Michelle obama apata adhabu airport

Michelle obama apata adhabu airport

Status
Not open for further replies.

AFRIKA KWETU

Member
Joined
May 21, 2013
Posts
29
Reaction score
8
Mke wa Rais wa Marekani Bi. Michelle Obama, amepata usumbufu wa kurekebisha kigauni chake kifupi na chepesi kutokana na hali ya upepo iliyotawala katika maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam. Haya yametokea katika uwanja wa ndege wa Mwl. Julius K. Nyerere wakati wa mapokezi ya Rais Obama uwanjani hapo. Michelle alionekana kukoswa utulivu kwani wakati wote mikono yake ilionekana kushughulikia uvutaji wa kigauni chake na kukirekebisha ili kikae sawa. Aidha, Michelle alionekana kuwa na kazi ya kuukabili upepo kwa kusimama katika mwelekeo utakaomsaidia kuikwepa aibu iliyokuwa inaelekea kumpata. Wakati huohuo, mwenyeji wake Mama Salma Kikwete alionekana kujiamini muda wote kwani kama ilivyo kawaida yake, alijisetiri ndani ya vazi lake la tenge la ukweli.
 
Na amfikishie sms mume wake, hatutaki sera za ushoga, km ye mapaja yake tu hataki tuyaone
 
Salma naye angetupia kimini flani hivi, waende sawa. Mara moja moja sio mbaya.
Naomba muongozo!
 
Mama Salma Kikwete alionekana kujiamini muda wote kwani kama ilivyo kawaida yake, alijisetiri ndani ya vazi lake la tenge la ukweli.

Uvaaji wake ni mfano bora wa kuigwa. a real black/african woman
 
Mke wa Rais wa Marekani Bi. Michelle Obama, amepata usumbufu wa kurekebisha kigauni chake kifupi na chepesi kutokana na hali ya upepo iliyotawala katika maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam. Haya yametokea katika uwanja wa ndege wa Mwl. Julius K. Nyerere wakati wa mapokezi ya Rais Obama uwanjani hapo. Michelle alionekana kukoswa utulivu kwani wakati wote mikono yake ilionekana kushughulikia uvutaji wa kigauni chake na kukirekebisha ili kikae sawa. Aidha, Michelle alionekana kuwa na kazi ya kuukabili upepo kwa kusimama katika mwelekeo utakaomsaidia kuikwepa aibu iliyokuwa inaelekea kumpata. Wakati huohuo, mwenyeji wake Mama Salma Kikwete alionekana kujiamini muda wote kwani kama ilivyo kawaida yake, alijisetiri ndani ya vazi lake la tenge la ukweli.

Ni kweli kabisa. Hata mimi niliona hivyo. Next time atakaporudi dar awe makini katika uchaguzi wa magauni. Napendekeza avae suruali.
 
Kweli ni kama anafanya makusudi kuwaelekeza ma Festiledi jinsi ya kuvaa
Kujifunika mavitenge ndio kujuwa kuvaa?

Kila mtu ana utamaduni wake, alivyovaa Michelle ndio utamaduni wa Kimarekani, msitake kulazimisha kila mtu aishi kama nyinyi.

Huyo Salma kama anajuwa sana maadili amuige Hawa Ghasia ndivyo Mwanamke wa Kiislamu anavyopaswa kujisitiri, nywele zake asubili akiwa na Mkwele chumbani ndio amuoneshe.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom