Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,508
- 911,249
- Thread starter
- #8,601
TAKUKURU yamng'ang'ania Mwakalebela
na Francis Godwin, Iringa
SIKU moja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Iringa kumwachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela, katika shitaka lake la rushwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Iringa Mjini, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani hapa imekusudia kuendelea na kesi hiyo.
Akizungumza na Tanzania Daima, Mwanasheria wa TAKUKURU mkoani hapa, Ntimu Mizizi, alisema maamuzi ya mahakama hiyo chini ya Hakimu Festo Lwila ameyakubali na kuwa mapungufu yaliyokuwemo awali katika kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2010, taasisi hiyo inayafanyia kazi na kufungua kesi yenye maelekezo ya mahakama.
Alisema maamuzi ya mahakama katika kesi hiyo yameonekana ni mazuri na yenye maelekezo ya kina zaidi kuliko ilivyokuwa kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, Joseph Mungai, ambapo mahakama haikuingia kiundani zaidi kama ilivyo katika maamuzi madogo ya kesi ya Mwakalebela.
Alisema kesho kutakuwa na majibu sahihi dhidi ya uamuzi wa TAKUKURU kuendelea na kesi hiyo ama la.
Mahakama hiyo chini ya Hakimu Lwila ambaye alikuwa anasikiliza shauri hilo, aliiondoa kesi hiyo na kumwachia huru mtuhumiwa huyo baada ya kuridhika na hoja moja ya upande wa utetezi kwamba kulikuwa na mapungufu ya kisheria kwenye hati ya mashitaka.
Mapungufu hayo ni mtuhumiwa kushitakiwa kwa makosa mawili kwenye hati moja ya mashitaka, hivyo kumfanya mtuhumiwa ashindwe kuelewa kwa usahihi kosa linalomkabili, kitu ambacho kinaweza kumfanya ashindwe kuandaa utetezi wake.
Aidha, Mwakalebela kesho ataendelea na kesi nyingine namba 8 ya mwaka 2010 ambayo inamkabili yeye pamoja na mkewe, Selina, ambayo ipo hatua ya kutolea hukumu pingamizi la kisheria iwapo iondolewe mahakamani au la.

PRINT