Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
TFF yapitisha panga kwa wageni Ligi Kuu Bara Tuesday, 15 February 2011 19:49

tenga1.jpg
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga

Sosthenes Nyoni
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amesema kuanzia msimu wa Ligi Kuu wa 2013-14, klabu za ligi hiyo zitaruhusiwa kusajili wachezaji watatu wa kigeni na si watano kama ilivyo sasa.

Tenga alitoa msimamo huo wa TFF jana katika semina ya uendeshaji wa ligi wakati akitaja maazimio yaliyofikiwa kupitia semina ya wenyeviti, makatibu na maofisa habari wa klabu za ligi hiyo inayoendelea kwenye Hoteli ya Whitesands, nje kidofo ya jiji la Dar es Salaam.

Alisema kuwa hatua ya kupungua idadi ya wachezaji wa kigeni kutoka watano hadi watatu itasaidia kupunguza wimbi la wachezaji wa nje kusajiliwa katika klabu za Ligi Kuu nchini huku uwezo wao ukiwa mdogo.

"Tumeazimia kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni kutoka watano hadi watatu kwa sababu lengo letu la awali lilikuwa watusaidie kuiboresha ligi yetu ili iwe bora lakini imekuwa tofauti.

"Tulitaka kulifanyia kazi suala hili kuanzia msimu ujao, lakini tumegundua kuna wachezaji wana mikataba, hivyo litatekelezwa msimu wa 2013-14 hii itasaidia klabu zitakazosajili wachezaji kutoka nje kuwa makini zaidi kabla ya kusajili mchezaji,"alisema Tenga.

Tenga alitaja azimio jingine kuwa ni klabu kulazimika kusajili wachezaji watano kutoka katika timu zao za vijana akisema hilo linapaswa kufanyiwa kazi kuanzia msimu ujao wa ligi.

"Hatuna mfumo mzuri wa kuwaendeleza vijana na huwezi kuwa na timu bora ya taifa na ligi na klabu ni mbovu hivyo kuanzia msimu ujao klabu zitalazimika kusajili wachezaji watano kutoka katika timu za vijana,"alisema Tenga.

Pia, Tenga alilisitiza klabu zote kuhakikisha zinawasilisha hesabu zao za ukaguzi akisema ile itakayoshindwa kufanya hivyo haitaruhusiwa kushiriki ligi kuu msimu ujao.

Takribani wachezaji 14 wanachezea klabu mbalimbali za Ligi Kuu ambapo Yanga ina watano kama ilivyo Simba, ambao ni Davis Mwape (Zambia) Yaw Berko,Ernest Boakye, Isaack Boakye(Ghana) na Ivan Knezevic(Serbia).

Simba inao Joseph Owino,Patrick Ochan, Emmanuel Okwi (Uganda), Jerry Santo na Hillary Echesa (Kenya), Azam nayo ina wanne, akiwemo Ibrahim Shikanda (Kenya), Peter Ssenyonjo (Uganda), Vladmir Niyonkuru (Burundi) na Patrick Mafisango kutoka Rwanda.

 
Mbinu, mikakati kuamua ushindi Arsenal, Barca leo
Tuesday, 15 February 2011 19:47

LONDON, Uingereza

MBINU na mikakati sahihi ya makocha na wachezaji wao ndiyo itatoa mshindi katika mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya Arsenal na Barcelona kwenye Uwanja wa Emirates jijini London.

Ukiondoa matokeo ya mwaka jana ambayo Barcelona iliitoa Arsenal kwa jumla ya mabao 6-3 katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo na fainali ya ligi hiyo mwaka 2006, ambayo Barca iliifunga Arsenal pungufu kwa mabao 2-1 mjini Paris, Ufaransa na kutwaa ubingwa, mchezo wa leo utakuwa wenye ushindani.

Kwa upande wake, kocha Arsene Wenger amejipa matumaini kwamba vijana wake wanaweza kutengeneza nafasi za mabao, kisha kuifunga Barcelona, akiwataka kwa muda wote wasiwaachie wapinzani wao nafasi ya kuchezea mpira wapendavyo.

"Tukiwaweka katika shinikizo, Barca hawawezi kucheza, msimu uliopita walituonyesha. Tulipobaini mbinu yao, tukawadhibiti," alisema Wenger.

Lakini, kocha huyo alieleza kuwa vijana wake hawana budi kucheza mchezo wao wa kawaida, wakishambulia na kuitia msukosuko ngome ya Barca na mabao yatapatikana.

"Ninaamini, tukifanikiwa kuwaweka katika shinikizo, tutakuwa na nafasi ya kutengeneza nafasi za kufunga mabao," alieleza.

"Kimsingi, hiki ndicho nimewaagiza vijana wangu kabla ya mchezo. Ni mchezo ambao hawana budi kuuchukulia kwa umakini, nina matumaini tutafaulu.

"Swali gumu ni mchezo ujao kwenye Uwanja wa Nou Camp ambako hatuna budi kubadilika. Tutacheza zaidi kwa kushambulia."

Kiungo Abou Diaby, hata hivyo amewaonya wenzake kutomfikiria zaidi mshambuliaji Lionel Messi

"Kama tunataka ushindi, tusimwangalie Messi, bali tujihami kama timu moja, matokeo yatakuwa tofauti," alieleza Diaby.

Messi, ndiye aliyeiadhiri Arsenal kwa mabao manne kwenye mchezo wa marudiano wa mwaka jana wa robo fainali kwenye Uwanja wa Nou Camp.

Akizungumzia mchezo huo wa leo, Messi alieleza: Ninataka kuzidi kuwa bora mbele yao."

Messi, alieleza kuwa atachungwa na jeshi la viungo, Abou Diaby, Alex Song au hata kikosi kizima, lakini atawasumbua.

"Ninaamini mchezo wangu dhidi yao mwaka jana utawachochea kunikamia, lakini nitajitahidi kusaka mabao," alieleza Messi.

"Mchezo wa mwaka jana ulikuwa maalum kwangu. Maoni yaliyotolewa na wengi baada ya mchezo ule yanaoyesha kwamba nilifanya vizuri.

"Haitokei mara nyingi kufunga mabao manne katika mchezo mmoja, tena kufanya hivyo kwenye michuano kama ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hatua ya robo fainali dhidi ya timu imara, tena katika mchezo ambao kila upande ulitaka kusonga mbele baada ya mchezo mgumu wa kwanza, ni jambo la kushangaza kwangu.

"Ninapenda kuwaona Arsenal wakicheza, nawafuatilia kwenye televisheni kwani wanacheza kama sisi, ninaupenda mchezo wao , lakini naamini sisi (Barca), ni wazuri kwa mbinu za mchezo kuliko kila mmoja. Lakini, tutaonyesha hilo kwa matokeo mazuri."

Aliongeza. "Zipo timu ambazo ni ngumu kwetu kukabiliana nazo, lakini Arsenal na Manchester United zinataka kucheza na kutushinda kwa mchezo ambao unafanana na ule wa kwetu, ndiyo maana inakuwa vigumu kucheza nao.

"Hatuichukulii kirahisi Arsenal hata kwa dakika moja, kwani mwaka jana walituonyesha kwamba wanaweza kuwa hatari ukipoteza umakini wakati wowote unapocheza dhidi yao.

Vijana hao wa Pep Guardiola, wamekuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo, wakiendeleza utawala wao wa soka wa Hispania kwingineko Ulaya.

 
Yanga wataka mkutano wa dharura
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 15th February 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 87; Jumla ya maoni: 0


02_11_2m4kqe.jpg

Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga



WANACHAMA wa Yanga matawi ya Dar es Salaam wamemtaka Mwenyekiti wao Lloyd Nchunga kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama ili kujadili mustakabali wa klabu hiyo baada ya kutokea migogoro isiyoisha.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzake katika ofisi za tawi la Yanga Buguruni, Bakili Makele alisema wameamua hivyo baada ya kuona kuna baadhi ya wanachama wanamtusi mdhamini wao Yusuf Manji pamoja na viongozi wao.

Kauli hiyo ya wanachama hao imekuja siku moja baada ya kuwepo taarifa za Manji kutangaza kujitoa kama mdhamini wa klabu hiyo.

"Hapa sisi tumekutana matawi 26 na tumefikia makubaliano kadhaa ambayo tutamwandikia barua Mwenyekiti wetu Nchunga tumueleze… tunamwomba aitishe mkutano mkuu wa dharura kwa lengo la kuwajadili wanachama wakorofi na kupata ufumbuzi wa hili.

"Pia tunalaani wenzetu kumtusi mfadhili wetu (Manji) pamoja na viongozi waliochaguliwa kihalali chini ya Nchunga, kwani hao wanaofanya hivyo ni wale wasioitakia mema Yanga na sisi baada ya kujadili kwa kina tumegundua kuwa wenzetu hao wanatumika.

"Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Manji ametufanyia vitu vingapi Yanga? Leo hii anataka ufanyike ukaguzi ndio awe mbaya? Haiwezekani mtu awe anatoa fedha zake zinatumika tu bila kujua mambo yanakwendakwenda vipi?

"Tunajua kuna watu wamefaidika kupitia Yanga, watu wamejenga nyumba kwa fedha hizo anazotoa mfadhili wetu, sasa tunaungana na mfadhili, tunataka ukaguzi ufanywe tangu enzi za uongozi uliopita mpaka huu,"alisema Makele.

Makele alisema, mkutano huo wa wanachama hauna lengo la kuwadhibiti wanachama wakorofi pekee, bali hata tofauti kati ya Mwenyekiti Nchunga na Makamu wake Davis Mosha zilizokuwa zimedaiwa kujitokeza watajadili.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Matawi yote ya Yanga, Mohamed Msumi alisema jana kuwa hana taarifa na mkutano uliofanywa na wanachama hao na kwamba yeye kama mwenye mamlaka ya kuitisha mkutano wa matawi atatoa tamko.

Jana vyombo mbalimbali vya habari viliripoti kuwa Manji amejiengua Yanga kutokana na sababu mbalimbali.
 
Mti waanguka, waua mcheza gofu Gymkhana Dar es Salaam
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 15th February 2011 @ 23:55 Imesomwa na watu: 65; Jumla ya maoni: 0


02_11_xsqs99.jpg

Marehemu Profesa Chris Kamuzora


JAMII ya gofu nchini imepata msiba kutokana na mchezaji mwandamizi wa mchezo huo kutoka Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Profesa Chris Kamuzora kufa baada ya kuangukiwa na mti uwanjani Februari 15 jioni.

Taarifa za kifo cha Kamuzora ambaye ni mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam zilithibitishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU) Dioniz Malinzi.

"Kuna taarifa mbaya, Kamuzora amefariki ndicho ninachoweza kueleza kwa sasa," alisema Malinzi.

Baadhi ya wachezaji waliokuwa uwanjani kushuhudia tukio hilo baya waliliambia HABARILEO kwamba Kamuzora alifariki kutokana na kuangukiwa na mti katika kiwanja namba moja Gymkhana Dar es Salaam akiwa kwenye mazoezi ya kawaida na wachezaji wengine watatu.

"Walikuwa wachezaji wanne katika kiwanja namba moja wakicheza, ghafla mti uliokuwa karibu na uwanja uliwaangukia na Kamuzora aligandamizwa vibaya kichwani na amekimbizwa Hospitali ya Aga Khan," alisema Hamis Ally.

Wachezaji wengine ambao walikumbwa na balaa hilo ni Profesa Mohabe Nyirabu, Michael Makala na Athumani Chiundu ambao walipata majeraha na kukimbizwa hospitali pia. Hata hivyo, Nyirabu anahofiwa kuumia zaidi mguu.

Shuhuda huyo alisema baada ya kuangukiwa na mti huo baadhi ya wachezaji waliokuwa karibu walifanya kazi ya ziada kuwanasua kutokana na mti kuwa mzito kabla ya polisi kufika eneo la tukio na kuwakimbiza hospitalini.

Alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alikiri kutokea kwa tukio hilo lakini alisema hakuwa na taarifa za kifo.

Alisema baada ya kupata taarifa ya kuwepo jambo hilo, polisi walifika eneo la tukio na kukuta majeruhi mmoja ambaye walimchukua na kumkimbiza Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wakati majeruhi wengine hali walikuwa wameshachukuliwa kupelekwa hospitalini.

Alisema majeruhi huyo mmoja hali yake walikuta ni mbaya na alikuwa anazungumza kwa shida na kwamba huenda wananchi wakawa wanafikiri huyo ndiye aliyefariki dunia.
 
Mti waanguka, waua mcheza gofu Gymkhana Dar es Salaam
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 15th February 2011 @ 23:55 Imesomwa na watu: 65; Jumla ya maoni: 0


02_11_xsqs99.jpg

Marehemu Profesa Chris Kamuzora



JAMII ya gofu nchini imepata msiba kutokana na mchezaji mwandamizi wa mchezo huo kutoka Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Profesa Chris Kamuzora kufa baada ya kuangukiwa na mti uwanjani Februari 15 jioni.

Taarifa za kifo cha Kamuzora ambaye ni mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam zilithibitishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU) Dioniz Malinzi.

“Kuna taarifa mbaya, Kamuzora amefariki ndicho ninachoweza kueleza kwa sasa,” alisema Malinzi.

Baadhi ya wachezaji waliokuwa uwanjani kushuhudia tukio hilo baya waliliambia HABARILEO kwamba Kamuzora alifariki kutokana na kuangukiwa na mti katika kiwanja namba moja Gymkhana Dar es Salaam akiwa kwenye mazoezi ya kawaida na wachezaji wengine watatu.

“Walikuwa wachezaji wanne katika kiwanja namba moja wakicheza, ghafla mti uliokuwa karibu na uwanja uliwaangukia na Kamuzora aligandamizwa vibaya kichwani na amekimbizwa Hospitali ya Aga Khan,” alisema Hamis Ally.

Wachezaji wengine ambao walikumbwa na balaa hilo ni Profesa Mohabe Nyirabu, Michael Makala na Athumani Chiundu ambao walipata majeraha na kukimbizwa hospitali pia. Hata hivyo, Nyirabu anahofiwa kuumia zaidi mguu.

Shuhuda huyo alisema baada ya kuangukiwa na mti huo baadhi ya wachezaji waliokuwa karibu walifanya kazi ya ziada kuwanasua kutokana na mti kuwa mzito kabla ya polisi kufika eneo la tukio na kuwakimbiza hospitalini.

Alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alikiri kutokea kwa tukio hilo lakini alisema hakuwa na taarifa za kifo.

Alisema baada ya kupata taarifa ya kuwepo jambo hilo, polisi walifika eneo la tukio na kukuta majeruhi mmoja ambaye walimchukua na kumkimbiza Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wakati majeruhi wengine hali walikuwa wameshachukuliwa kupelekwa hospitalini.

Alisema majeruhi huyo mmoja hali yake walikuta ni mbaya na alikuwa anazungumza kwa shida na kwamba huenda wananchi wakawa wanafikiri huyo ndiye aliyefariki dunia.
 
Simba, Toto mtihani muhimu Mwanza
Imeandikwa na Grace Chilongola, Mwanza; Tarehe: 15th February 2011 @ 23:50 Imesomwa na watu: 69; Jumla ya maoni: 0






TIMU ya Toto African ya jijini Mwanza, leo inashuka Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa kucheza na vinara wa ligi hiyo Simba ya Dar es Salaam.

Toto African yenye pointi 16 ikishika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi hiyo yenye timu 12 imetamba kwamba italipa kisasi cha kufungwa mabao 2-1 mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo kwenye uwanja huohuo.

Akizungumza wakati wa mazoezi ya timu hiyo Februari 15, Kocha msaidizi wa Toto African, Choki Abeid alisema wamejiandaa vizuri na mchezo na kuuona kama fainali, hivyo watapigana kiume kuhakikisha wanaibuka na ushindi licha ya ugumu wa mechi hiyo.

Abeid alisema timu yake baada ya kufungwa na Azam, imefanya mazoezi mengi ya maandalizi hasa katika safu ya ushambuliaji.

Aliwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu hiyo licha ya kwamba mchezo huo kuwa mgumu kwani Simba nayo inataka kuendeleza ushindi na wenyeji kuzinduka baada ya vipigo mfululizo.

Kocha wa Simba Mzambia, Patrick Phiri alipohojiwa juu ya mchezo huo alisema utakuwa mgumu, kwani Toto hawatakuwa tayari kufungwa mara mbili na Simba wakati timu yake itataka kuendeleza ushindi na raha kwa mashabiki wake baada ya kufuzu raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika.

Phiri aliwaomba mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kuwapa nguvu ya kushinda na waendelee kukaa kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 33 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 32, Azam inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 29.
 
Wachezaji wa nje magalasa wamkera Tenga
Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 15th February 2011 @ 23:45 Imesomwa na watu: 89; Jumla ya maoni: 0


02_11_yn7j57.jpg

Rais wa TFF Leodgar Tenga



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema litaweka utaratibu utakaozibana klabu nchini zisisajili wachezaji wa nje wasiokuwa na sifa.

Kauli hiyo imetolewa na Rais wa TFF Leodgar Tenga wakati akifungua semina ya siku tatu iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) inayowashirikisha viongozi wa klabu za soka na maofisa habari nchini.

Tenga alisema baadhi ya klabu zimekuwa na matumizi mabaya ya fedha hasa wakati wa kufanya usajili ambapo hutumia mwanya huo kujinufaisha.

Alisema wachezaji wengi wa nje ya nchi wanasajiliwa kwa fedha nyingi na hushindwa kuonesha kiwango kinachoendana na fedha walizosajiliwa nazo.

Aliwaambia viongozi waliohudhuria semina hiyo kuwa maendeleo ya klabu yanatokana na nidhamu pamoja na matumizi mazuri ya fedha.

Aliwaambia kuwa katika usajili ujao wanatakiwa kuzingatia ushauri huo kwa kuwa wapo wachezaji wa hapa nchini wenye uwezo wa kucheza kama hao wanaowasajili kutoka nje.

Katika hatua nyingine alisema timu zinazoshiriki Ligi Kuu zinatakiwa kuhakikisha hazisajili wachezaji zaidi ya 25 wa timu kubwa.

Alisema hatua hiyo ni kuhakikisha wanatoa nafasi kwa wachezaji wa timu za vijana katika klabu hizo kupata nafasi ya kucheza timu kubwa.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Elimu na Maendeleo ya Kiufundi kutoka Fifa, Jurg Nepfer aliwataka viongozi hao wa klabu kuwa na mikakati endelevu itakayosaidia kuendesha klabu hizo.
 
Njenje, Amini na Barnaba watesa Mwanza
Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Mwanza; Tarehe: 15th February 2011 @ 23:40 Imesomwa na watu: 28; Jumla ya maoni: 0








WAKATI wanamuziki wa kizazi kipya Amini na Barnaba wakiwasha moto katika siku ya wapendano mjini hapa, WanaNjenje walikata kiu ya muziki wa dansi mjini hapa katika maonesho makubwa mawili yaliyofanyika maeneo tofauti.

Kizazi kipya wakienda sambamba na vijana wenzao katika ukumbi wa Hoteli ya Nyumbani iliyopo Jengo la NSSF, Wana Njenje walikuwa Villa Resort wakiwapagawisha wapenzi wa rhumba na miondoko ya salsa.

Pamoja na kutoa burudani katika siku ya wapendanao ambayo ilipambwa na mavazi na vitambaa vya rangi nyeupe na nyekundu wanamuziki wa kizazi kipya walitumia nafasi hiyo kutambulisha nyimbo mpya na albamu.

Amini alitambulisha wimbo wake mpya na Barnaba yeye aliwaambia wananchi kuhusu albamu yake mpya ambayo alisema kwamba anatarajia kuingia Mwanza wakati wowote ule.

"Mnataka nini wananchi wa Mwanza," alisikika akisema Amin wakati alipotambulishwa na msema chochote (MC) katika hafla hiyo ya wapendanao iliyoandaliwa na kampuni mpya ya mawasiliano ya Mwanza inayoendeshwa na mfanyakazi wa zamani wa televisheni ya Star, Edith Subeti.

Wananchi waliofika katika ukumbi uliojaa pomoni waliimba mwambie... usimfiche bado robo saa nitakufa.... mambo ya mapenzi.

Pamoja na kukamua vya kutosha Amini alisababisha ukumbi kunyanyuka alipowashirikisha wapendanao katika kurudi muziki wa kizazi kipya na miondoko ya kiduku.

Ukumbi wa hoteli ya nyumbani hakukupagawishwa na Barnaba na Amini pekee bali kulikuwa na wacheza dansa wa Mwanza ambao walionesha miondoko mbalimbali ya Kimagharibi na vituko kutoka kwa mchekeshaji mmoja.

Katika ukumbi wa Villa, Njenje walidhihirisha kwamba wanaojua muziki kwa kuwapeleka na miondoko mbalimbali wapenzi wa muziki wa dansi.

Njenje walifanya kazi ya kuburudisha hadi saa tisa usiku huku wakichanganya muziki kiasi cha kuwafanya wale wanaojua rhumba, salsa na chacha kukonga nyoyo zao mpaka majogoo ya kwanza.

Wanamuziki wa Njenje ambao wengi wapo umri wa kati kwa jinsi walivyokusanya si watu wa kati tu bali na vijana wanaonesha kwamba muziki wa dansi bado unapendwa.

Mmoja wa wanamuziki Waziri Ally alisema wingi wa watu katika ukumbi huo wa Villa ni dalili ya wazi kuwa muziki wa dansi bado unatakiwa na wananchi.
 
Wengi waomba kutumbuiza Tamasha la Pasaka

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 15th February 2011 @ 23:35 Imesomwa na watu: 17; Jumla ya maoni: 0








KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka imesema imekuwa ikipokea maombi ya wasanii wengi wanaotaka kutumbuiza siku hiyo.

Akizungumza Februari 14, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Alex Msama alisema hali hiyo inawafanya washindwe kuwatangaza wasanii mapema zaidi.

"Tuna wasanii zaidi ya 30 wanaomba kutumbuiza, sasa jambo hili linatufanya tukune vichwa ili kuwapa kitu kizuri mashabiki wetu. "Lakini nawahakikishia kwamba wasanii wote mahiri watakuwepo, pia wasanii chipukizi nao tutawapa nafasi ya kuonesha vipaji vyao.

"Tamasha la mwaka huu tumelipanga vizuri, nina imani kubwa kwamba mambo yatajipa na itakuwa raha kwa watakaofika," alisema Msama.

Tamasha hilo kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu litafanyika sikukuu ya Pasaka Aprili 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Msama baada ya tamasha hilo pia litafanyika katika mikoa ya Shinyanga Jumatatu ya Pasaka Aprili 25 na Mwanza Aprili 26 ambayo itakuwa ni sikukuu ya Muungano.
 
Simba kuiendea Mazembe Zambia
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 14th February 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 520; Jumla ya maoni: 0


02_11_hes317.jpg

Kikosi cha Simba



SIMBA ya Dar es Salaam itaweka kambi nchini Zambia kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya mabingwa watetezi TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC).

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Rage amesema Simba itaweka kambi mjini Kitwe, Zambia ikiwa ni maandalizi ya kuivaa TP Mazembe na kuwa itacheza mechi chache za kirafiki ikiwa ni pamoja na kuivaa Kitwe United nchini Zambia.

Simba juzi iliifunga Elan de Mitsoudje ya Comoro mabao 4-2 katika mchezo wa marudiano raundi ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Kutokana na matokeo hayo imefuzu raundi ya kwanza ya michuano hiyo kwa jumla ya mabao 4-2, kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza uliofanyika Moroni, Comoro wiki mbili zilizopita timu hizo kutofungana.

Kulingana na ratiba ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Simba kwa kufuzu hatua hiyo, sasa itacheza na mabingwa watetezi wa michuano hiyo, timu ya TP Mazembe ya DRC.

TP Mazembe yenyewe raundi hii ya awali haikucheza na ilikuwa ikisubiri mshindi wa Simba na Wacomoro, ambapo mchezo wa kwanza utafanyika jijini Lubumbashi DRC kati ya Machi 18,19 na 20 wakati marudiano itakuwa kati ya Aprili 1, 2 na 3 jijini Dar es Salaam.

Rage ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), alisema ana matumaini makubwa maandalizi hayo yatakuwa msaada kwa Simba kwani TP Mzembe ni mabingwa watetezi na Simba yawapasa kufanya maandalizi ya nguvu.

Alisema wanajua Mazembe ina wachezaji sita raia wa Zambia, hivyo ni jambo zuri wakiweka kambi nchini humo ili kupata mambo ya kiufundi kwani uchezaji wao utakuwa unafanana na ule wa Zambia.

Baadhi ya nyota wa Mazembe ambao ni raia wa Zambia ni Given Singuluma, Stoppila Sunzu, Kalilo Kakonje na Rainford Kalaba.

Mazembe licha ya kuwa bingwa mtetezi wa kombe hilo kwa miaka miwili mfululizo, pia mwishoni mwa mwaka jana iliweka historia mpya kwa kuwa klabu ya kwanza Afrika kufika fainali ya michuano ya klabu bingwa ya dunia iliyofanyika nchini Brazil na kufungwa mabao 3-0 na mabingwa wa dunia Inter Milan.

Kwa mujibu wa Rage wanatarajia kuanza kambi hiyo wiki ya kwanza ya mwezi Machi ikiwa ni wiki mbili kabla ya kuivaa Mazembe na kwamba hawaiogopi timu hiyo.

Wakati huohuo, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri amesema timu yake haina hofu na wapinzani wao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika,TP Mazembe.

Akizungumza Jumapili, Phiri raia wa Zambia alisema wanajua wanakumbana na timu ngumu Afrika, lakini hilo haliwatishi vijana wake kuhakikisha wanaiondoa TP Mazembe kwenye michuano hiyo.

"Tunajua tunacheza na mabingwa watetezi ila hawatunyimi usingizi, wao ni kama sisi, ingawa wenzetu ni maarufu Afrika na duniani kwa ujumla, ila hilo si kikwazo kwetu.

"Tunashukuru tumevuka hatua hii ya awali ambayo ilikuwa ngumu, hawa Wacomoro ni wazuri tofauti na wengi walivyokuwa wakifikiri, sasa tunajipanga kuikabili Mazembe," alisema.

Kocha huyo alieleza kuwa atafanyia kazi dosari zilizojitokeza katika mechi ya juzi, ili watakapokutana na TP Mazembe timu yake iwe imara zaidi.

Wakati huohuo, mchezo kati ya Elan de Mitsoudje ya Comoro na Simba uliofanyika Jumapili Uwanja wa Uhuru uliingiza Sh 56,905,000.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mapato hayo yalipatikana kutokana na watazamaji 10,192 walioingia uwanjani kwa kukata tiketi.

Viingilio vilikuwa Sh 20,000 viti maalumu, Sh 15,000 jukwaa kuu, Sh 8,000 jukwaa la kijani na Sh 3,000 mzunguko.

 
Manji adaiwa kujichuja Yanga

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 14th February 2011 @ 23:55 Imesomwa na watu: 535; Jumla ya maoni: 2








MDHAMINI wa Yanga, ambaye pia ni mfadhili wa klabu hiyo, Yusuph Manji amedaiwa
kujiondoa katika klabu hiyo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zilizopatikana Dar es Salaam zimedai Manji ameamua kujiondoa ili kupumzisha afya yake baada ya kuchoshwa na kelele za baadhi ya wanachama wa klabu hiyo na pia ubadhirifu wa fedha za klabu kwa baadhi ya viongozi.

Kwa takriban mwezi sasa kumekuwa na mgogoro ndani ya Yanga ukihusisha baadhi ya viongozi na wanachama na wakati mwingine baadhi ya viongozi kwa viongozi.

Wiki iliyopita baadhi ya wanachama wa tawi la Yanga Tandale Kwa Mtogole walimtaka mfadhili huyo aondoke Yanga kwa madai anaivuruga klabu yao.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, kilichomfanya mdhamini huyo kujiondoa Yanga ni namna klabu hiyo isivyoendeshwa kwa mpangilio na kwamba fedha nyingi zinatoka lakini hazionekani
zinatumika vipi.

"Yanga kuna ubadhirifu unafanyika ndio maana Manji amekuwa akipiga kelele kila siku ufanyike ukaguzi ili wanachama wanaosema anaivuruga klabu waone nani ni mvurugaji,"kilisema chanzo hicho.

"Angalia mfano mdogo tu kuna kipindi Yanga ilikuwa inafanya mazoezi kwenye ufukwe wa Coco akawa anaambiwa kwa siku ni Sh 200,000, lakini alipochunguza akagundua si kiasi hicho bali mazoezi ni Sh 50,000 kwa siku, sasa jiulize timu ilifanya mazoezi kwa siku ngapi na hizo Sh 150,000 zilikuwa zinakwenda wapi," alisema mtoa habari huyo.

Chanzo hicho kilisema safari nyingine ya hivi karibuni ni ile ya Songea ambapo mdhamini huyo aliambiwa kuwa basi la klabu limeharibika hivyo haliwezi kwenda na aliombwa kutoa Sh 70,000 kama gharama ya nauli kwa kila mchezaji lakini matokeo yake timu ilienda kwa kutumia basi hilohilo la wachezaji hali iliyofanya liwaharibikie njiani.

"Unajua kuna vitu watu hawaelewi hapa Manji ni kama ametapeliwa tu fedha zake kwa sababu kuna nyingine anawakopesha, lakini hakuna mahali palipoandikwa kwamba anakopesha tena bila riba na ndio maana anataka ukaguzi ufanywe na chombo huru,"alisema mtoa habari huyo.

Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa kabla Manji hajaenda mapumziko ya mwisho wa mwaka nje ya nchi aliwapa Yanga Sh milioni 100 kwa sharti kwamba wafanye usajili wa dirisha dogo, mojawapo ni kumrudisha Mrisho Ngasa kutoka Azam na wafanye ukaguzi wa matumizi ya fedha anazowapa.

Hata hivyo aliporudi alikuta Yanga wametumia Sh milioni 18 tu kwa usajili na kwamba hundi moja ya Sh milioni 50 ikabidi kampuni yake iizuie na kuwa ukaguzi bado haujafanyika.

"Kwa hiyo ameamua kujiondoa Yanga baada ya miaka minne ya kuwa mfadhili na mwaka mmoja wa kuwa mdhamini, atatangaza hilo rasmi kwenye vyombo vya habari muda wowote wiki hii," alisema mtoa habari huyo na kuongeza kuwa tayari amewajulisha watu wake wa karibu kuhusu uamuzi huo.



Jumla Maoni (2) Maoni ni jambo la busara sana kwa Manji kujiondoa na hao mataperi. inasikitisha sana kuona gharama ni kubwa hakuna mafanikio yeyote. Yanga inafanya usajiri wa mamilioni ya pesa hakuna mafanikio yeyote yanayopatikana. bora hivo pesa uzitumie kwa kusaidia watoto yatima ALLAH atakuongezea na kukulinda na maradhi kuliko kupoteza pesa kwa hao wasanii tu. Maoni Bora manji jitoe tu kani kuna watu wana fanaya yanga mali yao maneno mengi bila vitendo kama kweli unaondoka tutakukumbuka kwa mengi sana na kwa kuifikisha hapo ilipo ila viongozi ndio wamekuangusha kwa utendaji wao mbaya tutafute viongozi makini sio hao wababaishaji wanaotaka kula hela za mfadhili YANGA IMARA TUTAKUKUMBUKA MANJI
 
Simba yasaka pointi kwa Toto leo Send to a friend Tuesday, 15 February 2011 19:46 0diggsdigg

Allan Goshashy, Mwanza

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo wanaingia uwanjani kupambana na Toto Afrika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza baada ya ya kuifunga Elan ya Comoro mabao 4-2 katika mechi ya Klabu Bingwa Barani Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 33 baada ya kucheza michezo 14 wakati Toto Afrika ikiwa na pointi 16 na inashika nafasi ya nane katika ligi hiyo.

Timu hiyo ilitua Mwanza juzi na kufanya mazoezi jana jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba imeweka kambi yake katika hoteli ya Ladison iliyopo Pasiansi huku Toto ikiweka kambi yake Bwiru, kilomita nne kutoka katikati ya jiji.

Akilizungumzia pambano hilo, kocha wa Simba, Patrick Phiri alisema Toto ni timu ngumu ambapo katika mechi walizowahi kucheza nayo ilionyesha soka ya kiwango cha juu.

"Tunafahamu hata katika mechi ya leo Toto watacheza soka nzuri, hivyo tutakuwa makini na mtazamo mzuri kwa sababu kwetu sisi ni muhimu kushinda mechi hii ili kuweza kutetea ubingwa,"alisema Phiri.

Alisema,"Kila mara tunapochezea Mwanza mechi huwa ngumu kwa sababu tunajua hapa kuna mashabiki wengi wa Yanga, hivyo umakini uwanjani ndiyo utakaotuwezesha kupata pointi tatu."

"Simba inashinda mechi zake kwa sababu tunafanya kazi kitimu, bila kufanya kazi kitimu katika michezo hakuna ushindi, tunashinda kwa sababu taasisi nzima ya Simba inafanya kazi kitimu, hivyo tutaendelea hivyo tutetee ubingwa na pia kufika mbali katika mashindano ya klabu bingwa Afrika."

Alisema katika mechi ya leo atawakosa nyota wake watano ambao ni majeruhi, Uhuru Suleiman, Emmanuel Okwi, Jerry Santo, Nico Nyagawa na Hillary Echessa.

Mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi alisema,"Mechi hii ni ngumu kwa sababu kila timu inayokutana na Simba kwenye ligi hujitutumua kutafuta ushindi au sare, ila malengo yetu katika mzunguko huu wa pili ni tusipoteze mechi hata moja ili tuweze kutetea ubingwa."

Pia, kipa Juma Kaseja ambaye alikuwa amempuzishwa kwa mechi kadhaa alisema,"Mechi itakuwa ngumu kwa sababu katika kipindi cha nyuma Toto imekuwa ikitusumbua, ila mwaka juzi na mwaka jana tuliifunga Toto kwa hiyo mechi haitakuwa rahisi, lakini tumejiandaa na tunaipa umuhimu mkubwa mechi hii."

Kocha wa Toto Africa, Choke Abeid alisema wamefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya pambano la leo na kikosi chake hakina majeruhi.

"Tumesahihisha makosa mengi yaliyotufanya tupoteze mechi nyingi katika ligi na tunafahamu Simba ni timu nzuri na inafanya vizuri katika ligi, lakini sisi tutaingia uwanjani kutafuta ushindi ili tujiweke katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi," alisema Choke.

Naye Clara Alphonce anaripoti kuwa uongozi wa Simba umeilalamikia ratiba ya ligi hiyo kuwa haijazingatia maandalizi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Makamu mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' aliilalamikia ratiba ya ligi hiyo kuwa inawabana sana kuweza kufanya maandalizi ya maana kabla ya kuikabiliTP Mazembe mwezi ujao.

Alisema walitakiwa wawe hata na wiki mbili za kufanya maanzalizi ya kucheza mechi mbili tatu za kimataifa na kuweka kambi nje ya nchi, lakini muda huo hawana kutokana na TFF, kutozingatia michuano hiyo mikubwa.

''Unajua tunacheza na TP Mazembe, mabingwa wa pili wa dunia, hivyo inatakiwa tujiandae vya kutosha lakini tunashindwa kusema lolote kutokana na ratiba kuwa ngumu kwani wiki moja kabla ratiba ya mechi hiyo ratiba inaonyesha kuwa tutakuwa Arusha kucheza na AFC halafu turudi Dar kwa ajili ya maandalizi ya kwenda Congo, '' alisema Kaburu.

''Ligi kuu sio kipimo cha Simba kusema watajiandaa vizuri kwa ajili ya TP Mazembe kwani ukweli bado unabaki palepale kuwa ligi yetu ni mbovu na timu zake siyo imara,'' alisema.

Ligi hiyo inaendelea pia kwa mchezo baina ya African Lyon na Azam jijini Dar es Salaam huku Yanga ikitarajiwa kucheza kesho mjini Bukoba dhidi ya Kagera Sugar.
 
Manji atikisa kiberiti Yanga
• Yadaiwa ameamua kujiweka kando

na Dina Ismail


amka2.gif
KUNA habari kuwa mfadhili na mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji, ameamua kuachana na klabu hiyo.
Kwa mujibu wa habari kutoka kwa mtu wa karibu na mfadhili huyo, Manji aliyetia mguu kwa mara ya kwanza Yanga Juni 2006, amefikia hatua hiyo akikerwa na shutuma dhidi yake.
Chanzo hicho kimedokeza kuwa kilichomkera zaidi Manji, ni hatua ya baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kumtaka awaachie Yanga yao.
Ijumaa iliyopita, wanachama wa tawi la Tandale kwa Mtogole, jijini Dar es Salaam, walimtaka mfadhili huyo aondoke, wakijenga hoja kuwa ndiye chanzo cha mivutano.
Imeelezwa kwamba baada ya Manji kutafakari kwa kina kauli za wanachama hao na hali halisi iliyoko Yanga kwa sasa, ameamua kujiweka kando na ataliweka wazi hilo siku yoyote.
"Yeye anasema haja yake ilikuwa ufanyike ukaguzi wa mapato na matumizi, lakini suala hilo limeibua shutuma nyingi dhidi yake, hivyo ameona heri ajiweke kando," kilidokeza chanzo hicho.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa kitu ambacho Manji anaamini ni baadhi ya watu kuona Yanga ni sehemu ya kuvuna, hivyo ameamua kuwaachia klabu yao," kilisema na kuongeza:
"Amesikitishwa sana na shutuma dhidi yake kwamba amekuwa akijinufaisha kupitia mgongo wa Yanga, anaona ni heri ajiweke kando."
Hii si mara ya kwanza kwa Manji kuripotiwa kujitoa, lakini kilichofuata ni kurejea kwa madai ya kuombwa na baadhi ya wanachama wakiongozwa na wazee.
Kuna wakati Manji aliwahi kutangaza kujitoa kwa maandishi kwa hoja ya kushauriwa na familia yake, lakini baadaye alirejea tena kwa madai ya kuombwa na wazee.
Chini ya ufadhili wake, Manji amekuwa akitoa zaidi ya milioni 550 kwa mwaka kwa matumizi ya klabu hiyo, lakini sasa amekuwa akitoa kwa sharti la kurejeshewa.
Sababu ya kufanya hivyo ni Manji kukosa imani na matumizi ya fedha ambazo amekuwa akizitoa.
Desemba mwaka jana, alitoa kiasi cha sh milioni 100 kwa ajili ya usajili, lakini akitaka zirejeshwe ndani ya siku 120.
Manji aliweka msimamo huo kwa lengo la kupigania nidhamu ya matumizi ya fedha zinazopatikana.
Juhudi za kumpata Manji mwenyewe na viongozi wa Yanga zilishindikana kutokana na wengi wao kuongozana na timu hiyo huko Ethiopia, ambako ililala kwa mabao 2-0 dhidi ya Dedebit hivyo kuondoshwa kwa jumla ya mabao 4-2 katika muchuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF). Timu hiyo ilitarajiwa kuwasili jana usiku.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom