchi ilipofika katika eneo la tukio saa 12:30 jioni na kukuta wahusika wameshatawanyika baadhi ya majirani pamoja na mjumbe wa nyumba kumi walithibitisha kuwapo kwa tukio hilo.

ìNi kweli mama mkwe alikuja juu na kupiga mlango huku akimtaka mkwe (Ngassa) atoke na kutoa talaka ili aondoke na binti yake kwani amechoshwa na tabia hizo chafu na za kudhalilishwa anazofanyiwa binti yake na kudai kwamba kila anapouliza binti yake anaishia kupigwa,î alieleza mmoja wa majirani.

Mwananchi ilimtafuta mama mkwe huyo, Octavia Kangati ambaye alisema: ìNi kweli tulifika nyumbani kwa mkwe wangu ili kufahamu undani wa tukio hilo, lakini sikuthubutu kujaribu kumpiga.î

ìMimi ni mama siwezi kuthubutu kumpiga mkwe wangu, bali hayo ni maneno ya mitaani wala mjomba wake hakumpiga, bali katika kusuluhisha tofauti zao kukatokea kupishana kwa maneno,îaliongeza mama huyo.

Hata hivyo, alipoulizwa chanzo cha tukio hilo alikataa kulizungumzia kwa madai kuwa alikuwa safarini kuelekea Kibaya, Kiteto mkoani Manyara ila akamtaka mwandishi wa Mwananchi amtafute siku nyingine.

Kwa upande wake, Ngassa alipoulizwa kuhusu tukio hilo alijibu, ìNi kweli nilikuwa na dada mmoja ambaye alihitaji kupanga nyumba katika nyumba yangu na alipoletwa kwangu na madalali nikamchukua hadi kwenye nyumba iliyopo Yombo Dovya, ghafla nikaona kundi la watu akiwemo mke wangu pamoja na mama yake.î

ìKaka, haya mambo ni magumu, tena yana lengo la kuniharibia, kunidhalilishana, mimi siwezi kufanya hivyo kwa sababu mke wangu nampenda, kwanza habari hizi mmezipata wapi, kwa sababu ni saa mbili tu tangu yalipotokea," alisema Ngassa.

Hata hivyo, alipotakiwa kueleza ukweli juu ya kunusurika kupigwa na mkwewe, mchezaji huyo alishindwa kulizungumzia na kumtaka mwandishi arudi siku nyingine ili apate ufafanuzi.

ìSiwezi kuzungumzia suala hilo kwa sasa nakuomba uniache kwanza kwa sababu kichwa changu kina mambo mengi, tafuta siku nyingine, lakini sio leo,îalisema Ngassa na kuingia kwenye gari na kuondoka katika eneo hilo.

Baba mzazi wa mchezaji, Khalfan Ngassa huyo alipotafutwa na Mwananchi alisema kwa simu, ìNimepokea taarifa za tukio hilo, ni masikitiko sana kwa sababu hayo mambo yana lengo la kumharibia mwanangu maisha yake ya soka.î

ìSifahamu lolote kuhusu suala hilo, lakini nitawatafuta wanangu wote niongee nao kwani nisipofanya hivyo nitachangia kumharibia mtoto wangu maisha yake hasa katika kipindi hiki cha kuisaidia timu yake kupata ubingwa wa Ligi ya Vodacom,îalisema Mzee Ngassa.

 
Mndela, JKT Queens zajitoa ligi ya wanawake Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 20:18

Salome Millinga

BINGWA mtetezi wa ligi ya soka ya wanawake mkoa wa Dar es Salaam timu ya Mndela Queens wamejitoa kwenye ligi hiyo inayoendelea kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo imejitoa kutokana na madai ya kutoona faida ya mashindano hayo na kuishia kucheza ligi ya mkoa bila kucheza ngazi ya taifa na pia kuchelewa kupewa taarifa.

Nayo timu ya JKT Queens pia imetijitoa kwenye ligi hiyo kutokana na majukumu ya kikazi.

Akizungumza na Mwananchi kocha wa Mndela Queens, Riziki Shawa alisema "Mfumo unaoendeshwa na Chama cha Soka la Wanawake Dar es Salaam ni mbaya na kwa sababu wanatumia gharama kubwa kuwasafirishia wachezaji wanaotoka mikoani.

"Mimi sioni faida yoyote ya ligi hiyo kwasababu tunaishia kushiriki ligi ya mkoa tu na kuambiwa tutacheza ligi ya taifa, matokeo yake hukuna chochote kinachofanyika na kupoteza gharama zetu bila faida yoyote," alisema Shawa.

"Tumeshiriki ligi hiyo miaka mitatu mfululizo na zote tumefanya vizuri mwaka 2007 tumekuwa washindi wa tatu, mwaka 2008 tumekuwa washindi wa pili, mwaka 2009 tumekuwa washindi wa kwanza na kuwa pia mabingwa wa Mkoa wa Dar es Salaam," alisema.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Soka la Wanawake Dar es Salaam (DWRFA), Stephania Kabumba alisema timu hiyo itashushwa daraja kutokana na kushindwa kutoa taarifa ya kujitoa kwenye ligi hiyo.

"Timu hiyo imeshindwa kutoa taarifa hiyo inabidi ligi ijayo waanze kucheza ngazi ya mkoa na kwa upande wa timu ya JKT Queens ilituma barua ya kutoshiriki ligihiyo kutokana na mujukumu ya kazi waliyonayo," alisema Kabumba.

Ligi hiyo inaendelea leo kwenye Uwanja wa Karume kwa mechi kati ya Uzuri Queens na Emima Queens na baadaye jioni kwa mchezo baina ya Sayari Women na Tanzanite Queens.

 
AC Milan yashinda 3-0 yajiimarisha kileleni Serie A Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 20:11

MILAN, Italia

MABAO ya Zlatan Ibrahimovic, Kevin-Prince Boateng na Alexandre Pato yaliipa AC Milan ushindi mnono dhidi ya Napoli walioko katika nafasi ya tatu ya Ligi Kuu Italia, Serie A.

Ibrahimovic alifunga bao katika dakika ya 49 kwa penalti baada ya mchezaji wa Napoli, Salvatore Aronica kuunawa mpira katika eneo la hatari na Boateng alifunga la pili katika dakika ya 77 baada ya kuunganisha krosi ya Pato.

Katika dakika ya 79, Pato aliipatia Millan bao la tatu baada ya kupiga shuti kali katikati ya mabeki wawili wa Napoli akiwa nje ya eneo la penalti.

Kwa matokeo hayo, Milan inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 58 ikifuatiwa na mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Inter Milan wenye pointi 53.

Napoli bado inashikilia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 52 na Lazio inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 48.

Huko Stoke nchini England, West Bromwich Albion imepanda na kujihakikishia nafasi ya kujiondoa kwenye janga la kushuka daraja msimu huu kwenye Ligi Kuu ya England, baada ya mshambuliaji wake, Carlos Vela kuisawazishia timu yake bao katika dakika ya 86 katika mchezo dhidi ya Stoke na kutoka 1-1.

Awali, Rory Delap aliipatia Stoke bao la kuongoza katika dakika ya 53, lakini West Bromwich walisawazisha bao huku bao hilo la Vela likionyeshwa kwenye marudio ya televisheni inaonekana mshambuliaji huyo alikuwa ameotea.

Vela, raia wa Mexico anayechezea West Brom kwa mkopo akitokea Arsenal, aliifungia pia bao West Brom katika mechi dhidi ya Wolverhampton wikiendi iliyopita.

Pia, huko Malaga nchini Hispania, Malaga imeondoka katika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi kuu ya huko baada ya kuichapa Almeria bao 3-1.

Hivi karibuni Malaga ilicheza mechi saba mfululizo bila kupata ushindi.

Walikuwa ni Almeria ambao walikuwa wa kwanza kupata bao ambalo lilifungwa Sofiane Feghouli katika dakika ya nane, lakini Malaga waliweza kupata mabao yao kutoka kwa Enzo Maresca katika dakika ya 52, Jose Rondon katika dakika ya 78 na Juanmi Jimenez kwenye dakika za majeruhi.

Katika mechi hiyo,Almeria ilimaliza ikiwa na wachezaji pungufu ya wachezaji wawili baada ya Jose Ulloa kupewa kadi za njano mbili, pia Antonio Luna alipewa kadi nyekundu katika dakika ya 88.

Malaga hivi sasa ina pointi 23 na inashika nafasi ya pili kutoka chini kwenye msimamo wa ligi kuu ya Hispania.

 
Uefa yaipa nafasi zaidi Ujerumani, Italia yashuka Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 20:13

ZURICH, Uswisi

SHIRIKISHO la Soka Ulaya (Uefa) limeipa nafasi zaidi za Ligi ya Mabingwa Ujerumani kuanzia msimu wa 2012/13 huku Italia ikipunguziwa nafasi ilizokuwa nazo.

Ujerumani imeipiku Italia na kupanda chati katika viwango vya ubora Uefa vinavyotokana na ubora wa ligi zao.

Kuanzia msimu wa 2012, timu nne za juu wa ligi ya nchi hiyo, Bundesliga zitashiriki ligi ya Ulaya badala ya tatu, wakati mshindi wa tano na sita watashiriki michuano ya Europa League.

"Italia imeporomoka, haishiki tena nafasi ya tatu msimu huu," lilieleza Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFL) katika taarifa yake juzi. "Kutokana na viwango hivyo vipya, timu tatu za ligi ya Ujerumani (Bundesliga) zitafuzu moja kwa moja, hatua ya makundi na ile ya nne itaanzia mtoano."

Katika uamuzi huo, timu tatu za Ligi Kuu ya Italia, Serie A badala ya nne zitacheza ligi hiyo ya Ulaya, huku mbili za kwanza zikikata tiketi ya moja kwa moja na moja zaidi kupitia mtoano.

Timu ya nne na tano katika ligi hiyo zitacheza michuano ya Europa League.

Kwa sasa, Ujerumani ipo nyuma ya England na Hispania katika viwango hivyo vya ubora ikiwa na pointi 68,103 na kuipitia Italia ambayo inazo 59,981, limeeleza shirikisho hilo, DFL.

Mtendaji Mkuu wa DFL, Reinhard Rauball alieleza matumaini yake kwa nchi yake kwamba itazidi kupanda kwa viwango barani Ulaya.

"Tukiwa kidogo na subira, nina hakika kwamba tunaweza hata kupitia Hispania ndani ya muda si mrefu ujao," alisema Rauball.

Jumatano iliyopita, mabingwa wa Ulaya, Inter walifungwa 1-0 nyumbani na washindi wa pili mwaka jana, Bayern Munich, wakati AC Milan na AS Roma, timu nyingine mbili za nchi hiyo zinazoshiriki ligi hiyo zilipoteza mechi zao za kwanza za mtoano, hatua ya 16 bora.

Sampdoria, pia ya Italia iliondolewa katika hatua ya mtoano ya kufuzu kucheza hatua ya makundi.

Siku moja baadaye, mwakilishi wa mwisho wa Italia katika michuano ya Europa League, Napoli, iliyotolewa kwa kufungwa 2-1 na Villarreal kutoka Hispania, ikimaanisha kwamba hakutakuwa na mwakilishi wa Italia katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Mbali ya Bayern iliyoshinda, Schalke 04 ilitoka sare na Valencia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakati VfB Stuttgart iliondolewa Europa League kwa kufungwa nyumbani naBenfica ya Ureno, Bayer Leverkusen ilifuzu kucheza 16 bora kwa kuiondoa Metalist Kharkiv.

Kwa miaka ya karibuni, mafanikio ya klabu za Italia barani humo yameporomoka. Kati ya mwaka 1990-1999, walishinda mataji 13 ya Ulaya, matatu ya Kombe la Ulaya, Ligi ya Mabingwa, saba ya Kombe la Uefa na matatu ya Kombe la Washindi. Lakini, tangu mwaka 2000 wameshinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 
Tujitokeze zaidi kusaidia mashindano ya ngumi ya taifa Send to a friend Sunday, 27 February 2011 22:20

MASHINDANO ya ngumi za ridhaa ya taifa yameanza jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa mwishoni mwa wiki na yanatarajiwa kumalizika Machi 5.

Michuano hiyo inafanyika kwa lengo la kutafuta mabondia bora ambao wataunda timu ya taifa ya mchezo huo ili iweze kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya kimataifa.

Tukizungumzia mashindano ya kimataifa tunamaanisha ni pamoja na Michezo ya Afrika iliyopangwa kufanyika Maputo, Msumbiji Septemba mwaka huu na michezo ya Olimpiki iliyopangwa kufanyika London nchini Uingereza, Julai 2012.

Jambo la kuhuzunisha ni kwamba mashindano hayo yameanza kufanyika kwa udhamini mdogo wa Shilingi 1.6 milioni kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati bajeti halisi kwa ajili ya mashindano hayo ilikuwa ni zaidi ya Sh40m.

Hali hiyo inayoonyesha kwamba Watanzania wameshindwa kuliunga mkono Shirikisho la Ngumi za Ridhaa (BFT) ili kuliwezesha kuendesha mashindano ya taifa ya mchezo huo kwa upande wa ngumi za ridhaa tena kwa ufanisi.

Tulitarajia kuwa taasisi, mashirika, kampuni na watu binafsi wangeona umuhimu wa kusaidia gharama za mashindano hayo kwa kutoa fedha, maji au zawadi kwa mabondia ambao ni vijana wetu.

Tunasema kitendo hiki cha kukosekana wadhamini kinaonyesha kuwa ni wazi vijana wetu hao mabondia watajikuta wakijigharamia wenyewe hadi mwisho wa mashindano na upo uwezekano wa kupunguza siku za mashindano hayo.

Tunasema hivyo kwa sababu tunafahamu BFT ilikuwa ikihitaji fedha kwa ajili ya usafiri wa ndani, chakula na malazi kwa mabondia wote wanaoshiriki mashindano hayo makubwa kitaifa kwa lengo la kupata timu bora ya taifa ya ngumi za ridhaa kwa ajili ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.

Ni wazi hivi sasa vijana wetu watakuwa wakipigana ngumi, lakini hawapati chakula kizuri na malazi pia yatakuwa hayaridhishi jambo ambalo siyo sahihi kwa mwanamichezo yeyote.

Tumekuwa tukiamini pia udhamini wa kutosha unahitajika ili kuwapa motisha wanamichezo wetu waweze kuongeza juhudi ya kuupenda mchezo husika ili wawe tegemeo katika timu ya taifa.

Kwa jumla, hatujafurahishwa hata kidogo na mashindano hayo ya ngumi kuanza bila ya kuwa na udhamini, hivyo tunaamini bado ipo nafasi kwa wenye nia ya kudhamini mashindano hayo ya taifa kufanya hivyo ili kuweza kuwasaidia vijana wetu.

Tunasema hivyo kwa sababu mabondia watakaopatikana katika mashindano hayo ya taifa wataunda timu ya taifa ambayo itawakilisha nchi katika michezo ya Afrika, ambapo hivi sasa nchi mbalimbali za Afrika zipo katika maandalizi ya michezo kwa ajili ya kuhakikisha zinatwaa medali nyingi katika mashindano hayo.

Ni jambo la kushangaza kwamba sisi Tanzania tunaanza kutafuta timu ya taifa ya ngumi katika mazingira ya kukatisha tamaa kwa mashindano ya ngumi ya taifa kuadha bila udhamini wa kutosha.

Tunaamini lengo la BFT la kuandaa mashindano hayo ya ngumi ya taifa lina maana na zuri ambalo linatakiwa kuungwa mkono haraka na wadau wa michezo, makampuni na serikali ili kuweza kupata timu bora ya taifa ya mchezo huo.

Ni imani yetu kwamba kitu kizuri lazima kiandaliwe na kama tunataka tuwe na timu nzuri ya taifa ya ngumi, lazima mashindano hayo ya taifa ya ngumi yawe mazuri ili mabondia mbalimbali kutoka mikoa yote ya Tanzania waweze kuonyesha uwezo wao vizuri.

Tunawakaribisha wadau mbalimbali wa michezo,viongozi wa michezo,serikali, wafanyabiashara na makampuni wajitokeze kusaidia BFT kwa fedha na misaada mingine katika kipindi hiki cha mashindano hayo ili malazi,chakula na usafiri kwa mabondia viwe vya uhakika na kisha kupata wawakilishi bora wa ndondi kimataifa.
 
Tunampongeza Tenga, ila atambue ana kazi kubwa mbele yake Send to a friend Friday, 25 February 2011 21:16

tengasafi.jpg
KATIKATI ya wiki, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Leodegar Tenga alichaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), akiwakilisha Ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati .

Tenga, pia ni Rais wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, Cecafa.

Sisi kama wadau michezo,tunapenda kumpongeza Tenga kwa kuchaguliwa kwake kuwa mjumbe wa kamati hiyo katika chombo hiki kikuu kinachosimamia soka barani Afrika.

Tunasema hivyo kwa sababu alishinda uchaguzi uliofanyika mjini Khartoum,Sudan Februari 23 kwa kura nyingi baada ya kupata kura 34 huku mpinzani wake kutoka Rwanda aliyekuwa akitetea kiti hicho akiambulia kura 19.

Uchaguzi huo waTenga katika mkutano wa 33 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ulioshirikisha viongozi mbalimbali wa mashirikisho ya soka Afrika unaonyesha imani waliyo nayo si kwake tu bali pia kwa nchi yake, Tanzania.

Kwa ushindi alioupata Tenga, amekuwa Mtanzania wa pili kuingia kwenye kamati hiyo tendaji ya CAF baada ya Said Hamad El Maamry ambaye aliwahi kushika nafasi hiyo mwanzoni mwa miaka ya '80 kwa vipindi viwili mfululizo.

Tunaamini waliomchagua Tenga walizingatia vigezo vingi, kwanza uwezo alionao katika uongozi na tunaamini kazi hiyo ya ujumbe itakuwa na manufaa kwa soka la Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Tunasema hivyo kwa sababu kwa muda mrefu ukanda huu umekuwa nyuma katika mchezo wa soka huku maendeleo ya mchezo kwa vyama vyake yakiwa pia duni.

Vingi kati yake vikiwa vimezungizrwa na migogoro, mizozo, rushwa,viongozi wababaishaji, kukosa wadhamini na serikali za nchi husika kushindwa kusaidia mchezo wa soka.

Kwa hiyo, tunaamini kwambaTenga hivi sasa atakuwa katika nafasi nzuri ya kuieleza na kuielimisha CAF kuhusu kitu hasa kinachokwamisha maendeleo ya soka Afrika Mashariki na Kati na kuhakikisha matatizo yaliyopo yanatafutiwa ufumbuzi.

Ukanda wa Afrika Mashariki na kati unaundwa na nchi za Burundi, Djibouti, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Uganda, Rwanda, Somalia, Sudan na Tanzania huku CAF ikiundwa na kanda sita.

Ni wazi watu wa Afrika ya Mashariki na Kati kwa sawa wana mateneo makubwa kwa Tenga ambaye pia ni Rais wa Cecafa na hivyo wanataka mengi kwake yakiwamo maendeleo ya soka la wanaume,wanawake katika ngazi zote kuanzia za watoto hadi watu wazima.

Pia, watu wa Afrika ya Mashariki na Kati wanataka kuona makocha hasa wazawa wanapata elimu na leseni, waamuzi wanapata elimu ya kuwawezesha kupata nafasi za kuchezesha michuano mikubwa ya Afrika na dunia.

Pia, nchi hizo zinakuwa na uongozi bora wa vyama vya soka kwa sababu CAF inatakiwa kushughulikia mambo ya kiufundi na elimu ya soka barani Afrika.

Ni wazi wajibu kazi aliyopewa Tenga hivi sasa ni kubwa na akiitumia vizuri Tanzania na ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati utanufaika na kupata kozi,semina na programu nyingi za maendeleo.

Tunasema hivyo kwa sababu ipo mipango mingi ya maendeleo iliyoanzishwa na CAF kwa ajili kukuza soka tangu hatua ya chini pamoja na kushughulikia miundombinu ya soka, lakini kutokana na uwakilishi dhaifu wa Afrika Mashariki na Kati tumeshindwa kunufaika na mipango hiyo ya maendeleo ya CAF.

Tunatarajia kuona Tenga kwa kushirikiana na viongozi wenzake wa soka la Ukanda wa Afrika Mashariki wakileta mabadiliko katika mchezo huo ambao unapendwa na watu wengi.

Pia, tunatarajia Tenga hataisahau Tanzania, ila atafanya kila awezalo iweze kunufaika na nafasi aliyonayo katika soka Afrika kwa sababu kamati hiyo ndiyo inayofanya maamuzi mengi ya maendeleo ya soka la Afrika.

Tunamtakia kila la heri Tenga, tukitambua kwamba wadau wa michezo watamsaidia katika kufanikisha mategemeo ya wengi na kwamba ipo siku moja ukanda huu ukapata nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano ya Afrika, ambayo haikuwahi kufanyika katika ukanda huo.

 
Chelsea 2-1 Manchester United


storypage_APlogo_01.png




PRINT RSS

398 comments »

Updated Mar 1, 2011 7:53 PM ET
Frank Lampard completed Chelsea's second-half fightback against Manchester United from the penalty spot Tuesday, securing a 2-1 victory that tightened the Premier League title race.
Lampard found the net in the 80th minute after Yuri Zhirkov was tripped by defender Chris Smalling. That ensured Chelsea would climb a place to fourth in the standings, 12 points behind leader United but with a match in hand.
Securing one of the four Champions League spots is Chelsea's main target, with a second successive title unlikely despite inflicting only United's second league loss of the season.

Mon., Feb. 28
AC Milan 3-0 Napoli | Recap
Tue., Mar. 1
Chelsea 2-1 Man United | Recap

Wed., Mar. 2
Arsenal vs. Leyton Orient
Sat., Mar. 5
Arsenal vs. Sunderland
Man City vs. Wigan
Juventus vs. AC Milan
Sun., Mar. 6
Liverpool vs. Man United
Wolves vs. Tottenham
Lazio vs. Palermo
Inter Milan vs. Genoa
Fox Soccer Scores | Video | Photo


"We're still a lot of points behind, but all we could do was win the game," Lampard said. "United are deservedly top of the league, but we've still got some fight in us and we showed that tonight."
United losing had seemed unlikely at halftime, with the visitors in control of a high-intensity encounter.
David Luiz started the defending champions' comeback in the 54th, volleying in his first goal for Chelsea to cancel out Wayne Rooney's first-half opener.
United captain Nemanja Vidic was sent off in stoppage time after receiving a second yellow card for a foul on Ramires, ruling the center back out of Sunday's match against Liverpool.
A third successive league loss to Chelsea leaves United four points in front of second-place Arsenal having played an extra game.
United manager Alex Ferguson selected an unchanged side for the first time in 165 matches. But he was fortunate to have Rooney available after the England striker escaped punishment for elbowing an opponent in an off-the-ball incident in Saturday's match at Wigan.
There was an early moment of frustration for Rooney at Stamford Bridge, heading a well-placed cross from Nani wide while facing away from goal.
But given the ball by Nani and with the freedom to twist and turn 25 meters (yards) from goal on the half-hour, Rooney seized his chance, striking a low shot past the diving Petr Cech.
It is the first time Rooney has scored in three straight league matches since a spell spanning February and March last year.
While Rooney has overcome his recent slump, Fernando Torres still awaits his first goal since moving from Liverpool in January for 50 million pounds (then $81 million).
Playing for Liverpool against United, the Spain striker had scored three times in his last four games but he never troubled goalkeeper Edwin van der Sar on Tuesday.
"I thought the front three were great, Fernando Torres' movement was top class," Lampard said.
But Torres was upstaged by Luiz, the 20 million pound defender who also joined on transfer deadline-day in January. From Branislav Ivanovic's headed flick-on, Luiz fired the bouncing ball into the bottom corner of the net.
Ivanovic could have scored just before halftime, but Van der Sar knocked the ball away in a goalmouth scramble after initially fumbling Lampard's free kick.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom