Michepuko inavunja ndoa ya jamaa

Michepuko inavunja ndoa ya jamaa

Ndoa hizi[emoji22][emoji22][emoji22]...Ila huyo mchepuko mpuuzi tu kajiskia raha gani kuvunja ndoa ya mwanamke mwenzie ! Angekaa kimya akahudumiwa huko angepungukiwa nn ?chefuuuuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
we wanawake tuonenei tu..... we are devil .......lakini hapo anafanya akijua anamkomoa mke kumbe anavuruga hadi watoto jamani
 
It is complicated.... Haya mambo yaishie tuu kwenye simulizi...
 
yani wewe unamjua mke wa jamaa kuliko yeye? aisee kama jamaa ananyimwa kipapa unajua? au kama mwanamke ndani ni wakununa tu unajua? au kama mwanamke mbinafsi chake chake tu na ndugu zake unajua? acheni tabia za kujifanya mnawajua wake za watu kuna wanaume wanakuwa na michepuko sio kwa sababu mke wa ana michepuko bali mwanamke unakuta ndani hapakaliki sababu ya mwanamke, kwa mfano kuna wanawake wajuaji kupitiliza na wanafanya maamuzi yao kulingana na marafiki zao huyo hana mchepuko ila anaweza kukufanya ukawa na michepuko maana kila unachosema au kufanya mwanamke haoni sawa hadi aambiwe na mashoga[/
Mkuu katika maisha kuna mambo ukiyafanya ukadhani ni siri lakini mungu mwishowe anakuja kukuumbua kama ilivyo kwa jamaa
 
Ni ngumu but kuna watu ni product ya mashetani, rafiki yangu ilimtokea hivyo Mme alizaa na shopkeeper wao, shopkeeper akajiona mshindi akaanza kutumia picha za mtoto Mara amwambie mke mwambie Mme wako alete pesa ya matumizi, mke akamjibu wakati mnapeana mimba sikuwepo kwa hiyo umtafute atunze mwanae mi wa kwangu natunza mwenyewe, mke alikuwa kimya wala haulizi Mme wala nini anaendelea na maisha alichofanya bosi wake alikuwa mwanamama wa kizungu akaenda kuomba transfer aende branch nyingine, basi akahamishwa mke akaondoka na mtoto wake kamuaga Mme nimepewa transfer nahama Mme anaomba abaki mke akamjibu si uko na shopkeeper wako why unanifuata fuata after all mapenzi yalishaisha ukinilazimisha naweza kukuchinja tu. So ndoa mpk Leo kama hakuna tu mke yuko Germany na mtoto baba kabaki mwenyewe na kagoma kuoa shopkeeper.
 
Too sad
 
Moja kwa moja kwenye mada..

Jamaa ameoa na ana watoto watatu, ndoa yake yaweza pata miaka 10 kwasasa, ila jamaa kiukweli sio mtulivu katika ndoa yake kabisa. Katika harakati zake za kupiga michepuko na kutokufahamika pongezi nazipeleka kwa mke wake.

Katika watu ninaowasifu kwamba wamepata mke basi ni jamaa, mke ni mtulivu sana, yuko katika msimamo wa dini ile kisawasawa, na anayajua malezi ya mume, ana mapenzi ya dhati juu ya familia yake na kwa mumewe pia ama kuhusu ya ndani basi mume ndo anajua, ila naweza KUMLIA KIAPO kuwa hajawahi kuchepuka hata mara moja.

Jamaa ana mradi wa duka la tigo pesa ambao amemuweka mdada, tena huyu mdada alimtafuta mke mwenyewe, basi jamaa alirudi home mapema akaingiza gari ndani kwasababu umeme ulikuwa umekatika basi akapita pale kwa yule binti akamwambia asifunge duka anakuja wapige mahesabu, dah basi jamaa akaenda akiwa amevaa pensi yake maana sio mbali, mke akaona mbona mchizi anachelewa kurudi hayo mahesabu mahesabu gani zaidi ya masaa2, hakumpigia simu akaamua kumfuata hukohuko mweeh akakuta geti limeegeshwa kama pamefungwa kumbe jamaa yuko ndani anafanya uchafu na yule mdada.

Mke akashindwa kuvumilia akalianzisha palepale kulikuwa na chupa za soda alimtwisha nayo mumewe kichwani akampasua jamaa kashonwa nyuzi sita, yule mdada alivunjika mkono na akamchana mdomoni. Kesi ikaenda polisi mke na mume wakalazwa lokap mke akiwa na mtoto wake mdogo. Wakaambiwa hapewi mtu dhamana mpaka mtuhumiwa namba 3 azinduke maana alizimia kwa kichapo.

Yule mdada alivyoamka kesi ikaishia palepale polisi kwa masharti jamaa amuhudumie yule mchepuko chini ya uangalizi wa serikali ya mtaa mpaka apone, jamaa kama kawaida kesi yeye na mkewe kaipeleka kwa wazazi wa mke coz jamaa ni mzungumzaji sana na hivyo ana pesa akawalaghai wale wazazi mpka akawa ameshinda mke ameamuliwa arudi kwa mumewe.

Sasa balaa jipya la hivi majuzi ni kuwa jamaa alikuwa na mchepuko wake kutoka masomoni nje ya nchi alidate nae kitambo tangu sekondari, bidada karudi kwenye ajira yake, bidada kamlaghai jamaa kuwa anataka mtoto tu hana nia na mahusiano yake hata kidogo coz anajua jamaa ana mke jamaa alivyo mwehu akafanya kama alivyoombwa. Huyu bidada baada ya kujifungua ndo vituko vimeeanza sasa, katafuta namba ya mke wa jamaa na amemtumia picha za mtoto, akamwandikia ‘mwambie mumeo mtoto anamuhitaji baba ake’, kiukweli mke presha ilimpanda akapelekwa hospitali.

Mume inaonekana alijua nini kinaendelea nyumbani alivyoambiwa mkeo ameanguka amepelekwa hospitali hakushangaa, kaenda hospitali kamkuta bidada hajitambui, baadae alivyozinduka kurudi home mke kamuonyesha picha za mtoto na picha ya yule mchepuko, jamaa kashindwa kukataa wala kukubali maana kama unavyojua watoto wa nje ya ndoa ni COPY RIGHT. Mke kasema hana anachohitaji zaidi ya NDOA KUVUNJWA na ametamka wazi kuwa akilazimisha kubaki atakachokifanya anajua mwenyewe.

Ninachohofia ni reaction ya mke baada ya hii kesi kuisha maana kama mnavyojua wanawake, ameweza kuvumilia matatizo yote haya kwa sababu ya watoto wake bado wadogo ila hili ni kubwa limeshamshinda.

AM JUST A FAMILY FRIEND, NANGOJA MAAMUZI YATAKAYOCHUKULIWA AND I WILL BRING HERE THE FEEDBACK!

Kichaa huyo pesa zinamzingua
 
Mwanaume mpumbavu hujisababishia kifo chake na cha familia yake mwenyewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom