Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Wolverhampton Wanderers 4-0 Blackpool


RivalsDM



PRINT RSS



Updated Feb 26, 2011 12:59 PM ET
Wolves lifted themselves out of the bottom three of the Premier League following a comprehensive 4-0 defeat of 10-man Blackpool at Molineux.
Matt Jarvis gave boss Mick McCarthy's men the perfect start with a second-minute opener before a moment of madness from Blackpool leading scorer DJ Campbell saw him sent off in the 43rd minute.
Sat., Feb. 26
Aston Villa 4-1 Blackburn | Recap
Everton 2-0 Sunderland | Recap
Newcastle 1-1 Bolton | Recap
Wigan 0-4 Man Utd | Recap
Wolves 4-0 Blackpool | Recap
Sun., Feb. 27
West Ham vs. Liverpool
Man City vs. Fulham
Mon., Feb. 28
Stoke City vs. West Brom
BPL Scores | Table | Fixtures


Wolves then made their numerical advantage count after the break as Jamie O'Hara and then substitute Sylvan Ebanks-Blake with a brace eased their club off the foot of the table into 17th.
The first half was one that started and ended in nightmare fashion for Blackpool boss Ian Holloway as his side proved you are only as good as your last game.
That had been a sensational 3-1 victory over Spurs in midweek, one that had eased the Seasiders clear of the relegation zone, sending belief soaring they can survive in the top flight this season.
But after just 116 seconds Blackpool were swiftly brought crashing back down to earth as a four-man move culminated in Jarvis scoring his fourth goal of the season.
From deep inside Wolves territory, Ronald Zubar played a ball down the right wing into David Edwards, fit again after missing the 1-1 draw at West Brom last Sunday with a groin injury.
Edwards' short run was incisive as he cut inside his marker prior to feeding Adam Hammill, also restored to the starting line-up, just inside the Blackpool area.
Although Hammill's pass to his left was scuffed, it had enough pace on it to find Jarvis who brilliantly curled beyond Richard Kingson a 12-yard right-effort that had the majority of the crowd on their feet.
Then just over two minutes from the interval, with Blackpool having failed to seriously test goalkeeper Wayne Hennessey, any hope of a comeback suffered a crucial setback.
Directly in front of Holloway, on the edge of his technical area, Campbell stupidly over-reacted to a slight shove in his back from Richard Stearman as the duo faced onto a long ball downfield.
The red mist descended as the much-shorter Campbell then turned on Stearman, and with both hands, shoved the centre-back in the face.
Making arguably his easiest decision all afternoon, referee Neil Swarbrick swiftly brandished the red card.
Turning on his heels, Campbell made the short walk to the dressing room, with not so much as an apologetic acknowledgement towards Holloway just yards from him.
The act of rage, from a player who had previously only been booked just once all season, will now see him miss the next three matches.
In between those two horror moments for Holloway, it was Wolves who had the better of the half, with Kingson pulling off one stunning save to deny Edwards from a 12-yard, left-foot half volley.
The home side did have the ball in the back of the net on a second occasion, only for Swarbrick to adjudge George Elokobi had fouled Kingson as he nodded the ball home.
As for a typically workmanlike Blackpool, their best opportunity was inadvertently set up by a stunning sliding challenge from Wolves captain Karl Henry on Keith Southern deep in his own half.
The home of the best LIVE soccer and rugby awaits at FoxSoccer.tv -- don't miss a second of the action.

But it was a tackle made facing his own goal as the ball flew into the path of Luke Varney, who had minutes earlier replaced Sergei Kornilenko, only for the striker to slice his shot wide.
That was as good as it got for Blackpool for within 10 minutes of the restart the 10 men caved in, and with it went the last remaining hope of salvaging a point.
After Kingson had denied substitute Kevin Foley and O'Hara in the two minutes immediately prior to Wolves doubling their advantage, the latter was not to be denied.
Thanks primarily to a defence that stood off him, O'Hara rifled in a 22-yard, left-foot shot that bounced over the outstretched left hand of Kingson into the corner of his net for his second goal in a week.
With the spirit and stuffing knocked out of Blackpool, and as one-way traffic developed, they duly conceded a third 12 minutes from time.
Ebanks-Blake, who had replaced Zubar just after O'Hara's strike, tapped home from a yard courtesy of a precision cross from Kevin Foley.
In front of a record crowd for the new Molineux of 29,086, Ebanks-Blake then took his tally to six for the season with an angled left-foot drive beyond Kingson on the stroke of full time.
 
Mr. II kuzindua Anti - Virus Bilicanas leo
• Pia kutoa shukrani kwa wananchi

na Dina Ismail


amka2.gif
MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Mr II ama Sugu, leo anatarajiwa kufanya onyesho maalumu kwa ajili ya kuwashukuru wananchi na mashabiki wake kwa kuwa naye pamoja mpaka sasa.
Sugu, mwasisi wa muziki wa hip hop hapa nchini kwa sasa ni mbunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Awali onyesho hilo lilikuwa lifanyike Jumapili iliyopita kabla ya kuahirishwa kutokana na milipuko ya mabomu iliyotokea katika kambi ya 511 KJ iliyopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam hivi karibuni, ambapo watu 26 wamefariki dunia.
Sugu atafanya onyesho hilo katika ukumbi wa kimataifa wa Club Billicanas kupitia usiku wa bongo Starz Nite, ambao hurindima ukumbini hapo kila siku za Jumapili.
Pamoja na shukrani hizo, Sugu atatumia onyesho hilo pia kuzindua albamu yenye nyimbo mchanganyiko za wasanii mbalimbali inayokwenda kwa jina la ‘Anti- Virus'.
Kama hiyo haitoshi, kutakuwa na wasanii mbalimbali watakaosindikiza wakiwemo Mkoloni, G-Solo, Salu T, Mapacha, kundi la Orijino Komedi na wengine wengi ambapo kiingilio kimepangwa kuwa sh 5,000 kwa kila mmoja.
 
Stara akaribishwa tamasha la Pasaka


na Mwandishi wetu


amka2.gif
KAMATI ya maandalizi ya tamasha la Pasaka, imesema iko tayari kumkaribisha mwanamuziki nguli wa zamani wa muziki wa Bongo Fleva, Stara Thomas, aliyegeukia muziki wa injili, ili atumbuize katika tamasha hilo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati hiyo, Alex Msama, kwa sasa wameamua kufuatilia kwa karibu nyendo za Stara ili kujiridhisha na kama itawezekana, watamkaribisha kwa moyo mkunjufu kuimba katika tamasha hilo la kimataifa litakalofanyika Aprili 24.
Msama ametoa msimamo huo siku chache baada ya Stara kusema ameamua kumtumikia Mungu katika nyimbo za Injili na yuko tayari kutumbuiza akipata nafasi katika tamasha la Pasaka la kumsifu Mungu litakalofanyika siku hiyo kwenye ukumbi wa Dimond Jubilee, Dar es Salaam.
"Hata hivyo, jambo la kufurahisha ni kwamba Stara tunamfahamu kwa muda mrefu ni mtu anayejiheshimu katika jamii tangu awali," alisema Msama.
Msama ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions iliyo mstari wa mbele kufanya kazi na wasanii wa muziki wa Injili, alisema pia wanamkaribisha kwa mikono miwili Stara afanye kazi na kampuni hiyo.
Stara alikaririwa akisema anaamini Mwenyezi Mungu atamuongoza kutengeneza albamu ya Injili itakayokuwa shukurani kwa Mungu.
"Sasa hivi nimeamua kumpa Bwana Yesu maisha yangu... nilipata mwito kutoka kwake kuwa anawaita watu wote wasumbukao na wenye kulemewa na mizigo waende kwake atawapumzisha, nami nimekuja kupumzika," alisema Stara.
"Kwa vile Mungu amenipa kipaji na kunijaalia afya njema, naahidi nitamtumikia kwa nguvu zote," alisema Stara
Awali, Stara alitamba na nyimbo za Bongo Fleva kama Sikia, Sitorudi Nyuma, My Body na Children's Right, Mimi na Wewe, Wasiwasi wa Mapenzi, Nipigie alizozipiga katika miondoko ya Zouk.



h.sep3.gif

 
Dogo Janja achezea kipigo Makongo


na Upendo Simon


amka2.gif
MSANII kutoka kundi la Tip Top connection Abdulaziz Abubakari ' Dogo Janja' ambaye anasoma Sekondari ya Makongo, juzi alipokea kipigo kitakatifu kutoka kwa mwalimu wake kutokana na kupishana kauli.
Janja anayesoma kidato cha kwanza shuleni hapo alikumbana na kitendo hicho kipindi cha mchana alipokuwa anakwenda kupata chakula cha mchana shuleni hapo.
Chipukizi huyo alikaririwa katika kituo cha redio Clouds na kudai kuwa chanzo cha ugomvi huo ni baada ya mwalimu yule kumuita kwa jina la ‘Dogo Jinga' na yeye kujibu mapigo kwa kumwambia ‘kubwa jinga njoo' kitendo ambacho kilimchukiza mwalimu huyo.
Anaongeza kuwa hakuwa akitambua kama yule ni mwalimu katika shule yao kutokana na kutokuwa na muda mrefu tangu ajiunge na shule hiyo, hivyo mwalimu wake kukasirika na kuanza kumtwanga ngumi.
"Nilijua ni mwanafunzi wa vidato vya juu anataka kunizingua, ndiyo maana nikawa namjibu kila alipokuwa ana nitukana na mpaka kuamua kunipiga," alisema Dogo janja.
Dogo alizidi kulalamika kuwa alipigwa sana hasa mdomoni, hali iliyomsababishia maumivu makali mwilini na kwamba alienda hospitali baada ya kushushiwa kipigo hicho.
Ameongeza kusema kuwa ni bora ahame katika shule hiyo kwa ajili ya kukimbia ngumi na mateke aliyoshushiwa na mwalimu huyo, kwani hata baada ya kupelekwa ofisini na mwalimu huyo alianza kumpa maneno ya kejeli mbele ya walimu wote.
 
Simba kukalia kiti cha ligi leo?


na Dina Ismail


amka2.gif
MABINGWA wa Ligi Kuu ya Vodacom, timu ya soka ya Simba, leo wanashuka katika Uwanja wa Uhuru kukwaana na wakata miwa wa Manungu, Mtibwa Sugar.
Mechi hiyo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa timu hizo pamoja na kila timu kutaka kushinda ili kujipatia pointi ambazo zitawaweka katika mazingira mazuri ya kuwania ubingwa.
Akizungumzia mechi ya leo, Kocha wa Simba Mzambia, Patrick Phiri, amesema ni mechi ngumu, ugumu huo unatokana kuwa Mtibwa ni timu nzuri hivyo hawatakubali kupoteza mchezo huo.
"Pia kipindi hiki ni cha lala salama, hivyo kila timu inahitaji kushinda ili kujipatia pointi tatu, hili halipo kwa mechi hii, bali ni kwa mechi zote," alisema.
Hata hivyo Phiri alisema amekiandaa kikosi chake kikamilifu na hivyo kazi kubwa imebaki kwa wachezaji wake kuhakikisha wanacheza kufa na kupona ili kuweza kushinda.
"Itakuwa ni mechi ngumu kutokana na kipindi hiki tulichopo cha lala salama, hivyo kila timu inahitaji kushinda ili ipate pointi tatu.
Naye Kocha Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime, alisema wanafahamu kuwa ni mechi ngumu lakini wana uhakika wa kushinda.
"Sisi tumejiandaa kikamilifu na ligi, si kwa mechi hii tu bali mechi zote zilizosalia, hivyo pointi tatu za leo nadhani tutaondoka nazo," alisema Mexime.
Iwapo Simba itashinda leo itafikisha pointi 37 na hivyo kukalia usukani wa ligi hiyo ambapo kwa sasa Azam FC inaongoza ikiwa na pointi 35 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 35.
 
Kili Marathon kuanza kutimua vumbi leo


na Tullo Chambo, Moshi


amka2.gif
WAKATI mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathon zikianza kutimua vumbi leo mjini hapa, kwa mara ya kwanza katika historia ya mbio hizo wanariadha kutoka Ethiopia wamejitokeza kushiriki.
Mbali ya Waethiopia, pia Waganda 18 wamewasili mjini hapa kwa ajili ya mbio hizo zitakazoanzia Uwanja wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Stadi za Biashara (MUCCoBS), na kupita barabara mbalimbali za mjini Moshi.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja hivyo jana, Mkurugenzi wa Ufundi wa mbio za Kili Marathon, John Bayo, alisema, mwamko wa washiriki mwaka huu umeongezeka ambapo takriban wakimbiaji zaidi ya 6,000 watashiriki kutoka nchi 35.
Bayo alisema kizuri zaidi mwaka huu wanariadha wawili kutoka Ethiopia na 18 kutoka Uganda wamejitokeza, jambo ambalo halijawahi kujitokeza katika mbio hizo, hivyo uwepo wa Wahabeshi hao utaleta ushindani mkubwa, kwani inaaminika duniani nchi hiyo kuwa na wakimbiaji bora wa mbio ndefu.
Mgeni rasmi katika mbio hizi ambazo ni msimu wa tisa sasa, anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, ambaye ndiye ataanzisha mbio hizo mapema leo asubuhi na baadaye atakabidhi zawadi kwa washindi.
Kwa upande wa burudani, mbio hizo zitapambwa na bendi ya African Stars ' Twanga Pepeta', TMK Wanaume Family pamoja na mshindi wa tatu wa shindano la kusaka Bongo Star Search (BSS), Joseph Payne, maarufu kama ‘Mzungu wa BSS'.
Mbio za Kili Marathon zimedhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ambao ndio wadhamini wakuu, Vodacom Tanzania, DT Dobie, Simba Cement, TPC Sugar, Tanzanite One, Precisionair, Kilimanjaro Water, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Keys Hotel huku waratibu ni Wild Frontiers na Executive Solutions.
Naye Charles Ndagulla anaripoti kuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya (CHADEMA) , leo anatarajia kushiriki mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run kwa ajli ya kukusanya fedha za kununua vitanda 50 kwa ajili ya kusaidia wagonjwa katika Hospitali teule ya wilaya ya St. Joseph.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa muda mfupi baada ya kujiandikisha kwenye Hotel ya Key's, Owenya alitoa wito kwa wasamaria wengine kusadia hospital hiyo kutokana na kuwa na uhaba wa vitanda unaosababisha baadhi ya wagonjwa kulala chini.
 
Matawi Yanga yampasha Manji


na Makuburi Ally


amka2.gif
VIONGOZI wa matawi ya Yanga mkoani Dar es Salaam wametoa pendekezo kwa viongozi wa Kamati ya Utendaji kwa kumtaka mdhamini Mkuu wa timu hiyo, Yusuf Manji, kutenganisha uongozi na ufadhili.
Mapendekezo hayo yametolewa jana katika kikao cha viongozi wa matawi, ambapo Mwenyekiti wa matawi hayo, Mohamed Msumi, alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kuwasilishiwa hoja ya kujiuzulu kwa Manji katika mkutano huo.
Msumi alisema hawakuishia katika mkutano huo pia wamependekeza zaidi kwa viongozi wa Kamati ya Utendaji kulipeleka suala hilo katika mkutano wa Kamati ya Utendaji inayoketi leo kwa ajili ya kuweka sawa mikakati ya maendeleo ya Yanga.
Aidha, Msumi alisema walipendekeza pia iwapo Manji ametangaza kuiacha timu hiyo, basi wito utolewe kwa wadau wengine wenye nia njema na Yanga kujitokeza kwa ajili ya kuisaidia timu yao.
Msumi alisema katika mkutano huo walijadili pia maendeleo ya Yanga katika Ligi Kuu Tanzania Bara inayoendelea hapa nchini ambako mkutano wao ulikutanisha viongozi wa matawi na wa Kamati ya Utendaji.
"Kikao cha kesho (leo) cha Kamati ya Utendaji ndiyo kitatoa jibu la mapendekezo yetu, tuliyowapa viongozi hao, hivyo Mwenyekiti Lloyd Nchunga kesho atatoa taarifa za makubaliano hayo," alisema Msumi.
 
Moro United kupunguza wachezaji


na Dina Ismail


amka2.gif
KATIKA kukiimarisha kikosi chake kwenye Ligi Kuu Bara msimu ujao, timu iliyopanda katika ligi hiyo ya Moro United ya Tabata imepanga kupunguza baadhi ya wachezaji ili kuongeza wachezaji wapya.
Mwenyekiti wa timu hiyo, Rodgers Peter, alisema jana kwamba wanasubiri taarifa ya mapendekezo ya wachezaji hao kutoka kwa Kocha wao Mkuu, Hassan Banyai.
Alisema kutokana na mikikimikiki ya Ligi Kuu hawana budi kukiimarisha kikosi chake kwa kuhakikisha kinakuwa na wachezaji ambao wataweza kuitumikia vema klabu hiyo, hivyo hawana budi kuwapunguza baadhi ya wachezaji.
"Tunakwenda katika ligi ngumu zaidi hivyo hatuna budi kuwa na wachezaji wenye viwango vya ligi hiyo, pia wenye jitihada na wanao jituma...tupo katika mchakato wa kusaka wachezaji wapya, huku tukisubiri taarifa za wachezaji kutoka kwa kocha wetu", alisema Rodgers.
Moro United imepanda kucheza ligi kuu msimu ujao pamoja na timu za JKT Oljoro ya Arusha, Coastal Union ya Tanga na Villa Squad ya Kinondoni.


h.sep3.gif

 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom