Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
- Thread starter
- #7,261
Taswa FC yapigwa jeki
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 19th February 2011 @ 23:50 Imesomwa na watu: 15; Jumla ya maoni: 0
HOTELI mpya ya New Avon imetangaza kuidhamini timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC .
Mkurugenzi Mtendaji wa New Avon Shaheed Dhanani alisema kuwa wanatambua mchango mkubwa wa timu hiyo katika maendeleo ya soka na michezo nchini.
Shaheed alisema kuwa kwa vile wanaingia rasmi katika biashara ya hoteli na kutokana na ubora wa hoteli yao, wameamua kuisapoti timu hiyo na wanaamini watafanya vyema kupitia udhamini wao.
"New Avon Hotel itatoa jezi zenye thamani ya dola za Marekani 900 ambazo kwa sasa zinachapishwa huko Dubai, ni jezi za kisasa na zina ubora wa hali ya juu," alisema Shaheed.
Alisema kuwa mbali ya jezi, pia watatoa soksi kwa wachezaji ili waonekane nadhifu kama ilivyo hoteli yao ambayo ipo katika makutano ya mitaa ya Aggrey na Jamhuri (Mnazi Mmoja).
Alisema kuwa wanatarajia kuongoza katika soko la hoteli nchini kutokana na huduma zao na ubora wa hoteli hiyo na ndiyo maana wameamua kuidhamini Taswa FC ikiwa ni timu bora ambayo toka kuanza kwa mwaka huu haijafungwa.
Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary aliipongeza New Avon Hotel na kuahidi kutoa ushirikiano mkubwa katika kuinadi hoteli hiyo katika mechi na shughuli zake.
"Tunajivunia kuwa na New Avon Hotel, tunakubali msaada wao na tunaahidi kufanya vyema katika mechi zetu kupitia msaada wa hoteli hiyo, " alisema Majuto.

PRINT