Michango ya ufadhili wa harusi ni wizi uliojificha

Michango ya ufadhili wa harusi ni wizi uliojificha

Baba Uzia

Senior Member
Joined
Jul 19, 2015
Posts
136
Reaction score
54
Suala la kuchapisha kadi za ufadhili na kuwagawia watu ili wakuchangie huo ni wizi uliobarikiwa. Unaoa wewe itakuwaje utuchangishe sisi?

Mchango ni hiari lakini ukikwama ukashindwa kutoa utayasikia maneno. Imeandikwa wapi ili sherehe ya harusi ikamilike inahitaji mamilioni ya pesa? Kwanini ufanye kitu kikubwa kuliko uwezo wako?

Kama uwezo wako ni sh. 500,000 kwanini usiipangilie vizuri kuwa nikialika watu kadhaa bajeti yangu itatosha au la! Au ndoa ili ibarikiwe inatakiwa ihudhuriwe na umati mkubwa wa watu?

Acheni kupiga dili badilikeni kama hauna kitu kikubwa kama fulani usijikweze.
 
Ni wizi.. Ukimwambia mtu kusanya marafiki na immediate family hawazidi watu mia anataka kufunga ndoa akaribishe watu 700halafu pesa mummtolee.. Jamani..

Tunayumbisha maendeleo kwa kuendekeza anasa na starehe. Ukiwa na milion mbili inatosha kabisa kufanya harusi.. Tafuteni wewe na mkeo mtukaribishe tule sio mnasumbua watu usiku wa manane ..[HASHTAG]#bro[/HASHTAG] mchango sijauona mkuu#
 
Wewe umesha funga ndoa?
Hapana najipanga, bajeti niliyopanga kulingana na uwezo wangu Siku ikifika ndio nafanya mkakati sitaki kuingiza gharama watu wengine. Kitakachofanyika ni mwaliko tu[emoji350]
Suala la kuchapisha kadi za ufadhili na kuwagawia watu ili wakuchangie huo ni wizi uliobarikiwa. Unaoa wewe itakuwaje utuchangishe sisi?

Mchango ni hiari lakini ukikwama ukashindwa kutoa utayasikia maneno. Imeandikwa wapi ili sherehe ya harusi ikamilike inahitaji mamilioni ya pesa? Kwanini ufanye kitu kikubwa kuliko uwezo wako?

Kama uwezo wako ni sh. 500,000 kwanini usiipangilie vizuri kuwa nikialika watu kadhaa bajeti yangu itatosha au la! Au ndoa ili ibarikiwe inatakiwa ihudhuriwe na umati mkubwa wa watu?

Acheni kupiga dili badilikeni kama hauna kitu kikubwa kama fulani usijikweze.
 
Kinachosumbua miongoni mwa vichwa vya watu ni ulimbukeni eti anataka anataka mtaa mzima awe wa mfano.
 
Kwani umelazimishwa kuchanga. Pambana na hali yako tuache sisi tuendelee na upendo na mshikamano wetu.
 
Back
Top Bottom