Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Azam yaitoa Yanga kileleni
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 21st February 2011 @ 08:42 Imesomwa na watu: 180; Jumla ya maoni: 0


02_11_0hutsh.jpg

Mchezaji wa JKT Ruvu, Pius Kasambale (kushoto) akiwania mpira na Luckson Kakolaki wa Azam wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Azam ilishinda mabao 2-0. (Picha na Fadhili Akida).





MAMBO yanakwenda kwa zama na zama zinakwenda kwa zamu, sasa ni zamu ya Azam kuongoza Ligi Kuu Tanzania Bara.

Pengine ukiulizwa swali kwa haraka haraka kuhusu Ligi Kuu Tanzania Bara na hasa matokeo ya mchezo kati ya Azam FC na JKT Ruvu uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam ndivyo ungeweza kujibu.

Azam imeifunga JKT Ruvu mabao 2-0 katika mchezo wa ligi hiyo na kuifanya ifikishe pointi 35 sawa na Yanga iliyokuwa ikiongoza, lakini Azam inakalia kiti cha uongozi kutokana na kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Azam ina tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa 21, wakati Yanga inayo 18. Simba iliyokuwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 34 sasa imeshuka hadi nafasi ya tatu.

Hata hivyo Azam imecheza michezo 17 hivyo kuizidi Yanga yenye michezo 16 na pia imeizidi michezo miwili Simba, hali ambayo kama timu hizo zitatumia vyema michezo yao ya viporo siku za Azam kukaa kileleni zitakuwa za kuhesabu.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Oden Mbaga, Azam ilipata bao la kwanza dakika ya 42 kutokana na shuti la mbali la Ibrahim Mwaipopo.

Wachezaji wa JKT wakiongozwa na Pius Kisambale, Yahya Akilimali na Mwinyi Kazimoto walijaribu mara kadhaa kutaka kusawazisha lakini umaliziaji haukuwa mzuri.

JKT Ruvu ilijikuta ikifungwa bao la pili dakika ya 72 baada ya beki Stanley Nkomola kujifunga wakati wa harakati za kuokoa.

Azam ingeweza kufunga mabao mengi, lakini Mrisho Ngasa, John Boco na Peter Senyonjo walishindwa kutumia nafasi walizozipata.

Naye Grace Chilongola anaripoti kutoka Mwanza kuwa timu ya Toto African imeifunga AFC Arusha mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Mabao ya Toto yalifungwa na Hussein Sued dakika ya 37 na Semmy Kessy dakika ya 60, wakati la AFC lilifungwa dakika ya 85 na Abdallah Juma.

Mchezo mwingine ulifanyika Bukoba, ambapo Kagera Sugar na African Lyon zilitoka 0-0.
 
Azam yakaa penyewe


*Yazishusha Yanga, Simba kileleni

Na Zahoro Mlanzi

TIMU ya Azam FC, imekwea mpaka kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara baada ya kuifunga
JKT Ruvy ya Pwani mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, Azam sasa imefikisha pointi 35 sawa na waliokuwa vinara wa ligi hiyo, Yanga ila inaongoza kwakuwa na uwiano mzuri wa mabao ukilinganisha na Yanga.

Kabla ya mchezo wa leo, Azam ilikuwa ikiongoza kwa tofauti ya mabao 19 na sasa itakuwa na mabao 21, Yanga ina mabao 18 na Simba ambayo ipo katika nafasi ya tatu kwa pointi 34 ina mabao 14.

Katika mchezo huo wa jana, timu zote zilianza mchezo kwa kukamiana kwa kuchezeana faulo na kutumia nguvu nyingi lakini Azam ilikuwa ya kwanza kubisha hodi langoni mwa JKT dakika ya 15 baada ya John Bocco na Mrisho Ngassa kuonana vyema lakini shuti la Bocco lilitoka nje.

JKT iliyoonekana kutawala mchezo huo kwa kupiga pasi nyingi, dakika ya 30, Bakari Kondo alishindwa kuifungia timu yake bao baada ya kubaki na Luckson Kakolaki ambapo alipiga shuti dhaifu na kutua mikononi mwa kipa Jackson Chove.

Ikiwa zimebaki dakika tatu kabla ya mchezo kuwa mapumziko, Ibrahim Mwaipopo aliifungia Azam bao la kwanza kwa shuti nje ya eneo la hatari baada ya kupokea pasi iliyotolewa kwa kifua na Bocco na kutumbukiza mpira wavuni.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo dakika ya 59, Azam ilipata pigo baada ya Mwaipopo kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kumchezea vibaya Kondo.

Timu hizo ziliendelea kushambuliana huku JKT ikitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini washambuliaji wake walishikwa ma kigugumizi cha miguu kila walipolikaribia lango la Azam.

Dakika ya 73, Shaibu Nayopa wa JKT katika harakati za kuokoa hatari golini kwake alijikuta akitumbukiza mpira wavuni kutokana na kona iliyopigwa na Ibrahim Shikanda na kufanya dakika 90 zikimalizika Azam kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Katika michezo mingine ya ligi hiyo, jijini Mwanza, Mwandishi Wetu, Daud Magessa anaripoti kwamba wenyeji Toto African imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Arusha FC.Mabao ya Toto yalifungwa na Hussein Swedi na Semmy Kessy na la AFC lilifungwa na Abdallah Juma.

Katika mchezo mwingine uliopigwa Kagera, Mwandishi Wetu, Theonista Juma anaripoti kwamba wenyeji Kagera Sugar ilitoka suluhu na African Lyon katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Kaitaba mkoani humo.

 
Simba SC yamtega Phiri


Na Zahoro Mlanzi

ZIKIWA zimebaki siku 26 kabla ya mabingwa wa soka Tanzania bara, Simba kuumana na TP Mazembe, uongozi wa timu hiyo umesema benchi la
ufundi ndilo litakaloamua kama wacheze michezo ya kirafiki ya kimataifa au vinginevyo kabla ya kuumana na timu hiyo.

Benchi hilo linaongozwa na Kocha Mkuu, Patrick Phiri akisaidiana na Amri Said watakuwa na kazi ya ziada kuhakikisha wanaiandaa vizuri timu hiyo ili iiondoshe Mazembe katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Wakati Phiri akitafakari hilo, tayari vyombo vya habari vimeripoti kwamba huenda timu hiyo ikapiga kambi nchini Zambia kabla ya kwenda Lubumbashi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kucheza na Mazembe.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Cliffold Ndimbo alisema maandalizi kwa ajili ya klabu bingwa yanaendelea na kwamba uongozi unasubili mapendekezo kutoka kwa benchi la ufundi.

"Maandalizi yanaendelea ila kwa sasa tunachosubili ni taarifa kutoka benchi la ufundi kama litahitaji mechi za kirafiki za kimataifa au la na baada ya kupokea ndipo sasa tutakaa na kujadili," alisema Ndimbo.

Alisema pamoja na kusubili taarifa hizo, michezo ya Ligi Kuu bara nayo itakuwa ni sehemu ya maandalizi yao katika kuhakikisha wanaing'oa timu hiyo na kuweka historia mpya.

Ndimbo alisema leo wataendelea na mazoezi kama kawaida kwani wanajiwinda na mchezo mgumu dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Jumapili ijayo.

Akizungumzia hali za wachezaji wao, alisema wachezaji wote wapo katika hali nzuri ila Uhuru Seleman na Hilary Echessa bado hali zao hazijatengemaa.
 
‘Tamasha letu litakuwa endelevu'

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 21st February 2011 @ 08:31 Imesomwa na watu: 9; Jumla ya maoni: 0









KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka imetamba kuwa tamasha lao litakuwa endelevu kama ilivyo Tamasha la Sauti za Busara la Zanzibar.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Alex Msama amesema kuwa kila mwaka wanalifanyia maboresho tamasha hilo na kuwa wana matumaini mambo yatakuwa mazuri.

"Zanzibar wanalo tamasha la Sauti za Busara limekuwa likifanyika kila mwaka na limekuwa na mafanikio makubwa.

"Nasi pia tunataka kila mwaka tufanye Tamasha la Pasaka likiwa na mafanikio makubwa, ili ikifika Januari wananchi wawe wanajua kwamba tamasha letu limekaribia.

"Hili ni tamasha la watu wa imani zote, maana pale ni nyimbo za kumtukuza na kumsifu Mungu, " alisema Msama.

Tamasha hilo kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu litafanyika sikukuu ya Pasaka Aprili 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Kulingana na waandaaji hao baada ya tamasha hilo la Dar es Salaam pia litafanyika katika mikoa ya Shinyanga Jumatatu ya Pasaka Aprili 25 na Mwanza Aprili 26 ambayo itakuwa ni sikukuu ya Muungano.
 
Villa Squad yarejea Ligi Kuu Bara

Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Tanga; Tarehe: 21st February 2011 @ 08:31 Imesomwa na watu: 39; Jumla ya maoni: 0








TIMU ya Villa Squad ya Dar es Salaam jana ilifanikiwa kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara licha ya kutoka 0-0 na Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Mchezo huo wa fainali za ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora ulikuwa na ushindani mkubwa na mashabiki walishuhudia dakika 90 zikimalizika bila miamba hiyo kufungana.

Matokeo hayo yameifanya Villa Squad iliyoshuka daraja msimu wa mwaka 2008/2009 ifikishe pointi 12 sawa na Polisi Morogoro ambayo jana iliifunga JKT Oljoro bao 1-0, lakini Villa ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Kulingana na msimamo wa ligi hiyo, Villa ina pointi 12 mabao 12 ya kufunga, matano ya kufungwa, wakati Polisi ina pointi 12 mabao manane ya kufunga na manne ya kufungwa.

Kwa mazingira hayo, Villa sasa inaungana na JKT Oljoro inayoongoza ligi ikiwa na pointi 15, Coastal Union inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 13 kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2010/2011.

Timu ya nne itategemea matokeo ya mchezo wa leo kati ya Moro United inayoshika nafasi ya sita ikiwa na pointi kumi na Morani inayoshika mkia ikiwa na pointi mbili, ambao utafanyika alasiri kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Kama Moro United itashinda mchezo huo itafikisha pointi 13, hivyo itakuwa imepanda daraja kwa kushika nafasi ya pili ama ya tatu kutegemeana na uwiano wake wa pointi na Coastal Union, lakini kama itafungwa ama kutoka sare basi Polisi Morogoro yenye pointi 12 ambayo inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi itakuwa ndiyo imepanda daraja.

Rhino ya Tabora inayoshika nafasi ya tano ikiwa na pointi 11 haina matumaini ya kupanda daraja kutokana na matokeo ya mechi za Februari 20.

Timu nne za juu ndizo zinapanda daraja katika ligi hiyo inayoshirikisha timu tisa.

Prisons ya Mbeya inashika nafasi ya saba ikiwa na pointi tisa, wakati TMK United inashika nafasi ya nane ikiwa na pointi sita na leo inamaliza ligi kwa kucheza na Coastal alasiri.
 
Corefa yahitaji 30m/- timu za vijana

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 21st February 2011 @ 08:31 Imesomwa na watu: 6; Jumla ya maoni: 0








KIASI cha Sh milioni 29 kinahitajika kwa ajili ya kuandaa timu mbili za Mkoa wa Pwani kushiriki mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Pwani (Corefa), Hassan Othman wakati wa Mkutano Mkuu wa chama hicho mjini Kibaha, Pwani.

Aliwaambia wajumbe waliohudhuria mkutano huo kuwa fedha hizo zitahusu maandalizi ya timu zake mbili za vijana zitakazoshiriki michuano ya Copa Coca-Cola itakayofanyika karibuni.

Alisema licha ya kutaka kuandaa timu hizo vyema, pia tayari Corefa imepata kiwanja eneo la Mlandizi na kuwa wanataka kujenga uwanja wa kisasa na kituo cha michezo ambacho kitatumiwa na timu zao na nyingine ambazo zitakuwa zinapangiwa na kuwaingizia mapato.

Alisema ili malengo hayo yafanikiwe chama kinawaomba wadau wajitokeze kusaidia shughuli hizo ikiwa ni pamoja na kuunda Kamati Maalumu ya Ushindi ya mkoa.

Naye mgeni rasmi katika mkutano mkuu huo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Bernard Nzungu, aliwaambia wajumbe wa Corefa wanaotoka katika wilaya za Kibaha, Rufiji, Kisarawe, Mafia, Bagamoyo na Mkuranga kuwa serikali ya mkoa itawasaidia kuhakikisha wanapata hati ya kiwanja hicho cha kituo cha michezo ambacho wamekipata.

Alisema pia atashirikiana na chama hicho kuhakikisha wafadhili na kamati ya kuchangisha fedha inaundwa ili Pwani iweze kuwa kinara katika mashindano mbalimbali wanayoshiriki.
 
Watoto wa Mgosi wapatikana mabomu ya Gongo la Mboto

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 21st February 2011 @ 08:04 Imesomwa na watu: 47; Jumla ya maoni: 0








MSHAMBULIAJI wa Simba ya Dar es Salaam, Mussa Mgosi, amesema amefanikiwa kupata watoto wake waliokuwa wamepotea baada ya milipuko ya mabomu ya Gongo la Mboto.

Mgosi amesema alipigiwa simu na mkewe Jumatano usiku akimjulisha kuwa watoto wao wawili pamoja na wafanyakazi wawili walikuwa hawapo nyumbani mara baada ya milipuko hiyo.

"Jumatano wakati milipuko inatokea nilikuwa Mwanza, ambapo siku hiyo Simba ilicheza na Toto African, nilipata taabu sana kuulizia kwa ndugu na jamaa kama wamewaona wanangu.

"Nashukuru watu wa vyombo vya habari pia walinisaidia jambo hili, hivyo naomba kuwajulisha kwamba wanangu niliwapata jioni ya siku iliyofuata.

"Mmoja alikimbilia maeneo ya Mbagala na mfanyakazi mmoja na mwingine alikuwa Uwanja wa Uhuru, lakini wote tumewapata," alisema na kuwataja wanawe kuwa ni Hassan na Naylat.

Mgosi anaishi eneo la Kitunda, Dar es Salaam ambapo alieleza umuhimu wa jamii kushirikiana na watu mbalimbali ambao wamepoteza watoto wao.

"Ni kipindi kigumu sana, lakini jamii tuwe na moyo wa ushirikiano kuwafariji wote waliopata matatizo kwa namna mbalimbali kwenye milipuko ya Gongo la Mboto," alisema.

Jumatano usiku kulitokea mlipuko wa mabomu kwenye kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), eneo la Gongo la Mboto na kusababisha watu 20 kufariki dunia na wengine kujeruhiwa.
 
Watoto wa Mgosi wapatikana mabomu ya Gongo la Mboto

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 21st February 2011 @ 08:04 Imesomwa na watu: 47; Jumla ya maoni: 0








MSHAMBULIAJI wa Simba ya Dar es Salaam, Mussa Mgosi, amesema amefanikiwa kupata watoto wake waliokuwa wamepotea baada ya milipuko ya mabomu ya Gongo la Mboto.

Mgosi amesema alipigiwa simu na mkewe Jumatano usiku akimjulisha kuwa watoto wao wawili pamoja na wafanyakazi wawili walikuwa hawapo nyumbani mara baada ya milipuko hiyo.

“Jumatano wakati milipuko inatokea nilikuwa Mwanza, ambapo siku hiyo Simba ilicheza na Toto African, nilipata taabu sana kuulizia kwa ndugu na jamaa kama wamewaona wanangu.

“Nashukuru watu wa vyombo vya habari pia walinisaidia jambo hili, hivyo naomba kuwajulisha kwamba wanangu niliwapata jioni ya siku iliyofuata.

“Mmoja alikimbilia maeneo ya Mbagala na mfanyakazi mmoja na mwingine alikuwa Uwanja wa Uhuru, lakini wote tumewapata,” alisema na kuwataja wanawe kuwa ni Hassan na Naylat.

Mgosi anaishi eneo la Kitunda, Dar es Salaam ambapo alieleza umuhimu wa jamii kushirikiana na watu mbalimbali ambao wamepoteza watoto wao.

“Ni kipindi kigumu sana, lakini jamii tuwe na moyo wa ushirikiano kuwafariji wote waliopata matatizo kwa namna mbalimbali kwenye milipuko ya Gongo la Mboto,” alisema.

Jumatano usiku kulitokea mlipuko wa mabomu kwenye kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), eneo la Gongo la Mboto na kusababisha watu 20 kufariki dunia na wengine kujeruhiwa.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom