Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
- Thread starter
- #7,621
Ligi netiboli yanoga Morogoro
Imeandikwa na John Nditi, Morogoro; Tarehe: 21st February 2011 @ 08:04 Imesomwa na watu: 6; Jumla ya maoni: 0
TIMU nane za netiboli kati ya 11 zilizojitokeza kushiriki ligi daraja la pili ngazi ya taifa, zimepenya mzunguko wa pili hatua ya makundi kwa ajili ya kinyang'anyiro cha kupanda ligi daraja la kwanza.
Mkufunzi Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Mary Protas, amesema hayo mjini hapa baada ya kumalizika michezo ya hatua ya awali ya makundi na timu nane kati ya 11 kuingia hatua hiyo.
Alisema michezo ya hatua ya pili inaanza leo kwa mtindo wa ligi na kuzitaja timu zilizoingia hatua hiyo kwa Kundi A ni Hamambe ya Mkoa wa Mbeya, Polisi Pwani, Ruangwa ya Lindi na Alliance One ya Mkoa wa Morogoro.
Alizitaja za Kundi B ni Polisi Arusha, Ruvu JKT kutoka Pwani, Tigo ya Dar es Salaam na Tandahimba ya Mkoa wa Mtwara.
Alizitaja timu zilizoshindwa kufuzu mzunguko huo wa pili ni Black Sister kutoka Pwani, Tupendane ya Lindi na Mzinga ya Morogoro.
Katika hatua nyingine, Mkufunzi Mkuu alisema uongozi wa chama hicho unaangalia uwezekano wa kupandisha timu zaidi kutoka ligi daraja la pili kwenda daraja la kwanza mwaka huu.
"Lengo ni kuongeza timu za kucheza ligi daraja la kwanza, kabla ya ligi hii kumalizika kamati itakutana kuangaliwa uwezekano huo kwa hizi timu nane za mzunguko wa pili," alisema Mkufunzi Mkuu huyo.
Hata hivyo alitoa mfano wa nia ya kuongeza idadi ya timu za ligi daraja la pili kwenda la kwanza msimu huu ni kutokana na kujidhihirisha wazi idadi ya timu ambazo hazikushiriki ligi hiyo msimu wa mwaka jana pamoja na baadhi kutoa taarifa rasmi na nyingine bila taarifa.

PRINT