Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Klabu za Ligi Kuu zavuna mamilioni


na Juma Kasesa


amka2.gif
KLABU 12 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kila moja imevuna kitita cha kiasi cha shilingi mil. 6.6 kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na haki ya televisheni iliyopata toka kampuni ya Sahara Media Group kwa kuonyesha ligi hiyo.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema kampuni hiyo ambayo ilishinda tenda ya sh mil. 40 kuonyesha ligi hiyo imeipa TFF sh mil. 100 ambazo zimegawanywa kwa timu hizo ambazo huvuna asilimia 80 ya malipo ya haki za kuonyesha mechi na timu zitalipwa kwa awamu.
Kwa mujibu wa mkataba wa TFF na Sahara awamu nyingine ya fedha hizo sh mil. 40 italipwa na Kampuni hiyo mara malipo yatakapofanywa.
Alisema Sahara Media Group wataonyesha mechi mbili kwa kushirikiana na kituo cha televisheni cha Super Sport ya Afrika Kusini kwa lengo la kujiongezea uzoefu kwenye eneo hilo la kuonyesha mechi moja kwa moja ‘live'.
Alizitaja mechi hizo kuwa ni ya leo baina ya Azam na Majimaji itakayochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na ile kati ya Yanga na Simba itakayochezwa Machi 5 katika Uwanja wa Taifa jijini.
Alifafanua kuwa klabu hizo zimelipwa sh milioni 5.2 kila moja kwa ajili ya nauli lakini zikiwa bado zinadai malipo ya nauli kwa ajili ya Machi ambapo zitalipwa fedha hizo mara baada ya malipo kufanywa na mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom.
Katika hatua nyingine, mechi baina ya Simba na Mtibwa Sugar iliyopigwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, imeingiza sh 39,954,000 huku ile ya Yanga na Ruvu Shooting iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ikiingiza sh 11,280,000.



h.sep3.gif

 
Kaijage: Kamati ilikiuka katiba


na Mwandishi wetu


amka2.gif
ALIYEKUWA Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Florian Kaijage, ameibuka na kuishutumu Kamati ya Uchunguzi wa sakata la kugoma kwa CD ya Wimbo wa Taifa wakati wa mchezo wa kimataifa baina ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, na Morocco kwa kudai kuwa imekiuka katiba ya shirikisho hilo katika kufikia uamuzi wake.
Kaijage aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaa jana kuwa kamati hiyo ilifikia uamuzi wa kummwagia lawama yeye kwamba alizembea ikiwa na wajumbe wawili wakati katiba ya ya TFF inataka maamuzi yoyote yafikiwe na wajumbe wasiopungua nusu ya akidi.
"Ibara ya 36 ya TFF inazungumzia kamati ya utendaji inavyoweza kufikia uamuzi; utafikiwa iwapo akidi itafikia nusu ambapo mara zote lakini mimi nilihojiwa na wajumbe wawili wa kamati hiyo, mwenyekiti na katibu wake jambo ambalo ni ukiukwaji wa katiba," alisema.
Kaijage alisema ameshangazwa na kamati hiyo kumtupia zigo hilo kwani siku ya tukio fundi mitambo raia wa China mwenye utaalamu wa kuwasha mitambo hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya Kichina hakuwepo katika eneo lake na kama angekuwepo lisingetokea hilo lakini kamati hiyo kwa sababu zake imeamua kumhukumu yeye.
Aliongeza kuwa siku ya tukio alikuwa na majukumu mengi ikiwa ni pamoja na kushughulikia vitambulisho vya wapiga picha ambao wanaingia eneo la karibu na uwanja, kugawa line- ups na alikuwa akifanya shughuli hizo kwa ushirikiano na ofisa habari aliyeomba TFF, Suleiman Jongo.
Kaijage alisimamishwa na TFF baada ya kutokea kwa tukio hilo la fedheha mbele ya Rais Jakaya Kikwete ili kupisha uchunguzi wa kamati hiyo iliyoundwa na rais wa TFF, Leodgar Tenga, ambayo ilikuwa chini ya mwenyekiti Hamidu Mbwezeleni.
Alisema anaamini siku ya tukio alitimiza majukumu yake na kwa sasa hawezi kuchukua hatua zozote dhidi ya kamati hiyo kwa kuwa si mwajiri wake na TFF haijamchukulia hatua baada ya kupokea ripoti ya kamati hiyo.
 
Mechi ya watani Jumamosi
• Simba yapata pigo, Echessa nje

na Mwandishi wetu


amka2.gif
WAKATI homa ya pambano baina ya watani wa jadi nchini Simba na Yanga ikizidi kupanda, mabingwa wa ligi hiyo Simba watamkosa kiungo wake wa kimataifa Hillary Echessa katika mechi hiyo itakayopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Ofisa habari wa Simba Clifford Ndimbo alisema jana kwamba mchezaji huyo anakabiliwa na maumivu ya goti na kwa mujibu wa daktari wa timu hiyo, hatoweza kucheza mechi hiyo.
Ndimbo alisema timu yake inaendelea vema na maandalizi ya mechi hiyo ambapo wachezaji wote wako kambini visiwani Zanzibar isipokuwa Echessa na Emmanuel Okwi ambaye anatarajia kujiunga wakati wowote na wenzake.
"Wachezaji wote wako katika hali nzuri wanaendelea na kambi Zanzibar lakini Echessa ndio hivyo ataikosa mechi na Okwi anatakiwa kupiga picha ya X-ray kabla ya kujiunga na wenzake," alisema Ndimbo.
Wakati Simba ikiwa Zanzibar, mahasimu wao Yanga wamejichimbia Bagamoyo kujiandaa na mechi hiyo ya marudiano.
Habari kutoka Yanga zinasema kwamba timu hiyo iliwasili jana mjini humo ikitokea Morogoro ilikocheza na Ruvu Shooting na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 hivyo kuongoza ligi hiyo kwa pointi 38, ikifuatiwa na Simba yenye pointi 37 na Azam ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 35.
Katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa Oktoba 16 katika dimba la CCM Kirumba mjini Mwanza Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji wake Jerry Tegete.
Naye Mwandishi Wetu Makuburi Ally anaripoti kuwa Yanga imeliandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumuomba kiungo wake anayeichezea timu ya vijana Omega Seme ashiriki katika maandalizi ya mechi yao na Simba.
Ofisa Habari wa Yanga Louis Sendeu alisema waliwasilisha barua hiyo TFF tangu wiki iliyopita lakini mpaka sasa haijajibu.
 
KT yawasaidia waathirika Chikundi


na Dina Ismail


amka2.gif
KLABU ya michezo na burudani ya KT juzi imetoa misaada ya aina mbalimbali kwa kijiji cha Chikundi kilichopo Ruangwa mkoani Lindi ili kiweze kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha Januari 27 mwaka huu.
Mvua hiyo ilisababisha hasara mbalimbali ikiwemo kubomoka kwa baadhi ya nyumba, nyingine kupauliwa mapaa yake na hivyo kupelekea nyumba 57 kubomoka na watu 628 kukosa makazi.
Mwenyekiti wa KT Aboubakar Juma alisema kama wanajamii wameamua kusaidia waathirika hao kutokana na kuguswa na athari zilizotokea katika kijiji hicho ili kuendesha maisha yao katika kipindi ambacho wanasubiri kupata makazi.
KT ilikabidhi tani mbili na nusu za unga pamoja na lita 125 za mafuta ya kula kwa mbunge wa jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Kassim Majaliwa.
Pia Juma alijitolea kukarabati msikiti ambao ulikumbwa na dhoryba hiyo kwa kuezuliwa paa sambamba na kununua majamvi, majuzuu 300 na mikeka 200.
Naye Majaliwa alishukuru kwa msaada huo kwa kusema utafika kulipokusudiwa na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia wahanga hao.
Latika hatua nyingine, mshirika wa Majaliwa Dk. David Onyango toka taasisi ya Heart to Heart ya Marekani ametoa dola 100 na kuahidi kutoa madawa yenye thmani ya shilingi 150, 000.
 
Mburahati Queens Sayari zaoneana haya


na Ruhazi Ruhazi


amka2.gif
TIMU za Mburahati Queens na Sayari Women juzi ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 katika mechi ya Ligi soka ya wanawake Mkoa wa Dar es Salaam, iliyopigwa kwenye dimba la Karume jijini Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo iliyovuta hisia za wengi, baada ya mwamuzi Helen Mduma kupuliza kipyenga cha kuanzisha pambano, timu zote ziliuanza mchezo kwa umakini na tahadhari kubwa.
Shambulizi la kushtukiza katika dakika ya kumi liliwapa Mburahati bao la kuongoza, likifungwa na Mwanahamisi Omari ‘Gaucho' na Sayari wakafanikiwa kusawazisha katika dakika ya 40 kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na Sofia Mwasikili, kutokana na mlinzi Mwanaidi Tamba kuunawa mpira wakati akijaribu kumzuia Mary Masatu.
Bao la pili la Sayari liliwekwa kimiani na mchezaji mkongwe wa timu hiyo Masha Kajo, dakika ya 42, aliyeachia shuti kali lililomshinda kipa Apendeki Juma, lakini Masha alijikuta akilimwa kadi ya njano na mwamzi Helen Mduma kutokana na kungo'a kibendera cha kona wakati akishangilia.
Katika kipindi cha pili wachezaji wa pande zote walionekana kupoteza umakini hivyo kucheza mpira chini ya kiwango na kushindwa kutengeneza nafasi za kupata mabao zaidi na hata walipopata bafasi walishindwa kuzitumia.
Mwanahamisi akaifungia Mburahati bao la kusawazisha dakika 55 na dakika chache baadaye Asha Rashidi ‘Mwalala' akaifungia Mburahati bao la tatu, lakini sayari wakasawazisha baada Ester Chabruma kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Apendeki na kumpasi Masha aliyeuweka wavuni dakikaya 77.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo kwa mechi kati ya EMIMA Queens watakaocheza na Evergreen Queens, wakati kesho Temeke Queens watakipiga na JKT Queens, mechi zote zikipigwa dimba la Karume.



h.sep3.gif

 
Mburahati Queens Sayari zaoneana haya


na Ruhazi Ruhazi


amka2.gif
TIMU za Mburahati Queens na Sayari Women juzi ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 katika mechi ya Ligi soka ya wanawake Mkoa wa Dar es Salaam, iliyopigwa kwenye dimba la Karume jijini Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo iliyovuta hisia za wengi, baada ya mwamuzi Helen Mduma kupuliza kipyenga cha kuanzisha pambano, timu zote ziliuanza mchezo kwa umakini na tahadhari kubwa.
Shambulizi la kushtukiza katika dakika ya kumi liliwapa Mburahati bao la kuongoza, likifungwa na Mwanahamisi Omari ‘Gaucho' na Sayari wakafanikiwa kusawazisha katika dakika ya 40 kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na Sofia Mwasikili, kutokana na mlinzi Mwanaidi Tamba kuunawa mpira wakati akijaribu kumzuia Mary Masatu.
Bao la pili la Sayari liliwekwa kimiani na mchezaji mkongwe wa timu hiyo Masha Kajo, dakika ya 42, aliyeachia shuti kali lililomshinda kipa Apendeki Juma, lakini Masha alijikuta akilimwa kadi ya njano na mwamzi Helen Mduma kutokana na kungo'a kibendera cha kona wakati akishangilia.
Katika kipindi cha pili wachezaji wa pande zote walionekana kupoteza umakini hivyo kucheza mpira chini ya kiwango na kushindwa kutengeneza nafasi za kupata mabao zaidi na hata walipopata bafasi walishindwa kuzitumia.
Mwanahamisi akaifungia Mburahati bao la kusawazisha dakika 55 na dakika chache baadaye Asha Rashidi ‘Mwalala' akaifungia Mburahati bao la tatu, lakini sayari wakasawazisha baada Ester Chabruma kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Apendeki na kumpasi Masha aliyeuweka wavuni dakikaya 77.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo kwa mechi kati ya EMIMA Queens watakaocheza na Evergreen Queens, wakati kesho Temeke Queens watakipiga na JKT Queens, mechi zote zikipigwa dimba la Karume
 
Mkutano Mkuu Yanga waota mbawa


*Waelekeza nguvu mechi ya Simba

Na Elizabeth Mayemba

MKUTANO Mkuu wa dharura wa Yanga ambao wanachama waliuomba umeota mbawa, baada ya Kamati ya Utendaji iliyokutana
Jumamosi kushindwa kuuzungumzia.

Awali Mwenyekiti wa klabu hiyo, Lloyd Nchunga alikaririwa katika vyombo vya habari kwamba mkutano huo, ungefanyika mara baada ya mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar.

Habari zilizopatikana Dar es Salaam jana kutoka kwa baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho wameeleza kuwa katika kikao hicho hakukuwa na ajenda yoyote inayohusu mkutano huo.

"Katika kikao chetu tulizungumza mambo mbalimbali, lakini hatukuthubutu kuzungumzia suala lolote la Mkutano Mkuu, kwani muda wa kufanya hivyo bado," alidai mmoja wa wajumbe hao ambaye hakutaka jina lake.

Alisema kamati hiyo inautambua Mkutano Mkuu wa kikatiba ambao hufanyika kila mwaka na mkutano huo bado haujapangiwa tarehe kwa kuwa sasa hivi timu inakabiliwa na mechi mbalimbali za Ligi Kuu ya Vodacom.

Mjumbe huyo alidai kwamba suala la Mkutano Mkuu ni la kikatiba zaidi na kama wajumbe wanalitambua hilo, hivyo muda utakapofika utafanyika kwa mujibu wa kanuni.

Awali baadhi ya wanachama wa klabu hiyo waliibuka na kuutaka uongozi wa klabu hiyo kuitisha Mkutano Mkuu wa wanachama haraka ili kuondoa malumbano ya viongozi ambao walikuwa hawaelewani na pia suala Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya Yanga, Yusuf Manji ambaye amekabidhi barua ya kujiudhulu.

Mjumbe huo pia walidai kuwa katika kikao hicho walipanga mikakati ya timu ili iweze kushinda mechi zote zilizosalia za Ligi Kuu ya Bara.

"Mechi zinazofuata ni ngumu, hasa kwa Simba na Azam FC, hivyo nguvu zote zimeelekezwa kwenye mechi hizo kwani kama tukipoteza michezo hiyo ndoto zetu za kutwaa ubingwa zitaota mbawa," alisema mjumbe huyo.

Alisema kwa sasa wanatumia muda mwingi kufikiria mechi zilizosalia kwa kuwa mzunguko huu ni wa lala salama na kila timu inataka kutwaa ubingwa.

Wakati huo huo, Yanga iliondoka jana Dar es Salaam kwenda mjini Bagamoyo kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Simba, unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 
Matangazo yaanza kunufaisha timu


Na Addolph Bruno

KLABU 12 za Ligi Kuu zimeanza kunufaika na fedha za matangazo kwa kupewa sh. milioni 6.6 kila moja kutoka Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF).

Fedha hizo ambazo ni haki ya televisheni iliyopata nafasi ya kutangaza ligi hiyo ya Sahara Media Group kupitia kituo cha Star TV kwa sh. milioni 14o.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema kutokana na mkataba kati ya kituo hicho na TFF, hadi sasa zimelipwa sh. milioni 100.

Wambura alisema katika mapato yote kila klabu inalipwa asilimia 80 ya malipo hayo ambazo zitalipwa tena mara malipo ya awamu ya mwisho ya sh. milioni 40 yatakapokamilishwa na kituo hicho.

Katika hatua nyingine, Wambura alisema mchezo kati ya Simba na Mtibwa uliochezwa Jumapili katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam umeingiza sh. 39,954,000 kati ya watazamaji 8,609 waliohudhuria.

Wambura pia alisema pambano kati ya Yanga na Ruvu Shooting, lililofanyika juzi katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro limeingiza sh. milioni 11,280,000 kati ya watazamaji 3,760 waliohudhuria pambano hilo.

 
Mbunge kusaidia mashindano Klabu Bingwa


Na Amina Athuman

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa, ameahidi kutoa zawadi ya medali 40 kwa mabondia wanaoshiriki mashindano ya ubingwa wa Taifa wa
ngumi za ridhaa, yanayoendelea katika Uwanja wa ndani wa Taifa, Dar es Salaam.

Jumaa ambaye ni mdau wa michezo na bondia wa zamani katika uzito wa middle, jana alikwenda kuangalia mashindano hayo ambayo yanashirikisha timu kutoka mikoa 24 ya Tanzania Bara.

Akiwa katika ukumbi huo, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Meja Mstaafu Michael Changalawe alimweleza changamoto zinazoyakabili mashindano hayo.

Miongoni mwa changamoto alizotajiwa ni pamoja na na ukosefu wa medali kwa mabondia, ambao watafanya vizuri katika uzito tofauti, ukata wa fedha za kuchapisha vyeti kwa timu zote pamoja na zawadi.

"Mimi ni mdau mkubwa wa mchezo huu, changamoto nimeziona hivyo nitahakikisha nazipeleka bungeni, ili uweze kurudisha heshima yake kama ilivyokuwa zamani," alisema Mbunge huyo.

"Nia kubwa ni kuhakikisha malengo yaliyowekwa na BFT yanafikiwa, nitawashawishi wabunge wenzangu waweze kuhudhuria mashindano mbalimbali ya ngumi za ridhaa," alisema.

Alisema mchezo wa ngumi una nafasi kubwa ya kuitangaza Tanzania kimataifa kama wadau mbalimbali, wataona umuhimu wa kufadhili mashindano yanayoandaliwa na BFT.

 
Rooney anusurika kibano FA


LONDON, England

KITUO cha televisheni cha Sky News cha Uingereza, kimesema kwamba mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney hatakumbwa na adhabu ya
utovu wa nidhamu kutokana na shutuma za kumpiga kwa kiwiko cha mkono kiungo wa Wigan, James McCarthy, kituo cha televisheni cha Sky News cha Uingereza kiliripoti juzi.

Katika mchezo huo Rooney alionekana kumpiga kwa kiwiko cha mkono kisogoni, McCarthy wakati wa kipindi cha kwanza cha mchezo ambao Manchester United iliibuka na ushindi wa mabao 4-0, dhidi ya Wigan uliofanyika Jumamosi.

Kosa hilo ndilo lililomlazimu mwamuzi, Mark Clattenburg kuamuru upigwe mpira wa adhabu na baadaye akakieleza Chama cha Mpira wa Miguu (FA) kwamba alifanya maamuzi sahihi jambo ambalo limekifanya chama hicho kushindwa kuchukua hatua za kinidhamu.

Hata hivyo kocha wa Wigan, Roberto Martinez anamshutumu vikali mwamuzi huyo kwa kushindwa kumuadhibu Rooney siku hiyo ya Jumamosi.

"Nadhani Rooney ana bahati sana. Ilikuwa apewe kadi nyekundu," alisema Martinez. "Nililiona wazi tukio hilo na mwamuzi alifanya hivyo kwa sababu alitoa mpira wa adhabu.

"Mwamuzi anapoamuru upigwe mpira wa adhabu inadhihirisha wazi ilistahili kutolewa kadi nyekundu, huku akisisitiza kwamba ukiangali mkanda wa video unaonesha wazi Rooney alimpiga kwa kiwiko James McCarthy," alisema.

Hata hivyo kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson anadhani mwamuzi Clattenburg alikuwa sahihi kutomuadhibu Rooney na akasema ana wasiwasi atakuwa akiwindwa na vyombo vya habari vya Uingereza.
 
Klabu Ligi Kuu zavuna mamilioni kutoka haki za TV Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 20:36

wamburatff.jpg
Sweetbert Lukonge

TIMU 12 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zimeanza kuvuna mafanikio ya mkataba mpya wa kurusha matangazo ya moja ya mechi zao kupitia televisheni.

Kwa kuanzia, timu hizo zimelipwa Shilingi 6.6 milioni kila moja kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mfumo huo, wiki hii utawawezesha mashabiki wa soka barani Afrika pia kuziona Yanga na Simba laivu Jumamosi kupitia Star TV kwa ushirikiano na kituo cha Supersport cha Afrika Kusini.

Fedha hizo zinatokana na haki ya televisheni iliyoipata Kampuni ya Sahara Media Group kuonyesha mechi za ligi hiyo kupitia katika kituo chake cha Star TV ambacho kilishinda zabuni hiyo kwa Sh 140 milioni.

Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa mkataba kati ya TFF na Sahara Media Group ni kuwa fedha hizo zitalipwa kwa awamu na mpaka sasa zimelipwa Sh100 milioni.

Alisema klabu ambazo zimepata asilimia 80 ya malipo hayo ya haki za kuonyeshwa mechi za Ligi Kuu zitalipwa tena mara malipo ya awamu ya mwisho ya Sh 40 milioni yatakapofanya na kampuni hiyo.

"Klabu zote Ligi Kuu zimepokea kiasi cha Sh 6.6 milioni kila moja kupitia kwetu (TFF) fedha hizo zinatokana na haki ya televishini iliyopata Sahara Media Group kupitia kituo chake, Star TV.

"Ni matumaini yetu kuwa kiasi ambacho bado hakijalipwa na kampuni hiyo pindi tu kitakapolipwa klabu zote ambazo zimepata aslimia 80 ya malipo hayo zitalipwa tena," alisema Wambura.

Kulipwa kwa timu hizo, kutaziwezesha kujiendesha na kuwa kama zile za mataifa mengine duniani ambao haki za televisheni zimekuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa klabu hizo.

Haki hizo za televisheni, kwa mfano katika England kumezifanya baadhi ya mechi kuchezwa au kupangwa kulingana na muda ambao utawawezesha mashabiki kuzifuatilia, jambo ambalo linaongeza ushabiki na ufuatiliaji wa mechi hizo.

Katika hatua nyingine kampuni hiyo itaonyesha mechi mbili za Ligi Kuu kwa kushirikiana na Super sport ya Afrika Kusini kwa lengo la kujiongezea uzoefu kwenye eneo hilo la kuonyesha mechi moja kwa moja (laivu).

Mechi zitakazoonyeshwa laivu kwa ushirikiano huo ni kati ya Azam na Majimaji ya Songea utakaofanyika leo kwenye Uwanja wa Uhuru pamoja na ile ya Simba na Yanga itakayofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 
Timbe: Yanga ipo kamili kila idara Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 20:21

Doris Maliyaga, Morogoro na Jesca Nangawe

KOCHA Mkuu wa Yanga, Sam Timbe amejinasibu kuwa kikosi chake kimeimarika kila idara na kuanzia jana alianza kazi maalum kimazoezi akitafuta mbinu za kuwafunga Simba.

Yanga ambayo ndiyo inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu kwa sasa, Jumamosi itacheza na Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mwananchi jana ilibaini kuwa timu hiyo itaweka kambi yake mjini Bagamoyo, Pwani na ilitarajiwa kuondoka jana jioni ama leo kuelekea huko kwa ajili ya maandalizi yao ya mwisho kabla ya mchezo huo.

Timbe alisema kabla ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting juzi ambayo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 alikuwa akiwaandaa wachezaji wake katika kutengeneza nguvu na hivi sasa ameanza kuwaandaa wachezaji wake kwa ajili ya kuikabili Simba.

"Kwa sasa kikosi ni kizuri nina kila sababu ya kusema hivyo kwa sababu awali hawakuwa kama walivyo sasa.

"Kila mechi naawandaa kutokana na timu tunayoenda kukutana nayo, tumecheza na Kagera awali niliwaandaa kwa mchezo huo na Ruvu, pia sasa ni zamu ya Simba kuona tunapata kile tunachokitaka,ííaliongeza Timbe, raia wa Uganda.

"Wachezaji wangu walijitahidi mechi dhidi ya Ruvu, lakini bado hawajafanya kile ambacho nilikuwa nataka kwao, sasa tunakwenda kukutana na Simba ni dhahiri mchezo utakuwa mgumu kufuatia historia ya timu hizi lazima tujirekebishe kwa muda huu mchache uliobaki,"alisema.

Wakati huo huo, Sostenes Nyoni anaripoti kuwa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amerejea nchini na jana mchana alitarajiwa kuelekea Zanzibar kujiunga na wenzake waliopiga kambi huko wakijiandaa na mechi dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga.

Kurejea kwa Okwi aliyekuwa kwao Uganda akipata matibabu ya enka kunazidi kumpatia matumaini zaidi kocha wa Simba, Patrick Phiri kuibuka na ushindi katika mechi hiyo.

Ofisa habari wa Simba, Clifford Ndimbo alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa kupona kwa Okwi kumekiongezea nguvu kikosi chao ambacho pia kinatarajia kuivaa TP Mazembe katika michuano ya Mabingwa Afrika baada ya pambano na Yanga.

"Kimsingi, kikosi chetu kimefika Zanzibar salama,labda jambo zuri zaidi ni kurejea kwa Okwi aliyekuwa majeruhi wa enka ambapo mchana huu (jana) ataelekea huko kujiunga na wenzake,"alisema Ndimbo.

Aidha, Ndimbo alisema baada ya Okwi kupona kikosi hicho sasa kimebakia na majeruhi watatu pekee ambao hawako kambini na wanaendelea na matibabu, akiwemo Joseph Owino,Hillary Echesa na Uhuru Suleiman.

Katika hatua nyingine, Ndimbo alisema mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Rage keshokutwa atatembelea matawi ya klabu hiyo yaliyofanya uchaguzi na kupata viongozi kwa ajili ya kugawa bendera na katiba.

Alisema pia fomu za kuomba uanachama wa klabu hiyo zimeanza kutolewa katika matawi kwa gharama ya Sh 2,000 ambapo waombaji watatakiwa kuzichukua huko kabla ya baadaye kupelekwa kwa kamati ya utendaji kwa ajili ya kupitiwa.

Ndimbo alisema kuanzia sasa wanachama wa klabu hiyo watatakiwa kulipia Sh 10,000 kama gharama ya kadi na Sh 12,000 kama ada ya uanachama kwa mwaka mzima na Sh 20,000 kwa ajili ya mchango wa ujenzi.

Aliongeza kuwa mwanachama yeyote atakayetoa mchango wa ujenzi wa uwanja unaozidi Shilingi 1milioni atapewa cheti maalumu cha kuthamini mchango wake
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom