Michango ya rambirambi misibani watu wengi huchanga kinafiki sana

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,549
22,095
Wadau,

Hatukatai watu uwezo wanazidiana lakini si kwa unafiki huu;

1. Mtu anachangia mia mbili au mia tano kweli? Halafu unaandika na jina kweli? Hivi kweli kama lengo ni kukusanya hela ya kusafirisha msiba au kutatua tatizo; ni kweli mia mbili yako itasaidia kweli? TUBADILIKE.

2. Unakuta misiba ya watu fukara daftari zima majina yamejaa jero jero, na elfu moja tu; hadi daftari linajaa ukijumlisha haifiki hata laki moja; huu si ni unafiki jamani?

3. Cha ajabu mtu yule yule masikini siku akienda msiba wa tajiri utashangaa anatoa elfu ishirini kisa tu kakuta watu wamechangia laki laki na kuendelea.
TOENI KWA MOYO SIYO KINAFIKI.

KABLA HUJATOA FIKIRIA KWANZA PESA YAKO UNAYOTOA ITAWEZA KUWASAIDIA WAFIWA?
*************************
Ni vyema zaidi tuwasaidie wagonjwa kadri tunavyoweza na ikitokea wamekufa; tujitolee kwa moyo.
*********************
Hivi misibani nini lengo la utaratibu wa kula ubwabwa kabla ya mazishi;? Hiki ndicho huenda hujaza wanafiki msibani.
 
Pole mkuu kwa yaliyokukuta hawa ndio binadamu wanakuthamini kwa ulichonacho.
 
Ile ni rambi rambi , suo mchamgo wa harusi kwamba uweke kiwango, alaf hali ni tight ndio mana mtu anajipinda 200..pia kupata hiyo jero ushukuru mana wengine wangepitisha kavu na msosi wakaula.
 
Ile ni rambi rambi , suo mchamgo wa harusi kwamba uweke kiwango, alaf hali ni tight ndio mana mtu anajipinda 200..pia kupata hiyo jero ushukuru mana wengine wangepitisha kavu na msosi wakaula.
Sasa huu ndio unafiki tiktiki
 
Haiwezekani mtu na akili zako unatoa jero msibani halafu ukienda kwa matajiri ili uonekane unauza mpaka kuku kwenda kujipendekeza
 
Na Nyie Mbwembwe za nini kusafirisha Maiti wakati uwezo huo hamna? Kwani akizikiwa hapa hatofufuka Siku ya Kiyama!

Badilikeni bana Mnasafirisha Mwili mpaka Mbeya kwa Milion 2 halafu mnamuacha Mtoto wa Marehemu bila ya Ada ya laki mbili anayodaiwa Shule ni akili kweli hizi?
 
Back
Top Bottom