Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,508
- 911,249
- Thread starter
- #8,701
Serikali kuelekeza nguvu kuogelea
na Samia Mussa
SERIKALI imeahidi kuelekeza nguvu zake katika mchezo wa kuogelea, pia imewataka makocha wa nchezo huo kuwapa kipaumbele wazawa katika kufundisha mchezo huo hapa nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya makocha, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara, alisema ni wakati muafaka kwa Watanzania kupewa nafasi ya kushiriki mchezo huo kwa sababu ni mchezo mzuri ambao unaweza kuitangaza nchi kimataifa.
Mukangara alisema Tanzania inatakiwa kuandaliwa hivi sasa ikiwa pamoja na kuwashawishi Watanzania kujitokeza kwa wingi kujifunza mchezo huo ambao kwasasa unachezwa sana na raia wa kigeni wanaokuja nchini.
Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Makocha wa kuogelea Tanzania (TSCA) kilichandaa mafunzo hayo, Amina Mfaume, alisema yamelenga la kuwaongezea ujuzi zaidi makocha hao chini ya ukufunzi wa rais wa Makocha mchezo nchini Marekani (ASCA) John Leonard,
Mfaume alitoa wito kwa makocha hao kuhakikisha kuwa wanakwenda kufundisha mazuri yote walioyapata kwenye klabu zao na shuleni ili kupata kupata vipaji vipya vya mchezo huo.
Mafunzo hayo yaliyokuwa yakifanyika katika shule ya kimataifa Tanganyika iliyopo Oyesterbay jijini Dar es Salaam, yanamalizika leo huku yakiwa yameshirikisha makocha 59 kutoka nchi za Afrika Uganda, Zambia, Kenya na Tanzania

PRINT