Michepuko inavunja ndoa ya jamaa

Michepuko inavunja ndoa ya jamaa

Zambotti

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2016
Posts
1,983
Reaction score
3,670
Moja kwa moja kwenye mada..

Jamaa ameoa na ana watoto watatu, ndoa yake yaweza pata miaka 10 kwasasa, ila jamaa kiukweli sio mtulivu katika ndoa yake kabisa. Katika harakati zake za kupiga michepuko na kutokufahamika pongezi nazipeleka kwa mke wake.

Katika watu ninaowasifu kwamba wamepata mke basi ni jamaa, mke ni mtulivu sana, yuko katika msimamo wa dini ile kisawasawa, na anayajua malezi ya mume, ana mapenzi ya dhati juu ya familia yake na kwa mumewe pia ama kuhusu ya ndani basi mume ndo anajua, ila naweza KUMLIA KIAPO kuwa hajawahi kuchepuka hata mara moja.

Jamaa ana mradi wa duka la tigo pesa ambao amemuweka mdada, tena huyu mdada alimtafuta mke mwenyewe, basi jamaa alirudi home mapema akaingiza gari ndani kwasababu umeme ulikuwa umekatika basi akapita pale kwa yule binti akamwambia asifunge duka anakuja wapige mahesabu, dah basi jamaa akaenda akiwa amevaa pensi yake maana sio mbali, mke akaona mbona mchizi anachelewa kurudi hayo mahesabu mahesabu gani zaidi ya masaa2, hakumpigia simu akaamua kumfuata hukohuko mweeh akakuta geti limeegeshwa kama pamefungwa kumbe jamaa yuko ndani anafanya uchafu na yule mdada.

Mke akashindwa kuvumilia akalianzisha palepale kulikuwa na chupa za soda alimtwisha nayo mumewe kichwani akampasua jamaa kashonwa nyuzi sita, yule mdada alivunjika mkono na akamchana mdomoni. Kesi ikaenda polisi mke na mume wakalazwa lokap mke akiwa na mtoto wake mdogo. Wakaambiwa hapewi mtu dhamana mpaka mtuhumiwa namba 3 azinduke maana alizimia kwa kichapo.

Yule mdada alivyoamka kesi ikaishia palepale polisi kwa masharti jamaa amuhudumie yule mchepuko chini ya uangalizi wa serikali ya mtaa mpaka apone, jamaa kama kawaida kesi yeye na mkewe kaipeleka kwa wazazi wa mke coz jamaa ni mzungumzaji sana na hivyo ana pesa akawalaghai wale wazazi mpka akawa ameshinda mke ameamuliwa arudi kwa mumewe.

Sasa balaa jipya la hivi majuzi ni kuwa jamaa alikuwa na mchepuko wake kutoka masomoni nje ya nchi alidate nae kitambo tangu sekondari, bidada karudi kwenye ajira yake, bidada kamlaghai jamaa kuwa anataka mtoto tu hana nia na mahusiano yake hata kidogo coz anajua jamaa ana mke jamaa alivyo mwehu akafanya kama alivyoombwa. Huyu bidada baada ya kujifungua ndo vituko vimeeanza sasa, katafuta namba ya mke wa jamaa na amemtumia picha za mtoto, akamwandikia ‘mwambie mumeo mtoto anamuhitaji baba ake’, kiukweli mke presha ilimpanda akapelekwa hospitali.

Mume inaonekana alijua nini kinaendelea nyumbani alivyoambiwa mkeo ameanguka amepelekwa hospitali hakushangaa, kaenda hospitali kamkuta bidada hajitambui, baadae alivyozinduka kurudi home mke kamuonyesha picha za mtoto na picha ya yule mchepuko, jamaa kashindwa kukataa wala kukubali maana kama unavyojua watoto wa nje ya ndoa ni COPY RIGHT. Mke kasema hana anachohitaji zaidi ya NDOA KUVUNJWA na ametamka wazi kuwa akilazimisha kubaki atakachokifanya anajua mwenyewe.

Ninachohofia ni reaction ya mke baada ya hii kesi kuisha maana kama mnavyojua wanawake, ameweza kuvumilia matatizo yote haya kwa sababu ya watoto wake bado wadogo ila hili ni kubwa limeshamshinda.

AM JUST A FAMILY FRIEND, NANGOJA MAAMUZI YATAKAYOCHUKULIWA AND I WILL BRING HERE THE FEEDBACK!
 
Mkuu huyo jamaa kama kulivuruga amevuruga kweli kweli.
Hapo inabidi waende kwa kiongozi wao wa dini asuluhishe hili imani ya kidini hapo itasaidia aiseeh.
 
Moja kwa moja kwenye mada..

Jamaa ameoa na ana watoto watatu, ndoa yake yaweza pata miaka 10 kwasasa, ila jamaa kiukweli sio mtulivu katika ndoa yake kabisaa. Katika harakati zake za kupiga michepuko na kutokufahamika pongezi nazipeleka kwa mke wake.

Katika watu nnaowasifu kwamba wamepata mke basi ni jamaa, mke ni mtulivu sana, yuko katika msimamo wa dini ile kisawasawa, na anayajua malezi ya mume, ana mapenzi ya dhati juu ya familia yake na kwa mumewe pia ama kuhusu ya ndani basi mume ndo anajua, ila naweza KUMLIA KIAPO kuwa hajawahi kuchepuka hata mara moja.

Jamaa ana mradi wa duka la tigo pesa ambao amemuweka mdada, tena huyu mdada alimtafuta mke mwenyewe, Basi jamaa alirudi home mapema akaingiza gari ndani kwasababu umeme ulikuwa umekatika basi akapita pale kwa yule binti akamwambia asifunge duka anakuja wapige mahesabu, dah basi jamaa akaenda akiwa amevaa pensi yake maana sio mbali, mke akaona mbona mchizi anachelewa kurudi hayo mahesabu mahesabu gani zaidi ya masaa2, hakumpigia simu akaamua kumfuata hukohuko mweeh akakuta geti limeegeshwa km pamefungwa kumbe jamaa yuko ndani anafanya uchafu na yule mdada.

Mke akashindwa kuvumilia akalianzisha palepale kulikuwa na chupa za soda alimtwisha nayo mumewe kichwani akampasua jamaa kashonwa nyuzi sita, yule mdada alivunjika mkono na akamchana mdomoni. Kesi ikaenda polisi mke na mume wakalazwa lokap mke akiwa na mtoto wake mdogo . wakaambiwa hapewi mtu dhamana mpaka mtuhumiwa namba 3 azinduke maana alizimia kwa kichapo.

Yule mdada alivyoamka kesi ikaishia palepale polisi kwa masharti jamaa amuhudumie yule mchepuko chini ya uangalizi wa serikali ya mtaa mpaka apone, jamaa kama kawaida kesi yeye na mkewe kaipeleka kwa wazazi wa mke coz jamaa ni mzungumzaji sana na hivyo ana pesa akawalaghai wale wazazi mpka akawa ameshinda mke ameamuliwa arudi kwa mumewe.

Sasa balaa jipya la hivi majuzi ni kuwa jamaa alikuwa na mchepuko wake kutoka masomoni nje ya nchi alidate nae kitambo tangu sekondari, bidada karudi kwenye ajira yake, bidada kamlaghai jamaa kuwa anataka mtoto tu hana nia na mahusiano yake hata kidogo coz anajua jamaa ana mke jamaa alivyo mwehu akafanya kama alivyoombwa. Huyu bidada baada ya kujifungua ndo vituko vimeeanza sasa, katafuta namba ya mke wa jamaa na amemtumia picha za mtoto, akamwandikia ‘mwambie mumeo mtoto anamuhitaji baba ake’, kiukweli mke presha ilimpanda akapelekwa hospitali.

Mume inaonekana alijua nini kinaendelea nyumbani alivyoambiwa mkeo ameanguka amepelekwa hospitali hakushangaa, kaenda hospitali kamkuta bidada hajitambui, baadae alivyozinduka kurudi home mke kamuonyesha picha za mtoto na picha ya yule mchepuko, jamaa kashindwa kukataa wala kukubali maana kama unavyojua watoto wa nje ya ndoa ni COPY RIGHT. Mke kasema hana anachohitaji zaidi ya NDOA KUVUNJWA na ametamka wazi kuwa akilazimisha kubaki atakachokifanya anajua mwenyewe.

Nnachohofia ni reaction ya mke baada ya hii kesi kuisha maana kama mnavyojua wanawake, ameweza kuvumilia matatizo yote haya kwa sababu ya watoto zake bado wadogo ila hili ni kubwa limeshamshinda.

AM JUST A FAMILY FRIEND, NANGOJA MAAMUZI YATAKAYOCHUKULIWA AND I WILL BRING HERE THE FEEDBACK!!!!

yani wewe unamjua mke wa jamaa kuliko yeye? aisee kama jamaa ananyimwa kipapa unajua? au kama mwanamke ndani ni wakununa tu unajua? au kama mwanamke mbinafsi chake chake tu na ndugu zake unajua? acheni tabia za kujifanya mnawajua wake za watu kuna wanaume wanakuwa na michepuko sio kwa sababu mke wa ana michepuko bali mwanamke unakuta ndani hapakaliki sababu ya mwanamke, kwa mfano kuna wanawake wajuaji kupitiliza na wanafanya maamuzi yao kulingana na marafiki zao huyo hana mchepuko ila anaweza kukufanya ukawa na michepuko maana kila unachosema au kufanya mwanamke haoni sawa hadi aambiwe na mashoga
 
Ipo siku siku ataletewa ukimwi ama kaswende huyo mdada .... Mume kwangu atabaki kuwa mume ila kwa uzinzi samahani namwachia tu awe free akafanye yooote na dini inaruhusu kwa habari ya uzinzi tunaaachana ... maana unaeza kuta huko anapewa tigo sasa mie saa ngapi nifyatue tigo yangu nimpe naheshimu marinda yanguuu ... Thubutu aende tuuuuu
 
A married man eti unaombwa na mtu mzae, jamaniiiiiiii. Afu sio michepuko ndo imevunja ndoa yake, ni yeye ndo amevunja ndoa yake kwa upumbavu wake
 
kwa kuwa bidada ameona inatosha na kaamua kuondoka nadhani yupo sahihi kabisa aondoke asijefanya majanga zaidi...

ila wanaume mjifunze kama unampenda mkeo mlinde na mtunze kama michepuko unashindwa kuacha hakikisha unalinda famiia yako..

na kama unaona humpendi mkeo na huwezi mpenda kuwa wazi kuwa sikupendi mpe haki zake na weka mikakati ya kutunza familia achana na mkeo na si kumsababishia magonjwa afe mapema aache watoto wadogo huku hiyo michepuko yako haiwezi lea mwanao ...

wanawake usikubali kuachika mikono mitupu hakikisha anaanza moja ... nasisitiza hakikisha unapata faida ya huo muachiko ... nirushieni mawe nitakwepa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom