Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Valencia coach keeps the faith


RivalsDM



PRINT RSS

1 comments »

Updated Feb 16, 2011 8:13 AM ET
Unai Emery has faith Valencia can still reach the Champions League quarter-finals despite being held 1-1 at home by Schalke on Tuesday night.
Roberto Soldado gave in-form Valencia a flying start to the last-16 first-leg encounter at the Mestalla when he netted 17 minutes in, but Schalke drew level in the second half through former Spain and Real Madrid striker Raul.


That away goal means Schalke hold the slight upper hand going into the return leg, but Emery is staying positive, saying: "It's not the best result, but neither is it the worst.
"Schalke have earned a slight advantage for the return game, but we have to be optimistic because we've had good games away from home in the Champions League this season, in fact we haven't lost.
"We have to look for goals as well in Germany and prepare thoroughly for the game so things go better.
"They are a good team. We've suffered against (Klaas-Jan) Huntelaar and Raul. We also had a number of chances, but we're not so upset because anything that isn't a defeat or a goalless draw in the second leg could see us through.
"I'm still convinced about our chances of qualifying."
Soldado added: "We're ambitious in the dressing room. It's true that we hoped to get a positive result and maybe this isn't what we hoped for, but we've worked too hard to get this far to give up now.
"We all want to be in the quarter-finals and we are going to do everything possible to get into the next round. That's the dream we have. We can recover."
 


newreply.php



MAKE A DENT

Serie A Roundup: Juventus checked Inter Milan's pursuit of leader AC Milan with a 1-0 win on Sunday. RELATED

Cavani: Napoli deserved victory

Italian Serie A Wrap, Feb. 12

Milan hit fab four against Parma







1
2






Serie AHeadlines




More News »

fscLeagueFrontStandingsHdr.gif

#
Team
GP
Pts

1
25
52

2
25
49

3
25
45

4
24
44

5
25
43

6
25
41

7
25
40

8
24
39

9
25
35

10
24
32

Full Standings »


FOX Sports Blog of the Day


Jamie Trecker
Follow @FoxSoccer on Twitter


More Blogs »

More than Sports on MSN


Sports Illustrated's swimsuit models





fscLeagueFrontFixturesHdr.gif

Week 25​

Final

4-0

Match Stats

Final

0-2

Match Stats

Final

2-4

Match Stats

Final
Bari

0-0

Match Stats

Final

0-2

Match Stats

Final

3-1

Match Stats

Final

4-1

Match Stats

Final

3-2

Match Stats

Final

0-3

Match Stats

Final

1-0

Match Stats

liveIndicator.png


1-2

Match Stats

liveIndicator.png


0-1

Match Stats
 
Wizara yasitisha usambazaji filamu ya ‘Shoga'


na Janet Josiah


amka2.gif
WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeiagiza Kampuni ya kutengeneza filamu ya Al-Riyamy Production kuwasilisha filamu ya ‘Shoga' kwa Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Filamu kwa ajili ya ukaguzi.
Taarifa iliyotolewa na kitengo cha habari na mawasiliano cha wizara hiyo, kilisema kampuni hiyo inatakiwa kuwasilisha kanda hiyo kabla ya leo.
Aidha, kampuni hiyo pia imeagizwa kutoisambaza filamu hiyo na kusitisha hatua nyingine zinazohusiana nayo kuendelea hadi hapo Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Filamu itakapomaliza ukaguzi wake.
"Bodi itakapojiridhisha kuwa filamu hiyo inakidhi kuonyeshwa hadharani kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Filamu na Michezo ya Jukwani Namba 4 ya mwaka 1976, itaendelea kusambazwa," ilisema taarifa hiyo
Kwa mujibu wa sheria hiyo, hairuhusiwi kutengeneza filamu bila kupata kibali cha kufanya hivyo.

Hata hivyo, kifungu cha 4 (1), kinaelekeza bayana kuwa kila anayetengeneza filamu anatakiwa kuwasilisha maombi kwa maandishi kwa waziri, chini ya sheria hii yakiambatana na muswada na maelezo ya filamu inayotarajiwa kutengenezwa.
Pamoja na mambo mengine, katika kifungu cha 14 (2), sheria inaipa bodi ya filamu mamlaka ya kukagua filamu, picha ya matangazo au maelezo yake, kwa makusudi ya kuamua kuonyesha na ikiwaruhusu, itatolewa maonyesho yawe kwa namna gani.
Katika sheria hiyo kifungu cha 15 (1), kinapiga marufuku kwa mtu yoyote kuongoza, kusaidia, kuruhusu au kushiriki katika maonyesho ya filamu bila kuwa na kibali cha bodi.
Sheria hii ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa waraka Namba 22 wa mwaka 1974.
 
Chai Jaba, Kazinja watua Rufita Connection


na Mariana Mathias


amka2.gif
BENDI ya Rufita Connection jana ilitambulisha wanamuziki wake wapya na kuunda uongozi mpya wa bendi hiyo yenye makazi yake Tabata jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja Masoko wa bendi hiyo, Juma Abajalo, alisema wameamua kusaini mkataba na wanamuziki wapya kwa lengo la kuisuka upya na kuleta changamoto mpya katika sekta ya mziki.
Alisema, katika mziki wa sasa kuna changamoto nyingi zinazotokea, hivyo inabidi kuwa na mbinu mbalimbali katika kukabiliana nazo, hasa katika kuhakikisha wanawaburudisha mashabiki wao na kuhakikisha wanaongeza kiwango kikubwa cha wapenzi kutoka pande zote za dunia.
Abajalo, aliwataja wasanii hao wapya kuwa ni rapa Chai Jaba ambaye atakuwa rais wa bendi hiyo na wameingia naye mkataba wa miaka miwili na Hafsa Kazinja waliyeingia naye mkataba wa mwaka mmoj ambaye atakuwa Makamu wa Rais.
Wengine ni wanenguaji Violet na Jack kutoka bendi ya Diamond Musica na Jimmy ambaye atakuwa katibu wa bendi.
Hata hivyo, katika malengo mapya waliyoweka wasanii hao walioingia mkataba mpya ni pamoja na kuhakikisha wanaleta utofauti katika maendeleo ya bendi hiyo na kwamba wameishafanya mikakati ya kupanga mbinu za kukonga nyoyo za mashabiki wao pindi watakapokuwa wakiwaburudisha katika jukwaa.
Kwa upande wao viongozi hao wapya, Chai Jaba na Hafsa Kazinja, walisema watashirikiana katika kufanya kazi na Watanzania hasa mashabiki wao na kuwa watarajie vitu vizuri kutoka kwao.
Chai Jaba alisema amekuja na nguvu mpya na ameandaa rapu tatu katika albamu ya ‘Munira' ambazo ni ‘Matumbo', ‘Wewe ni Wangu' na ‘Moja'.
Aliongeza kuwa amejipanga kwa staili mpya ya kurapu katika kipindi hiki kipya alichoingia katika bendi hiyo na anatarajia kuwashangaza watu na kuweka historia mpya ya mwaka 2011.
Alisema ushirikiano ndio ngao kubwa katika kutengeneza mafanikio yoyote na amewataka wanamuziki waache kubaguana na badala yake wawe kitu kimoja katika kuendeleza muziki Tanzania.
 
Hassanali na ‘Siku ya Mwanamke' kwa mitindo


na Dina Ismail


amka2.gif
KATIKA kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania na miaka 100 ya ‘Siku ya Mwanamke Kimataifa', mbunifu nguli wa mavazi nchini, Mustafa Hassanali, kwa kushirikiana na wabunifu waalikwa wa kimataifa kutoka Uingereza watafanya onyesho maalumu litakalolenga kusaidia uzazi salama.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Hassanali alisema maonyesho hayo yatafanyika Machi 4-5 na anaamini mitindo inaweza kutumika kama njia mbadala ya kuchangia, kuhamasisha na kueneza taarifa kwa jamii zinazohusiana na masuala ya afya.
"Kwa kushirikiana na Shirika la Utepe Mweupe la Tanzania kwa pamoja tumeamua kufanya maonyesho ya mavazi kwa siku mbili, lengo si tu kuonyesha mavazi ya Mustafa Hassanali kwa mwaka 2011 na utu mwanamke, bali pia kuhamasisha uzazi salama nchini," alisema na kuongeza:
"Kila dakika moja dunia inapoteza mwanamke mmoja kwa matatizo ya uzazi, tunahitaji kufanya mabadiliko, hususani katika kipindi hiki ambacho dunia inasherehekea miaka 100 ya Siku ya Mwanamke na miaka 50 toka uhuru, hivyo hatuna budi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha tunampa mchango mwanamke katika suala zima la afya ya uzazi," alisema Hassanali.
Naye Meneja Mauzo na Masoko wa Hassanali, Hamis Omari, alisema kuwa maonyesho haya yataenda sambamba na utoaji elimu bure kuhusu afya ya uzazi salama, teknolojia husika na haki ya kila raia, ambako aliwaomba wadau na kampuni mbalimbali kujitokeza ili kudhamini onyesho hilo lenye nia njema.
Hassanali, mwenye elimu na uelewa mzuri wa udaktari, ndiye aliyeanzisha mpango wa ‘Fashion 4 Health', ambao amekuwa akifanya maonyesho ya mavazi katika kusaidia masuala mbalimbali yahusuyo afya tangu mwaka 2008 na moja kati ya harakati zake, ni pamoja na ile ya kuchangia hospitali ya wenye matatizo ya akili huko Zanzibar, ambako kiasi cha sh milioni 23 zilipatikana kutokana na mradi huo.
 
Toto yaipunguza kasi Simba Kirumb
• Azam yainyatia kileleni, Yanga kujiuliza Kaibata leo

na Sitta Tumma, Mwanza


amka2.gif
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam jana ilibanwa mbavu na Toto Africa ‘Wana wa Kishamapanda' baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 kwenye dimba la CCM Kirumba jijini hapa.
Katika mechi hiyo iliyohudhuriwa na maelfu ya mashabiki, ilianza kwa timu zote kushambuliana kila mara, ambapo walikuwa ni Toto Africa ndio walioanza kujipatia bao dakika ya 25, baada ya Hussein Swed, kupiga faulo iliyounganishwa kwa kichwa na Tete Kang'anga, kilichomshinda kipa Juma Kaseja na kujaa wavuni.
Baada ya bao hilo, Simba walicharuka na kusaka bao la kusawazisha, ambako dakika 35 walifanikiwa kupata penalti baada ya Haruna Shamte kupanda na kupiga krosi ambayo beki Maregesi Mwangwa aliunawa mpira katika eneo la hatari.
Lakini kipa wa Toto, Wilbert Mweta, aliucheza mkwaju wa Rashid Gumbo ‘Chiddy' dakika ya 36 na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Hadi mwamuzi Zacharia Jacob wa Dodoma anapuliza filimbi kuashiria dakika 45 za kwanza kumalizika, Toto walitoka kifua mbele kwa bao hilo moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, ambapo dakika ya 46 Simba nusura ijipatie bao baada ya mpira wa adhabu wa Banka kutoka sentimita chache, kabla ya dakika ya 47 Semmy Kessy kupachika bao lakini alikuwa ameotea, jambo ambalo lilisababisha mashabiki kushusha lawama kwa refa kuwa anaibeba Simba.
Dakika ya 48, Kocha wa Toto, Choki Abeid aliondolewa kwenye benchi baada ya kuzozana na mwamuzi kwa madai ya kuibeba Simba.
Dakika ya 60, Simba ilifanikiwa kusawazisha baada ya kona iliyopigwa na Gumbo mashariki ya uwanja kumparaza kipa Mweta na mpira kujaa nyavuni.
Baada ya bao hilo, timu zote zilizidi kushambuliana vikali na dakika ya 70 Juma Nyosso aliifungia bao la pili timu yake baada ya kumtoka kipa Mweta na kuutumbukiza mpira wavuni.
Toto walicharuka baada ya bao hilo na kuliandama kama nyuki lango la Simba ambapo huku mashabiki wakiamini Toto imelala, walifanikiwa kuchomoa bao hilo mfungaji akiwa Mohammed Sudi dakika ya 90, baada ya kumchambua kipa Juma Kaseja. Hivyo hadi filimbi ya mwisho, timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya 2-2.
Kocha wa Simba, Mzambia Patrick Phiri, alikiri timu yake kukumbana na upinzani mkali na kuwa mechi ilikuwa ngumu sana na timu yake jana haikufanya vema kama alivyotarajia, huku Abeid akishusha lawama lukuki kwa mwamuzi Jacob ambaye alidai ni mwana Simba kwa kuwabeba Wekundu hao wa Msimbazi.
Kutokana na hali hiyo, waamuzi pamoja na timu ya Toto walibaki uwanjani kwa dakika kadhaa huku milango ya uwanja ikiwa imefungwa na wao kubaki vyumbani huku polisi wakiimarisha ulinzi uwanjani hapo, ambapo hadi tunakwenda mitamboni walikuwa bado hawajatoka uwanjani hapo.
Kwa matokeo hayo, Simba bado iko kileleni ikiwa na pointi 34 huku ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 32 sawa na Yanga, ingawaje zinatofautiana kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Simba: Juma Kaseja, Haruna Shamte, Amir Maftah, Juma Nyosso, Kelvin Yondani, Mohammed Banka/ Juma Jabu, Rashid Gumbo, Patrick Ochan/ Shija Mkina, Ahmed Ali Shiboli/ Amri Kiemba, Mbwana Samatta na Mussa Hassan Mgosi.
Toto: Wilbert Mweta, Philemon Mwandesile, John Bosco, Laban Kambole, Maregesi Mwangwa, Ladslaus Mbogo, Jacob Massawe, Tete Kang'anga, Semmy Kessy, Hussein Swed na Mohammed Sudi.
Wakati huo huo Mwandishi Wetu, Makuburi Ally anaripoti kuwa, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Wauza Lambalamba, Azam FC, iliilaza African Lyon kwa mabao 3-0.
Mabao ya Azam yalifungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 9, Himid Mao dakika ya 37 na Ramadhani Chombo ‘Redondo' dakika ya 87.
Ligi hiyo inaendelea tena leo kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ambako wenyeji Kagera Sugar itawakaribisha Watoto wa Jangwani, Yanga Afrika ya jijini Mwanza ambayo itashuka uwanjani ikiwa na uchovu wa kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Dedebit ya Ethiopia na kusukumizwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).
 
Waziri Nchimbi kubariki Kili Marathon 2011


na Nuru Yanga


amka2.gif
WAZIRI wa Habari, Vijana na Utamaduni, Emmanuel Nchimbi, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathon ambazo zitarindima Jumapili Februari 27 mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, ambako maelfu ya wanariadha kutoka nchi zaidi ya 35 wanatarajiwa kushiriki.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, ambao ndio wadhamini wakuu wa mbio hizo, George Kavishe, alisema jijini Dar es Salaam jana kwamba, Waziri Nchimbi amekubali kuwa mgeni rasmi na atashiriki kwenye kuanzisha mbio hizo na kwenye sherehe ya kutoa zawadi, ambako atahusika kukabidhi zawadi kwa washindi 10 wa kwanza katika mbio ndefu za kilomita 42.195 kwa wanawake na wanaume.
"Uwepo wa Waziri unadhihirisha kwamba, mbio hizi zinaungwa mkono na serikali, jambo ambalio limekuwa likifanyika kila mwaka," alisema Kavishe.
Naye John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema: "Mbio ndefu za kilomita 42 zitaanza saa 12:30 asubuhi. Washiriki wataanzia kwenye uwanja wa Ushirika na kuteremka na njia ya kwenda mjini, halafu watafuata njia ya kwenda Dar es Salaam kwa umbali wa kati ya kilometa 8 hadi 9 mpaka Kiboriloni kabla ya kugeuza na kupitia katikati ya mji wa Moshi na badaye kupandisha hadi Mweka ambapo watageuzia wakiwa tayari wamekimbia kilometa 32.
Baada ya hapo watashuka na kurejea uwanjani. Njia nzima itakuwa na vituo vya kutosha vya maji ya kunywa ili kuhakikisha washiriki wote wanafurahia mbio hizi."
Kwa upande wa nusu marathon kilomita 21 zitaanza saa 1:00 asubuhi kuanzia kwenye uwanja wa Ushirika na kupandisha hadi Mweka ambapo watageuza na kurudi uwanjani, wakati mbio za kujifurahisha za Vodacom 5 km Fun Run zitaanzia kwenye geti la upande wa mashariki saa 1:30 asubuhi na kupita katikati ya mji kupitia barabara za Kibo, Boma, Arusha na kuishia kwenye uwanja wa Ushirika.
Mbio hizi zimedhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager na Vodacom (5 km Fun Run), CFAO DT Dobie, KK Security, TanzaniteOne, TPC Sugar, Precisionair, Kilimanjaro Water, Tanzania Tourist Board na Tanga Cement. Waratibu wa mbio hizo ni Wild Frontiers na Kaelo za Afrika Kusini, Executive Solutions na Riadha Tanzania (RT).


h.sep3.gif

 
Coastal Union kufungua njia leo?


na Mwandishi wetu, Tanga


amka2.gif
HATUA ya fainali ya tisa bora Ligi Daraja la Kwanza inatarajiwa kuendelea tena leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa ambako matokeo yake yataanza kutoa mwanga endapo wenyeji Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya' itarejea Ligi Kuu msimu ujao ama la.
Katika mechi za leo, timu ambazo zinaburuza mkia katika msimamo wa ligi hiyo, Morani FC ya Manyara iliyocheza michezo sita hadi sasa huku ikiwa na pointi moja, itashuka dimbani kuumana na wanaowafuatia kutoka chini, maafande wa Polisi Moro wenye pointi tatu ambao wameshuka uwanjani mara tano.
Baada ya mechi hiyo ya kwanza itakayoanza majira ya saa 8:00 mchana, itafuatiwa na ile kati ya wenyeji Coastal Union na maafande wa Tanzania Prisons ya Mbeya ambako inatarajiwa kuwa mechi kali na yenye upinzani mkubwa hasa kutokana na kila timu kusheheni vipaji kadhaa huku zote zikiwa na nafasi ya kutinga Ligi Kuu.
Coastal iliyocheza mechi tano hadi sasa iko nafasi ya nne ikiwa na pointi tisa, huku Prisons iliyocheza mechi tano na yenyewe inakamata nafasi ya tano ikiwa na pointi nane. Timu nne za juu katika ligi hiyo zitakata tiketi ya kupanda Ligi Kuu msimu ujao.
Hadi sasa timu tatu zilizoko juu na pointi zao kwenye mabano ni JKT Oljoro ya Arusha (12), Moro United ya Dar es Salaam (10), zote zikiwa zimecheza michezo sita huku nafasi ya tatu inashikiliwa na Rhino Rangers ya Tabora (9), ikiwa na mechi saba.



h.sep3.gif

 
Simba wapewa somo kuikabili Mazembe


na Makuburi Ally


amka2.gif
BAADHI ya wadau wa soka hapa nchini, wamependekeza Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam kujipanga vilivyo kuikabili TP Mazembe katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hasa kwa kucheza mechi za kimataifa za kirafiki za kutosha.
Simba itawakabili mabingwa hao watetezi Afrika, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kati ya Machi 18 hadi .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti hivi karibuni, wadau hao walieleza kwamba, michezo hiyo itaisaidia Simba kufanya kweli katika mchezo wake na TP Mazembe utakaochezwa Lubambashi DRC.
Mwanachama wa Simba, Hussein Simba, wa Temeke Dar es Salaam alisema pamoja na kwamba Mazembe ni mabingwa wa Afrika, lakini Simba ina wachezaji bora ambao wanacheza soka ya kueleweka na lolote wanaweza kulifanya.
Simba alisema kikubwa ni kwamba wachezaji wakaze uzi na wasiogope jina la Mazembe, badala yake wakumbuke mwaka 2003, walivyoiadhibu Zamalek ambao walikuwa mabingwa wa Afrika 2002.
Ken Mwaisabula ambaye ni kocha mahiri na maarufu hapa nchini, alisema Simba kucheza michezo ya kimataifa ya kirafiki itasaidia kuikabili Mazembe ambao ni mabingwa wa Afrika na kusisitiza suala la upande wa beki lifanyiwe kazi kubwa na Kocha Phiri.
Mwaisabula alisema kikosi cha Simba sasa hivi ni bora, lakini akaonyesha hofu yake upande wa beki na kuwa kutokuwepo kwa Mganda Joseph Owino, ambaye ni mtu muhimu sana, pengo lake limeonekana.
Naye Paschal Mosha, aliwataka Simba wafanye mazoezi ya nguvu na waache mpira wa magazetini kama mahasimu wao Yanga wenye maskani katika mitaa ya Jangwani na Twiga.
 
Tanga watakiwa kuisapoti zaidi Coastal Union


na Shehe Semtawa


amka2.gif
WADAU wa soka mkoani Tanga wametakiwa kuongeza mshikamano uliopo katika kuisaidia timu ya Coastal Union ili iweze kufanya vema katika Ligi Daraja la Kwanza hatua ya tisa bora inayoendelea Uwanja wa Mkwakwani.
Kitwana Seif, ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Chama cha Soka wilayani Pangani miaka ya hivi karibuni, alisema jijini Dar es Salaam juzi kuwa kutokana na mshikamano ulioonyeshwa tangu kuanza kwa michuano hiyo ya Ligi Daraja la Kwanza, bado unahitajika zaidi katika hatua hii ya mwisho ambayo inaonekana kuwa ngumu zaidi.
Seifu alisema pamoja na hatua hiyo ya mwisho kuwa ngumu, kikubwa cha kujivunia ni vijana wako vizuri na morari wao uko juu, kuhakikisha wanafanya vema na kuuingiza Mkoa wa Tanga katika Ligi Kuu, kitendo ambacho kitauletea sifa.
"Ugumu katika hatua hiyo ya mwisho, unakuja baada ya timu karibu tano kuwa na pointi zinazokaribiana, lakini hata hivyo timu hizo zitategemea kuingia Ligi Kuu kutokana na zitakavyocheza michezo yao iliyobaki," alibainisha Seif.
Alizitaja timu ambazo hadi sasa zinaonekana kuwa na nafasi ya kutinga Ligi Kuu ukiiacha timu hiyo ya Tanga kuwa ni JKT Oljoro ambao wanaongoza ligi hiyo, Moro United, Rhino Rangers na Tanzania Prisons.
Aidha, Seif alimwaga tambo kuwa uwepo wa Mwenyekiti wa timu hiyo, Ahmed Aurora, kumekuwa chachu kubwa ya mafanikio ya timu hiyo, hivyo anatarajia itafika mbali.
Naye Mashaka Mhando, aliyewahi kuwa Msemaji wa timu hiyo alisema, matumaini ni makubwa Coastal kutinga Ligi Kuu, kwani wachezaji hawana tatizo, uongozi unajitahidi kutimiza mahitaji kwa vijana ili watekeleze jukumu lao uwanjani.
Alisema kilichobaki ni kwa wadau wote kuhakikisha timu inashinda michezo yote iliyobaki, ikianzia na ule utakaochezwa leo kati yake na Prisons ya Mbeya, ambao unaweza kumaliza ubishi, ambako Coastal itafikisha pointi 13 zitakazoanza kutoa mwanga wa kuelekea Ligi Kuu msimu ujao.
 
Jeshi Stars kushiriki wavu Afrika


na Makuburi Ally


amka2.gif
TIMU ya mpira wa wavu ya Jeshi Stars wanawake inatarajia kushiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika yanayotarajiwa kuanza Machi 30 hadi Aprili 10 jijini Nairobi nchini Kenya.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA), Agustino Agapa, alisema Jeshi Stars wanawake ndio mabingwa kwa Tanzania katika mashindano yaliyofanyika mwaka jana.
Agapa alisema hivi karibuni wamewasilisha barua ya ushiriki wa mashindano hayo kwa Jeshi Stars, ambako wanatakiwa wajiandae vilivyo kwa ajili ya mashindano hayo.
Aidha, Agapa alisema kwa mujibu wa kalenda ya TAVA, mwaka huu wamejipanga kutoa elimu ya mchezo huo kwa walimu wa shule za msingi na sekondari kwa mikoa sita, ambako wataanza kuanzia Mei hadi Desemba.
Agapa aliitaja mikoa ambayo itapata elimu ya mchezo huo kuwa ni pamoja na Dar es Salaam, Mtwara na Morogoro, ambako mafunzo hayo yatatolewa na baadhi ya makocha wa mchezo huo wenye sifa za kufundisha mchezo huo.
Alisema baada ya mafunzo hayo, TAVA watatoa kozi ya kimataifa ya hatua ya kwanza ambayo itatolewa na mkufunzi wa kimataifa kuanzia Julai Mosi hadi 10 jijini Tanga, wakati kozi ya juu hatua ya pili inatarajiwa kutolewa Septemba.
"Mwaka huu tumejipanga pia kuandaa mashindano ya kuwania Kombe la Taifa, ili tuweze kuandaa timu ya Taifa itakayotokana na mikoa, ambako pia inatakiwa tufahamu mikoa inakochezwa mchezo huo," alisema Agapa.




 
Azam yatoa raha , Simba yavutwa sharubu Send to a friend Wednesday, 16 February 2011 21:45

azamfc%20copy.jpg

Allan Goshashy, Mwanza na Clara Aphonce
AZAM imewapa raha ya sikukuu ya Maulid mashabiki wake baada ya kung'ara na kufanya vizuri katika mechi yake ya Ligi ya Tanzania Bara baada ya kuilaza African Lyon na Toto African ikiikaba koo Simba na kwenda sare ya mabao 2-2 katika mechi zilizofanyika jana.

Kwa matokeo hayo, Simba imeendelea kuongoza ikiwa na pointi 34 ambazo zinaweza kufikiwa na Yanga ambayo leo inaikabili Kagera Sugar katika mchezo mwingine wa ligi hiyo kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba huku Azam ikiwa na pointi 32 sawa na Yanga.

Kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, bao la dakika ya 10 la Mrisho Ngassa linaipa uongozi Azam dhidi ya African Lyon baada ya mshambuliaji huyo kupiga mpira wa adhabu ndogo.

Awali, John Boko 'Adebayor'alikosa bao dakika ya saba baada ya pasi murua ya Ngassa na mshambuliaji huyo mrefu kupiga kichwa dhaifu ambacho kipa wa Lyon alikizuia.

Lyon walikosa bao dakika ya 17 baada ya Sunday Juma kupiga shuti la mbali ambalo kipa Jackson Chove alilipangua na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Dakika tano baadaye, mshambuliaji huyo alikosa tena nafasi nyingine ya kusawazisha baada ya pasi safi ya beki Aziz Sibo.

Katika dakika ya 37, Himid Mau aliiandikia Azam bao la pili kutokana na pasi ya Ngassa ambaye jana aliisumbua mno ngome ya Lyon.

Dakika ya 87, Ramadhan Chombo 'Redondo' aliipa Azam bao la tatu, likitokana pia na pasi ya Ngassa.

Nako kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, mpira ulianza kwa kasi na Ally Ahmed 'Shiboli' alikosa bao la dakika ya kwanza akiwa na kipa Wilbert Mweta wa Toto African ambaye alipangua shuti hilo baada ya pasi ya kifua ya Mbwana Samatta.

Dakika za 5 na 6, kipa Mweta ambaye alikuwa shujaa wa timu yake kipindi cha kwanza alifanya kazi ya ziada ya kupangua mashuti mawili ya Rashid Gumbo.

Dakika ya 12, Patrick Ochan alikosa bao akiwa na lango alipounganisha krosi ya Haruna Shamte.

Toto, kwa upande wao wanapanda vizuri na mipira kuelekea lango la Simba, lakini wanakosa mbinu za kuupasua ukuta wa wapinzani wao na kulazimika kupiga wakiwa nje ya eneo la hatari.

Vijana hao wa Mtaa wa Uhuru jijini hapa waliiduwaza Simba kwa bao la dakika ya 25 baada ya Tete Kang'ang'a kumtungua kipa Juma Kaseja kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa adhabu ndogo wa John Bosco alioupiga akiwa nje ya eneo la hatari ambako mabeki wa Simba walimchezea vibaya Hussein Sued.

Dakika ya 36, Simba walipata penalti iliyotokana na beki Laban Kambole wa Toto kuunawa mpira, lakini Gumbo alipiga mkwaju ambao kipa Mweta aliupangua.

Kipa huyo, hata hivyo alitibua rekodi yake kwa kuonyeshwa kadi ya njano dakika ya 38 na mwamuzi Zakaria Jacob baada ya ushujaa huo kwa madai ya kupoteza muda. Kadi kama hiyo pia ilitolewa kwa Mohammed Sudi dakika ya 40 kwa kucheza rafu.

Beki Amir Maftah wa Simba alilazimika kutumia uzoefu wake kuokoa shuti kali la Semmy Kessy na hivyo kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko ukiwa na matokeo ya 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kocha Patrick Phiri kumtoa kumpumzisha Shiboli ambaye alishindwa kufurukuta mbele ya ukuta wa Toto ukiongozwa na Ladislaus Mbogo na nafasi yake kuchukuliwa na Amri Kiemba.

Dakika ya 47, Kessy alipiga shuti kali nje ya eneo la hatari la Simba na mpira kwenda kimiani, lakini bao hilo lilikataliwa na mwamuzi msaidizi kwa madai ya kuotea kwa wachezaji wa Toto, jambo ambalo liliwashangaza mashabiki.

Kocha wa Toto, Choke Abeid alionyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi kwa kulalamikia kukataliwa kwa bao hilo.

Samatta, ambaye Jumapili aling'ara dhidi ya Wacomoro nusura aisawazishie timu yake dakika ya 54 baada ya kumpiga chenga John Bosco, lakini mpira wake ukatoka nje.

Dakika ya 59, Simba walisawazisha kwa bao la Gumbo baada ya kupiga kona iliyokwenda moja kwa moja wavuni.

Mshambuliaji huyo aliipatia timu yake bao la kuongoza dakika ya 70 kutokana na pasi safi ya Mgosi, akampiga chenga kipa na kuujaza mpira huo wavuni.

Phiri, pia alimpumzisha Ochan na nafasi yake kuchukuliwa na Shija Mkina, dakika ya 79 ya mchezo huo.

Mohamed Sudi alifuta machozi na kuipa Toto pointi moja muhimu kwa kusawazisha bao dakika za majeruhi katika mchezo huo uliokuwa mkali na kuvutia.

Vikosi katika mchezo huo, vilipangwa kama ifuatavyo:

Toto: Wilbert Mweta, John Boseow, Phillemon Mwendasile, Laban Kambole, Ladislaus Mbogo, Maregesi Mwangwa, Jacob Massawe, Semmy Kessy, Hussein Sued, Mohammed Sudi, Tete Kang'ang'a

Simba: Juma Kaseja, Haruna Shamte, Amir Maftah, Juma Nyosso, Kelvin Yondani, Mohammed Banka, Rashid Gumbo, Patrick Ochan, Ally Ahmed Shiboli, Mbwana Samatta, Mussa Hassan Mgosi

Mwamuzi- Zakaria Jacob na mgeni rasmi Meya wa Jiji la Mwanza, Josephat Manyerere (Chadema)
 
Yanga yaafiki mkutano wa wanachama Send to a friend Wednesday, 16 February 2011 21:41

Clara Alphonce na Vicky Kimaro
KAMATI ya Utendaji ya Yanga iliyokutana juzi ilibariki maombi ya wanachama wa klabu hiyo ya kutaka mkutano mkuu wa dharura ufanyike kwa ajili ya kuinusuru na mpasuko unaoweza kutokea kwenye malumbano yanayoendelea ndani ya klabu hiyo kwa sasa.

Kwa siku za karibuni kumetokea mgawanyiko wa wanachama wa klabu hiyo ambao wamekuwa wakimtaka mfadhili na mdhamini wa klabu hiyo, Yusuf Manji ajitoe akidai kuwa yeye ndiye chanzo cha migogoro huku wengine wakitaka aendelee kubakia kwenye klabu hiyo ya Mtaa wa Twiga na Jangwani.

Mzozo huo umewafanya wanachama hao kutoelewana na kudai kufanyika kwa mkutano mkuu.

Matatizo hayo yalijizidi kushika kasi baada ya Manji kumtambulisha Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu kuwa mmoja ya wajumbe wa bodi ya wadhamini wa klabu mbele ya wachezaji wa Yanga bila kushirikisha uongozi.

Pia, uamuzi wa mwenyekiti wa klabu hiyo, Lloyd Nchunga kukubali kusaini mkataba wa kutaka Francis Kifukwe atafute wanachama 100 ambao watatoa Shilingi 50 milioni kwa mwaka bila kwa ajili ya kuanzisha kampuni bila kuhusisha kamati ya utendaji ya klabu hiyo, ulizua mzozo.

Kwa upande wake, Nchunga aliiambia Mwananchi jana kuwa juzi walikutana katika kamati ya utendaji ya klabu hiyo na kukubaliana wote kwa pamoja kuwepo na mkutano mkuu wa dharura katika klabu hiyo mapema iwezekanavyo.

''Maombi ya wanachama wa Yanga yamekuja wakati muafaka wakati hata sisi tulikuwa mumeshakubaliana kufanya mkutano mkuu wa dharura mara baada ya kumalizika kwa mechi ya leo dhidi ya Kagera Sugar'' alisema Nchunga akiwa safarini kwenda Bukoba kwa mchezo huo.

"Jumanne ijayo tutakaa tena kamati ya utendaji na kupanga siku ya kufanya mkutano wa wanachama, lakini utafanyika mapema iwezekanavyo ili kuinusuru klabu yetu, tutawajadili wanachama waliokwenda Maelezo (Idara ya Habari) na kumtukana mdhamini wetu (Manji), kitendo ambacho kimemkasirisha na kutangaza maamuzi ya hasira ya kujiondoa,"aliongeza Nchunga

"Migogoro inayoendelea inaathiri hata ushiriki wa timu yetu kwenye mashindano yote, sasa hivi ni hatua ya lala salama ya Ligi Kuu inatakiwa tuzike tofauti zetu na tuelekeze nguvu zetu zote kwenye timu ili tutwae ubingwa,"alisema.

Hata hivyo, habari za ndani ambazo Mwananchi ilizipata jana zilieleza kuwa katika kikao hicho cha juzi, Manji aliwasilisha barua rasmi ya kujitoa kwenye udhamini wa klabu hiyo, lakini wajumbe wa kamati hiyo wamepanga kumwandikia barua ya kumuomba abadilishe uamuzi wake huo.

Katika hatua nyingine, Yanga leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kucheza na wenyeji Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Timu hiyo ambayo iliwasili jana mkoani Kagera baada ya kutoka Ethiopia, leo itakuwa na wakati mgumu sana kutokana na historia ya timu hiyo kuonyesha upinzani mkubwa hasa wanapokuwa nyumbani.

Awali, kocha wa timu hiyo, Sam Timbe na viongozi wa Klabu hiyo waliandika barua baada ya kuwasili Dar es Salaam wakiomba kusogezewa mbele kwa mchezo huo kwa kuhofia huenda leo timu yao ikashindwa kucheza vizuri kutokana na uchovu wa safari ya Ethiopia.

Hata hivyo, Timbe alisema kuwa anajua timu yake inawakati mgumu katika mchezo wa leo, lakini akasema watahakikisha wanacheza kwa umakini ili kufanya vizuri katika mchezo huo na kujihakikishia nafasi ya kuchukua ubingwa.

''Ligi kwa sasa ni ngumu na mchezo utakuwa mgumu, hivyo timu yangu haihitaji kupoteza mchezio hata mmoja kwa sasa kwani utakavyofanya makosa kidogo mwenzako anakupita , nasi huu ni kama mtihani tutajitahidi na kushinda,'' alisema Timbe.

Mwenzake wa Kagera, Jackson Mayanja ambaye ni raia wa Uganda alisema kuwa Yanga wasitegemee mteremko kutoka katika timu yake kwani wao wako katika vita na hawawezi kumuachia adui yao hapite kilahisi.

Alisema watautumia uwanja wa nyumbani vizuri kuhakikisha wanapanda juu kaitka msimamo kutoka pointi 25 walizo nazo sasa na kwani wanachotaka kwa sasa ni kuchukua moja ya nafasi tatu za juu msimu huu.
 
Azam all out to depose Yanga




By The guardian reporter



16th February 2011




Azam%288%29.jpg

Azam Football Club



Azam Football Club plot to displace crisis-ridden Yanga from their second spot should they post a win against stubborn African Lyon at the Uhuru Stadium in Dar es Salaam today.
The ice-cream makers aim to close the existing three-point gap against second placed Yanga in the Mainland premiership soccer league.
However, Azam will have to work above the call of duty to tame the Lyon side which is at the middle of the standings with 17 points.
Yanga are not in action today as they have their 16th round match against Kagera Sugar at the Kaitaba Stadium in Bukoba tomorrow.
In the event of Azam's victory over Lyon, still they need to pray for troubled Yanga to lose their match against Kagera Sugar for their victory to be advantageous.
Seventh-placed Lyon is six points adrift of the relegation borderline and a win would assure them a move inside the safe horizon.
While Yanga's second spot is at stake, pace makers and holders Simba have a tough assignment against hosts Toto Africa at the CCM Kirumba Stadium in Mwanza.
Opening a narrow one-point gap over their rivals Yanga, Simba must maintain their winning ways to stay perched at the standings table.
A win for Simba might need extra efforts as the host side would be seeking to avenge the first leg defeat after going down by 2-1 goals at the same venue on September 25 last year.
Avenging the first leg defeat is also a top priority for Lyon who lost to Azam by 2-1 goals when they visited Mkwakwani Stadium on September 25.
Likewise, Yanga will certainly have an uphill task to underline their supremacy over Kagera Sugar who will be out to inflict defeat to their visitors as a revenge for the first leg loss in Morogoro by 2-0 goals.
 
Nchimbi kuanzisha mbio Moshi Send to a friend Wednesday, 16 February 2011 21:34

Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio za tisa za Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika Februari 27 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema juzi kwamba Dk. Nchimbi amekubali kuwa mgeni kwa kuanzisha mbio hizo na kwenye sherehe ya kutoa zawadi.

Washindi kumi wa kwanza katika mbio ndefu za kilomita 42.195 kwa wanawake na wanaume watajinyakulia zawadi mbalimbali kutoka kwa Waziri Nchimbi, alieleza Kavishe.

Awali ilielezwa kuwa mbio za marathon za kilomita 42, zitaanza saa 12:30 asubuhi kwenye Uwanja wa Ushirika na kupitia njia ya kwenda mjini halafu watafuata njia ya kwenda Dar es Salaam kwa umbali wa kati ya kilometa 8 hadi 9 hadi Kiborloni.

Baada ya mbio hizo, wakimbiaji wote watageuza kupitia katikati ya mji wa Moshi hadi Mweka na watakuwa wamekimbia kilometa 32 . Baada ya hapo watashuka na kurejea uwanjani.

Mbio ya nusu marathon zitaanza saa 1:00 asubuhi kwenye Uwanja huo wa Ushirika na kupandisha hadi Mweka na kurudi wakati mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run zitaanzia kwenye lango la upande wa Mashariki saa 1.30 asubuhi na kupita katikati ya mji kupitia Barabara za Kibo , Boma, Arusha na kuishia kwenye Uwanja wa Ushirika.

Mbio za Kilimanjaro Marathon mwaka huu zimedhaminiwa na TBL kuopitia bia ya Kilimanjaro, Vodacom (5km Fun Run), CFAO DT Dobie, KK Security, TanzaniteOne, TPC Sugar, Precisionair, Kilimanjaro Water, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Tanga Cement.

 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom